SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Prophetic Medicine

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

VIUMBILE VYA MWENYEEZI MUNGU

Mwenyeezi Mungu ameumba viumbe vyake kwa hekima anayoijua yeye mwenyewe peke yake. Binaadamu, Wanyama, Mimea na Kila Kitu Ulimwenguni vimeumbwa katika vipimo vya hali ya juu na vya kupendeza sana na angependa angegeuza viumbe vyake katika sura na Hekima anayojua yeye Mwenyewe peke yake.

Mwenyeezi Mungu anasema katika Sura Ya Al-Infitar Namba 82 Aya Namba 6 mpaka 8

يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡڪَرِيمِ (٦) ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّٮٰكَ فَعَدَلَكَ (٧) فِىٓ أَىِّ صُورَةٍ۬ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ (٨)

TAFSIRI

6. Ewe mwanaadamu! Ni nini kikudanganyacho na Mola wako Mtukufu (hata ukamuasi)

7. Aliyekuumba na kukutengeneza, kisha akakulinganisha sawa 

8 . Katika sura yoyote Aliyoipenda Amekutengeneza.

MABADILISHO YA HATARI

Kubadili Umbile kunaweza kusababisha Matatizo yasiyo na Dawa yeyote.

Suala la Kwanza.

Siku za leo Wataalamu wameendeleza Suala la Urembo kwa kutumia Viombo vya Kisasa na  kubadili Miili kwa Kuichora kwa kutumia  LASER. Michoro hiyo inajulikana kama TATOO. 

Suala La Pili

Kufanya Mwanya katika Meno ili kuzidisha Uzuri. (Beutification)

Suala La Tatu

Kubadili Rangi ya Macho kwa kutumia LASER (kama vile kubadili Rangi Nyeusi kuifanya Blue).

Suala La Nne

Kuvaa Nywele za Bandia

Suala la Tano

Kubadili Rangi Ya Ngozi kwa kutumia Madawa.

Suala la Sita

Kubadili Umbile kama vile Mwanamke au Mwanamume Kwa kutumia Madawa Ya Hormones. 

Suala La Saba

Kubadili Mimea (Vyakula Vya Asili). Kwa Sababu zisizo na Msingi.

Na Kuna Mifano mingine mbali mbali ya aina hii. Binaadamu wanataka kugeuza maumbile kwa sababu zisizo na maana yeyote. Kwa Kweli Ni Hatari Sana. 

USHAHIDI WA HADITHI ZA MTUME 

HADITHI 1

عن ابن عمر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم لعن الواصلة والمستوصلة والواشمة والمستوشمة ‏(‏‏(‏متفق عليه‏)‏‏)‏‏.‏

Hadithi  hii ambayo imekusanywa na Sahih Muslim na Bukhari ipo katika Riyad as-Salihin namba 1645

TAFSIRI

Mtume Wa Mwenyeezi Mungu amemlaani Mtengenezaji na Mwenye Kuvaa Nywele za Bandia. Wenye Kufanya Tatoo na Wenye Kufanyiwa Tatoo.

HADITHI YA 2

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، وَعُثْمَانُ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، – وَاللَّفْظُ لإِسْحَاقَ – أَخْبَرَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ وَالنَّامِصَاتِ وَالْمُتَنَمِّصَاتِ وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ ‏.‏ قَالَ فَبَلَغَ ذَلِكَ امْرَأَةً مِنْ بَنِي أَسَدٍ يُقَالُ لَهَا أُمُّ يَعْقُوبَ وَكَانَتْ تَقْرَأُ الْقُرْآنَ فَأَتَتْهُ فَقَالَتْ مَا حَدِيثٌ بَلَغَنِي عَنْكَ أَنَّكَ لَعَنْتَ الْوَاشِمَاتِ وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ وَالْمُتَنَمِّصَاتِ وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ وَمَا لِيَ لاَ أَلْعَنُ مَنْ لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ فِي كِتَابِ اللَّهِ فَقَالَتِ الْمَرْأَةُ لَقَدْ قَرَأْتُ مَا بَيْنَ لَوْحَىِ الْمُصْحَفِ فَمَا وَجَدْتُهُ ‏.‏ فَقَالَ لَئِنْ كُنْتِ قَرَأْتِيهِ لَقَدْ وَجَدْتِيهِ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏{‏ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا‏}‏ فَقَالَتِ الْمَرْأَةُ فَإِنِّي أَرَى شَيْئًا مِنْ هَذَا عَلَى امْرَأَتِكَ الآنَ ‏.‏ قَالَ اذْهَبِي فَانْظُرِي ‏.‏ قَالَ فَدَخَلَتْ عَلَى امْرَأَةِ عَبْدِ اللَّهِ فَلَمْ تَرَ شَيْئًا فَجَاءَتْ إِلَيْهِ فَقَالَتْ مَا رَأَيْتُ شَيْئًا ‏.‏ فَقَالَ أَمَا لَوْ كَانَ ذَلِكِ لَمْ نُجَامِعْهَا ‏

TAFSIRI-(ENGLISH) Mungu akipenda nitaifasiri kwa kiswahili baadaye)

Abdullah reported that Allah had cursed those women who tattooed and who have themselves tattooed, those who pluck hair from their faces and those who make spaces between their teeth for beautification changing what God has created. This news reached a woman of the tribe of Asad who was called Umm Ya’qub and she used to recite the Holy Qur’an. She came to him and said: What is this news that has reached me from you that you curse those women who tattooed and those women who have themselves tattooed, the women who pluck hair from their faces and who make spaces between their teeth for beautification changing what God has created? Thereupon ‘Abdullah said: Should I not curse one upon whom Allah’s Messenger (ﷺ) has invoked curse and that is in the Book also. Thereupon that woman said: I read the Qur’an from cover to cover, but I did not find that in it. whereupon he said: If you had read (thoroughly) you would have definitely found this in that (as) Allah, the Exalted and Glorious, has said:” What Allah’s Messenger brings for you accept that and what he has forbidden you, refrain from that.” That woman said: I find this thing in your wife even now. Thereupon he said: Go and see her. She reported: I went to the wife of ‘Abdullah but found nothing of this sort in her. She came back to him and said: I have not seen anything. whereupon he said: Had there been anything like it in her, I would have never slept with her in the bed.

Aya Za kuruani zinatuhimiza Tutii maamrisho ya Mtume Mohamad ﷺ Mweyeezi Mungu anasema:

Sura Ya Al-Nisaa Aya Namba 59

يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَأُوْلِى ٱلۡأَمۡرِ مِنكُمۡ‌ۖ فَإِن تَنَـٰزَعۡتُمۡ فِى شَىۡءٍ۬ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأَخِرِ‌ۚ ذَٲلِكَ خَيۡرٌ۬ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلاً (٥٩) 59.

TAFSIRI 

Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyie (Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitalifiana juu ya jambo lo lote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa.

Na Pia anasema 

AL-Hashr Namba 59 Aya Namba 7

مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَـٰمَىٰ وَٱلۡمَسَـٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ كَىۡ لَا يَكُونَ دُولَةَۢ بَيۡنَ ٱلۡأَغۡنِيَآءِ مِنكُمۡ‌ۚ وَمَآ ءَاتَٮٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَہَٮٰكُمۡ عَنۡهُ فَٱنتَهُواْ‌ۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ (٧) 1·

TAFSIRI

Mali Aliyoleta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ( vilivyo karibu na Madina) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.(Basi yatatumika kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu), na kwa ajili ya Mtume (wake, basi atachukua mwenyewe) na jamaa (zake) na mayatima na maskini na msafIri aliyekuwa katika shida, ill wasiwe kinyang’anyiro baina ya matajiri wenu tu. Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na muogopeni Mwenyezi Mungu; kwa yakini Mwenyezi Mungu ni. Mkali wa kuadhibu

Aya mbili hizi zinatuamrisha tutii amri ya Mtume ﷺ wake.

SAYANSI ZINATHIBITISHA MAAMRISHO YA MTUME ﷺ 

Madakitari na Wataalamu mbali mbali wanazungumzia masuala haya kiajabu sana na bila wao kujua kwamba Mtume Mohamad aliyakataza. kuanzia Karne  14 zilizopita. Yaani katika karne ya 7.. Sasa Mtume ﷺ alisomea wapi Elimu hizi ambazi zinahitaji Vyombo vya utafiti wa hali ya juu. Hii inathibitisha Utume wake. Na kwamba alikuwa akipewa Wahyi (Revelation yaani Alikuwa akifunuliwa na Mwenyeezi Mungu).

SUALA LA KWANZA-TATOO NA HATARI ZAKE

Tatoo haikuanza leo bali zamani sana na Hata Mtume ﷺ aliizungumzia ijapokuwa imekuwa mashuhuri hivi karibuni  kwani imeendelezwa kiasi ambacho vyombo mbali mbali vya hali ya juu kama vile LASER vinatumika katika kuchora michoro ya aina hii katika Ngozi za Binaadamu.

Tunaambiwa na Madakitari na Wataalamu hatari za michoro hii katika kusababisha Maradhi mbali mbali kama vile Cancer ya Ngozi, Kuvunja Nguvu za “Mfumo wa Kinga”  (Immune System), na Maradhi mengineyo ambayo yanaweza kusababishwa na ule Wino ambao hakuna nayejua iwapo nik Msafi. Ukiwa umebeba Vijidudu basi unapochorwa inakuwa njia rahisi ya kuwaingiza mwilinui mwako. Ndugu Waislamu Kueni Macho sana na Haya Maendeleo yenye kuweza kuleta hatari. Usifuate Nyuki  hovyo hovyo ili upate asali kwani wakati mwingine utajikuta umeelekezwa katika tundu la nyoka. 

Sikiliza Maneno yanayotoka kutoka kwa wataalamu na Tafsiri Yake kwa Kiswahili. Allahu Akbar. Inathibitisha Maonyo ya Mtume ﷺ Allahu Akbar. 

(A recent report from the European Commission warns that tattoo ink often contains “hazardous chemicals” such as heavy metals and preservatives that could have serious health consequences, including bacterial infections)

(Ripoti ya hivi majuzi kutoka Tume ya Ulaya inaonya kwamba wino wa tattoo mara nyingi huwa na “kemikali za hatari” kama vile metali (metals)nzito na vihifadhi (presevartives) ambavyo vinaweza kuwa na madhara makubwa ya afya, ikiwa ni pamoja na maambukizi ya bakteria)

(A separate study issued earlier this month by the Australian government reveals that 22% of the inks tested contained chemical compounds known to cause cancer)

Utafiti mwingine uliotolewa mapema mwezi huu na serikali ya Australia unaonyesha kuwa 22% ya wino zilizojaribiwa zilikuwa na misombo (compounds) ya kemikali inayojulikana kusababisha saratani.

(Tattoos work by injecting the ink into the second layer of skin known as the dermis, where the ink remains permanently unless it is removed using laser technology)

Tattoo hufanya kazi kwa kuingiza wino kwenye safu ya pili ya ngozi inayojulikana kama dermis, ambapo wino hubakia milele isipokuwa kuondolewa kwa teknolojia ya leza.(Na hata hivyo haiondoki yote na baadhi yake inakwenda katika Lymph Nodes)

(“Where does the pigment go?” The pigment may still be there, and that it could be toxic”)

“Tunataka kujua Kuhusu wino,”  “Pigment inakwenda wapi?”  rangi hiyo inaweza kuwa bado iko, na kwamba inaweza kuwa na sumu.

“The composition of tattoo ink has changed over time so it also means that new and potentially dangerous agents could be introduced into tattoo ink at any time,”

“Muundo wa wino wa tattoo umebadilika kwa wakati, kwa hivyo inamaanisha kuwa madawa mengineyo mapya ya kisasa yenye hatari yanaweza kuingizwa kwenye wino wa tattoo wakati wowote.”

Tunaambiwa na wataalamu kwamba “Mfumo wa Kinga” (Immune System). Utafanya Kazi kubwa katika kuulinda mwili kwa kushughulika na chochote kigeni kinapoingia mwilini kama vile ndani ya Ngozi na pia sehemu nyinginezo ndani ya mwili.

White Cells  (Celi Nyeupe) na System nyinginezo mwilini ambazo ni Askari wa kuulinda mwili hufanya kazi kubwa kuondoa chochote kigeni katika mwili wako kama vile Wino wa Tattoo unapoingizwa kwa ajili ya marembo.

System hizo ambazo zimepewa kazi hiyo ya kuulinda mwili zitakuwa zinashughulishwa bila sababu muhimu na na kazi hiyo ya kuondoa Wino huo kwa kiasi ambacho Mwili unakua na kinga Dhaifu katika  kuulinda mwili kwa kupigana na Vijidudu vinginevyo ambavyo vina hatari zaidi kuliko Wino.

Kwani Askari wa mwili wako kama vile White Cells hazijui kutofautisha kati ya Wino wa Marembo na Vijidudu vinginevyo. Ijapokuwa kuna Utafiti mbalimbali ambazo nyinginezo zinapinga Hatari hizi kwa hoja zisizo na Msingi wowote.

Wataalamu wamegundua Takataka za Wino wa Marembo katika Sehemu za Lymph za mwili wa Binaadamu.

Immune System au Mfumo wa Kinga umekusanya Vifaa Mbalimbali vyenye kufanya kazi ya kuulinda mwili wako. kwa lugha nyingine ni  Askari wa Mwili. Vifaa Vikubwa ni kama vufuatavyo:

White blood cells, Antibodies, The Complement System, The Lymphatic System, The Spleen, The Thymus, and The Bone Marrow

Na Kazi kubwa Ya vifaa hivi ni kusafisha taka taka katika mwili wa Binaadamu  ni kama vile Seewage System.Kwa Mfano  Lymph System ina Vifundo Vidogo vidogo vinavyojulikana kwa jina kama Lymph Nodes na kazi yake kubwa ni Usafishaji Mwilini. Soma Definition ya Lymph Nodes hapa Chini:

A small bean-shaped structure that is part of the body’s immune system. Lymph nodes filter substances that travel through the lymphatic fluid, and they contain lymphocytes (white blood cells) that help the body fight infection and disease.

Kwa hiyo Nasiha iliyo nzuri tumfuate Mtume Mohamad ﷺ kwani Maneno na Vitendo Vyake sio Bure Bure bali Ni Wahyi (Revelation) Kutoka kwa Mwenyeezi Mungu kwa hiyo msibabaike na Wataalamu wengine ambao wanababaika na hata hao hawajui huo Wino wa Mrembo unapokwenda ndani ya mwili wa Binaadamu.