UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
RAMANI YA WEBSITE HII
Alhamdulilah leo Tarehe 05/11/2022 nakukaribisheni tena kwa mikono miwili katika Website hii ili tushirikiane katika Utafiti wa Kuruani Tukufu.
Hapo Mwanzoni Nilikuwa Naandika Muhtasari wa Habari mbalimbali wa kila Utafiti katika Website Hii. Nilifanya hivyo katika Mlango wa Kwanza wa “ELIMU” Na kisha Mlango wa “MUHTASARI WA UTAFITI-1. Kwa hiyo leo hii Nimefungua Mlango huu wa RAMANI YA UTAFITI-1 ili kuwaongoza Wasomaji katika kila Ninachoandika kwa kila Mara. Hakuna Tofauti Milango Hii yote Mitatu lengo lilikuwa ni Kuwaongoza Wasomaji katika Kutafuta Topic au Utafiti Mbalimbali.
Kwa sasa Nimeona Bora Nisifungue Milango Mipya lakini Nitakuwa Nikiongeza Mapya katika Milango Iliyopita kwani Bado kuna Nafasi Nyingi huko.
Kwa hiyo Ramani hii Itasaidia Kwa Kila Jipya. Kwa kweli Kuna Miujiza Mingi sana ambayo Mwenyeezi Mungu akinipa Nafasi Nitaiandika kwa hiyo Karibu Usome Maajabu yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
05/11/2022
1-Alhamdulilahi Leo Nimeongeza Utafiti Mbili katika Mlango wa
“DARASA ZA WIKI-1”
Utafiti wa Kwanza unahusiana na WAHYI (Revelation) Ya Kuruani kwa Mtume Mohamad ﷺ Muujiza wa Miaka 40
Na Utafiti wa Pili unahusu Sura Ya Al-Fil (The Elephant) Muujiza Wa Uzito wa Mtoto wa Tembo na Muda anapokuwa katika Tumbo la Kizazi yaani kabla ya Kuzaliwa. Allahu Akbar.
20/11/2022
Alhamdulilah Leo nimeongeza Muujiza wa Aya inayohusiana na Nyuki katika Mlango wa
“MAAJABU YA KURUANI-1” Habari hizi zinahusiana na NUQTA na maajabu yake.
Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kuniwezesha Kuongeza Muujiza Mwingine wa Pili. Unaohusiana na Siku ya Laylatu-Alqdr. Utafiti wa Swahaba Ibn Abbas na Kisha Utafiti wa Wanavyuoni wa Kisasa katika Kuitafuta Siku Hiyo. Nimeelezea Habari hizi kwa urefu katika Mlango huu huu wa “MAAJABU YA KURUANI-1”
Alhamdulilah namshukuru Mwenyeezi Mungu kuongeza Muujiza wa Tatu katika Mlango Huu huu wa MAAJABU YA KURUANI-1 Muujiza Huu unahusikana na Kometi inayorudi na kuonekana na watu wanaoishi Ardhini kila baada ya Miaka 76. Allahu Akbar. Kwa kweli Kuruani Ni Muujiza Mkubwa sana. Soma Maajabu haya Mapya.
MWAKA MPYA WA 2023
07/01/2013
Salaam Nyingi Kwa Ndugu Wasomaji wa Website Hii. Nakutakieni kila la kheri na Baraka katika Mwaka Huu Mpya wa 2023. Mda mrefu umepita na sikuweza kuwaandikia Mapya. Kwa kweli nilikuwa nimeshughulishwa na Utafiti Mbalimbali unaohusiana na Kuruani Tukufu na Kwa kweli Nimesoma Mengi ya Maajabu ambayo yatakushangaza sana. Katika Utafiti Mbalimbali ambao watafiti wengi wameshiriki nilishangaa sana tena sana kusoma kwao maajabu yasiyo na mwisho katika Kuruni. Mwenyeezi Mungu akipenda na nikipata nafasi nitaanza kuwajuulisha Maajabu haya yasiyo na Mwisho. Haya Mambo hayana mwisho na ni makubwa. Kuruani inatosha kuthibitisha kwamba Maneno ya Kuruani ni ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Haiwezekani kuwa ni Maneno ya Binaadamu hata kidogo. Ninarudia tena kusema kwamba Kuruani siyo maneno madogo hata kidogo. Ni Muujiza Mkubwa sana tena sana. Tujifunze Kuruani na Kisha Tuifuate. Hakuna Ujanja Mwingine wowote.
Elimu zote Duniani zipo chini ya Kuruani.
Kama una PHD zako ulizopata kutoka katika University yeyote ile Duniani tafadhali kaa ukielewa kwamba Kama huamini na hufuati kuruani basi huna chochote na unajinyima Elimu kubwa sana. Na Utabaki na ujinga mpaka mwisho wa maisha yako. Fumbua Macho.
Alhamdulilah Leo Nimeelezea Habari mbili zifuatazo katika Mlango wa
“MAAJABU YA KURUANI-1”
1/NAMBA Pi “π” NA MAAJABU YAKE KATIKA KURUANI TUKUFU
2/MAAJABU YA IDADI ZA HERUFI KULINGANA NA IDADI ZA AYA ZA KURUANI TUKUFU
Na Mwenyeezi Mungu akipenda kwa Munasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao utaanza mwezi wa March 2023 nitaanza kudokeza mapya kwa hiyo ningekushauri kwanza uje katika Ramani Hii kwa kila Jipya nitakaloongeza ili upate kuelewa sehemu ambayo nitaelezea habari hizo
26/02/2023
Alhamdulilah leo Nimefungua Mlango Mpya wa “Ramadhani-2023” ambao utakusanya Mada Mbali kuanzia Leo kwa Munasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Yenye Uhusiano na Namba za Aya za Kuruani zenye Kuashiria Miji iliyotajwa katika Aya hizo. Nakukaribisha katika Mlango huo kwa marefu zaidi.
Katika siku ya leo nimezungumzia Muujiza wa Longitude na Latitude katika Baadhi ya Aya Za Kuruani.
09/04/2023
Alhamdulilah Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kuniwezesha siku ya leo kuelezea Miujiza Miwili mifupi katika Mlango wa “Ramadhani-2023”
Muujiza Wa Kwanza Ni Muashirio wa Kiajabu Katika Aya Namba Mbili ya Sura Ya Al-Kawthar, Muashirio wa Mwezi wa 12 unaojulikana kama Dhulhijja.
Na Muujiza wa Pili unahusiana na Umbali baina Ya Jua Na Ardhi ambao umeshiriwa kiajabu sana katika Sura Ya Al-Shams. Allahu Akbar. Maelezo zaidi yapo katika Mlango huo. Allahu Akbar.
20/02/2025,
Nimeanza kukusanya Dhana mbalimbali potofu zinatokana na kutokufahamu vizuri kwa Aya za Qur’an katika Mlango wa UTAFITI-8. Kwa sasa nimeandika kwa lugha ya kiingereza na Inshaallah nimenuia kuifasiri katija lugha ya kiswahili na nyinginezo Mwenyeezi Mungu akipenda.
I started writing an article about misconceptions in the Quran on page UTAFITI-8 in English. I plan to translate it into other languages later, if Allah wills.