SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Muhtasari/Utafiti-1

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

DUA ZENU NI MUHIMU SANA KATIKA MAENDELEO YA WEBSITE HII.

HABARI ZA SEPTEMBER KUANZIA TAREHE 01 MPAKA

30 MWAKA 2022

Alhamdulilah hivi karibuni neliongeza milango mingine ambayo sikutaja Muhtasari wake katika Mlango huu. Mwenyeezi Mungu akipenda nitaiongeza hivi karibuni  ili kuwapa wasomaji Ramani ya Website hii.

HABARI ZA AUGUST KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 31

MWAKA 2022

06/08/2022

Alhamdulilah leo nimefungua milango Mipya mitatu DARUBINI-2/KURUANI, DARUBINI-3/KURUANI  na KURUANI/NYONGEZA. Kuna  Habari Mbalimbali nimeongeza  humo. Mlango  wa Nyongeza unahusu mambo  nilyokwisha kuelezea katika milango  mingineyo bali  ni Nyongeza baada ya Utafiti Mpya.  Allahu Akbar.

HABARI ZA JULY KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 31 MWAKA 2022

31/07/2022

Alhamdulilah leo  nimefungua mlango mpya wa  DARUBINI-1/KURUANI. Mwenyeezi Mungu akipenda nitakuwa nikiweka humo Tafsiri ya Baadhi ya Aya za Kuruani Tukufu.

24/07/2022

Alhamdulilah leo nimefungua mlilango  miwili mipya  katika Website hii inayoitwa “HESABU/MSHANGAO-1” na “HESABU/MSHANGAO-2” Nimeelezea katika mlango wa Kwanza Sehemu nne za Kushangaza sana: Buibui, Iblis, Nyuki na Sura Zenye Jina na Sifa za Mtume. Mohamad.ﷺ na katika mlango wa pili  kuna Vipande vya kushangaza sana ambavyo ni Muujiza katika Miujiza isiyo na mwisho katika Kuruani Tukufu.

HABARI ZA JUNE KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 30 MWAKA 2022

26/06/2022

Alhamdulilah Leo Nimefungua mlango mpya wa “STRUCTURE/KURUANI”  ambao Utakusanya Mishangao Mbalimbali. Ni Mambo yanayoshangaza au Kwa lugha nzuri ni Miujiza Midogo Midogo iliyopo miongoni mwa Miujiza Mikubwa katika Kuruani Tukufu. Allahu Akbar.

19/06/2022

Alhamdulilah leo nimefungua mlango mpya wa Elimu ya Geology (Elimu ya Muundo wa Ardhi) na Nimeuita  “GEOLOGY/KURUANI” na Nimesherehesha baadhi Ya Aya za Kuruani kwa kadiri Mwenyeezi Mungu alivyojaalia. Natumai Utafiti huu utanifaa na pia wasomaji. Allahu Akbar. Namuomba Mweenyeezi Mungu atakabali kazi hii.

12/06/2022

Alhamdulilah Leo nimefungua mlango mpya wa “SAYANSI ZA DUNIA-4”  na nimeelezea habari za “NAFAKA” na Mwenyeezi Mungu akipenda nitaendelea kuelezea Habari za Milima na Muundo wa Ardhi. Allahu Akbar.

02/06/2022

Alhamdulilah. Leo nimeoneza Mlango Mpya wa TIBA/KURUANI ambao nitaorodhesha Aya Za Kuruani Tukufu Mbalimbali za Kujitibu na Matatizo ya Kimaisha. Kwa njia safi unasoma Aya hizi na kumomba Mwenyeezi Mungu mahitaji yako.

Na Pia Nimefungua Mlango mwingine  wa   “BLOG”  ambayo nitaorodhesha habari mbalimbali. Ili usome habari hizo tafadhali bonyeza  “READ  MORE”  au “KICHWA CHA HABARI” cha  Topic  yeyote uitakayo. Ukifanya hivyo utaweza kuisoma habari hiyo. Na ukitaka kuchagua Habari nyingine basi itabidi  Ubonyeze Tena  Jina la Mlango  “BLOG” na kisha uchague Topic yeyote nyingine uitakayo. Alhamdulilah

HABARI ZA MAY KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 31 MWAKA 2022

28/05/2022

Alhamdulilah leo  nimefungua Mlango  Mpya wa  “MIUJIZA YA KURUANI-9” . Nimeelezea humo Miujiza Miwili. Wa kwanza ni Mpangilio wa maneno  Na hesabu zake na wa Pili ni  “Mfumo  wa DNA katika Kuruani. Allahu Akbar. Namuomba Mwenyeezi Mungu atakabali  Utafiti Huu.

22/05/2022

Alhamdulilah Leo nimefanya Nyongeza ya Tafsiri ya Aya Namba 3 kutoka katika  Sura ya Alwaqia namba 56. katika mlango wa “LINGUISTICS/KURUANI” 

21/05/2022

Alamdulilah Leo nimeelezea Muujiza mkubwa wa Chromosomes za Binaadamu kutoka katika Aya zinazotaja Jina  “Al-Insan”  Yaani “Binaadamu” katika Mlango wa  “MIUJIZA YA KURUANI-7”  Allahu Akbar.

20/05/2022

Alhamdulilah Leo nimefanya  Nyongeza ya Muujiza wa Aya inayohusiana na Nyuki katika mlango  wa  “LINGUISTICS/KURUANI” 

14/05/2022

Alhamdulilah Leo katika Mlango wa “Miujza Ya Kuruani-7”  nimezungumzia Muujiza unaohusiana na  Aya namba 23, Sura ya Qaf. na pia Ningependelea kuwajuulisha kwamba wiki iliyopita nilifungua milango miwili katika Website hii. 

Mlango  Wa Kwanza ni  “MASUALA NA MAJIBU”  na wa pili ni REPRODUCTIVE SYSTEM”

Na pia niliongeza Video za Mwanachuoni Wa hapo zamani aliyekuwa Mashuhuri. Sheikh Ngariba katika Mlango wa “WANAVYUONI WALIOPITA”  na Pia Baadhi wa Wanavyuoni wa Hivi sasa katika Mlango wa “WANAVYUONI WA SASA”

02/05/2022

Alhamdulilah Leo Nimeongeza Mlango Mpya wa  “APPLICATIONS/KURUANI” ambao  Mwenyeezi Mungu akipenda nitakuwa nikiorodhesha Aya za Kuruani na Matumizi yake katika Maisha.

HABARI ZA APRIL KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 30 MWAKA 2022

23/04/2022

HABARI YA KWANZA

Alhamdulilah Leo Nimefungua Mlango Mpya  wa  “CHANGAMOTO/CHALLENGE”  Ni  Masuala aliyotoa  Mwenyeezi Mungu. Na kuanzia Kuumbwa kwa Dunia mpaka leo hakuna aliyeweza Kutatua Masuala Hayo. Allahu Akbar.

HABARI YA PILI

Alhamdulilah leo nimefungua Mlango mpya wa  “MIUJIZA YA KURUANI-7” ambao nimeelezea Miujiza Mbalimbali kutoka katika Kuruani Tukufu.

17/04/2022

Alhamdulilah leo nimemaliza Maudhui ya Tohara katika Mlango wa “FIQH/TOHARA” na Mwenyeezi Mungu akipenda nitaanza Maudhui ya “Sala” hivi Karibuni katika Mlango wa “FIQH/SALA” ambao utakusanya Kila Jipya linalohusiana na Sayansi katika Kuruani Tukufu. Nashukuru Mungu pia kuniwezesha siku ya leo Kufungua Mlango Mpya unaojulikana kama “Dialogue/Kuruani” ambao nitaorodhesha Mazungumzo yaliyopo Katika Kuruani Tukufu kama vile Mazungumzo baina ya Mwenyeezi Mungu na Mitume Yake au baina ya Mitume yake na Mataifa ya wakati huo. Alhamdulilah. Allahu Akbar.

HABARI ZA MARCH KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 31 MWAKA 2022

25/03/2022

Alhamdulilah Leo Nimeelezea muujiza mkubwa wa Aya ifuatayo katika Mlango wa “Mwezi Shaaban 2022” 

قُل لَّٮِٕنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِمِثۡلِ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُہُمۡ لِبَعۡضٍ۬ ظَهِيرً۬ا (٨٨) 

Allahu Akbar.

08/03/2022

Alhamdulilah Leo Nimezungumzia Katika Mlango wa “Miujiza Ya Kuruani-6”  Habari za  Kushangaza sana.

Kwanza ni Umbali wa Misikiti Miwili: Masjid Al-Haram (Mecca) na Masjid Al-Aqsa (Palestine) ni Maili  767  na Namba hii ni idadi ya Aya Baina ya Misikiti Hii Miwili katika Kuruani Tukufu.  Je Unaona Ya Kushangaza? Allahu Akbar.

Pili na La kushangaza Zaidi ni Sura ya Israa ambayo inaelezea Safari Ya Israa Na Miraji.

Na katika Miraji Mtume ﷺ alipewa Maamrisho ya Sala 5  na Baadaye akafundishwa na Jibril namba ya Kuswali na Katika Kuswali akafundishwa idadi za Rakaa 17.

La kushangaza ni Kwamba Sura Ya Israa ni Ya 17 Pia!!!! Je unaona Muashirio mwingine.

Hapo awali Sura za Kuruani na Aya hazuikuwa na Namba. Ziliongezwa baadaye kwa ajli ya kuwarahisishia wasomaji. 

Muujiza huu tunagundua katika Enzi hizi za Sayansi na Technologia. Mwenyeezi Mungu alipanga haya na alijua. Zimepangwa kwa makusudi ili iwaongoze na kuwapa imanii waumini na pia iwe hoja kwa wengineo.

Na siyo kwamba ilipangwa na Mtume ﷺ haiwezekani hata kidogo.

Mwenyeezi Mungu anajua zaidi iwapo tumesibu utafiti huu. 

Allahu Akbar. Angalia Maajabu Yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar.

HABARI ZA FEBRUARY KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 28 MWAKA 2022

20/02/2022

Alhamdulilah Nimeelezea Miujia Miwili Mipya Katika Mlango wa “Miujiza Ya Kuruani-6”. Muujiza Wa Kwanza ni Kuhusu  MVI au UZEE na Wa Pili Ni Mbegu za HARADALI (Mustard Seed).  Allahu Akbar. Ulimwengu Wote Katika Kuruani. Ni Saini Ya Mwenyeezi Mungu. Kuruani Ni maneno yaliyo hai. Kila Herufi, Neno au Aya Ina Miujiza Isiyo na Mwisho. Allahu Akbar.

13/02/2022

Mlango wa “HISTORIA YA UISLAMU” -Alhamdulilahi Leo Nimeendelea kuzungumzia Matukio Katika Mwaka 630

Mlango wa “MISEMO YA WANAVYUONI” -Alhamdulilah Leo  Nimezungumzia Kuhusu Imamu Hambali na Pia Kauli Zake

Mlango wa “PROPHETIC MEDICINE”  Alhamdulilah Leo  Nimezungumzia Mabadiliko tunayofanya katika Miili yetu na hatari zake kwa Mfano TATOO katika Kuremba Ngozi ya Mwili. Sayansi Inathibitisha Hatari Hizi na Pia Hadithi za Mtume Zinakataza Mabadiliko tunayoyafanya kwa ajili ya Marembo yasiyo na Msingi wowote.

05/02/2022

KWANZA

Alhamdulilah Leo nimezungumzia Mkataba Uliofanywa na Mtume ﷺ unaojulikana kama Mkataba wa Hudaybiya katika Mwaka  628  (CE) katika Mlango wa “Historia Ya Uislamu”

PILI

Nimedokeza Katika Mlango wa  “Waandishi Duniani” Kitabu Cha Mwandishi Mkristo anayejulikana kwa jina kama Dr. Craig Considine. Aliandika Kitabu Cha Maadili Mazuri Ya Mtume ﷺ  Kitabu hiki kinajulikana kwa jina la “The Humanity of Muhammad: A Christian View. Ni Kitabu kinachomsifu Mtume katika Kuleta Uhusiano Mzuri wa Kidini na Mengineyo ya Uadilifu Duniani.

TATU

Alhamdulilah Nimegusia historia fupi na kukusanya Kauli za Imamu Maliki (Rahimahullah) katika Mlango wa “Misemo Ya Wanavyuoni”

04/02/2022

MAAJABU YA KWANZA

Alhamdulilah leo Nimezungumzia katika Mlango wa “ENGINEERING/KURUANI Maajabu Ya Aya namba 68 na 69 ya Sura Ya Al-Nahl Yaani Nyuki. Miujiza Saba ya Kushangaza. Aya Hizi Mbili Pekee zimekusanya Maajabu Yasiyo na Mwisho Kuna tunayoyajua na tusiyoyajua. Nakukaribisha kwa mikono miwili katika sherehe hiyo. Allahu Akbar.

MAAJABU YA PILI

Alhamdulilah katika Mlango wa “HESABU NA KURUANI” nimezungumzia Muujiza Wa Sura Ya Al-Nasr Namba 110. 

Sura Hii iliwasikitisha Maswahaba kwani Walifahamu undani wake kwamba Maisha Ya Mtume ﷺ yatakuwa mafupi. Na kweli hivi ndivyo ilivyotokea kwani baada ya Muda siyo mrefu Mtume akaaga Dunia. Sura Hii ilificha Umri wa Mtume ﷺ atakaoishi Duniani. Na hakuna aliyejua wakati huo. Habari za Muujiza Nimeelezea katika Mlango wa “Hesabu Na Kuruani”

HABARI ZA JANUARY KUANZIA TAREHE 15 MPAKA 31

MWAKA 2022

30/01/2022

Alhamdulilah leo nimezungumzia Namba 19 na Muujiza wa Namba hii katika Mlango wa “ENGINEERING/KURUANI”

Mpangilio wa Sura, Aya, Maneno na Herufi katika Kuruani ni Engineering Ya Hali Ya Juu hakuna Mfano wa kitabu chochote Duniani. Kuruani Ni Hotuba Ya Mwenyeezi Mungu Ulimwenguni. Inatisha na Kusisimua. Mpangilio huu wa Sura, Aya, Maneno na Herufi Ni Saini Yake na inathibitisha kwamba Kuruani ni yake. Allahu Akbar.

29/01/2022

Alhamdulilahi Leo nimefanya Nyongeza katika Mlango wa “Hesabu na Kuruani” ni  Muujiza Unaoshangaza sana na  ambao una uhusiano na Idadi ya Milango ya Motoni na Peoponi. Habari Hii nilianza kuizungumzia katika Mlango Wa “Elimu” Muda uliopita. Allahu Akbar.

28/01/2022

Alhamdulilahi Leo Nimeongeza Baadhi ya Miujiza katika Mlango wa “Historia Ya Uislamu” Na Kufanya Marekibisho kama nilivyoahidi. Ninapopata Uhakika au Muujiza ninarudi tena katika Maandishi na Kurekibisha, Kupunguza au Kurekibisha basi Naomba Mola Atakabali Kazi hii Ya Mja wake Dhaifu. Allahu Akbar.

23/01/2022

Alhamdulilah leo Nimefungua Mlango Wa “Historia Ya Uislamu” ambao Mwenyeezi Mungu akipenda Nitaorodhesha Histroria Fupi Ya Kiislamu Kuanzia Kuzaliwa kwa Mtume ﷺ katika karne ya 6 mpaka sasa. Yaani karne ya 14. Hii ndiyo nia yangu. Mwenyeezi Mungu akinipa uzima na umri. Nitaiandika  kwa kuongeza, kuirakibisha, kuipunguza baada ya Utafiti na Kuichuja vizuri mpaka iwe safi kabisa. Kwa hiyo usishangae kila mara kutakuwa na Mabadiliko. Na Mola anajua zaidi iwapo Tutapata 100 %  (asilimia  100) kama ilivyokuwa. lakini hilo ndilo lengo. 

22/1/2022

Matumizi ya kiajabu ya Neno  رجل (RAJUL) yaani Mwanaume na Neno  امرا  / امرات       (IMRAAT) Lenye Maana Ya Mwanamke. Neno RAJUL na IMRAAT yametajika katika Kuruani Mara  24 kila Moja. Kutajika au Kukariri Sawa Sawa kwa kufanana kunaonyesha kwamba Kuruani Imepangwa kwa Makusudi na kimaana na siyo bure bure. Kufanana kunaonyesha Wote wawili wameamrishwa kumuabudu Mungu na Wote wawili watalipwa sawa sawa. Haki za wote wawili duniani ni sawa pia na Mengineyo tusiyoyajua. Allahu Akbar. Aya  zote zilizotaja Maneno haya Mawili nimezikusanya katika Mlango wa “HESABU NA KURUANI”.  Alhamdulilah. 

16/01/2022

Alhamdulilah Katika Mlango wa “VISA NA MATUKIO” Nimezungumzia Kisa cha Mtu aliyefishwa kwa muda wa Miaka Mia Moja na kurudishiwa uhai tena. Kisa hiki kinashangaza. Herufi za Kisa pia ni 100. Kuruani haikuelezea kirefu cha kisa hiki lakini  Habari (Sources) zinazohusiana na kisa hiki zinasema kwamba Mtu huyu alipofishwa  alikuwa na umri wa miaka 40 na alipofufuliwa pia alikuwa na miaka 40. Aliporudi nyumbani kwake alimkuta mtoto wake aliyekuwa bado hai ana umri wa 118. Sasa angalia maajabu  Baba ana umri wa miaka 40 na mtoto ana umri wa miaka 118. Allahu Akbar. Kwa kweli Kwa Mwenyeezi Mungu kila kitu anaweza na tusishangae. Anaumba wakati anaotaka na kwa namba anayotaka. Allahu Akbar.

15/01/2022

HABARI YA KWANZA

Alhamdulilahi. leo Nimeelezea katika Mlango wa “HERUFI/MANENO/AYA” Hekima Ya Makusudio katika mpangilio wa Kutangulizaألخبر AL-KHABAR (Predicate) Kabla Ya ألمبتدأ Al-Mubtadaa (Subject) Katika Aya. Kuna sababu Mbalimbali lakini katika Aya nilizochagua nimeelezea Sababu Moja peke yake.

HABARI YA PILI

Alhamdulilah Leo Nimezungumzia katika mlango wa “MATUKIO NA VISA” Kisa kinachoelezea sababu ya Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)kuamrisha Kuchomwa moto kwa Msikiti unaojulikana kwa Jina kama Masjid Al-Dhirar  مسجد الضرار  huko Madina katika Karne ya 7. Ilikuwa mwanzoni mwa Uislamu na Baada tu ya kurudi kutoka safari ya Tabuk.