UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
ELIMU YA MAWINGU KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU
Sura Namba 78 Aya Namba 13
(وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا * وَأَنْزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا) [النبأ: 13-14].
TAFSIRI
13. Na tukaifanya taa ing’arayo na yenye joto kubwa (And made [therein] a burning lamp, And sent down, from the rain clouds, pouring water)
Sura Namba 30 Aya Namba 48
اللَّهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَاباً فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاء كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفاً فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ) [الروم: 48].
TAFSIRI
48.Mwenyezi Mungu ndiye Anayezileta pepo zikaharikisha mawingu, kisha Akayatandaza (hayo mawingu) mbinguni kama Apendavyo, na Akayafanya mapande mapande, kisha unaona mvua ikinyesha ndani yake; na Anapoifikisha kwa awatakao katika waja wake, mara utawaona wamefurahi. (It is Allah who sends the winds, and they stir the clouds and spread them in the sky however He wills, and He makes them fragments so you see the rain emerge from within them. And when He causes it to fall upon whom He wills of His servants, immediately they rejoice)
Sura Namba 24 Aya Namba 43
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يُزْجِي سَحَابًا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيْنَهُ ثُمَّ يَجْعَلُهُ رُكَامًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مِنْ جِبَالٍ فِيهَا مِنْ بَرَدٍ فَيُصِيبُ بِهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَصْرِفُهُ عَنْ مَنْ يَشَاءُ يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ يَذْهَبُ بِالْأَبْصَارِ) [النور: 43]
TAFSIRI
43· Je, huoni ya kwamba Mungu Anayaendesha mawingu, kisha Huyaambatisha pamoja, kisha huyafanya mirundi? Basi utaona mvua ikitoka katikati yake; Naye Huteremsha-kutoka juu katika milima ya mawingu-mvua ya mawe, akamsibisha nayo amtakaye na kumuepusha nayo Amtakaye; hukurubia mwanga wa umeme wake kupofoa macho. (Do you not see that Allah drives clouds? Then He brings them together, then He makes them into a heap, and you see the rain emerge from within it. And He sends down from the sky, Mountains (Clouds like Mountains) within which is hail, and He strikes with it whom He wills and averts it from whom He wills. The flash of its lightening almost takes away the eyesight).
Sura Namba 13 Aya Namba 12
(هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفاً وَطَمَعاً وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ) [الرعد: 12]
TAFSIRI
I2. Yeye ndiye anayekuonyesheni umeme kwa (kukutieni) khofu (ya kuuawa na radi) na tamaa (ya kupata mvua); na huyaleta mawingu mazito (ya kuleta . mvua). (It is He who shows you lightening, [causing] fear and aspiration, and generates the heavy clouds).
SHEREHE YA SAYANSI ZA MAWINGU KUTOKANA NA AYA TULIZOZITAJA HAPA JUU
Katika Aya Zilizopita tonasoma kwamba Jua Ni Moja ya Sababu Kubwa zinazochangia katika Kujenga Maumbile ya Mawingu. Jua linasababisha Uvukizi wa Chembe Za Maji kutoka Katika Mabahari na Maumbile Mengineo Ya Maji kama vile Mito na Maziwa. Upepo Unasukuma Chembe Za Maji na Vumbi kukaribiana Pamoja na Kuzalisha Chembe zinayojulikana kwa Jina Kama “Aerosols” Na Msuguano baina ya Chembe hizi unasababisha kuzaliwa kwa Nyanja Za Umeme na Smaku (Electromagnetic Fields) zenye Chembe Hasi Na Chanya (Negative and Positive Particles) katika Matabaka Ya Mawingu. Upepo Unasukuma Matabaka Ya Mawingu Angani na hapo hapo matabaka haya yanaungana. Kwa kweli Kuna Mengi ambayo Bado Kueleweka na bado wataalamu wanasoma. Matokeo Ya kuungana kwa Matabaka ya Mawingu ni Kusababisha Kujengeka kwa Mirundo ya Matabaka Kila moja Juu ya lingine kama Umbile la Mlima ulivyo. Na Wingu likiwa kubwa sana linapewa na Wataalamu Jila la Cumulonimbus. Aina hizi za Wingu huwepo katika Sehemu ya Anga Karibu na Ardhi. Mvua Ya Mawe na Mingurumo ya Radi pia huzaliwa katika aina hizi za Wingu. Mawingu ya aina hii ni makubwa sana mfano wa umbile la Vilima Vya Ardhini. Katika Aya hapa Juu tunasoma pia kwamba Mwanga unatokana na Mawe (ya Mvua Ya Mawe). Herufi Ya HA katika Neno بَرْقِهِ (BARKI-HI) Katika Kipande Cha Aya يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ (YAKADU SANA BARKI-HI)Inarudi na katika neno بَرَدٍ (BARDIN) katika Aya Hii lenye maana ya Mawe (Ya Mvua Ya Mawe). kwa hiyo Mwanga wa Radi asili yake ni Mawe (ya Mvua Ya Mawe) (Kwa Kiingereza Hail).
KUJENGEKA KWA MAWINGU
Wataalamu wa hali ya hewa wamefanya utafiti wa Mawingu ya aina ya Cumulonimbus yanavyojengeka na Uhusiano wake na Mvua Ya Maji, Mvua Ya Mawe na Mwanga Wa Radi na Wamegundua kwamba Mawingu ya aina hii yanapitia hatua tatu zifuatazo katika kuzalisha Mvua
1/MAWINGU YANASUKUMWA NA UPEPO
Mapovu ya Bahari hupasuka na kusababisha Chembe za maji kurukaruka. Chembe hizi zenye Chumvi kama vile maji ya Baharini hubebwa na Upepo Kuelekea Angani. Na Hizi pamoja na Chembe za Vumbi Angani hujulikana kwa jina kama “Aerosols” Huwa kama Mitego ya maji katika kuendelea kukusanya mvuke wa maji uliopo angani na hizi ndizo huwa Chembe za Mawingu.
2.KUUNGANA KWA MAWINGU
Mawingu Yanajengeka Kutokana na Mvuke wa Maji ya Bahari au Aerosols ambazo asili yake ni Mvuke Wa Maji Ulioyayuka (Condense)Katika Fuwele za Chumvi (Salt Christals) na Chembe za Vumbi (Dust Particles) Hewani. Upepo Unachangia kusukuma Mawingu, kuunganisha na kusambazisha angani bila tatizo. Na hivyo ndivyo Mawingu yanavyopanda na kujengeka Angani.
3/KUJIPANGA
Chembe za maji ambazo zinazunguka Chembe za Chumvi na Vumbi Yaani Aerosols huendelea kujijenga na kujipanga mpaka Kuzaliwa kwa Mapande makubwa ya Mawingu. Mpangilio wa Chembe hizi kila moja juu ya lingine na kicha kila kipande cha wingu juu ya lingine Ndiyo husababisha kujengeka kwa Mawingu. Na zile Chembe ambazo nzito kuliko Hewa husababisha kumiminika Ardhini kama Mvua.
MAWE (Mvua Ya Mawe)
Mawe (Mvua Ya Mawe) ni Sababu Kubwa Ya Kusababisha Radi na Mwanga Wa Radi. Ili tupate kuelezea vizuri habari hii inatubidi tuigawe mbingu katika matabaka mawili. Tabaka la chini karibu na ardhi lenye hali ya hewa ya kawaida na tabaka la juu ambalo kuna hewa baridi sana. Kwa hiyo Mawingu yanaposukumwa na Upepo na kufikia Tabaka la Juu Basi Maji yaliyopo katika Mawiingu yataanza kuganda na hatimaye kuzaliwa kwa Chembe Chembe za Barafu. Hizi Chembe za Barafu ambazo zipo ndani ya Wingu yatakuwa katika kusuguana daima kwani upepo unachangia katika kuzisukuma sukuma . Msuguano wa Chembe hizi utasababisha Kujengeka kwa Electrical Charges (Umeme). Kwa kawaida Umeme unakuwa na Chembe Hasi Na Chanya (Negative and Positive Particles) ambazo zitagawanyika katika mafungu mawili. Zile Chembe Chanya (Positive) ambazo nyepesi kwa uzito zitapanda Juu ya Wingu na Zile Hasi (Negative) ambazo Nzito zitashuka Chini ya Wingu. Juu ya Ardhi na Kila Kilipo juu ya Ardhi kama vile Majengo, Miti na vinginevyo vyote ninakuwa na Chembe Chanya (Positive Particles) za Umeme. Katika Sayansi Tunasoma kwamba Chembe Hasi Na Chanya (Negative and Positive Particles) huvutana. Kwa hiyo Chembe zilizopo chini ya Mawingu ni Negative na Zilizopo Juu ya Ardhi ni Positive na zinapokutana Ndiyo kunatokea Mpasuko wa Mwanga Na Radi. Na Hii Ni aina ya Kwanza Ya Mpasuko Huu ambao unaanzishwa na Umeme kutoka Angani. Hii Aina Ya Kwanza tutaita NEGATIVE CHARGES FROM THE CLOUDS TO THE EARTH Aina Ya pili ni Kutoka Ardhini. Umeme wa Positive Charges Utasafiri Kutoka Ardhini na Kupanda Juu na hatimaye kukutana na Negative Charges ambazo zipo Chini ya Mawingu na Kusababisha Mwanga na Mpasuko wa Radi aina Hii tutaita POSITIVE CHARGES FROM THE EARTH TO THE CLOUD. Aina ya Tatu ni Baina Ya Wingu na Wingu. Yaani Ikiwa Wingu Moja Lina upande wake mmoja Positive Particles na lingine lina Negative Particles basi chembe hizi zitavutana na kutatokea Mpasuko na Mwanga Wa Radi aina hii ni NEGATIVE AND POSITIVE CHARGES FROM CLOUD TO CLOUD na Pia kuna aina ndani ya Wingu. Kama tunavyoelewa kwamba Ndani ya wingu kuna Negative na Positive Particles. Kuna wakati Charges zinapozidi Chembe hizi huvutana na kusababisha Mwanga na Radi ndani ya Wingu. Tunaweza kuita aina hii kama “NEGATIVE AND POSITIVE CHARGES INSIDE THE CLOUD”
Wataalamu Wa Hali ya Hewa Wamegundua na Kusoma Habari hizi zinazohusiana na Umbile na Harakati (Functions) za mawingu kwa kutumia Vyombo Vya Hali Ya Juu kama vile Ndege, Satellites, Computers, Baloons, Na Vyombo Vinginevyo vya hali ya Juu. Wamefanya utafiti katika kusoma Hewa na Mielekeo Yake (Wind Directions), Kupima Humidity (Viwango mbalimbali vya Kiasi cha Maji katika Hewa) na Kutafuta Viwango na Tofauti za Shinikizo za Hewa Angani. (Atmospheric Pressure)
AINA ZA MAWINGU NA MAJINA YAKE (BASIC TYPES)
Kuna aina Tatu za Mawingu, Cumulus, Stratus, na Cirrus
1/Cumulus hufanana na Pamba. Mawingu ya Aina Ya Cumulus ambayo yamejengeka kuwa siyo marefu kwenda Juu ni dalili ya hali ya hewa nzuri, Na zikiwa zimejengeka kwa ukubwa wa kwenda juu kama vile milima basi huenda kukawa na Mwanga, Mingurumo ya Radi na Mvua. Na Mawingu haya ya Cumulus yanakuwa karibu sana Ya Ardhi.
2/Mawingu Ya Stratus Ni sawa na Mapande ya Mawingu. Mawingu haya hukaa Mbinguni kwa muda mrefu. kwa kawaida Mawingu Ya Aina Hii Huzuia Mwanga Na kufanana na wakati wa Jioni.
3/Mawingu ya Cirrus yanafanana na Manyoya, Yanakuwa Juu sana na Yamejengeka kwa Chembe za Barafu. Yanaonyesha hali ya hewa nzuri na ya kawaida. Yanakuwa yamesambaa Angani.
AINA NYINGINEZO ZA MAWINGU
Kuna Pia Aina Nyinginezo Za Mawingu kama vile Nimbus, Cumulonimbus, Nimbostratus, na Fog Kuna Mawingu Mengine ambayo Yameongezwa neno Nimbus kama vile Cumulinimbus katika Neno Cumulus na NimboStratus katiks Neno Stratus. Jjina Nimbus lina maana ya Kunyesha Mvua.Kwa Kifupi Fog Ni Ukungu. Mawingu Ya Cumulonimbus ni mawingu yenye kuleta Mwanga, Radi na Upepo Mkali, Mvua ya Mawe na Mvua Ya Maji. Nimbostratus Ni Mawingu ambayo yanaleta Mvua inayopiga kwa muda mrefu.
CHEMBE ZA MAWE YA BARAFU (MVUA YA MAWE) Hail
Ni Chembe ndogo ndogo na kubwa kubwa za Barafu. Hail zinapokuwa Nzito au Kasi ya Upepo kuzisukuma Juu Angani inapopungua basi Hail zitaanza kuanguka ardhini kama Mvua Ya Mawe. Mgawanyiko wa Aina Za Mawingu na Sehemu Zake Angani
1/Milima Ya Juu Sana Ni Aina Tatu katika Sehemu Ya Juu Angani (High Level Clouds)
Umbali Kutoka Ardhini mpaka Chini Ya Mawingu Haya ni karibu Futi 20.000 au zaidi ya Futi hizi. (Ch ni Kifupisho chenye maana ya HIGH CLOUDS)
Cirrus -Ci
Cirrocumulus-Cc
Cirrostratus-Cs
2/Milima Ya Katikati Ni Aina Tatu , yaani Baina Ya Futi 6,500 (Mita 2,000) mpaka Futi 20,000 (Mita 6,000)(Cm ni Kifupisho chenye maana ya MEDIUM CLOUDS)
Altocumulus-Ac
Altostratus-As
Nimbostratus-Ns
3/Milima Ya Chini Ni Aina Tatu Kuanzia Chini Ya Mawingu Haya Mpaka Ardhini ni karibu Futi 6500 au Mita 2000. (Cl ni Kifupisho chenye maana ya LOWER CLOUDS)
Stratocumulus-Sc
Stratus-St
Cumulus-Cu
Cumulonimbus-Cb
MUUJIZA MKUBWA
MAONI NA SHEREHE YA ELIMU YA MAWINGU (CLOUDS) KUTOKANA NA KURUANI NA SAYANSI
Kuruani Siyo Kitabu Cha Physics au Sayansi yeyote ile bali Ni Kitabu Cha Dini Kinachokusanya Mwongozo wa Binaadamu Na Majini katika Ulimwengu. Lakini Mwenyeezi Mungu ameongeza Miujiza Mbali Mbali Ili Kututhibitishia Ukweli Wa Maneno Yake. Mwenyeezi Mungu hakutuma Mitume ili waje watufundishe Sayansi Za leo kama Vile Chemistry au Physics na Nyinginezo. Lakini Elimu hizi Zimegusiwa kiajabu sana katika Kuruani na Hii Inathibitisha Kwamba Haya yaliyopo katika Kuruani siyo maneno ya Binaadamu.
Ukichunguza Aya Zinazohusiana Na Mawingu Utaona Ni yale yale tunayofundishwa na Sayansi za leo. Allahu Akbar. Asili ya Kujengeka Kwa Mawingu, Mwanga Wa Radi, Na Radi, ni sawa sawa baina Ya maneno yaliyopo katika Aya Hizi na Sayansi. Huu Ni Muujiza Siyo Mdogo.
(وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا * وَأَنْزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا) [النبأ: 13-14].
Katika Aya hii Namba 13 na 14 ya Sura Ya Al-Nabaa Mwenyeezi Mungu ametaja kwanza Jua سِرَاجًا وَهَّاجًا na Kisha Mawingu الْمُعْصِرَاتِ Kwani Jua Ndiyo Asili ya Evaporation (Kuzalisha Mvuke Wa Maji)na Kusababisha Kujengeka kwa Mawingu kama tulivoona hapa Juu.
اللَّهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَاباً فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاء كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفاً فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ) [الروم: 48
Aya Hii Ya Sura Ya Al-Rum. Aya Namba 48 Imekusanya Sayansi Ya Hali Ya Juu katika Kujenga Mawingu. Kwanza Upepo Kusukuma Mawingu. Pili Kuyajaalia Kuwa Vipande Vipande Tatu Mvua Inatoka humo. Na haya Ndiyo tuliyosoma hapa Juu katika Sherehe ya Sayansi Upepo ni Muhimu kwani usingekuwapo basi kusingekuwa na Mawingu na wala Vipande vya mawingu na kusingelikuwa na mvua. Na hivi ndivyo Sayansi Inavyotuambia. Allahu Akbar.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يُزْجِي سَحَابًا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيْنَهُ ثُمَّ يَجْعَلُهُ رُكَامًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مِنْ جِبَالٍ فِيهَا مِنْ بَرَدٍ فَيُصِيبُ بِهِ مَنْ يَشَاءُ وَيَصْرِفُهُ عَنْ مَنْ يَشَاءُ يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ يَذْهَبُ بِالْأَبْصَارِ) [النور: 43]
Aya Hii kutoka Katika Sura Ya Al-Nuur Namba 43 Inaelezea Sayansi Ya hali ya Juu. Kwanza Kusukuma Mawingu, Pili Kuyaunga na Kuyajenga na Tatu Kuyajaalia Mrundo kama Vile Kilima (Moja baada ya Lingine). Na Mvua itatoka humo na La Kushangaza zaidi Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba Mvua Hiyo itapiga kutoka katika Mawingu Makubwa Mfano wa Milima جِبَالٍ Yaani Neno Hili lina maana ya Majabali. Sasa Mtume aliona Vipi Wingu mfano wa Jabali? Je huoni Muujiza Mkubwa kama Huu. Ili kuona Wingu mfano wa Mlima itabidi Ndege au Satellite yaani Uwe Juu ya Mawingu na Uwe na Vyombo mbali mbali vya Kuchunguza na Kupiga Picha. Huwezi kuona Shape au Jengo la Wingu kama hili. Sasa Mtume Mohamed (Sala na Amani yake mola Zimfikie) aliona Vipi Wingu kama Hili) je huoni Huu Ni Muujiza Mkubwa. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Na la kushangaza zaidi Neno بَرْقِهِ ambalo lina maana ya Mwanga wa Radi. Na Herufi HA hapa katika Neno BARKI-HI inarudi katika Neno بَرَدٍ Katika Aya Hii. Yaani BARAD maana yake ni Mawe (Ya Mvua Ya Mawe).Kuruani hapa inasema kwamba Mwanga Wa Radi unatokana na Mawe haya. Tumeona Sayansi inavyosema hapa Juu katika maelezo kwamba Mwanga wa Radi unatokana na Mawe haya. Angalia Aya Moja Ina maana Chungu Nzima. Allahu Akbar. Aya Imepangwa Kiajabu. Sayansi Ya Hali Ya Juu sana. Wana Sayansi Bado wana hangaika Kusoma. Hapa Kuruani ipo Mbele sana. Na Hii Ni ushahidi kwamba Mwenyeezi Mungu Ndiye aliyeshusha Kuruani Hii. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Je huu siyo Muujiza Mkubwa. Je huoni Maajabu Ya kushangaza? Allahu Akbar. Sasa Aya Ifuatayo ni Muujiza Mwingine wa Ajabu sana
(هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفاً وَطَمَعاً وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ) [الرعد: 12]
Tunasoma Katika Aya Hii Kutoka katika Sura Ya Al-Raad Aya Namba 12 kwamba Mawingu ni Mazito sana. Ajabu Ni Kwamba Yapo Angani. Na yanabeba Maji Matani Na Matani (Tons and Tons) Maji Mengi sana yanabebwa na haya Mawingu. Sasa Leo Sayansi inasema haya pia. Sasa Mtume alisoma wapi elimu hii? Alijua Vipi haya Mawingu ni Mazito? Nani angeweza kufikiria kwamba Mawingu Ni Mazito sana na kuweza kutoa Aya Ya kuruani na kutaja haya bila ya wasiwasi wowote kwa kusema “Mawingu Ni Mazito” hakuna anayeweza kusema maneno haya isipokuwa Mwenyeezi Mungu Peke Yake. Hakuna Yeyote. Na Ya Ajabu Kuruani Ni Ya Karne ya 7 Mtume alijua Vipi wakati huo elimu kubwa kama hii. Je huoni Muujiza. Wingu dogo sana miongoni mwa mawingu makubwa kwa jina CUMULUS peke yake wataalamu wanasema lina maji karibu Tani Milioni 1.1 ya maji!!!! Allahu Akbar. Hapa Tuanzungumzia Kawingu Kadogo tu sasa je Mawingu Makubwa. Sasa Kuruani Haikukosea iliposema kwamba وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ
kutoka katika Aya Ifuatayo
(هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفاً وَطَمَعاً وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ) [الرعد: 12] وَيُنْشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ
Yaani Amumba Mawingu Mazito. Sayansi Inatuambia Habari zifuatazo za kushangaza
We still need to answer the question of how much a cloud weighs. To confuse things more, the weight depends on how you define it:
The weight of the water droplets in the cloud •
The weight of the water droplets plus the weight of the air (mostly above the cloud, pressing down)
A large cumulus cloud that you might find on a nice summer day is made up of about 1 million pounds of water drops. A thunderstorm cloud contains enough water drops to fill up approximately 275 million gallon jars. That’s about 2.3 billion pounds, or 1.1 million tons of water.
An everage Cloud weight, One estimate of cumulus cloud density is given a density of about 0.5 gram per cubic meter. A 1 cubic kilometer (km3) cloud contains 1 billion cubic meters. Doing the math: 1,000,000,000 x 0.5 = 500,000,000 grams of water droplets in our cloud. That is about 500,000 kilograms or 1.1 million pounds (about 551 tons). That’s the equivalent of 100 elephants. But, that “heavy” cloud is floating over your head because the air below it is even heavier— the lesser density of the cloud allows it to float on the dryer and more-dense air.)
Ukifikiri sana Utashangaa na kumuogopa Mwenyeezi Mungu na kuifuata Kuruani Yake. Allahu Akbar.
Nani Angeweza Kufikiri habari Hizi.
Na Mtume alijua Vipi Habari kama hii.? Elimu hii bado wataalamu wanahangaika kusoma lakini kuruani imeshagusia tangu karne 14 zilizopita yaani miaka 1400 iliyopita. Kama Kawaida kila kitakachogunduliwa tutakikuta katika Kuruani na Inshaallah hayatakuwa mageni kwani yote yanaonyesha ukubwa wa Elimu ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu.
Na Pia Inaonyesha Kwamba Yule Yule aliyeshusha Kuruani ndiye yule yule aliyeumba Ulimwengu huu. Allahu Akbar.
AINA ZA MAWINGU NA MAJINA YAKE




Picha hizi zinatuonyesha aina za Mawingu na Umbali kutoka katika Ardhi. Usibabaike kwani Huenda ukakuta watafiti wa kisayansi wanaturodheshea vipimo mbalimbali lakini ihtilafu siyo kubwa. Ni Approximation.
وَتَرَى ٱلۡجِبَالَ تَحۡسَبُہَا جَامِدَةً۬ وَهِىَ تَمُرُّ مَرَّ ٱلسَّحَابِۚ صُنۡعَ ٱللَّهِ ٱلَّذِىٓ أَتۡقَنَ كُلَّ شَىۡءٍۚ إِنَّهُ ۥ خَبِيرُۢ بِمَا تَفۡعَلُونَ (٨٨)
Na unaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mawingu (yanavyokwenda). Ndiyo sanaa ya Mwenyezi Mungu, (matengenezo yake) aliyekitengeneza kila kitu; bila shaka anazo babari za yote mnayoyatenda.
And you see the mountains, thinking them rigid, while they will pass as the passing of clouds. [It is] the work of Allah , who perfected all things. Indeed, He is Acquainted with that which you do.
PICHA ZA MILIMA




UKIANGALIA UTAONA MAWINGU NI KAMA MILIMA KWA UMBILE NA HARAKATI ZAKE PIA. SASA ANGALIA USHAHIDI. PICHA ZA JUU NI MAWINGU UMBILE KAMA MLIMA NA PICHA ZA CHINI NI MILIMA DUNIANI. UNAONA MUUJIZA. JE MTUME ALIONA VIPI HAYA KWA WALE WANODAI KWAMBA MTUME KAANDIKA HII KURUANI KWA KWELI KUONA UMBILE KAMA HILI INAHITAJIA VYOMBO MBALI MBALI VYA KISASA KUWEZA KUONA MLIMA WA MAWINGU HAKUNA ANGEWEZA KUONA KATIKA WAKATI HUO HUKO MECCA. INAHITAJI NDEGE AU SATELLITES AU VYOMBO VINGINEVYO VYA KISASA VYA UTAFITI WA HALI YA JUU. ALLAHU AKBAR. KURUANI INASEMA KWAMBA MAWINGU NI KAMA VILIMA VYA DUNIANI.
Physics Video 1 Inaelezea Elimu Ya Mawingu, Mwanga Wa Radi na Radi. Elimu hii inalingana na Elimu Tunayosoma katika Kuruani Tukufu. Allahu Akbar
Physics Video 2 Inaelezea Elimu Ya Mawingu, Mwanga Wa Radi na Radi. Elimu hii inalingana na Elimu Tunayosoma katika Kuruani Tukufu. Allahu Akbar