UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
UPO KATIKA MAANDALIZI KWA HIYO USISHANGAE UNPOUONA UNABADILIKABADILIKA KILA WAKATI.
MIONGONI MWA MIUJIZA MIKUBWA
Tarehe 09/10/2022
SURA FUPI TATU ZENYE MAAJABU MAKUBWA
Kwanza ningependelea kuzinukulu Sura hizi Tatu na Tafsiri yake na Kisha Nitaelezea Hadithi Za Mtume ﷺ kuhusu Sura Hizi na Baada Ya Hapo Tutachambua Muujiza Wa Kiajabu. Allahu Akbar.
SURA NAMBA 1-SURA YA AL-IKHLAS
سُوۡرَةُ الإخلاص
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
TAFSIRI
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
1 .Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu).
2. Mwenyezi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe Vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea).
3. Hakuzaa wala Hakuzaliwa
4· Wala hana anayefanana Naye hata mmoja.
SURA NAMBA 2-SURA YA AL-FALAQ
سُوۡرَةُ الفَلَق
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢) وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (٣) وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥)
TAFSIRI
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
1. Sema: Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote
2. Na shari ya Allvyoviumba
3. Na shari ya giza Ia usiku liingiapo
4· Na shari ya wale wanaopulizia mafundoni,
(wakavunja mashikamano yaliyo baina ya watu)
5· Na shari ya hasidi anapohusudu
SURA NAMBA 3-SURA YA ANNAS
سُوۡرَةُ النَّاس
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (١) مَلِكِ النَّاسِ (٢) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (٣) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (٤) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (٥) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (٦)
TAFSIRI
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu, kuneemesha neema kubwa kubwa na kuneemesha neema ndogo ndogo.
1. Serna: Ninajikinga kwa Bwana mwenye kuwalea
2. Mfalme wa watu
3. Muabudiwa wa watu
4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma
5. Atiaye wasiwasi nyoyoni mwa watu
6. (Ambaye ni) katika maiini na watu
HADITHI ZA MTUME ﷺ ZINAZOSHEREHESHA SURA HIZI TATU
Kwa kweli kuna Sura Nyingi lakini Nitachagua Chache katika Mlango huu kwani Lengo la Mlango huu ni Muujiza Utakaofuata. Lakini nimeona bora niongeze baadhi ya Hadithi zenye kuonyesha Thamani, Fadhila au Utukufu wa Sura Hizi.
SURA ZOTE TATU (AL-IKHLAS+ AL-FALAQ +ANNAS)
Hadithi ambayo ipo katika kitabi cha Riyadh Aswalihiyn.
وعن عبد الله بن خُبيب -بضم الخاء المعجمة- رضي الله عنه قال: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم: “اقرأ: قل هو الله أحد، والمعوذتين حين تمسي وحين تصبح، ثلاث مرات، تكفيك من كل شيء”. رواه أبو داود والترمذي وقال حديث حسن صحيح .
SHEREHE
Hadithi inayotokana na Abdullahi Ibn Khubayb. (رضي الله عنه). Alisema kwamba Mtume ﷺ alimwambia asome Sura ya Al-Ikhlas, Alfalaq na Annas kila siku Jioni na Asubuhi kwani kufanya hivyo Atapata faida kubwa. Kwanza Mwenyeezi Mungu atamlinda na kila Shari, Atambariki kila atakachikifanya siku hiyo na Atamsaidia na Kila Mahitaji yake. Kwa kifupi hadithi Hii inatupa faida hii. Tukizisoma KIla siku mara mbili basi tutapata Faida hizi. Tufanye hivi na hali tuna Imani, Bila kujilazimisha. Tufanye kwa Hamu kubwa yakupata zawadi hizi. Hii ndiyo maana ya Hadithi hii.
TRANSLATION
‘Abdullah bin Khubaib (May Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (ﷺ) said to me, “Recite Surat Al-Ikhlas and Al- Mu’awwidhatain (Surat Al-Falaq and Surat An-Nas) three times at dawn and dusk. It will suffice you in all respects.” [Abu Dawud and At-Tirmidhi].
SURA YA AL-IKHLAS
Hadithi ya Kwanza ya Bukhariy-Hadithi Sahihi Pia ipo katika Kitabu cha Riyadh Aswalihiyn
وعن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال في:{ قل هو الله أحد}:” والذي نفسي بيده، إنها لتعدل ثلث القرآن”. وفي رواية: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال لأصحابه:” أيعجز أحدكم أن يقرأ بثلث القرآن في ليلة” فشق ذلك عليهم، وقالوا: أينا يطيق ذلك يارسول الله: فقال :” {قل هو الله أحد} ثلث القرآن.”. (( رواه البخاري)).
SHEREHE
Hadithi Iliyosimuliwa na Said Al-khudri kwamba Mtume ﷺ alisema “Naapa kwa yule ambaye Roho yangu ipo mikononi mwake. (Sura Hii) ni sawa na Theluthi Moja ya Kuruani na Pia Kuna hadithi nyingine inayohusu habari hizi inayosema Mtume ﷺ “Aliwauliza Maswahaba zake “Je miongoni mwenu kuna yeyote asiyeweza kusoma kiwango cha Theluthi ya Kuruani katika Usiku mmoja? Suala Hili lilikuwa gumu na kwa hiyo wakajibu “Ewe Mtume wa Mwenyeezi Mungu “Hakuna kati yetu anayeweza kusoma kiwango hicho kwa muda wa Usiku mmoja”. Theluthi Moja ni Fungu moja la Sura za Kuruani ukigawa Kuruani katika Mafungu Matatu. Mtume akawajibu kwa kusema
“Sura Moja tu ya Al-Ikhlas ukiisoma itakuwa kama umesoma Theluthi moja ya Kuruani yaani Fungu moja kati ya Mafungu matatu ya Sura 114 ya Msahafu. (ukigawa sura 114 katika mafungu matatu).
Kwa hiyo Sura Hii ina Mengi mazuri ambayo katika Mlango huu Mdogo Wa Website hii inatkuwa vigumu kuelezea kila kitu. Nitachagua Zile hadithi chache ili tupate angalau Mwanga Mdogo.
TRANSLATION
Abu Sa’id Al-Khudri (May Allah be pleased with him) reported about Surat Al-Ikhlas (Chapter 112): The Messenger of Allah (ﷺ) said, “By Him in Whose Hand my soul is, it is equivalent to one-third of the Qur’an.” According to another version, he (ﷺ) said to his Companions, “Is anyone of you incapable of reciting one-third of the Qur’an in one night?” They considered it burdensome and said: “O Messenger of Allah, which of us can afford to do that?” He (ﷺ) said, “Surat Al-Ikhlas [Say: He is Allah (the) One] is equivalent to one-third of the Qur’an.” [Al- Bukhari].
Hadithi Ya Pili Katika Kitabu Cha Sunnan Jamii At-irmidhiy-Hadithi ni Dhaifu lakini Baadhi ya Wanavyuoni wanathibitisha Kwamba Grade au Kiwango cha Hadithi ni Hasan
حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ مَنِيعٍ، حَدَّثَنَا أَبُو سَعْدٍ، هُوَ الصَّغَانِيُّ عَنْ أَبِي جَعْفَرٍ الرَّازِيِّ، عَنِ الرَّبِيعِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِي الْعَالِيَةِ، عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ الْمُشْرِكِينَ، قَالُوا لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم انْسُبْ لَنَا رَبَّكَ . فَأَنْزَلَ اللَّهُ : ( قلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ * اللَّهُ الصَّمَدُ ) فَالصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ لأَنَّهُ لَيْسَ شَيْءٌ يُولَدُ إِلاَّ سَيَمُوتُ وَلَيْسَ شَيْءٌ يَمُوتُ إِلاَّ سَيُورَثُ وَإِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لاَ يَمُوتُ وَلاَ يُورَثُ : ( لَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ ) قَالَ ” لَمْ يَكُنْ لَهُ شَبِيهٌ وَلاَ عِدْلٌ وَلَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ”
SHEREHE
Hadithi hii inatokana na Ubayy Ibn Ka’b. Alisema kwamba Makafiri wale ambao waliokuwa wakiabudu Masanamu walikuja kwa Mtume ﷺ na kumpa Mtihani kwa kumwambia yafuatayo:
Ewe Mtume wa mweyeezi Mungu Tutajie Ukoo wa Mwenyeezi Mungu” yenye maana ya “Je Mungu ni nani” “Je ana Familia?” “Je amezaliwa?”
Kwa kweli hivyo ndivyo Makafiri walivyofikiri kwamba Mwenyeezi Mungu ni sawa na Masanamu yao.
Walitaka kujua Ukoo wa Mwenyeezi Mungu kama vile Baba yake Babu yake Mama yake au Bibi yake.
Kwa kweli ukifikiri utaona Suala silo Rahisi. Jaribu kufikiri Ikiwa mimi au wewe Tunaishi wakati huo wa karne ya Sita na Tumeulizwa Suala kama hili.
Lakini Mwenyeezi Mungu akamsadia Mtume ﷺ na Kumshushia Jibu awajibu Makafiri hawa.
Na ndiyo maana Mwanzoni mwa Sura Hii Mwenyeezi Mungu ametumia neno قُلۡ “KUL” lenye maana ya “SEMA” yaani “Wajibu kwa Kusema” na baada ya hapo ikafuatia jawabu katika Sura Hii.
Tafsiri ya Sura Hii Angalia Hapa Juu.
Kwa kifupi Sura Hii inamtakasa Mwenyeezi Mungu kwamba Yeye ni Mmoja tu. Hategemei Viumbe wake bali sisi tunamtegemea. Hakuzaliwa na Hakuzaa na Hakuna Chochote kinachofanana naye katika Viumbe vilivyo hai na Pia viumbe visivyo hai.
TRANSLATION
Abu Al-Aliyah narrated from Ubayy bin Ka’b: “The idolaters were saying to the Messenger of Allah: ‘Name the lineage of your Lord for us.’ So Allah, Most High, revealed: Say: “He is Allah, the One. Allah As-Samad.” So As-Samad is ‘the One Who does not beget, nor is He begotten,’ because there is nothing born except it will die, and there is nothing that dies except that it will be inherited from, and verily. Allah, the Mighty and Sublime, does not die, nor is He inherited from. ‘And there is none comparable to Him.’ He said: ‘There is nothing similar to Him, nor equal to Him, nor is there anything like Him.’”
SURA YA ANNAS NA AL-FALAQ
Hadithi ya Kwanza-Ipo katika Sahih Muslim na Riyadh Aswalihiyn.
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال : “ ألم ترَ آيات أنزلت هذه الليلة لم يرَ مثلهن قط ؟ قل أعوذ برب الفلق، وقل أعوذ برب الناس ”.((رواه مسلم)).
SHEREHE
Hadithi hii inatokana na ‘Uqbah bin ‘Amir (رضي الله عنه) Inasema kwamba Mtume ﷺ alisema kwamba Aya za Kuruani zimeshishwa usiku wa leo ambazo hakuna mfano wake. Na baada ya hapo akazisoma Aya zifuatazo:
قل أعوذ برب الفلق
وقل أعوذ برب الناس
TRANSLATION
‘Uqbah bin ‘Amir (May Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (ﷺ) said: “Do you not know that last night certain Ayat were revealed the like of which there is no precedence. They are: ‘Say: I seek refuge with (Allah) the Rubb of the daybreak’ (Surah 113), and ‘Say: I seek refuge with (Allah) the Rubb of mankind’ (Surah 114).” [Muslim].
Hadithi ya Pili-Ipo katika Vitabu Vya Imamu Al-Bukhariy na Muslim na Pia Riyadh Aswalihiyn
وعن عائشة، رضي الله عنه، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم، كان إذا أخذ مضجعه نفث في يديه، وقرأ بالمعوذات ومسح بهما جسده. ((متفق عليه)). وفي رواية لهما: “أن النبي صلى الله عليه وسلم، كان إذا أوى إلى فراشه كل ليلة جمع كفيه، ثم نفث فيهما فقرأ فيهما: قل هو الله أحد، وقل أعوذ برب الفلق، وقل أعوذ برب الناس، ثم مسح بهما ما استطاع من جسده، يبدأ بهما على رأسه ووجهه، وما أقبل من جسده، يفعل ذلك ثلاث مرات”. ((متفق عليه)). قال أهل اللغة : (( النفث )) نفخ لطيف بلا ريق
SHEREHE
Hadithi inayotokana na Aisha (رضي الله عنه) Mke wa Mtume ﷺ anaelezea kuhusu Mtume ﷺ kwamba unapofika wakati wa kulala na anapokuwa kitandani basi Hupulizia Viganja Vya Mikono yake miwili kwa kupulizia na kisha Husoma Sura ya Al-Falaq na Annas zinazojulikana kama Muawidhatayni. Maana ya Neno hili ni “Kinga Mbili”. Na baada ya hapo hujipaka Mwili wake wote katika sehemu zote za mwili ambazo huweza kufikia Mikono yake.
Na kuna Riwaya au Version Ya hadithi nyingine inayosema Hupulizia Viganja Vya Mikono yake miwili na Kisha Husoma Sura Tatu: Al-Ikhlas, Al-Falaq na Annas na kisha baada ya hapo hujipaka Mwili wake wote katika sehemu zote za mwili ambazo huweza kufikia Mikono yake. Huanza Kujifuta au kujipaka kuanzia Uso na kichwa na kisha Mwilini. Alikuwa akifanya hivyo Mata Tatu. Yaani Alijipaka Mwili wake mara Tatu. Kisomo cha Sura Tatu ni mara moja lakini Kujipaka mara tatu. Katika Kupulizia Viganja Vya Mikono upulizie pumzi ya polepole na siyo kwa nguvu na kujiepusha na Mate na ndiyo maana ya ibara
النفث قال أهل اللغة : (( النفث )) نفخ لطيف بلا ريق
Gentle blowing without saliva
Kufanya Hivi kuna faida nyingi. Kuna faida tunazozijua na zile ambazo hatuzijui. Kwanza Mwenyeezi Mungu anatuepushia na Shari tusizozijua kama vile Mashetani na Maradhi. Na ikiwa Utafariki dunia usingizini inakuwa bora Iwe baada ya Kisomo hicho kuliko Kulala hovyo hovyo kwani Kila Mtu anatamani Mauti yanapofika angalau awe katika Kumtaja Mwenyeezi Mungu na kwa hiyo Unapolala hujui litakalokupata. Na Lazima tukumbuke kwamba Usingizi Ni Nusu ya Mauti.
TRANSLATION
‘A ishah (May Allah be pleased with her) reported: Whenever the Messenger of Allah (ﷺ) went to bed, he would blow upon his hands recite Al-Mu’awwidhat; and pass his hands over his body. [Al-Bukhari and Muslim].
Katika Sura hizi Tatu. Sura Iliyotangulia kushuka ni Sura Ya Al-Falaq, Ikafuatiwa na Sura Ya Annas na baada ya hapo ikafuatiwa na Sura ya Al-Ikhlas.
Fadhila ya Sura Hizi Tatu ni Nyingi ambazo Website ndogo kama hii haiwezekani kuzinukulu hadithi zote za Mtume zenye Maelezo Mbalimbali Kuhusu Sura Hizi Tatu. Pia Kuna Kauli Mbalimblai za Wanavyuoni kuhusu Sura Hizi Tatu ambazo ningependelea kuzinukulu lakini haitawezekana kwa ajili ya lengo la mlango huu ni uchambuzi wa Muujiza na kwa hiyo nitaishia hapa Lengo la Mlango huu ni Muujiza Unaofuata.
Kwa kifupi Sura Ya Al-Ikhlas inamtakasa Mwenyeezi Mungu na Tunaambiwa Tumwite Mwenyeezi Mungu kwa Jina Lake ambalo ni “Allah” na pia tunaweza kumwita kwa zile Sifa Zake. Lakini tusitumie majina mengineyo bila mpango. Hata Binaadamu hawapendi Kugeuzwa Majina Basi Hivyo hivyo Mwenyeezi Mungu inabidi tuwe macho sana.
Sura Ya A-Lfalaq Inatupa Fundisho tumuombe Mwenyeezi Mungu atuepushie na Shari ya Viumbe vyake tunavyovijua na tusivyovijua. Yaani tumuombe Mwenyeezi Mungu atukinge na Shari hizo.
Sura Ya Annas Inatupa Fundisho Tumuombe Mwenyeezi Mungu atuepushie na Shari ya Mashetani wa Kijini na Kibinaadamu ambao Hutia Wasiwasi katika Nyoyo zetu.
Mashetani hatuwaoni lakini wapo. Ukiwa Muislamu basi lazima Uamini Kila Kilichotajwa katika Kuruani kama vile Pepo, Moto wa Jahannam, Malaika, Mashetani. Na hii ndiyo imani ya Ghayb. Lazima Uamini ikiwa wewe Muislamu na Kama huamini basi huna Dini. Kufuatana na Miujiza Tuliyoiona katika Website hii kwa kweli lazima Tuamini kwani Miujiza siyo Midogo. Na Miujiza Hii yote imegusia Mashetani, Malaika, Pepo (Jannah) Na Moto (Jahannam) Tumeona Hesabu zinavyodhirisha Muujiza, Namba tulizoziona katika Muujiza wa Kihesabu zinatosha tuamini bila tatizo lolote.
Baada ya Kuzielezea Sura Hizi Tatu naona Wakati umefika Wa Kuanza Kuchambua Sura Hizi Tatu ili tuone Maajabu ambayo siyo madogo. Maajabu Haya Yamepangwa kwa makusudi. Kama Nilivyosema katika Kila Muujiza wa Website hii kwamba Kuruani ni Muujiza Mkubwa sana. Kuruani Imekusanya Vitu Viwili. kwanza ni Ujumbe na Pili ni Miujiza. Na huu ndio Ujumbe wa mwisho ulivyokusudiwa.
Mitume iliyopita walipewa Ujumbe na Miujiza ambayo ilikuwa ni Kithibitisho kwamba Ujumbe wao ni wa kweli Lakini Mtume wa Mwisho Muhamad ﷺ kapewa Miujiza ya kuthibitisha Ujumbe wake na Pia Muujiza wa Kuruani ambayo Muujiza wake bado unaendelea na itakuwa hivyo mpaka Mwenyeezi Mungu atakapopenda au Mwisho wa Ulimwengu utakapofika.
Sasa tuanze na uchambuzi wa maajabu katika sura hizi tatu.
DARUBINI KATIKA SURA HIZI TATU
SURA NAMBA 112
سُوۡرَةُ الإخلاص
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
——————————
SURA NAMBA 113
سُوۡرَةُ الفَلَق
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ
ٱلرَّحِيمِ قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢) وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (٣) وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥)
—————————-
SURA NAMBA 114
سُوۡرَةُ النَّاس
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ
ٱلرَّحِيمِ قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (١) مَلِكِ النَّاسِ (٢) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (٣) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (٤) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (٥) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (٦)
Nitapanga miujiza kutoka katika Sura Hizi Tatu kwa namba kama ifuatavyo:
MUUJIZA WA KWANZA
Namba za Sura zinashangaza sana kwani Ijapokuwa Namba hizi ziliongezwa baadaye kwa ajili ya kuwasaidia Wasomaji wa Kuruani lakini Nyongeza yoyote ilikuwa chini ya Uangalizi wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu na katika Muujiza huu wa kwanza Utaona Ukweli huu. Mwenyeezi Mungu ameahidi kuitunza Kuruani hii yeye mwenyewe baada ya Vitabu vya Manabii waliotangulia kuharibiwa. Kuruani ipo chini ya Uanagalizi wa mwenyeezi Mungu.
hebu sasa Tuchunguze Namba za Sura.
Sura Ya Ikhlas ni Namba 112 Na ina Aya 4
Sura Ya Al-Falaq Ni Namba 113 Na ina Aya 5
Sura Ya Annas Ni Namba 114 Na ina Aya 6
Muujiza upo wazi. Hebu tujimlishe Namba za Sura.
Al-Ikhlas Sura Namba 112 tukijumlisha Namba 1 + 1 + 2=4 Na Ajabu ni kwamba Jumla ya Namba hii ni 4 Na Namba 4 ni Jumla ya Aya za Sura Hii
Al-Falaq Sura Namba 113 tukijumlisha 1 + 1 + 3 =5 Na Ajabu ni kwamba Jumla ya Namba hii ni 5 na Namba 5 ni Jumla Ya Aya za Sura Hii
Al-Nas Sura Namba 114 tukijumlisha 1 + 1 + 4 =6 Na Ajabu ni kwamba Jumla ya Namba hii ni 6 na Namba 6 ni Jumla Ya Aya za Sura Hii
Angalia maajabu. Dalili ya Mvua ni Mawingu. Kabla Ya Uchambuzi Mkubwa tunapata Muujzia wa Kwanza Bado Mapema Ya Asubuhi. Haya siyo Madogo kwani Kuruani siyo kitabu kama vitabu vinginevyo hata kidogo. Hebu tuendelee na Muujiza za pili.
MUUJIZA WA PILI
Muujiza wa pili utahusu Sura Ya A-Ikhlas. Mwenyeezi Mungu anatuamrisha Tutumie Jina lake la “Allah” Katika Aya ya Kwanza ya Sura Hii aliposema
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) .
Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu).
Kwa hiyo Kuna Aya Nyingine katika Sura Ya Al-AaRaf Namba 7 Aya Namba 18 Inayotupa Ruhusa kumwita kwa kutumia Majina Yanayojulikana kama “Asmaa Alhusna” Aya hiyo inasema:
و لله الاسما الحسني فادعوه بها و ذروا الذين يلحدون في اسميه سيجزون ما كانوا يعملون
Katika Aya hii Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba majina yake mengineyo ni Hizo sifa zake zinazojulikana kama Asmaa Alhusna na Anaahidi Wanaotumia majina ambayo siyo yake au yale ambayo yana Ukafiri basi Watalipwa Kwa ubaya huo.
Sura Ya Al-Hashr namba 59 Aya Namba 23 na 24 imetaja baadhi ya majina Haya ambayo yanajulikana kama “Asmaa Alhusna”
هو الله الذي لا اله الا هو الملك القدوس السلم المومن المهيمن العزيز الجبار المتكبر سبحن الله عما يشركون
هو الله الخلق الباري المصور له الاسما الحسني يسبح له ما في السموت و الارض و هو العزيز الحكيم
Almaliki/Alqudusi/Asalaam/Almuumin/ Almuhaymin/Alaziz/ Aljabar/Almutakabir/ Alkhaliq/Albaruy/.
Jumla Ya Sifa za Mwenyeezi Mungu ni 99. na kila moja ya Sifa hizi zina maana. Na ni Vizuri tuzitaje Sifa hizi kufuatana na Maombi yetu. Tunapomumba Mwenyeezi Mungu Riziki basi tumwite kwa Kusema “Ewe Razaq” Yaani Ewe mwenye Kumiliki Riziki. Na kisha uombe ulitakalo. Na hivyo hivyo ukidhulumiwa Umwite kwa kusema “Ewe Hakimu” Yaani Ewe Jaji au Hakimu Mkubwa. Na Baadaye umuombe ulitakalo. Kila Jina Linaonyesha Ukubwa wake Mwenyeezi Mungu Katika Dunia na Ulimwenguni kwani yeye ndiye anayemiliki kila kitu.
SIFA AU MAJINA AMBAYO TUNAWEZA KUMWITA MWENYEEZI MUNGU YANAYOJULIKANA KAMA “ASMAA ALHUSNA, MATAMSHI NA MAANA YAKE KWA LUGHA YA KIINGEREZA.
The 99 Names of Allah (SWT) with Transliteration and meaning
1 الرَّحْمَنُ AR-RAHMAAN The Beneficent
2 الرَّحِيمُ AR-RAHEEM The Merciful
3 الْمَلِكُ AL-MALIK The King
4 الْقُدُّوسُ AL-QUDDUS The Most Sacred
5 السَّلاَمُ AS-SALAM The Source of Peace, The Flawless
6 الْمُؤْمِنُ AL-MU’MIN The Infuser of Faith
7 الْمُهَيْمِنُ AL-MUHAYMIN The Preserver of Safety
8 الْعَزِيزُ AL-AZIZ All Mighty
9 الْجَبَّارُ AL-JABBAR The Compeller, The Restorer
10 ُالْمُتَكَبِّر AL-MUTAKABBIR The Supreme, The Majestic
11 الْخَالِقُ AL-KHAALIQ The Creator, The Maker
12 الْبَارِئُ AL-BAARI The Evolver
13 الْمُصَوِّرُ AL-MUSAWWIR The Fashioner
14 الْغَفَّارُ AL-GHAFFAR The Great Forgiver
15 الْقَهَّارُ AL-QAHHAR The All-Prevailing One
16 الْوَهَّابُ AL-WAHHAAB The Supreme Bestower
17 الرَّزَّاقُ AR-RAZZAAQ The Provider 1
8 الْفَتَّاحُ AL-FATTAAH The Supreme Solver
19 اَلْعَلِيْمُ AL-‘ALEEM The All-Knowing
20 الْقَابِضُ AL-QAABID The Withholder
21 الْبَاسِطُ AL-BAASIT The Extender
22 الْخَافِضُ AL-KHAAFIDH The Reducer
23 الرَّافِعُ AR-RAAFI’ The Exalter, The Elevator
24 الْمُعِزُّ AL-MU’IZZ The Honourer, The Bestower
25 ٱلْمُذِلُّ AL-MUZIL The Dishonourer, The Humiliator
26 السَّمِيعُ AS-SAMEE’ The All-Hearing
27 الْبَصِيرُ AL-BASEER The All-Seeing
28 الْحَكَمُ AL-HAKAM The Impartial Judge
29 الْعَدْلُ AL-‘ADL The Utterly Just 3
0 اللَّطِيفُ AL-LATEEF The Subtle One, The Most Gentle
31 الْخَبِيرُ AL-KHABEER The All-Aware
32 الْحَلِيمُ AL-HALEEM The Most Forbearing
33 الْعَظِيمُ AL-‘AZEEM The Magnificent, The Supreme
34 الْغَفُور AL-GHAFOOR The Great Forgiver
35 الشَّكُورُ ASH-SHAKOOR The Most Appreciative
36 الْعَلِيُّ AL-‘ALEE The Most High, The Exalted
37 الْكَبِيرُ AL-KABEER The Most Great
38 الْحَفِيظُ AL-HAFEEDH The Preserver
39 المُقيِت AL-MUQEET The Sustainer
40 اﻟْﺣَسِيبُ AL-HASEEB The Reckoner
41 الْجَلِيلُ AL-JALEEL The Majestic
42 الْكَرِيمُ AL-KAREEM The Most Generous, The Most Esteemed
43 الرَّقِيبُ AR-RAQEEB The Watchful
44 ٱلْمُجِيبُ AL-MUJEEB The Responsive One
45 الْوَاسِعُ AL-WAASI’ The All-Encompassing, the Boundless
46 الْحَكِيمُ AL-HAKEEM The All-Wise
47 الْوَدُودُ AL-WADUD The Most Loving
48 الْمَجِيدُ AL-MAJEED The Glorious, The Most Honorable
49 الْبَاعِثُ AL-BA’ITH The Infuser of New Life
50 الشَّهِيدُ ASH-SHAHEED The All Observing Witnessing
51 الْحَقُ AL-HAQQ The Absolute Truth
52 الْوَكِيلُ AL-WAKEEL The Trustee, The Disposer of Affairs
53 الْقَوِيُ AL-QAWIYY The All-Strong
54 الْمَتِينُ AL-MATEEN The Firm, The Steadfast
55 الْوَلِيُّ AL-WALIYY The Protecting Associate
56 الْحَمِيدُ AL-HAMEED The Praiseworthy
57 الْمُحْصِي AL-MUHSEE The All-Enumerating, The Counter
58 الْمُبْدِئُ AL-MUBDI The Originator, The Initiator
59 ٱلْمُعِيدُ AL-MUEED The Restorer, The Reinstater
60 الْمُحْيِي AL-MUHYI The Giver of Life
61 اَلْمُمِيتُ AL-MUMEET The Creator of Death
62 الْحَيُّ AL-HAYY The Ever-Living
63 الْقَيُّومُ AL-QAYYOOM The Sustainer, The Self-Subsisting
64 الْوَاجِدُ AL-WAAJID The Perceiver
65 الْمَاجِدُ AL-MAAJID The Illustrious, the Magnificent
66 الْواحِدُ AL-WAAHID The One
67 اَلاَحَدُ AL-AHAD The Unique, The Only One
68 الصَّمَدُ AS-SAMAD The Eternal, Satisfier of Needs
69 الْقَادِرُ AL-QADEER The Omnipotent One
70 الْمُقْتَدِرُ AL-MUQTADIR The Powerful
71 الْمُقَدِّمُ AL-MUQADDIM The Expediter, The Promoter
72 الْمُؤَخِّرُ AL-MU’AKHKHIR The Delayer
73 الأوَّلُ AL-AWWAL The First
74 الآخِرُ AL-AAKHIR The Last
75 الظَّاهِرُ AZ-ZAAHIR The Manifest
76 الْبَاطِنُ AL-BAATIN The Hidden One, Knower of the Hidden
77 الْوَالِي AL-WAALI The Sole Governor
78 الْمُتَعَالِي AL-MUTA’ALI The Self Exalted
79 الْبَرُّ AL-BARR The Source of All Goodness
80 التَّوَابُ AT-TAWWAB The Ever-Pardoning, The Relenting
81 الْمُنْتَقِمُ AL-MUNTAQIM The Avenger
82 العَفُوُ AL-‘AFUWW The Pardoner
83 الرَّؤُوفُ AR-RA’OOF The Most Kind
84 َمَالِكُ ٱلْمُلْكُ MAALIK-UL-MULK Master of the Kingdom, Owner of the Dominion
85 ذُوالْجَلاَلِ وَالإكْرَامِ DHUL-JALAALI WAL-IKRAAM Lord of Glory and Honour, Lord of Majesty and Generosity
86 الْمُقْسِطُ AL-MUQSIT The Just One
87 الْجَامِعُ AL-JAAMI’ The Gatherer, the Uniter
88 ٱلْغَنيُّ AL-GHANIYY The Self-Sufficient, The Wealthy
89 ٱلْمُغْنِيُّ AL-MUGHNI The Enricher
90 اَلْمَانِعُ AL-MANI’ The Withholder
91 الضَّارَ AD-DHARR The Distresser
92 النَّافِعُ AN-NAFI’ The Propitious, the Benefactor
93 النُّورُ AN-NUR The Light, The Illuminator
94 الْهَادِي AL-HAADI The Guide
95 الْبَدِيعُ AL-BADEE’ The Incomparable Originator
96 اَلْبَاقِي AL-BAAQI The Everlasting
97 الْوَارِثُ AL-WAARITH The Inheritor, The Heir
98 الرَّشِيدُ AR-RASHEED The Guide, Infallible Teacher
99 الصَّبُورُ AS-SABOOR The Forbearing, The Patient
HADITHI YA MTUME ﷺ KUHUSU MAJINA YA HUSNA
حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَبُو الزِّنَادِ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمَا مِائَةً إِلاَّ وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ ”.
SHEREHE
Hadithi hii imekusanywa na Bukhariy katika Vitabu vyake vya hadithi.
Hadithi inatokana na Swahaba wa Mtume ﷺ
Abiy Hurayra. Anasema kwamba Mtume ﷺ alisema kwamba “Mwenyeezi Mungu ana Majina 99 atakeyeyajua (Kuyataja, kuyafahamu na Kuyazingatia) majina haya ataingia Peponi”
TRANSLATION
Narrated Abu Huraira:
Allah’s Messenger (ﷺ) said, “Allah has ninety-nine names, i.e. one-hundred minus one, and whoever knows them will go to Paradise.” (Please see Hadith No. 419 Vol. 8)
Baada ya Sherehe hii kuhusu Sura Ya Al-Ikhlas ninaona umefika wakati wa Kuelezea Muujiza Wa Sura Hii Ya Al-
Ikhlas: Tutachunguza Vokali au Voyel inayojulikana kama “KASRAH”. Katika Lugha ya Kiarabu kuna Vokali (Voyels) Sita. zinajulikana kama FATHA (Fupi na Ndefu), KASRA (Fupi na Ndefu) NA DHUMMA (Fupi na Ndefu). Yaani Vokali Tatu Fupi zinajulikana kama a, i na u
Na Vokali Tatu Ndefu Zinajulikana kama aa, ii, uu
Kabla ya Kuendelea ningependelea kutaja kwamba Hizi Vokali (Voyel) ziliongezwa baada ya Wahyi wa Kuruani Tukufu ili kurahishisha Usomaji wa Kuruani. ili kuwasaidia Wasomaji wasifanye Makosa katika Matamshi Kwa mfano Herufi QAF katika Neno
قلب Likitiwa KASRA chini yake قِ matamshi yatakuwa “Qi” na Ikitiwa FATHA Juu yake قَ matamshi yatakuwa “Qa” na Ikitiwa DHUMMA Juu yake قُ
Matamshi yatakuwa “Qu” na hii inasaidia sana kwa wageni wa Lugha ya Kiarabu kwani Waarabu wa hapo zamani katika Enzi ya Mtume ﷺ alipokuwa hai walikuwa hawahitaji Alama hizi kwani walijua Lugha yao Vizuri, lakini kwa Wageni au wasomi wa Lugha hii wanahitaji Alama hizi kwani zinasaidia Kutamka Maneno kama Inavyotakikana. Kwani Kama hakuna Alama Hizi basi Matamshi huenda yakabadilika na ikiwa hivyo basi maana pia itabadilika.
Yaani maana ya neno litabadilika kwa Kugeuza Matamshi ya Herufi.Kwa Hiyo Utafiti wetu Utakuwa katika Vokali au Voyel Moja tu nayo ni KASRA fupi.
Hii Kasrah Fupi ndiyo tutakayoifanyia Utafiti katika Mlango huu.Kwa Kweli Ni Muujiza siyo Mdogo kwani Aya Ya Kwanza Kushushwa Herufi Ya Kwanza katika Aya hiyo ilitiwa KASRAH. Angalia Aya Ya Kwanza Kushushwa na Herufi ya Kwanza ambayo ina KASRAH chini yake na Inatamkwa “i” katika Neno iKRAA
اِقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ
Matamshi Yanakuwa IQRAA yenye maana ya “SOMA”
Kwa hiyo Alama Ya KASRA imetumika Katika Aya ya
kwanza Kushushiwa Mtume. ﷺ Hebu tuchunguze Sura Ya Kwanza Aya ya Kwanza na Pia Sura Ya mwisho Aya ya Mwisho katika Mpangilio wa Msahafu kwani Mpangilio ni tofauti na Kushushwa kwa Kuruani. Kwa Hiyo Mpangilio unatokana na Malaika Jibril siyo bure bure tu na ndiyo maana Kuna Miujiza mingineyo ambayo inatokana na Mpangilio wa Sura za Kuruani Tukufu.
Aya Ya Kwanza Kushushwa ni
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
Angalia Alama ya Kasra katika Herufi ya Kwanza “BAA” Ya neno la Kwanza “BISMI” ya Aya Ya Kwanza katika Sura Ya Kwanza Kufuatana na Mpangilio wa Msahafu. Utaona Herufi Baa Imetiwa Kasrah na Inatamkwa BISMI
Na Aya Ya Mwisho Kushushwa ni
مِنَ الْجِنَّةِ وَ النَّاسِ
Angalia Alama ya Kasra katika Herufi ya Kwanza “MIM” Ya neno la Kwanza “MINA ya Aya Ya Mwisho ya Sura Ya Mwisho Kufuatana na Mpangilio wa Msahafu. Utaona Herufi Baa Imetiwa Kasrah na Inatamkwa “MINA”Kwa hiyo kuna maajabu ya kushangaza. Herufi KASRA ina Maajabu. Imechaguliwa Iwe ya Kwanza Kutumika katika Neno la Kwanza ya Aya Ya Kwanza Kushuka. Na Pia ya Kwanza Katika Neno la kwanza ya Sura Ya Kwanza Katika Mpangilio wa Msahafu na Pia katika neno la Kwanza ya Aya ya Mwisho katika Sura Ya Mwisho katika Mpangilio wa Msahafu.Kwa hiyo Utafiti wetu wa leo tutachunguza Alama Hii ya KASRA ambayo ni Vokali au Voyel Fupi katika Sura Ya Al-Ikhlas. Kama tulivyoona kwamba Alama Hii au Harakati hii ya KASRA ina maajabu maajabu. Tumeiona Ni Ya kwanza katika Aya tilizozitaja hapa Juu na Sasa tuichunguze katika Sura Ya Al-Ikhlas.
MAAJABU YA ALAMA YA VOKALI AU VOYELI AU HARAKA INAYOJULIKANA KAMA KASRA KATIKA SURA YA AL-IKHLAS
سُوۡرَةُ الإخلاص
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
Sura Hii imeshushwa ili kuwajibu makafiri walipomuuliza mtume ﷺ kuhusu Mwenyeezi Mungu ni nani? Sura ikashushwa kuwajibu suala hilo. Sura inahusu kumpwekesha Mwenyeezi Mungu. Angalia Maajabu Kuna Alama ya KASRA moja tu katikati ka SURA hii je unaiona? ipo chini ya Herufi LAM ya neno يَلِدۡ herufi hii inatamkwa “LI” kwa ajili ya hiyo KASRA. KASRA ipo katikati chini ya Herufi Lam na matamshi ni “LI” Hebu tuchunguze zaidi. Alama hii ni kama inazungumza Kwani Sura Hii inampwekesha Mwenyeezi Mungu na Alama Hii ni Moja tu. inathibitisha kwamba Mwenyeezi mungu ni Mmoja tu peke yake. Sasa tuiangalie vizuri. Ngoja Nisogeze Darubini tuone Vizuri. Katika Sura Hii Jumla ya Herufi za Upande wa Kushoto wa Herufi hii ya LAM ambayo imetiwa KASRA ni 23 na Herufi za Upande wa kushoto wa Herufi Hii ya LAM ambayo imetiwa KASRA ni 23 pia. Angalia Maajabu. Yaani Alama ya KASRA chini ya herufi Lamu inatupa Maajabu Mengineyo. Imegawa Aya za Sura Hii kiherufi. Yaani herufi 23 kushoto na herufi 23 kulia. Haya kweli siyo madogo. Huenda kuna Siri ngoja tuendelee na Safari hii huenda Mwenyeezi Mungu atatufunulia mengineyo. Hebu tuchunguze zaidi. Maneno pia Yamegawanywa. Kushoto kuna maneno Saba na Kulia Kuna maneno Saba pia!!!!! Angalia Maajabu. Herufi Lamu imefanya Kazi ya Kugawa Herufi Na maneno sawasawa. Yaani Herufi na maneno upande wa kushoto na kulia wa Herufi Lam ambayo imetiwa Alama ya Kasra ni sawa sawa utafikiri Computer imefanya hivyo. Haya siyo madogo. hebu tuendelee kwani kuna Mengi ya Ajabu yanakuja mbele.
Ajabu ni kwamba Binaadamu ameumbwa na Chromosomes 46. Mbegu za Mama ni 23 na Baba 23. Kila kiumbe kina Mbegu zake tofauti na Kiumbe kingine. Nimegusia katika Milango ya Webiste hii kuhusu Mbegu hizi za Binaadamu na baadhi ya viumbe vinginevyo. Kwa hiyo ukichunguza Namba 23 za upande wa Kushoto wa Herufi LAM iliyotiwa KASRA katika Sura hii ya Al-Ikhlas utaona Maajabu mengine yanayojitokeza. Mtume ﷺ alipoulizwa Suali na Makafiri Kuhusu Dhati ya Mwenyeezi Mungu au asili yake ni nini au ukoo wake ni upi kwani hao Makafiri hao walikuwa wakifikiri Mwenyeezi Mungu ni sawa na Binaadamu basi Mwenyeezi Mungu akashusha Jibu kwa Njia ya Sura Hii. Kwani alipojibu Suala lao kwa kusema kwamba “Mwenyeezi Mungu ni mmoja, Hategemei na Amejitosheleza, Hakuzaa na Hakuzaliwa na Hakuna Mfano wake na chochote” Jawabu hili linatosha Kujibu Suali la makafiri lakini Aya hizi zimebeba Siri nyinginezo ambazo tunazigundua siku za leo kama kwamba Mwenyeezi Mungu alikuwa akisema kwamba
“Yeye hana Mfano na siyo kama Binaadamu ambaye nimemuumba kwa njia ya Manii ambayo asili yake ni Chromosomes 23 za baba na 23 za Mama”. Aya hizi hazikusema habari hizi za Chembe cha uzazi kiwaziwazi (Chromosomes) lakini zimebeba habari hizi kiajabu sana kwa njia ya Hesabu. Na hii imekuwa Muujiza mkubwa katika Karne yetu hii ya leo ambayo imajaa elimu za Sayansi. Kwa hiyo ukifikiri utaona Kama kwamba Mwenyeezi Mungu alikuwa an maana hiyo kutufahamisha kwamba Yeye hana mfano wa chochote lakini nyinyi nimewaumba kwa chembe za uzazi 23 za Baba na 23 za Mama.
15/10/2022
Alhamdulilah leo siku ya Jumamosi Tarehe 15/10/2022 Nia yangu ni kuendelea na Muujiza wa Sura Ya Al-Ikhlas niliyoanza kuelezea hapa Juu. Na Pia Sura za Al-Falaq na Al-Nas.
Kama tulivyoona hapa Juu kwamba Sura Hii imegawanyika katika Mafungu mawili kwa Herufi ya Al-am ambayo imetiwa KASRA.
Tumeona kwamba Jumla Herufi ambazo zipo upande wa kushoto wa Herufi Ya Al-Lam ambayo imetiwa Kasra chini yake ni 23 na zile Herufi ambazo zipo Upande wa Kulia wa herufi ya Al-Lam pia 23
Hii namba 23 pia tunaikuta tena imetajika kiajabu sana. Hebu tuchunguze zaidi.
Ukihesabu Herufi za kiarabu za Kisasa kuanzia Mwanzo mpaka Herufi ya Al-Lam utaikuta Herufi hii ni ya 23 pia.
Kwa hiyo Herufi Ya LAM Katika Mpangilio wa Herufi za Kiarabu za Kisasa (HIJAI SYSTEM) yaani kuanzia A mpaka Z yaani Kiarabu Alif mpaka Herufi ya “Yaa” utaikuta Lam ni ya 23 pia!!!!!
Je unaona Muashirio wa Kiajabu yaani Inaashiria Chromosomes za Binaadamu. Hebu tuendelee na Safari ya Uchunguzi. Sasa Tuchunguze Uhusiano baina ya Lam hii ya katikati na Lamu za nyuma na mbele yake.
INAENDELEA HAPA CHINI
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
Tukichukulia kipimo cha idadi ya herufi za Jina la mwenyeezi Mungu اللّٰه ambalo lina Herufi NNE na kwa hiyo hebu tuhesabu herufi za LAM nyuma na Mbele ya LAM ilityotiwa KASRA katika Sura ya Al-Ikhlas mara 4
Upande wa kushoto kuna Lam ya 4 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Upande wa kushoto kuna Lam ya 8 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Upande wa kushoto kuna Lam ya 11 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Yaani uhesabu kuanzia LAM iliyotiwa KASRA jumla ni LAM 4
Sasa tujumlishe LAM hizi Nne
4 + LAM 8 + LAM 11=23
Je unaona Tunapata LAM 23!!! Tunapata tena namba 23
Sasa tufanye hivyo hivyo upande wa Kulia.
Upande wa kulia kuna Lam ya 4 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Upande wa kulia kuna Lam ya 8 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Upande wa kuliakuna Lam ya 11 Kuanzia LAM iliyotiwa KASRA
Sasa tujumlishe LAM hizi Nne
LAM 4 + LAM 8 + LAM 11=23
Je unaona Tunapata LAM 23!!! Tunapata tena namba 23!!!!
Je unaona Maajabu.
Kila Upande tumehesabu herufi za LAM. Katika upande wa kushoto kuanzia LAM iliyotiwa KASRA na Upande wa Kulia hivyo hivyo na baada ya kuzijumlisha tumepata Namba 23!!!
Katika Sura Hii ya Ikhlas Herufi Ya Kwanza ni QAF na Ya Mwisho ni DAL, Katika Mpangilio wa Herufi za ABJAD (ABJAD System) Herufi Ya QAF ni ya 19 na Herufi Ya DAL ni ya 4 tukijumlisha 19 + 4 tunapata Jawabu 23 !!!!!
Allahu Akbar Angalia Maajabu Namba 23 ilivyokariri.
haya siyo madogo hata kidogo. Namba za Kiajabu sana tena sana. Inaashiria Chromosomes tena zaidi ya Mara moja Allahu Akbar.
Katika Lugha ya Kiarabu Mpangilio wa Herufi zake wa kisasa ni tofauti na hapo zamani. Na Tukichunguza Sehemu au Positions za Herufi hizo za zamani zinazojulikana kama ABJAD Syatem kisha tukipachika katika Sura hii tutapata maajabu mengine makubwa ya kushangaza.
Ukipachika Namba hizi katika Sura Hii utashangaa kupata maajabu mengine. Kwa mfano Neno قُلۡ litakuwa 19 + 12 na hivyo hivyo ukigeuza Herufi zote katika namba utapata Jumla ya Namba katika Upande wa Kushoto wa Herufi Ya LAM iliyotiwa KASRA ni 198 na katika Upande wa Kulia wa Herufi ya LAM iliyotiwa Kasra ni 198 pia!!! sasa mbona namba hizi zinafanana kiajabu sana utafikiri zilipimwa na Computer. Kila Mfano unashagaza. Mbona Namba hizi zinalingana sana kiajabu sana tena sana.
Lenye kushangaza zaidi ni kwamba Namba tuliyopata ya 198 kila upande inaashiria Jumla ya Herufi za Sura Tatu yaani
Sura Ya ALIKHLAS ina Herufi 47
Sura Ya Al-Falaq ina Herufi 71
Na Sura ya Al-Nasi ina Herufi 80
Tukijumlisha tunapata maajabu. (47 + 71 + 80=198!!!)
Allahu Akbar. Allahu Akbar. Angalia Maajabu. Tumepata namba 198 na Namba hii ni Jumla ya Sehemu au Positions za Herufi za Sura Ya Al-Ikhlas. ambayo tumeona Hapa juu ni 198
Je kuna Siri gani katika Namba 198? Inaashiria Jumla ya herufi za Sura Zote Tatu. Labda Linaashiria Uhusiano wa Sura Hizi tatu. Na ikiwa ni hivyo basi inakubaliana na Hadithi tulizosoma hapa juu kuhusu Sura Hizi tatu na umuhimu wake. Hizi Sura Zimeficha Makubwa. Udugu wa Sura Hizi tatu unathibitika na hadithi tuliyoisoma haa juu kuhusu Mtume alikuwa akizisoma Sura Hizi tatu kabla ya Kulala na kisha kujipaka Mwilini. Allahu Akbar. Kwa kweli kuna Mengi bado hatujui. Na Mwenyeezi Mungu ni Mkubwa Sana. Kuruani imeficha Makubwa yasiyo na Mfano.