UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
SWAHILI LANGUAGE/LUGHA YA KISWAHILI
I believe the videos speak for themselves and no need for English translation.
05/09/2022
Alhamdulilah Hivi sasa ni Saa nne za Usiku na Katika wakati huu ambao kuna kimya na utulivu nimeona bora nikusanye Video nilizoziona hivi Karibuni ambazo nzuri sana. Kuruani kwa pamoja. Mwenyeezi Mungu awabariki watoto wote hawa. Amin
——————–
Video za Dua na Kuruani hapa chini nilizipenda na nikaona bora nizikusanye na kuzihifadhi katika website hii. Kuna Video za Kutoka Nigeria, Senegal na kama sikosei Nchi nyingine za West Africa. Nimepata Video Moja tu ya Watoto wadogo hapo Zanzibar ambayo inatuonyesha namna Wanavyofundisha Watoto ambao bado wapo darasa la chini au wale ambao bado hawajaanza kusoma Kuruani yaani Mwanzoni. Video zote nzuri sana. Ni Kumbukumbu ya maisha. Allahu Akbar.
Tangu Enzi Ya Mtume mpaka leo hivi ndivyo Quran inavyohifadhiwa kimoyomoyo. Na hivi ndivyo Mwenyeezi Mungu alivyotaka ifanyike. Ni Njia pekee ya Kuihifadhi Kuruani. Hakuna anyeweza au aliyeweza kuigeuza Kuruani. Kuruani Imehifadhiwa. Ikitokea mtu yeyote akafanya utundu katika kugeuza chochote katika Msahafu bali utakosolewa kwani ipo moyoni. Haiwezekani Kuigusa hata kidogo. Angalia watoto wanavyohifadhishwa. Hata Watoto wapo Tayari Kusahihisha makosa licha Watu wakubwa. Angalia Muujiza. Huu siyo Muujiza Mdogo. Mwenyeezi Mungu amesema katika Kuruani kwamba Ataihifadhi Mwenyewe sasa unaona anavyoihifadhi? Allahu Akbar.
QURAN-NIGERIA
DUA ZA WATOTO (WEST AFRICA)
QURAN WATOTO (WEST AFRICA)
QURAN WATOTO (WEST AFRICA)
QURAN WATOTO (WEST AFRICA)
QURAN WATOTO (WEST AFRICA)
QURAN WATOTO (ZANZIBAR).
MADRASA ALGERIA MWAKA 1928