SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Sayansi Za Ardhi

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

KUPUNGUZWA KWA USO WA GAMBA LA ARDHI (EROSION)

KUPUNGUZWA KWA USO WA GAMBA LA ARDHI (EROSION)

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinachangia katika kukwangua uso wa gamba la ardhi au kwa lugha nyingine kupunguza unene wa gamba la ardhi kwa njia inayojulikana kama Mmomonyoko (Erosion):

Hewa ni sababu ya kwanza inayochangia katika kupunguza unene wa gamba la ardhi. Hewa ina nguvu na huweza kubeba mchanga,udongo na mawe kutoka sehemu moja na kupeleka sehemu nyingine.

Maji ni sababu ya pili katika kula na kupunguza unene wa uso wa gamba la ardhi kwa njia mbalimbali kama vile mvua, mito, mafuriko, mabwawa and mabahari katika kubeba chembe za udongo na mchanga na kusababisha hata kupotea kwa visiwa kamili kama utakavyoona katika Video hapa chini. Mvua ni mojawapo ya sababu kubwa ya kula (erosion) ardhi kwa nia mbalimbali zinazojulikana katika elimu ya Geology kwa majina mbalimbali kama vile Splash Erosion, Sheet Erosion, Rill Erosion au Gully Erosion. Hizi ni aina mbalimbali za kumomonyoka kwa ardhi.     

Mito ni sababu ya Tatu ambayo inasababisha mmomonyoko wa ardhi kwa kukuna, kuondoa na kubeba udongo na mchanga na kusababisha mmomonyoko wa ardhi. Mabonde yanapanuliwa na maji na hatimaye kukuzwa kwa upana na urefu. Bonde la Mto wa samaki (fish river) huko kusini mwa Namibia ni mfano wa Mmomonyoko wa Bonde. Hili ni Bonde kubwa katika Africa Nzima. Lina Urefu wa Kilomita 160 (99 Maili), Upana wa Kilomita 27 (maili 17), na Urefu wa Bonde hili ni mita 550 (1084 feet).

Bahari Ni sababu ya Nne ya mmomonyoko wa Miamba ya Mawe,Udongo na Mchanga huko Pwani. Mawimbi yanavunja Miamba (rocks) na kuwa Mawe na Mawe yanavunjwa na kuwa mchanga. Maji ya bahari yanaondoa na kubeba mchange kutoka katika ufukwe na kusababisha bahari kupanuka kwa kusababisha kurudi nyuma kwa ukanda wa pwani kuelekea sehemu za Bara.

Barafu Ni sababu ya Tano ambayo inasababisha mmomonyoko wa ardhi kwa njia mbalimbali. Miamba inayobebwa na Barafu hukwaruza ardhi na kusababisha mmommonyoko wa ardhi na pia kuvunjika kwa miamba hiyo.

Joto ni sababu ya Sita inayochangiakatika Mmomonyoko wa ardhi katika mito au katika ukanda wa pwani.

Magamba Ya Ardhi (Plate Tectonics) Ni Sababu ya Saba. Magamba Ya Ardhi Yanapokutana na Kugongana na kusababisha Mtetemeko wa Ardhi pia husababisha  Mimomonyoko ya Ardhi kwa njia mbalimbalia. 

Sayansi za kisasa baada ya utafiti kwa kutumia viombo mbalimbali wataalamu wanasoma na kuendelea kusoma na kutufahamisha Elimu hii ya Earth Erosion (Moomonyoko wa Ardhi).

Na Kufuatana na Habari tunazoletewa na NASA (national Aeronautics and Space Administration) zinasema kwamba Radius ya Ardhi katika sehemu za Equator ni 6378.5 km na Radius ya Polar ni 6357 km tofauti ya 0.3% Upungufu huu katika sehemu za Poles (Kusini na kaskazini ya Ardhi) huenda unatokana na Mmomonyoko (Erosion) na Unaashiria kupungua kwa unene wa ardhi kwa ajili ya mzunguko wa ardhi katika mhimili (axis) wake yenyewe. kama tunavyoelewa ardhi inajizunguka yenyewe kwa muda wa saa 24 na kusababisha usiku na mchana.

Na Aya Mbili zifuatazo Katika Sura Ya Raad na Sura Ya Ambiyaa zinathibitisha Sayansi tuliyosoma hapa juu kwa neno “Tunaipunguzapunguza” lenye maana ya kuendelea katika kupunguza;

Chapter (13) sūrat l-raʿd (The Thunder)

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا نَأۡتِى ٱلۡأَرۡضَ نَنقُصُہَا مِنۡ أَطۡرَافِهَا‌ۚ وَٱللَّهُ يَحۡكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكۡمِهِۦ‌ۚ وَهُوَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ (٤١

TAFSIRI YA AYA

Je Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi yao (makafiri).Tunaipunguzapunguza katika mipaka yake? Na Mwenyeezi Mungu huhukumu (kwa uadilifu). Na hakuna wa kupinga ukumu Yake. Naye ni Mwepesi wa kuhesabu.

Chapter (21) sūrat l-anbiyāa (The Prophets)

بَلۡ مَتَّعۡنَا هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡعُمُرُ‌ۗ أَفَلَا يَرَوۡنَ أَنَّا نَأۡتِى ٱلۡأَرۡضَ نَنقُصُهَا مِنۡ أَطۡرَافِهَآ‌ۚ أَفَهُمُ ٱلۡغَـٰلِبُونَ (٤٤)

TAFSIRI YA AYA

Bali Tuliwastarehesha (makafiri) hawa na baba zao mpaka umri wao umetawilika, (umekuwa mrefu)juu ya hayo, Je, hawaoni ya kwamba Tunaiendea ardhi yao Tukiipunguza mipaka yake? Basi Je! Wao ni wenye kushinda? Tunaona muujiza katika maana ya aya hizi mbili kwamba “Ukubwa wa Ardhi unapunguzwa katika uso wa Gamba la ardhi” kilugha neno hili “Tunapunguzapunguza” ni kitendo cha kuendelea na siyo kitendo kilichokwisha. Ni kitendo cha kuendelea daima.

Na ajabu kubwa sayansi ya leo hii inatuambia hivyo hivyo kama ulivyoona sherehe hapa juu kwamba ardhi inapungua kutokana na sababu mbalimbali. Sasa tujiulize Suali.

Je Mtume alijua vipi habari kama hii? Je hatuoni Muujiza ambao upo wazi mbele ya macho yetu.

Elimu hii imeshughulikiwa kwa uchache sana kwani ni elimu mpya.Na hii inathibitisha kwamba Kuruani imeitangulia sayansi tangu muda mrefu sana. Tusidanganyike na elimu hizi za kisasa tukadhani ndiyo maendeleo na tukaacha uislamu na kuudharau.

Tukifanya hivyo basi tutarudi nyuma sana tena sana. Sayansi na Dini zinakwenda pamoja kama uhusiano baina ya Yai na kuku. Bila kuku hupati yai na bila ya yai hupati kuku. Kwa kweli kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu. Ukitaka kuzungumza na Mwenyeezi Mungu basi Rattil (Soma)Kuruani. Video Zifuatazo zinatoa Mwanga zaidi kuhusu Elimu hii.

Kupotea kwa kisiwa huko Canada kutokana na Mmomonyoko.

mmomonyoko wa udongo ulimwenguni

Angalia Mmomonyoko wa ardhi huko pwani ya Pacifica (kusini ya San Fransisco) ambao unatokana na Bahari

KAZI ZA MATABAKA YA MBINGU NA BONDE LA UFA KATIKA ARDHI

Chapter (86) sūrat l-ṭāriq (The Night-Comer) From Ayat 11-13

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ (١١) وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ (١٢) إِنَّهُ ۥ لَقَوۡلٌ۬ فَصۡلٌ۬ (١٣)

Tafsiri Ya Aya 11.Naapa kwa mawingu yanayoleta mvua 12.Na kwa ardhi inayopasuka (ikatoa mimea) 13. Kuwa hii (Qurani) ni kauli ipambanuayo haki

Sherehe Ya Kisayansi Ya Aya

Tafsiri Ya Hapo Zamani (Aya Namba 12) Nimeiacha hapa juu kama ilivyo lakini Tafsiri Ya Kisayansi  tumeizungumzia hapa Hapa chini.

Mbingu ina kazi Mbalimbali kama Mwenyeezi Mungu aliposema Amejaalia kila Tabaka la Mbingu Kulipa Kazi Yake.

فَقَضَٮٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَـٰوَاتٍ۬ فِى يَوۡمَيۡنِ وَأَوۡحَىٰ فِى كُلِّ سَمَآءٍ أَمۡرَهَا 12

Basi akazifanya mbingu saba katika siku mbili, na kila uwingu akaufunulia kazi yake.  

Aya Namba 11 hapa juu Mwenyeezi Mungu anaapia kwamba amejaalia Mbingu kuwa yenye kurudisha yaani kwanza kuwa kama Bati Letu katika kutukinga na miale ya Jua ambayo inaweza kutudhuru Yaani Mbingu inarudisha miale hiyo angani na kwa hiyo haitufikii (Kwa Mfano Mojawapo ni UVC Rays Zinazuiwa na Tabaka la mbingu linalojulikana kama Ozone Layer yaani Miale  inayosababisha Maradhi ya Cancer)na pia Mbingu inaturudishia kwetu maji kama Mvua ambayo ni Uhai wetu.Kiapo chake Mwenyeezi Mungu inaashiria utukufu wa umbile hilo.(Angalia Elimu Ya Mzunguko wa maji katika sehemu nyingine ya Website Hii kwani tumezungumzia kwa urefu kuhusu “Natural Water Circle System”).

Aya Namba 12 inayofuatia Mwenyeezi Mungu anaapia Bonde Katika Ardhi Na Kiapo cha Mwenyeezi Mungu kinaashiria utukufu wa Umbile hilo.

Wataalamu wanatuambia kwamba Mfumo wa Bonde  La Ufa Ulimwenguni ni Muungano wa Mabonde Duniani na zote kuhesabiwa kama Bonde Moja Kubwa La Ufa Duniani na yote yameungana chini ya Gamba La Ardhi Kavu Na pia chini ya Gamba La Ardhi ambalo lipo chini Ya Mabahari.Na Mabonde haya yanazuka wakati Tabaka Linalojulikana kama Lithosphere linapotanuka na Kuchanika, baada ya hapo ardhi chini yake itazama kusababisha mashimo ambayo tunayaita Mabonde nayo Utakuta yamezungukwa na Kuta za Miamba ya mawe na udongo inayojulikana katika lugha ya kiingereza kama Horsts. Mfano wa Mabonde Makubwa Katika Ardhi kavu ni The East African Rift (Bonde La Ufa La Africa Mashariki), The Baikal Rift Valley (Bonde La Ufa La Balkal), the West Antarctic Rift (Bonde La Ufa la Antartic), and the Rio Grande Rift (Bonde La Ufa La Rio Grande) Ni Aina Ya Mabonde Ya Ufa Makubwa katika Ardhi Kavu yaliyo Hai, Na hali kadhalika katika Bahari Kuna Mabonde Mbalimbali.

Binaadamu bado wanasoma na kwa hiyo Elimu zetu bado changa. Wataalamu Wanasema kwamba hizi Bonde Zote (au Nyufa za Gamba la ardhi zimesambaa na Kuungana pamoja). Tunaambiwa kwamba “The Great Rift Valley” Ndilo Bonde Kubwa sana ambalo limeunganisha Mabonde Mbalimbali Duniani. Wataalamu wanatuambia yafuatayo kuhusu “Great Rift Valley”

(The Great Rift Valley is a series of contiguous geographic trenches, approximately 7,000 kilometres (4,300 mi) in total length, that runs from the Beqaa Valley in Lebanon which is in Asia to Mozambique in Southeast Africa. While the name continues in some usages, it is rarely used in geology as it is considered an imprecise merging of separate though related rift and fault systems.Today, the term is most often used to refer to the valley of the East African Rift, the divergent plate boundary which extends from the Afar Triple Junction southward across eastern Africa, and is in the process of splitting the African Plate into various plates.Somalian Plate, African Plate, and Indian Plate).

Tafsiri Ya maneno hapa juu:

Ni Kwamba Mabonde haya ni Mashimo mbalimbali yaliyoungana kwa urefu unaofikia kilomita 7000 yaani maili 4300.Kuanzia Bonde la huko Lebanon katika Asia Mpaka Msumbiji (Mozambique) Afrika Ya Kusini. Bonde hili linajulikana kama Bonde la Africa Ya Mashariki. Na bado linaendelea kupanuka na kusababisha mgawano wa Gamba la ardhi la Afrika Ya Mashariki katika Mapande mbalimbali. Gamba La Somali, Gamba La African Continent, Gamba La India.

Aya ya Kuruani inayoashiria Bonde inasema

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ

“Ninaapa Kwa ardhi yenye Bonde”

1-Na huenda likawa hili Bonde la East Africa ambalo kubwa sana (Urefu wake kilomita 7000, yaani maili 4300, Upana wake ni 220 kilomita Yaani Maili 140 na urefu chini ya ardhi ni kilomita 2 yaani Maili Moja.

2-Au Huenda Aya Inashiria Mabonde Makubwa Duniani Yameungana chini ya ardhi na Kufanya Bonde Moja. 

3-Au huenda likawa Bonde Moja katika Mabonde mengine Makubwa Duniani ambalo bado hatulijui.

Sisi tunasoma haya lakini Mwenyeezi Mungu anajua zaidi.Na huenda kuna mengi hatujui na kutagundulikana baadaye wataalamu watakaposoma zaidi kwani Mwenyeezi Mungu amejaalia Miujiza ya kisayansi kugundukika katika kila Karne. Haya ya sayansi yalitajwa katika kuruani tangu Karne ya 7 na baada ya karne 1400 tunagundua aya zinazohusiana na sayansi na hivyo hivyo karne zitakazokuja wataalamu watagundua haya na yatakuwa ni sababu ya kuwazidishia imani.

PICHA YA BONDE LA AFRICA MASHARIKI

Bonde La Africa Mashariki (East African Rift Valley)

PICHA YA BONDE LA AMERICA KASKAZINI

PICHA YA BONDE KATIKA BAHARI

VIDEO INYOHUSIANA NA AFRICAN RIFT VALLEY

Video Inayohusiana na Great Rift Valley (East African Rift Valley) Je unaona Mgawanyiko unavyofanyika. Wataalamu Wanasema kwamba Miaka inayokuja Afrika Itagawanyika na Kusababisha Bara La Afrika Jipya Litakalojulikana kama Nubian Continent na Bahari kama Nubian Ocean.