UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MUUJIZA WA KURUANI KUPANGA MANENO KWA KUTUMIA MIZANI YA LUGHA YA HALI YA JUU
Muujiza wa Majina Mawili Ya Jengo La Ibada Huko Mecca. (BAYT AL-HARAM الْبَيْتَ الْحَرَامَ na KAABAH الْكَعْبَةِ )
Majina الْبَيْتَ الْحَرَامَ na الْكَعْبَةِ yana maana moja. Ni Jengo la ibada huko Mecca. Haya Majina Mawili yametajika katika Aya 3 pekee Zifuatazo katika Kuruani yote. Sasa angalia Mwenyeezi Mungu alivyozipanga. Inaonyesha dalili kwamba ni upangaji wake na hakuna mwingine na siyo bure bure.
Katika Aya Namba 2 Sura Ya Al-Maidah Jengo la ibada huko Mecca limetajika mara moja kwa jina la “Bayt Alharam”
(وَ لَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِنْ رَبِّهِمْ وَ رِضْوَانًا) [المائدة: 2]
Na Katika Aya Namba 95 Sura Ya Al-Maidah Jengo la ibada huko Mecca Limetajika Mara Moja Pia kama ifuatavyo:
(يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِنْكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ) [المائدة: 95]
Sasa Tuangalie Muujiza katika Aya Hizi Mbili;
Muujiza katika Aya hizi mbili Ni Aya ya kwanza ambayo ni Namba 2 na Aya ya pili ambayo ni Aya Namba 95 ambazo kila moja imetaja Jina la Kaabah Na Bayt Alharam mara moja moja ambazo zina maana moja.
Muujiza Ni kwamba Maneno haya mawili ambayo yana maana moja kila moja limetajika mara moja katika Aya namba 2 na 95 na Ukijuumlisha Namba 2 na Namba 95 utapata jawabu 97 ambayo inaashiria Aya namba 97 na katika Aya hii namba 97 katika sura hiyo hiyo ya Al-Maidah tunakuta Majina Yote mawili ya Kaabah na Bayt Alharam.
Ni sawa sawa na kusema “ukijumlisha Aya namba 2 na 95 basi utayakuta majina yote mawili katika Aya moja namba 97 ambayo ni sawa na kujumlisha Aya Mbili namba 95 na 2”
Je unaona Mpangilio huu wa Kiajabu?,
Katika Aya Ifuatayo Kaaba imetajika mara mbili kwa Majina Mawili: “Kaaba” na “Bayt Al-Haram”. Majina Yote mawili yana maana ya jengo la “Kaabah” huko Mecca na majina yote mawili katika Aya Moja namba 97 Sura Ya Al-Maidah
(جَعَلَ اللَّهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِلنَّاسِ) [المائدة: 97]
Lazima tuelewe kwamba kuruani yote imeshuka kwa Mtume (S.A.W) kwa muda wa miaka 23 na alikuwa akiambiwa sehemu za kuziweka katika Kuruni na leo hii tunagundua Miujiza ya kushangaza kama huu na Wala Mtume (S.A.W) hakujua haya mapya.. Allahu Akbar. Allahu Akbar
MUUJIZA WA MANENO MAWILI YENYE MAANA YA “MWAKA” (Neno Sanaa سنة Na Neno A’am عام)
Haya Maneno mawili;
Neno Sanaa سنة Na Neno A’am عام yaana Maana moja yaani “MWAKA” lakini kuna tofauti katika matumizi, Mwaka uliyo na Neema yaani mwaka mzuri neno “A’m” عام linatumika na mwaka ulio na matatizo au shida basi neno “Sanat” سنة linatumika.
Kwa kifupi maneno haya mawili yana maana moja yaani “MWAKA” lakini سنة ni “Mwaka Mbaya” na عام ni “Mwaka Mzuri”
Muujiza wa kwanza;
ni Kwamba Mpangilio wa kuruani ni wa hali ya Juu sana. Neno سنة limetumika mara 7 tu katika Aya 7 na neno عام limetumika mara 7 tu katika Aya 7 Angalia Muujiza wa kwanza wa Kukariri mara 7 kila jina katika majina yenye maana moja ambayo hata kukariri kunafanana.
Sasa Unafuata Muujiza wa Pili Ukijumlisha namba hizi mbili yaani 7 mara mbili unapata 14 na ajabu ni kwamba maneno yote mawili yanaashiria Aya moja namba 14 Sura Ya Al-Ankaboot.
(وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا) [العنكبوت: 14].
Sasa angalia huu Muujiza. Aya hii ni namba 14 ni sawa na imekusanya maneno yote mawili سنة NA عام ambayo yametajika katika Aya 7 kila moja. Ukijumlisha Aya za sura hizi mbili unapata Jumla Aya 14 (7 + 7=14) ambayo inaashiria Aya Namba 14 katika Sura Ya Al-Ankabut !!!
Unaona Muujiza mbele ya macho yako. Allahu Akbar.
Katika Kuruani yote kila neno katika Maneno haya mawili yametumika mara 7 katika Aya Zifuatazo;
NENO سنة limetajika katika Aya 7 Zifuatazo
1- (يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَنْ يُعَمَّرَ) [البقرة: 96].
2-(قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ أَرْبَعِينَ سَنَةً يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ) [المائدة: 26].
3-(وَإِنَّ يَوْمًا عِنْدَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ) [الحج: 47].
4-(وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا) [العنكبوت: 14].
5-(يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ) [السجدة: 5].
6-(حَتَّى إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ) [الأحقاف: 15].
7-(تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ) [المعارج: 4].
Na Neno عَامٍ Limetajika katika Aya 7 Zifuatazo
1- (فَأَمَاتَهُ اللَّهُ مِئَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ) [البقرة: 259].
2- (قَالَ بَلْ لَبِثْتَ مِئَةَ عَامٍ) [البقرة: 259].
3- (إِنَّمَا النَّسِيءُ زِيَادَةٌ فِي الْكُفْرِ يُضَلُّ بِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُحِلُّونَهُ عَامًا) [التوبة:37].
4-(وَيُحَرِّمُونَهُ عَامًا لِيُوَاطِئُوا عِدَّةَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ) [التوبة:37].
5-(أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ) [التوبة:126].
6-(ثُمَّ يَأْتِي مِنْ بَعْدِ ذَلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ) [يوسف: 49].
7-(وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا) [العنكبوت: 14].
Mpangilio huu unaonyesha Kwamba Kuruani Ni Maneno yake Mwemyeezi Mungu kwani Binaadamu hana uwezo kama huu. Allahu Akbar.
MIUJIZA YA KUKARIRI KA MANENO NA AYA KIAJABU SANA KATIKA KURUANI
1/ Neno DUNIA (الدنيا) limekariri (limetumika) katika Kuruani mara 115 na Neno ( الآخرة) Pia Limekariri (Limetumika) katika Kuruani mara 115. Nimehakikisha na Kufanya utafifi kwa hiyo siwezi kutaja hizo Aya Zote hapa kwa ajili ya Nafasi katika Website. Nikitaja kila kitu maandishi yatakuwa marefu sana.
1/Jina MALAIKA (الملائكة) limekariri (limetumika) katika Kuruani mara 68 na Jina ( الشيطان) Pia Limekariri (Limetumika) katika Kuruani mara 68. Nimehakikisha na Kufanya utafifi kwa hiyo siwezi kutaja hizo Aya Zote hapa kwa ajili ya Nafasi katika Website. Nikitaja kila kitu maandishi yatakuwa marefu sana.
La kushangaza zaidi ni Majina yanayotokana na Malaika na Shetani Pia namba zilizokariri katika kuruani zinafanana. Angalia hapa chini:
Derivatives au MUSHTAQAATI zinazitokana na JINA AL-MALAIKA (الملائكة)
ملَك Jina MALAK Limekariri mara 10
ملَكاً Jina MALAKAN Limekariri mara 3
الملَكَين Jina MALAKAYNI Limekariri mara 2
ملائكته Jina MALAIKATUHU Limekariri mara 5
Jumla Ya Majina Yanayotokana na Jina Malaika ni 20
Sasa Tuchunguze Derivatives au MUSHTAQQAAT yanayotokana na Jina
(الشيطان)
شيطاناً Jina SHAYTWANAN Limekariri mara 2
الشياطين Jina Al-SHAYATWIIN Limekariri mara 17
شياطينهم Jina SHAYATWIYNIHIM Limakariri mara 1
Jumla Ya Majina Yanayotokana na Jina SHAYTWAN ni 20
Angalia Muujiza mbele ya macho yako!!!
Allahu Akbar. Malaika Na Mpinzani wake Shetani majina haya mawili yametumika na kukariri katika kuruani sawa sawa kihesabu!!! na hata MUSHTAQAATI au Derivatives zake pia sawa sawa Kihesabu!!!! Allah Akbar. Allahu Akbar. Huu sio Muujiza Mdogo.
Hii inaonyesha Ukubwa wa Mwenyeezi Mungu. Angalia Kuruani Ilivyopangwa. Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akatuambia kwamba Watu wote duniani wangekusanyika Pamoja Na Majini wote na kusaidiana katika Kuandaa Kitabu mfano wa kuruani Tusingeliweza. Na hata Sura au Aya tusingeliweza Pia, Sasa tuanona Ushahidi Mbele ya macho yetu. Huu sio muujiza mdogo. Angalia Namba zinavyozungumza. Hili ni tonye tu katika Elimu yake Mwenyeezi Mungu. Tonye katika Bahari. Allahu Akbar.
KUKARIRI KWA IBARA (PHRASE). KUPENDA NA KUCHUKIA KWA MWENYEEZI MUNGU
KUKARIRI KWA IBARA الله يحبُّ YAANI MWENYEEZI MUNGU ANAPENDA NA الله لا يحبُّ. YAANI MWENYEEZI MUNGU HAPENDI
Ibara الله يحبُّ Yaani Kupenda Imekariri (Imetumika) katika Kuruani yote Mara 16 na Pia Ibara – الله لا يحبُّ. Yaani Mwenyeezi Mungu Anachukia Imekariri (Imetumika) Katika Kuruani Mara 16 Pia!!! Angalia Mizani Ya Maneno. Angalia Muujiza Unaojitokeza mbele ya Macho Yako).
Hapa Chini Nimekusanya Aya Zote Za Kupenda na Kuchukia Kwa Mwenyeezi Mungu. Sura Na Namba Za Aya Pia Nimeashiria.
KUPENDA KWA MWENYEEZI MUNGU الله يحبُّ
1- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [البقرة: 195].
2- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ) [البقرة: 222].
3- (فَإِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ) [آل عمران: 76].
4- (وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [آل عمران: 134].
5- (وَاللَّهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ) [آل عمران: 146].
6- (وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [آل عمران: 148].
7- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ) [آل عمران: 159].
8- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [المائدة: 13].
9- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ) [المائدة: 42].
10- (وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) [المائدة: 93].
11- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ) [التوبة: 4].
12- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ) [التوبة: 7].
13- (وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ) [التوبة: 108].
14- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ) [الحجرات: 9].
15- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ) [الممتحنة: 8].
16- (إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُمْ بُنْيَانٌ مَرْصُوصٌ) [الصف: 4].
Na Hivyo Hivyo Kuchukia Kwa Mwenyeezi Mungu Zipo Aya 16 Pia. Hii kweli inashangaza. Utafikiri Mwenyeezi Mungu alikuwa anapima Kwa kutumia Mizani.
KUCHUKIA KWA MWENYEEZI MUNGU الله لا يحبُّ.
1- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ) [البقرة: 190].
2- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ) [البقرة: 205].
3- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ) [البقرة: 276].
4- (فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ) [آل عمران: 32].
5- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ) [آل عمران: 57].
6- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ) [آل عمران: 140].
7- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ مَنْ كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا) [النساء: 36].
8- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ مَنْ كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا) [النساء: 107].
9- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ) [المائدة: 64].
10- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ) [المائدة: 87].
11- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ) [الأنفال: 58].
12- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ) [الحج: 38].
13- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ) [القصص: 76].
14- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ) [القصص: 77].
15- (إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ) [لقمان: 18].
16- (وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ)[الحديد: 23].
Je Uanona Maajabu Ya Mpangilio wa Maandishi ya Kuruani? Huu ni uthibitisho kwamba haya siyo maneno ya binaadamu. Inashangaza sana. Allahu Akbar. Kuna Mengi ya kushangaza kwani haya tuliyoyataja ni Tonye katika Bahari. Allahu Akbar.
Tumezungumzia Pia katika Website hii kuhusu Neno YAWM Yaani Siku, Neno SHAHR yaani Mwezi, Neno QAMAR yaani Moon na Neno AYAM yaani Masiku. Maneno haya pia yamekariri kiajabu sana. Kwani
Neno YAWN limekariri katika kuruani tukufu mara 365 yaani sawa sawa na idadi ya masiku katika Mwaka
Neno SHAHR limekariri katika kurruani mara 12 yaani sawa sawa na Idadi ya Miezi katika Mwaka.
Neno QAMAR limekariri katika kuruani mara 30 yaani sawa sawa na idadi ya masiku ya Mwezi.
Neno AYAM limekariri mara 27 ambayo ni idadi ya Masiku ya Mwezi unapozunguka Ardhi mara moja.
Siku zilizopita nilizungumzia katika Video Zangu habari hizi kwa urefu katika Mlango wa “Sauti Za Mwandalizi”
Kuruani Ni Muujiza Mkubwa Sana ambayo ni zawadi Kubwa tuliyopewa na Mwenyeezi Mungu. Inatubidi tuisome na Tumshukuru Mungu kwa neema hii. Ni Muujiza katika Mikono yetu. Allahu Akbar. Allahu Akbar.
MIZANI KATIKA AYA ZA KURUANI
SAINI YA MWENYEEZI MUNGU KATIKA KURUANI
Saini Ya Mwenyeezi Mungu ni Lugha Ya Mwenyeezi Mungu katika Kuruani Tukufu. Ni Lugha Ya Ajabu Kubwa. Kuruani ni Hotuba Yake Mwenyeezi Mungu kwetu sisi Bonaadamu na Majini. Mpangilio wa Sura, Aya Na Maneno ni wa hali ya Juu sana. Na hauko sawa na vitabu vinginevyo. Na hii ndoyo Saini yake Mwenyeezi Mungu. Saini hii inathibitisha kwamba Kuruani Hakuandika binaadamu.
SAINI YA KWANZA
Aya Ifuatayo inahusu mazungumzo baina ya Watu wachoyo. Walidhamiria kuvuna asubuhi mapema ili watu wasiwaone na wasiombwe lakini walipewa adhabu baada ya kukuta Shamba lao limeungua na walipoliona limeungua wakajua makosa waliyoyafanya na wakatubia. Kuanzia Aya namab 21 mpaka 32 ni Mazungumzo tu baina ya watu hao.
1/MPANGILIO WA KUSHANGAZA (Sura Ya Al-Qalam Namba 68.Aya Namba 21-32)
Kilugha Neno أَوْسَطُهُمْ asili yake ni وسط lina maana ya “KATIKATI” na katika Aya hii neno hili lina maana ya “WA KATI YAO” yaani MMOJA WAO kati ya hao marafiki. Ukichunguza mazungumzo haya utaona Muujiza Mwingine wa idadi ya maneno kabla Ya neno hili na baada ya neno hili. Kabla ya neno hili kuna idadi ya maneno 31 na baada ya neno hili kuna maneno 31 pia!!!
Na hii ndiyo saini ya Mwenyeezi Mungu. Kuruani inashangaza. Neno hili kihisabu lipo katikati ya mazungumzo baina ya marafiki hawa yaani Katika Aya Hizi kuanzia namba 21 mpaka 32. na neno hili lina maana ya “KATIKATI pia.
(فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ أَنِ اغْدُوا عَلَى حَرْثِكُمْ إِنْ كُنْتُمْ صَارِمِينَ فَانْطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ أَنْ لَا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُمْ مِسْكِينٌ وَغَدَوْا عَلَى حَرْدٍ قَادِرِينَ فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ قَالُوا يَوَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ عَسَى رَبُّنَا أَنْ يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِنْهَا إِنَّا إِلَى رَبِّنَا رَاغِبُونَ)
[القلم: 21-32].
TAFSIRI
21. Asubuhi wakaitana
22. Ya kwamba: “Nendeni mapema kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna (bila kuonekana na maskini).”
23. Basi walikwenda wakinong’onezana
24. Ya kuwa:”Leo maskini asingie humo mwenu”
25. Na wakenda asubuhi,bali wanadhani kuwa wanao uwezo wa kuzuia (maskini).
26. Basi walipoliona (limeungua vile walidhani kuwa silo) wakasema: “Bila shaka tumepotea, (Siko huku; silo shamba letu hili; tumepotea) ” ·
27.(Walipotazama zaidi wakayakinisha kuwa ndilo walisema).- “Bali tumenyimwa (mavuno yake).” .
28. Mbora wao akasema: “Je! Sikukuambieni(msitie nia mbaya ya kuwazuilia haki yao maskini? Sasa) rejeeni kwa Mola wenu, mtubie kwake.”
29.Wakasema: “Utukufu ni wa Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu. (Basi tusamehe Mola wetu).”
30. Basi wakakabiliana kulaumiana.
31. Wakasema: “Hasara yetu! Hakika tulikuwa tumeruka mipaka (ya Mwenyezi Mungu).”
32. “Asaa Mola wetu atatubadilishia (shamba) lililo bora kuliko hili; hakika sisi tunajipendekeza (sasa) kwa Mota wetu.”
SAINI YA PILI
kisa hiki cha pili kinahusiana na aliyetajirishwa na Mwenyeezi Mungu na akakufuru neema hizo alipojibizana na Mwenziwe kwa kutamba na kujisifu kwa kuwa na mali na wafuasi wengi na kama katika kisa kilichopita mali yake yote iliharibika na kuangamizwa. Baada ya hapo akajuta sana na kutamani asingesema aliyoyasema. Aya zifuatazo mbili zinaelezea Mabustani Hayo Mawili aliyoruzukiwa huyo Mtu.
2/MPANGILIO WA KUSHANGAZA (Sura Ya Al-Kahf Namba 18.Aya Namba 32-33)
Ukichunguza Aya zifuatazo utaona Neno بَيْنَهُمَا lipo katikati baina ya maneno 12 kabla ya Neno Hili na Maneno 12 baada ya neno hili.Yaani ukihesabu neno hili utaliona lipo katikati .Na Ajabu ni kwamba neno hili kilugha lina maana ya “KATI YA”. Neno بَيْنَهُمَا asili yake neno بين maana yake “BETWEEN” Hesabu na Lugha zinakwenda sambamba
(وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلًا رَجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا * كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آَتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِمْ مِنْهُ شَيْئًا وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا)
[الكهف: 32-33]
TAFSIRI
32.Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimfanyia (tulimpa) mabustani mawili ya mizabibu, na tukaizungushia mitende, na pia katikati yake tukatia miti ya nafaka (nyingine).
33.Haya mabustani mawili yote yalijaa matunda yake wala hayakupunguza chochote (katika uzazi wake); na ndani yake tukapitisha mito
MPANGILIO WA KUSHANGAZA WA SURA YA AL-MASAD (LAHAB) AMBAO HATA SUPERCOMPUTER HAIWEZI KUPANGA MPANGILIO KAMA HUU.
Sura Namba 111 Aya 1-5
سُوۡرَةُ لهب
المَسَد
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)
TAFSIRI
I-Kutaangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia. 2.Hayatamfaa mali yake wala alivyovichuma. 3.(Atakapokufa) atauingia Moto wenye mwako (mkubwa kabisa) 4.Na mkewe, mchukuzi wa kuni (za fitina),(fattani, anayefitinisha watu wasiingie katika dini; atauingia naye Moto huo) · 5.(Kama kwamba) shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayochukulia kuni za fitina hizo).
SABABU YA KUSHUKA SURA HII
Mwanzoni mwa kupewa Utume bwana wetu Muhammad (s.a.w.) aliamrishwa awabashirie jamaa zake walio karibu naye kwa kizazi; akawakusanya akawabashiria na kuwakhofisha na adhabu ya Akhera, Abu Lahab, Ami yake, akakasirika, akamwambia ‘Mwana kuangamia wee! Ndilo ulilotwitia hili?’ Ndiyo sababu ya kushuka sura hii kuapizwa Abu-Lahab na mke wake, Ummu-jamil, aliyekuwa akijipinda sana katika kumuudhi Mtume, na kuwashakiza makafiri wamuue na kufanya kila aliwezalo katika kuizuilia dini isifuatwe. “Yana kuangamia mikono miwili ya Abu-Lahab!” ni maapizo ya kuapizwa Abu-lahabi aangamie yeye, badala ya Mtume (s.a.w.). Na kwa vile Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuapiza, imekuwa hapana shaka maapizo hayo ni yenye kumpata, na kwa hivyo Mwenyezi Mungu anatupa habari kuwa “amekwishaang:amia.” Huyu mke wa Abu-Lahab alikuwa fattani (sakubimbi). Kazi yake kuchukua maneno ya huku akipeleka huku kwa kutaka kutia fitina na fisadi. Na mtu namna hii Waarabu humshabihisha na “mchukuzi wa kuni.” Na desturi, mchukuzi wa kuni huwa na “kamba” katika shingo yake ya kufungia hizo kuni zake, na kuni ndizo zinazowasha moto. Na huyu mwanamke akiwasha moto wa kuwazuilia watu wasisilimu na kuwatoa waliosilimu
NIDHAMU KATIKA UTAFITI
Kabla Ya Kuanza kuelezea Utafiti huu ningependelea kelezea kwamba Herufi za Lugha Ya Kiarabu na Nyinginezo ambazo asili yake zinazotokana na Phoenicians kama vile Grec, Gothic, Copte, Cyrillic, Hebrew, na Arameen zote hizi zilikuwa zikiwakilishwa na Namba katika wakati huo. Kwani kulikuwa hakuna Namba tunazotumia hivi sasa na kwa hiyo lugha hizi walitumia herufi katika hesabu zao za kila siku.Waarabu Walikuwa wakitumia Herufi za Abgad katika kuwakilisha Namba(Before the Hindu–Arabic numeral system, the abjad as numbers were used for all mathematical purposes) Mungu Akipenda Katika Utafiti wetu tutageuza herufi za maneno yafuatayo katika Namba zilizokuwa zikiwakilishwa na Herufi wakati huo na Tutachunguza Namba za Odd na Even. (Number za Odd (Witr) ni Namba isiyogawanyika kwa mbili. Na Namba Even (Shafiii) Ni namba ambayo unaweza kugawa kwa mbili. Kwa mfano namba 3 huwezi kugawa kwa mbili bila mabaki kwa hiyo ni namba Odd. Na Namba 4 unaweza kugawa kwa mbili bila mabaki kwa hiyo ni Even).
MAAJABU MAKUBWA YASIYO NA MWISHO
Tukifanya Utafiti katika Aya 5 za Sura Ya Al-Masad Utakuta Mpangilio wa hali ya Juu sana na Wa Kushangaza. Utafiti Huu unathibitisha kwamba Kuruani Ni maneno ya Mwenyeezi Mungu. Na Hakuna Kiumbe chochote Katika Binaadamu au Majini ambao hata wakisaidiana pamoja haiwezekani kuandika mfano wa Aya moja Ya Kuruani. Allahu Akbar.
Hebu tufafanue Aya Za Sura Hii.
تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)
1/Ukikusanya Maneno ya ODD kama vile Neno la kwanza, la tatu, la tano na kuendelea katika Aya 5 hapa Juu na kisha ukageuza Herufi Zake katika Namba zilizotumika wakati huo utapata kama ifuatavyo. Jumla Ya Herufi za Odd katika maneno yote Ya Sura Ya Al-Masad Ni 3049 Na Jumla Ya Herufi za Odd katika maneno Odd Peke yake Ya Sura Ya Al-Masad Ni 3049 (Yaani bila kuhesabu Maneno EVEN)
2/Ukikusanya Maneno ya EVEN kama vile Neno la pili, la Nne, la Sita na kuendelea katika Aya 5 hapa Juu na kisha ukageuza Herufi Zake katika Namba zilizotumika wakati huo utapata kama ifuatavyo. Jumla Ya Herufi za Even katika maneno yote Ya Sura Ya Al-Masad Ni 2382 Na Jumla Ya Herufi za Even katika maneno Even Peke Yake Ya Sura Ya Al-Masad Ni 2382 (Yaani bila kuhesabu Maneno ODD)
3/Ukikusanya Herufi za Odd katika Maneno Even kisha Ukageuza Herufi zake katika Namba zilizotumika wakati huo utapata kama ifuatavyo. Jumla Ya Herufi za Odd katika Maneno Even Ni 916
4/Ukikusanya Herufi za Even katika maneno Odd kisha Ukageuza Herufi zake katika Namba zilizotumika wakati huo utapata kama ifuatavyo. Jumla Ya Herufi za Even katika Maneno Odd Ni 916
Je Unaona Mpangilio wa Herufi unavyoshangaza? Tunaona Vizuri kwa sababu tumegeuza Herufi hizi katika namba. Utafikiri Herufi na Maneno yamepimwa katika Mezani. Allahu Akbar.
Tuendelee na Muujiza wa Kushangaza kwani bado kumaliza. Allahu Akbar.
ODD NUMBER IMETUMIKA KIAJABU SANA
1/Sura Namba 111 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2 bila ya mabaki. (Namba Ya ODD inagawanyika lakini kutakuwa na mabaki na namba EVEN ni ile yenye kugawanyika kwa 2 bila ya kubaki chochote. Kwa hiyo ODD zote hapa chini ni mfano huu)
2/Aya za Sura Hii ni 5 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
3/Jumla Ya Maneno katika Sura ni 23 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
4/Jumla Ya Herufi katika Sura Ni 81 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
5/Aya Ya Kwanza ina Herufi 15 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
6/Aya Ya Pili ina Herufi 19 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
7/Aya Ya Tatu ina Herufi 15 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
8/Aya Ya Nne Ina Herufi 17 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
9/Aya Ya 5 Ina Herufi 15 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
10/Jina A-lMasad Lina Herufi 5 Na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
11/Jina la Sura المَسَد “Al-Masad” Ukiligeuza katika Namba zilizokuwa zikiwakilishwa na Herufi wakati huo utapata Jumla Ya Herufi Zake ni Namba 135 ambayo ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
12/Neno La Katikati katika Sura Hii ni سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) Kuna maneno 11 Kabla ya Neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) na Namba hii ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
13/Na Kuna Maneno 11 Baada ya neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) Na Namba hii 11 ni ODD kwani haigawanyiki kwa 2
Angalia Odd Numbers ilivyokariri kiajabu sana tena sana. Allahu Akbar.
Sasa Tuangalie Maneno na herufi Katika Kila Upande wa Neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla)
تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)
Tumesema kwamba Katika Sura hii kuna maneno 23. Neno La katikati ni سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) na limezungukwa na Maneno 11 kushoto na 11 kulia yake.
Aya Mbili kabla ya Neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) zinazungumzia Maneno ya Mwenyeezi Mungu Kumkemea Abu Lahab na Baada ya Neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) Ni Malipo ya Moto atakayolipwa na habari inayohusu Sifa Mbaya Ya Mke wake.
Haya Maneno 11 yamegawanywa na Mwenyeezi Mungu kiajabu sana kama ifuatavyo:
Herufi 11 za ODD zipo kabla ya neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) katika Maneno 6 yaliyo Odd
Herufi 11 za ODD zipo Baada ya neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) katika Maneno 6 Yaliyo Odd
Maneno 5 ya EVEN yapo Kabla ya neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla)
Maneno 5 ya EVEN yapo Baada ya neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla)
Angalia Huu Mpangilio wa Herufi unavyoshangaza. Neno سَيَصۡلَىٰ (Sayasla) katika Sura Hii lipo katikati na kila upande Herufi zimehesabiwa sawa sawa yaani ODD na EVEN.
Wanaodai kwamba Mtume (Sala Na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) ndiye aliandika Kuruani Hii watashangaa kuona Vipimo kama hivi. Nani anaweza kuleta Ujumbe kisha kupima maneno kama tulivyoona katika Utafiti Huu. Hakuna Mwingine isipokuwa Mwenyeezi Mungu Peke Yake. Allahu Akbar.
Hata Computer inayojulikana kama SuperComputer haiwezi Kufanya Haya. Haiwezekani kabisa, Iwapo ingewezekana basi mbona mpaka leo baada ya Karne 1400 ya kushuka Kuruani haijatokea Mtu kuandika Angalau Aya Moja Mfano wa Kuruani. Allahu Akbar.
Angalieni Muujiza ambao Unatutoa Mapovu Vinywani. Hata Kuuelewa tunahangaika wacha kuandika mfano kama huu. Kwa Kweli Mwenyeezi Mungu ni Mkubwa Sana na Elimu yake kubwa sana. (ALIYM)
MAAJABU YA NENO تَنزِيلاً۬ KATIKA KURUANI TUKUFU
Neno تَنزِيلاً۬ limeshuka katika kuruani katika Aya Nne tu zifuatazo
Sura Namba 17 Al-Israa Aya Namba 106
وَقُرۡءَانً۬ا فَرَقۡنَـٰهُ لِتَقۡرَأَهُ ۥ عَلَى ٱلنَّاسِ عَلَىٰ مُكۡثٍ۬ وَنَزَّلۡنَـٰهُ تَنزِيلاً۬ (١٠٦)
TAFSIRI
Na Qurani tumeigawanya sehemu mbalimbali (kwa kuiteremsha kidogo kidogo) ili uwasomee watu kwa kituo; na tumeiteremsha kidogo kidogo (iwe wepesi kuhifadhika).
SHEREHE
Herufi Za Aya Ni 44 Aya Ya Kwanza Neno تَنزِيلاً۬ limewekwa mwisho wa Aya na ni neno la 9
Sura Namba 20 Twaha Aya Namba 4
تَنزِيلاً۬ مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَـٰوَٲتِ ٱلۡعُلَى (٤)
TAFSIRI
4.Kiteremsho kinachotoka kwa Yule Aliyeumba ardhi na mbingu (hizi) zilizoinuka juu.
SHEREHE
Herufi Za Aya Ni 29 Aya Ya Pili Neno تَنزِيلاً۬ limewekwa mwanzo wa Aya na ni neno la 1
Sura Namba 25 Al-Furqan Aya Namba 25
وَيَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلسَّمَآءُ بِٱلۡغَمَـٰمِ وَنُزِّلَ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ تَنزِيلاً (٢٥)
TAFSIRI
37.Na (wakumbushe) siku zitakapopasuka mbinGU zilete chungu ya mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi.
SHEREHE
Herufi Za Aya ni 37 Aya Ya Tatu Neno تَنزِيلاً۬ limewekwa mwisho wa Aya na ni neno la 7
Sura Namba 76 Al-Insan Aya Namba 23
إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ تَنزِيلاً۬ (٢٣)
TAFSIRI
23.Hakika sisi tumekuteremshia Qurani sehemu sehemu (kidogo kidogo)
SHEREHE
Herufi Za Aya Ni 28 Aya Ya Nne Neno تَنزِيلاً۬ limewekwa mwisho wa Aya na ni neno la 6
MATOKEA WA UTAFITI
Ukijumlisha Namba za Sura Utapata 138 kama ifuatavyo 17 + 20 + 25 + 76=138 Na Ukijumlisha Herufi Za Aya Hizi utapata namba 138 Pia kama ifuatavyo: 44 + 29 + 37 + 28=138
Sasa Tuangalie Positions (Sehemu)za Neno تَنزِيلاً۬ katika Aya Hizi Nne.
Ukiangalia Namba hizi za Positions (Sehemu) utaziona ni 9, 1,7, na 6 Jumla ya Namba hizi ni 23 ( 9 + 1 + 7 + 6=23) na 23 ni miaka ya WAHYI yaani miaka ya kushuka kwa Kuruani kwa Mtume (Sala na Amani za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) na WAHYI maana yake ni تَنزِيلاً۬ TANZILA yaani kushuka kwa kuruani.
Na pia ukizipanga namba hizi kuanzia chini kwenda juu na kuzifanya namba moja itakuwa ni 6719 au Namba mbili itakuwa ni 67 na 19 . Inashangaza kugundua pia kwamba namba 67 katika Elimu ya Hesabu ni Prime Number ya 19
Je unaona Mpangilio wa kiajabu?
Kwanza Jumla Ya Namba za Sura na herufi zinafanana yaani 138
Pili, Na tulipochunguza Positions za neno تَنزِيلاً۬ tukapata namba 6, 7, 1,9 Na tukizijumlisha hizi namba tunapata 23 ambayo ni miaka ya kushuka kuruani kwa Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)
Tatu, Na tulipoziunga namba 6 na 7 tukapata 67 na 1 na 9 tunapata 19 ambayo inashangaza pia kuona kwamba namba 67 ni Prime Number ya 19 katika Prime Numbers.
Allahu Akbar. Kuruani imepangwa kwa mpangilio wa hali ya juu sana. Allahu Akbar. Hakuna awezaye katika viumbe wote na hata wakishirikiana pamoja kuandika kitabu kama hiki. Hii inathibitisha kwamba Hii Kuruani ni yake Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Allahu Akbar.