UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA MBALIMBALI
28/05/2022
Ndugu wasomaji Ningependelea kuwaletea katika mlango huu utafiti mbalimbali wenye uhusiano na Kuruani Tukufu.
Maneno ya Mwenyeezi Mungu ni yenye uhai kama alivyo aliyeyashusha maneno haya ambaye ni hai pia, hana mwanzo na hana mwisho. Ukitaka kumjua Mwenyeezi Mungu basi jiangalie wewe mwenyewe. Na ninakuhakikishia kwamba Hutaweza na hakuna Dakitari au kiumbe anayeweza kusema kwamba Binaadamu tumekwisha kumsoma na hakuna jingine la kumsoma. Ukisema hivyo utakuwa umejidanganya. Ukimaliza kazi hiyo sasa uendelee kusoma viumbe vinginevyo.
Kwa kweli Sayansi bado haijamaliza kumsoma Binaadamu na viumbe vinginevyo pia.
Katika Mlango huu tutasoma Mlango wa DNA ambao ni moja ya milango mbalimbali ya Elimu ya Genetics. Ni Mlango unaohusiana na Maumbile.
Kabla ya kuanza Kuchambua DNA ningependelea kuwaletea Muujiza Wa Aya Ya Kuruani ambao hauna Uhusiano na Mada ya DNA lakini nimeona Bora nianze na Aya hii ikiwa kama Ufunguo wa Mlango huu wa Elimu ya Genetics-DNA
MUUJIZA WA MANENO MAWILI YENYE KUWAKILISHA KURUANI TUKUFU
KWANZA – AYA KUTOKA KATIKA SURA YA YUNUS NAMBA 35
قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآٮِٕكُم مَّن يَہۡدِىٓ إِلَى ٱلۡحَقِّۚ قُلِ ٱللَّهُ يَہۡدِى لِلۡحَقِّۗ أَفَمَن يَہۡدِىٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَہِدِّىٓ إِلَّآ أَن يُہۡدَىٰۖ فَمَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ (٣٥)
TAFSIRI
35· Sema “Je! Yuko katika hao mnaomshirikisha Mwenyezi Mungu aongozaye katika haki?” Sema: “Mwenyezi Mungu ndiye anayeongoza katika haki.” Basi aongozaye katika haki siye anayestahiki zaidi kufuatwa au ( anastahiki) yule asiyeongoka (hata yeye mwenyewe) isipokuwa aongozwe? Basi mumekuwaje? Mnahukumuje?”
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anatufundisha katika Aya hii kwamba yeye tu ndiye anastahiki kuabudiwa na siyo mwingine katika viumbe vyake. Na anatufundisha namna ya kuwajibu wasiomfuata. Hii ndiyo madhumuni ya Aya hii. Mtume ﷺ Mohamad anafundishwa namna ya kuhojiana na makafiri kwa njia ya Hekima. Na sisi ndivyo inatupasa tuhojiane na wasiomfuata Mwenyeezi Mungu kwa njia ya Kielimu na siyo Matusi.
HESABU ZA KUSHANGAZA KATIKA AYA HII
Hebu tuchunguze maneno mawili katika Aya hii
Neno “Uongofu” na neno “Haki”
Neno يَہۡدِىٓ lenye maana ya Uongofu ni la 6 katika Aya hii
Neno ٱلۡحَقِّۚ lenye maana ya Haki ni la 8 katika Aya hii
Neno يَہۡدِى lenye maana ya Haki ni la 11 katika Aya hii
Neno لِلۡحَقِّۗ lenye maana ya Haki ni la 12 katika Aya hii
Neno يَہۡدِىٓ lenye maana ya Uongofu ni la 14 katika Aya hii
Neno ٱلۡحَقِّ lenye maana ya Haki ni la 16 katika Aya hii
Neno يَہِدِّىٓ lenye maana ya Haki ni la 22 katika Aya hii
Neno يُہۡدَىٰۖ lenye maana ya Uongofu ni la 25 katika Aya hii
Hebu tujumlishe namba hizi za (Positions za maneno haya katika Aya Hii)
6 + 8 + 11 + 12 + 1 4 + 16 + 22 + 25=114
Je unaona ya kushangaza!!!!
Maneno haya mawili, la kwanza lina maana ya Uongofu na la pili Lina maana ya Haki. Ukijumlisha Pisitions zake kihesabu unapata jawabu 114 na namba hii inaashiria Jumla ya Sura zote za kuruani tukufu ambazo ni 114. Allahu Akbar. Na hii inathibitisha kwamba Kuruani INALETA UONGOFU NA HAKI. Angalia mwenyewe kwa macho yako. Hata aiyejua lugha ya kuruani anaweza kufuata maelezo haya. Ni Rahisi kueleweka. Namba peke yake zinaonyesha muujiza. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA DNA
DNA NA CHROMOSOMES
Sasa Ningependelea Kuanza kuelezea Habari za DNA kama nilivyoahidi katika mazungumzo yangu hapo awali. Pia Nimeweka Picha mbalimbali hapa chini ili habari hii ieleweke vizuri zaidi.
Katika Celi (Cells) za Viumbe vyote venye uhai kama vile Binaadamu, Wanyama, Wadudu, Njiwa, Na hata Miti na kila kitu kuna Chromosomes au Kwa kiswahili kizuri nitaita “KANDA” Kwa kifupi Chromosomes zinatokana na DNA na Proteins. Binaadamu ana Chromosome au Kanda 46, na kila kiumbe kinatofautiana idadi ya Chromosomes (Kanda). Katika Cells au Celi kuna Nucleus (Kiini Tete) na Katika Nucleus kuna Chromosomes na hizi ndizo zinazobeba GENES na hizi ndizo zinazobeba Elimu za Maumbile na Maamrisho ya Ujenzi wa Proteins. Chromosomes ni ndogo sana na huwezi kuona kwa macho bila kutumia vyombo vya sayansi vya hali ya juu.
UMBILE LA CHROMOSOMES
Chromosome lina umbile la “MSUKO” au kwa kiswahili kizuri ni Umbile la Kusuka Kusuka kama vile Kamba ilivyosukwa au Spring. Wataalamu wamepima Mapindo ya Misuko hiyo na kutufahamisha kwamba kuna Mapindo au Groove Kubwa na Ndogo (Angalia Picha hapa chini na utaelewa haya ninayoelezea). Groove Ndogo una upana wa Angstroms karibu 12 (Namba hii inabadilika badilika lakini 12 ni mojawapo wa kipimo hiki.) Na Groove Kubwa una Upana wa Angstroms 22 (Namba hii inabadilika badilika lakini 12 ni mojawapo wa kipimo hiki). Ukijumlisha Mapindo (Groove) hizi mbili utapata Urefu wa Pindo moja ni Angstroms 34. Pindo moja ni Jumla ya Mapindo mawili. (Minor na Major Groove). Nadhani Imeeleweka vizuri. Vipimo hivi ni vidogo sana na inahitaji Vyombo y=vya kitaalamu vya hali ya juu. Na ndiyo maana Kumetumika Kipimo cha Angstroms kwani ni kipimo maarufu kinachotumika kwa kupimia viungo vidogo kama hivi. Katika Physics tunaelezewa kwamba Angstroms ni
(Angstrom (Å), unit of length, equal to 10−10 metre, or 0.1 nanometre. It is used chiefly in measuring wavelengths of light. (Visible light stretches from 4000 to 7000 Å.) It is named for the 19th-century Swedish physicist Anders Jonas Ångström)
DNA na Chromoses kwa Kiingereza Inaelezewa kama ifuatavyo:
(Deoxyribonucleic acid (DNA) is an organic chemical that contains genetic information and instructions for protein synthesis. It is found in most cells of every organism. DNA is a key part of reproduction in which genetic heredity occurs through the passing down of DNA from parent or parents to offspring.DNA tells a cell how to make proteins through the genetic code. Both DNA and proteins are long molecules made from strings of shorter building blocks. While DNA is made of nucleotides, proteins are made of amino acids, a group of 20 different chemicals with names like alanine, arginine, and serine. A chromosome is made up of proteins and DNA organized into genes. Each cell normally contains 23 pairs of chromosomes)
AYA YA KURUANI YENYE KUSHANGAZA
فَوَجَدَا عَبۡدً۬ا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا (٦٥)
TAFSIRI
Basi wakamkuta mja katika waja wetu (Sisi Mwenyezi Mungu) tuliyempa rehema kutoka kwetu na tuliyemuelimisha ilimu (nyingi) zinazotoka kwetu.
SHEREHE
Aya hii inahusiana na Kisa cha Nabii Musa na Al-Khidri. (Inasemekana kwamba Al-Khidri alikuwa Nabii) Huu ni miongoni mwa Miujiza Mikubwa. Nabii Musa akakutana na Kiumbe chake Mwenyeezi Mungu alichokipa Elimu kubwa. Ilikuwa ni Hekima kubwa kwani Nabii Musa alipojidhania kuwa ana Elimu kubwa basi Mwenyeezi Mungu akamkutanisha na Al-Khidri ambaye alipewa Elimu kubwa. Hili lilikuwa fundisho kwa Nabii Musa na kila Kiumbe kwamba tusijigambe kwa hizi Elimu zetu ndogo. Kuna Mengi ambayo hatuyajui.
Alama aliyopewa Nabii Musa ya kumfahamisha kuwa mahala hapo ndipo atakapokutana na huyo AI-Khidri ni kuwa samaki wake aliyekwisha kupikwa atafufuka atoke kikapuni ende zake baharini. Basi walipofika mahala fulani karibu na bahari wakatua hapo kupumzika, Nabii Musa alilala kidogo, na yule kijana mdogo aliyekuwa msaidizi wake) alikuwa yupo macho. Mara akamuona yule samaki aliyekwisha kupikwa anatoka kikapuni anafuala njia katika ufuko wa pwani na huku inafanya alama hiyo njia anayopita, mpaka akaingia baharini. Akasema yule kijana moyoni mwake kuwa akiamka Nabii Musa nitampa habari ya ajabu, lakini alisahau. Alipoamka Nabii Musa, hao wakaondoka na kwenda mbele. Hata baada ya kufika mbali ukafika wakati wa kula. Nabii Musa akataka chakula, hapo ndipo yule kijana alipokumbuka akamjuvya Nabii Musa habari ile. Basi Nabii Musa akamwambia warejee huko ulipotokea muujiza huo kwani hapo ndipo watakapomkta huyo wanayemtafuta. Basi wakarejea kwa njia ile ile; na walipofika hapo wakamkuta huyo Nabii AI Khidri; yakatokea hayo tuliyosimulia. Lakini tafsiri ya vitendo hivyo alivyovifanya Nabii AI Khidri vitasimuliwa katika juzuu ya 16 inayofuatia juzuu hii. Hapa utaona mshangazo lakini ukishakuona tafsiri yake utakutoka mshangao huu
UTAFITI WA KUSHAGAZA KUHUSU DNA NA VIPIMO VYAKE
Katika Kuruani Kuna Maneno zaidi ya Mia yenye Herufi Dal, Nun na Alif lakini Aya hii ni Pekee kwa sababu ina maneno Matatu yenye Herufi hizi Tatu.
Hebu tuichunguze Aya hii. Jambo linalonishagaza ni kwamba Maneno Matatu yaana maana kama ifuatayo hapa chini:
عِبَادِنَآ Neno lenye maana ya waja wetu
عِندِنَا Neno lenye maana ya (Kutoka) kwetu
لَّدُنَّا Neno lenye maana ya (zinazotoka) kwetu
Maneno haya Matatu Kila moja Lina Herufi Tatu. Herufi Ya kwanza ni DAL, Ya pili ni NUN na Ya Tatu ni ALIF. Ninajiuliza Swali, Je hizi Herufi Tatu zinaashiria DNA tuliyosoma hapo Juu? Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi. Ninajiuliza Swali hili kwani Sura ya Aya ni Namba 18 na Aya ni Namba 65. Ukiweka namba hizi pamoja yaani 1865 unapata Mwaka ambao Sheria za Elimu ya Genetics ilipogunduliwa. Kwa mara ya Kwanza na Mtaalamu anayejulikana kama Gregor Mendel. (1865 – Mendel Develops his First Theories of Inheritance)
La kushangaza zaidi ni Vipimo vya GROOVES (MAPINDO) tuliyoyataja katika Sherehe hapa Juu. Hebu tuchunguze Vipimo hivi kwa kuhesabu Herufi za Aya Hii.
فَوَجَدَا عَبۡدً۬ا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا (٦٥)
Ukihesabu herufi za kipande cha Aya utapata jumla ya herufi ni 22
عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا
Na ukihesabu kipande cha herufi cha pili utapata jumla ya herufi ni 12
وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا
Namba 22 ni Kipimo cha Angstroms cha Groove (Pindo) la kwanza na Namba 12 ni Kipimo cha Angstroms ya Groove (Pindo) la pili.
Ukijumlisha Vipimo hivi viwili utapata urefu wa Pindo moja ni Angstroms 34 kama wanavyotuambia wataalamu wa Elimu hii. Allahu Akbar.
Kwa kweli inashangaza sana. Elimu hizi ni za kisasa na Kuruani ilishuka karne ya 7 kwa Mtume asiyejua kusoma na kuandika. Sasa Elimu kubwa kama hii ambayo inahitajia Vyombo na Utaalamu wa hali ya juu sana je inawezekana vipi kuwa kuruani siyo maneno ya Mwenyeezi Mungu. Hata kidogo. Kuruani ni Muujiza Mkubwa sana kwa wenye kufikiri. Hebu fikiri. Kama huu siyo Muujiza basi nieleze ni Kitu gani? Hebu fikiri. DNA ipo ndani ya Nucleus ambayo huwezi kuona kwa macho. Kisha Chrosmosomes ambazo ndogo sana. Na Vipimo Vyake. Hii inathibitisha kwamba Yule Yule aliyeshusha Kuruani ndiye yule yule aliyeumba kila kitu. Allahu Akbar. Hapa Chini nitaweka Picha za Habari hizi ieleweke Vizuri zaidi. Allahu Akbar. Na zaidi Anajua Mwenyeezi Mungu iwapo tumesibu. Na huenda akatupa angalau thawabu kidogo kwa juhudi na hata kama tumekosea. Alhamdulilah. Rehema zake zipo kila mahali
Vipimo vya herufi za Aya Ya Kuruani na Vipimo vya Mapindo ya Chromosome. Chromosome na Mapindo Yake. Vipimo Vya Groove Kubwa na Ndogo na pia Urefu wa Pindo Moja. Pindo ni Mfano wa Kamba Ilivyosukwa. Nimeelezea habari hizi katika Sherehe hapa juu.




Hapa juu Picha Ya Chromosome Na Grooves Zake. (Mapindo Yake)


Picha Ya DNA ambayo ina Chromosomes na Proteins.Mfumo au Structure ya DNA. Ndani ya Nucleus kuna Chromosome na hizi Chromsomes zinabeba Genes. Genes ndizo zenye Kubeba Habari ya Maumbile