SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Mtume Katika Biblia

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

KUTAJIKA KWA MTUME MOHAMAD (S.A.W.), NABII MUSA NA ISA KATIKA BIBLIA- NA PIA UTAFITI KWA NJIA YA HESABU

MUUJIZA WA KUTAJIKA KWA MITUME WATATU “NABII MUSA, ISA NA MOHAMAD (S.A.W.) KATIKA AGANO LA KALE. CHAPTER NAMBA 33 VERSE NAMAB 2

Katika Kitabu Cha Deutoronomy  Chapter  33 Verse 2

Maneno Ya Aya Hii kwa Lugha Ya Asili ya Kiyahudi  (Hebrew)

בוַיֹּאמַ֗ר יְהֹוָ֞ה מִסִּינַ֥י בָּא֙ וְזָרַ֤ח מִשֵּׂעִיר֙ לָ֔מוֹ הוֹפִ֨יעַ֙ מֵהַ֣ר פָּארָ֔ן וְאָתָ֖ה

:מֵרִֽבְבֹ֣ת קֹ֑דֶשׁ מִֽימִינ֕וֹ אֵ֥שׁ דָּ֖ת (כתיב אשדת) לָֽמוֹ

TAFSIRI

2 Akasema,Bwana alitoka Sinai,Akawaondokea kutoka Seiri;Aliangaza katika kilima cha Parani,Akaja Meribath-Kadeshi.Upande wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.

2. He said: “The Lord came from Sinai and shone forth from Seir to them; He appeared from Mount Paran and came with some of the holy myriads; from His right hand was a fiery Law for them

SHEREHE

Biblia Inasema kwamba hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.

1.Katika maneno aliyosema inatubainishia waziwazi kwamba Mwenyeezi Mungu alimpa Ujumbe Nabii Musa katika Mlima wa Sinai. Na ndiyo sehemu Mwenyeezi Mungu alipotokea na Kuzungumza na Nabii Musa

2.Mwenyeezi Mungu Akampa Ujumbe Nabii Isa katika sehemu Ya Seiri ambayo Alizaliwa Nabii Isa. Seiri Ni Milima Kaskazini na Kusini ya Bahari ya “Dead Sea” Milima Imeenea kupitia Jerusalem na Bethlehem, alipozaliwa nabii Isa.

(Seir is a reference to Jesus (pbuh).It is usually associated with the chain of mountains West and South of the Dead Sea extending through Jerusalem, and Bethlehem, the birthplace of Jesus (pbuh). It was later extended to include the mountains on the East side as well (Dictionary of the Bible, John L. McKenzie, S.J., p. 783). However, Seir is also identified with the Northern border of the tribal territory of Judah and usually with Saris near Kesla (Chesalon), barely nine miles West of these two cities (The Eerdmans Bible Dictionary, by Allen C. Myers, pp. 921-922, and The Interpreter’s Dictionary of the Bible, V4, p. 262) Prophet Moses (pbuh) never in his lifetime entered Palestine, and thus, this could not be a reference to him).

3.Na Neno Aliangaza katika Kilima Cha Parani ni Mecca  katika Pango la Hiraa. Hapo Ndipo Jibril alipomkabili Mtume Mohamed (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Imfikie).

Paran is a reference to the city of Makkah in the Arabian Peninsula. The wilderness of Paran is where Abraham’s wife Hagar and his eldest son Ishmael settled (Genesis 21:21) in the Arabian desert, specifically, Makkah. Makkah is, of course, the capital of Islam in Arabia and the birthplace of Mohammed (pbuh). Mount Paran is the chain of mountains in that same region which the Arabs call the “Sarawat mountains”. Muhammad (pbuh) received his first revelation in the cave of “Hira’a” located in these mountains (see Fig. 9). Jesus never in his life traveled to Paran. Mohammed, however, was born there. He became the prophet of Islam there. And it was the capital of the Islamic religion in that day and this. No prophet of the Bible ever came from the Arabian city of Paran (Makkah). Prophet Muhammad (pbuh) is the only prophet of God who has ever fulfilled this prophesy.

Kwa hiyo Maneno Ya Nabii Musa hapa Juu anasema kwamba Mwenyeezi Mungu alitokea mara ya Kwanza SINAI, Mara Ya Pili BETHLEHEM  na Mara ya Tatu  MECCA. Yaani Kwanza alimpa Ujumbe Nabii Musa, Nabii Isa na Kisha Nabii Mohamad..

Maneno haya yapo wazi na yamebaki hivyo hivyo katika Biblia. Ni ushahidi ambao huwezi kuugeuza. 

Na Ili tupate Uthibitisho zaidi kama Mtume Mohamed  ni wa kweli na ndiye aliyepewa Ujumbe Mecca (Yaani katika Mlima wa Paran) tutafanya Hesabu.

MUUJIZA WA HESABU AMBAO UNATHIBITISHA KWAMBA MTUME KWA JINA “AHMAD” AMETAJIKA KATIKA DEUTORONOMY 18:18

Sasa Tuchambue Maneno Ya Aya Hii kwa Lugha Ya Asili ya Kiyahudi (Hebrew) kwa njia ya Hesabu. Lengo letu ni Kutafuta Jina La Mtume. Yaani “Ahmad” Na tutaendelea katika Kutafuta Jina la Mtume “Mohamad” katika sehemu nyingine ya Biblia. Katika Kuruani Majina Yote Mawili yametajika. AHMAD NA MOHAMAD kwa hiyo ni majina yake Mtume na tusibabaike.

Kwa Mfano Katika Sura Ya Mohamad Namba 47 Aya Namba 2 kumetajwa jina la Mohamad

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ۬ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّہِمۡ‌ۙ كَفَّرَ عَنۡہُمۡ سَيِّـَٔاتِہِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ (٢)

Na Jina La Ahmad katika Sura Ya Al-Saff Namba 61  Aya Namba 6

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَـٰبَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ إِنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقً۬ا لِّمَا بَيۡنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَٮٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٍ۬ يَأۡتِى مِنۢ بَعۡدِى ٱسۡمُهُ ۥۤ أَحۡمَدُ‌ۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَـٰتِ قَالُواْ هَـٰذَا سِحۡرٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٦)

Sasa tutafute Jina La AHMAD katika Bibilia. Katika Kitabu Cha Deutoronomy Chapter 18 Verse 18 Maneno Ya Aya Hii kwa Lugha Ya Asili ya Kiyahudi (Hebrew). 

יחנָבִ֨יא אָקִ֥ים לָהֶ֛ם מִקֶּ֥רֶב אֲחֵיהֶ֖ם כָּמ֑וֹךָ וְנָֽתַתִּ֤י דְבָרַי֙ בְּפִ֔יו וְדִבֶּ֣ר

: אֲלֵיהֶ֔ם אֵ֖ת כָּל־אֲשֶׁ֥ר אֲצַוֶּֽנּוּ

TAFSIRI

18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu

18. I will set up a prophet for them from among their brothers like you, and I will put My words into his mouth, and he will speak to them all that I command him.

Nilizungumzia Sherehe Ya Verse  Hii kwa urefu katika Website Hii Katika Mlango wa  “Mengineyo Mbalimbali” kwa Hiyo Sitarudia tena Maelezo hayo kwa urefu. Kwa kifupi Kuna Uthibitisho kamili kwamba Aliyekusudiwa hapa ni Mtume Mohamed. Kwani Ndiyo pekee anayefanana na nabii Musa kwa Sifa Zote. Na ndiye pekee aliyepewa maneno ya Kwanza ya Kuruani na Jibril alipokuwa katika Pango la HIRAA huko Mecca.  Leo Hii Mungu akipenda ningependelea Kuchambua maneno haya Kwa kutumia Hesabu ili kutafuta Jina La “AHMAD”  ili kuthibitisha Kwamba ndiye aliyekusudiwa. Hesabu Zinazungumza na kwa hiyo tutatumia Hesabu ili tupate ushahidi kikamilifu. Kwamba ni Yeye na siyo Nabii Isa au Mwingine. Katika Sherehe niliyoieleza hapo awali nilitoa ushahidi wa kutosha lakini Alhamdulilahi Leo Tutafunga mlango huu kwa kutoa ushahidi Mwingine mkubwa wa Hesabu.

Tukichunguza Maneno ya Kiyahudi (Hebrew) Hapa Juu utaona Herufi za Jina Ahmad kama zifuatazo:

א  Herufi Ya 5 ni  A  (Alif)

חֵ  Herufi ya 17 ni H  (Haa)

מ֑ Herufi ya 22 ni M  (Mim)

דִ Herufi ya 39 ni D  (Dal)

Herufi hizi Nne ndizo jinajenga jina  “AHMAD”

  אחֵמ֑דִ   Ukiunga herufi hizi Nne utapata Jina “AHMAD”

Sasa Muujiza wa kushangaza ni kwamba Utafiti huu unahesabu Herufi ya kwanza ni Ya 5, Kwa nini hatukuchukua Herufi Ya Kwanza ile ya 4 kwani pia ni  Alif yaani pia ni herufi  “A”  

Tumeona kwamba herufi hizi nne zipo katika sehemu (positions) zifuatazo 5, 17, 22, 39

Hesabu zinatuambia kwamba  5 + 17=22  na 22 + 17=39

Tunapata namba (Positions) 22 na 39 kwa kujumlisha namba hizi.

kwa hiyo hatuwezi kuchukua Herufi nyinginezo zilizofanana na hizi nne katika maneno ya Biblia hapa juu. Ili kupata muiano mzuri huu inabidi tuchague Herufi hizi katika sehemu (Positions) hizi tu. Yaani 5, 17, 22 na 39

Jumla ya Herufi za Lugha ya Kiyahudi ni 22 na ukizihesabu kuanzia ya kwanza mpaka mwisho na ukazipa namba yaani 1 mpaka 22 na utapata thamani ya kila herufi. Kwa hiyo  tukichunguza  Herufi za jina Ahmad utapata kama ifuatavyo:

א Herufi Ya 5 ni A (Alif) – Thamani yake ni  1

חֵ Herufi ya 17 ni H (Haa)- Thamani yake ni 8

מ֑ Herufi ya 22 ni M (Mim)- Thamani Yake ni 13

דִ Herufi ya 39 ni D (Dal)- Thamani yake ni  4

Tufanye Hesabu  Multiplication Baina ya Positions na Values za Kila herufi

(5 X 1) + (17 x 8) + (22 x13) + (39 x 4)=

5 + 136 + 286 + 156= 583.

Namba Hii 583  inashangaza kwani  ukihesabu herufi Zote Zilizopo katika Deutoronomy Chapter 18 Verse 18  na ukapachika Values. Kutoka katika orodha ya Herufi  1 mpaka 22 ya Herufi za Lugha Ya Hebrew (Kiyahudi) nilizozielezea Hapa Chini  Na kisha Ukizijumlisha utapata Jumla ni 583 sawa na Values za Jina la “AHMAD” kama tulivyoona. 

א‎ Alef = A = 1   / ב‎ Bet = B=2   / ג‎ Gimel = G=3‎   / ד‎ Dalet = D=4 ‎  / ה‎ He =H= 5   /. ו‎ Waw/Vav = O/W/U=6  / ז‎ Zayin = Z=7   / ח‎ Chet =H”= 8  / ט‎ Tet = T”=9   / י Yod = e /I /Y=10   / כ / ך kaf =K=11  / ל‎ Lamed =L=12   / מ‎/ם‎ Mem =M=13   / נ / ן‎ Nun =N=14  / ס Samech =S=15  / ע Ayin =Ain=16  / פ / ף‎ Pe =F=17  / צ‎ / ץ‎ Tsadik =S”=18  / ק‎ Qof =Q=19  / ר‎ Resh =R=20  / ש‎ Shin =SH=21  / ת‎ Tav =T= 22

Yaani Huu ni Uthibitisho kwamba Jina La Mtume Mohamed katika Aya Hii tuliyoitaja ndilo lililokusudiwa katika Verse hii ya Biblia. 

Thamani ya herufi zote za Verse namba 18 kutoka Deutoronomy  Chapter  18 ni 583 na namba hii inalingana na Herufi Nne tu ambazo tumezi- Multiply na Positions Zake. Herufi hizo nimezikusanya hapa chini katika picha ifuatayo:

Hii ni Jibu kwa hao wanaomkataa Mtume Mohamed. Hesabu Hapa zinathibitisha hayo.  Mayahudi wanaelewa Elimu hii vizuri sana na wanaitambua. Wanatumia Hesabu katika Utafiti. Na walijua Kwamba Mtume Mohamed Atakuja. 

Hii ndiyo Hoja Inayowakabili. Wanaokataa Ukweli na hali wanaujua. Allahu Akbar. 

Kwa leo Naishia Hapa. Mwenyeezi Mungu akipenda Nitafanya Utafiti wa Mfano huu kwa Kutafuta Jina La pili  “Mohamed” (Sala na Amani Zake Mola Zimfikie) Na Nabii Musa Pia. 

UTAFITI HUU WA KWANZA ULIHUSU JINA LA “AHMAD” NA INSHAALAAH MWENYEEZI MUNGU AKIPENDA NITAENDELEA NA UTAFITI WA PILI UNAOHUSU JINA  “MOHAMED” NA UTAFITI WA TATU WA JINA LA  NABII MUSA. KWA KUTUMIA HESABU KAMA TULIVYOFANYA HAPA.

Herufi Za Agano La Kale Kitabu Cha Deutoronomy Chapter 18 Verse 18 Na Thamani Ya Herufi zake kwa Lugha Ya kiyahudi. Jumla ya Thamani hizo ni 583 na namba Hii inalingana na Jumla ya Thamani za Herufi za Jina La Mtume “AHMAD” ambazo tumezi Multiply na Positions zake katika Verse Hii Hii namba 2. Angalia Mlingano wa kushangaza. Hii inathibitisha kwamba Aliyekusudiwa katika Maneno haya ni Mtume (Sala na Amani yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Allahu Akbar.