SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Sayansi Za Dunia-1

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

SAYANSI YA MAWIMBI NA GIZA LA BAHARI KATIKA KURUANI TUKUFU

AYA ZINAZOHUSIANA NA KAFIRI NA MAAJABU YA ELIMU YA SAYANSI ILIVYOTUMIKA NA KUELEZEWA KWA HALI YA UFUNDI MKUBWA

MAFUNDISHO KATIKA AYA HIZI MBILI

Katika Aya Hizi Mbili hapa chini Mwenyeezi Mungu anatuelezea vitendo na imani ya kafiri.

Katika Aya Ya kwanza Mola Ametoa mfano wa kitendo chochote cha kafiri hakina faida yeyote na wala hapati chochote na atalipwa hesabu kwa haraka na Mwenyeezi Mungu kama ipasavyo.

Mfano wake ni kama mtu ukiwa na kiu kisha ukaona maji kwa mbali yanang’aa (kama tunavyoona jua linapokuwa kali) na unapokaribia hukuti chochote na kiu kipo pale pale hujapata maji ya kujisaidia.

Na katika Aya ya pili Imani ya kafiri ambayo inakwenda kinyume na dini ya kiislamu ni upotevu mkubwa na mfano wake ni kama Giza kubwa ndani ya bahari ambalo giza hilo linazidishwa na Mawimbi ndani ya Mabahari na Pia Mawingu angani ambayo yanazuia Jua lisifike ndani ya Mabahari.

Giza hilo linasababisha mtu asiuone hata mkono wake ambao ndiyo karibu yake sana naye.kwa hiyo Mwenyeezi Mungu anamfananisha Mtu ambaye amezama katika Giza la ukafiro na Giza la ndani ya bahari.

وَٱلَّذِينَ ڪَفَرُوٓاْ أَعۡمَـٰلُهُمۡ كَسَرَابِۭ بِقِيعَةٍ۬ يَحۡسَبُهُ ٱلظَّمۡـَٔانُ مَآءً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَهُ ۥ لَمۡ يَجِدۡهُ شَيۡـًٔ۬ا وَوَجَدَ ٱللَّهَ عِندَهُ ۥ فَوَفَّٮٰهُ حِسَابَهُ ۥ‌ۗ وَٱللَّهُ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ (٣٩)

Tafsiri Ya Aya Na Wale waliokufuru, vitendo vyao (wanavyoviona vizuri)ni kama mazigati(mangati-sura ya maji) jangwani, mwenye kiu huyadhani ni maji, akiyaendea hayaoni chochote(Na wao watakapoziendea amali zao siku ya kiama hawatapata chochote kwani waliupinga Uislamu, Na hali ya kuwa wanajua ndiyo dini ya haki);Wamkute Mwenyeezi Mungu hapo, awalipe hisabu yao sawasawa; Na Mwenyeezi Mungu ni mwingi wa kuhisabu.

أَوۡ كَظُلُمَـٰتٍ۬ فِى بَحۡرٍ۬ لُّجِّىٍّ۬ يَغۡشَٮٰهُ مَوۡجٌ۬ مِّن فَوۡقِهِۦ مَوۡجٌ۬ مِّن فَوۡقِهِۦ سَحَابٌ۬‌ۚ ظُلُمَـٰتُۢ بَعۡضُہَا فَوۡقَ بَعۡضٍ إِذَآ أَخۡرَجَ يَدَهُ ۥ لَمۡ يَكَدۡ يَرَٮٰهَا‌ۗ وَمَن لَّمۡ يَجۡعَلِ ٱللَّهُ لَهُ ۥ نُورً۬ا فَمَا لَهُ ۥ مِن نُّورٍ (٤٠)

Tafsiri Ya Aya Au (amali zao zile mbaya) Ni kama giza katika bahari yenye maji mengi;inapofunikwa na mawimbi juu ya mawimbi; na juu yake kuna mawingu;giza hili juu ya hili;anapoutoa mkono wake anakaribia asiuone (kwa kiza kilivyoshtadi);na ambaye Mwenyeezi Mungu hakumjaalia nuru hawi na nuru.

SAYANSI KATIKA AYA YA PILI

Mwenyeezi Mungu anatuelezea katika hizi aya mbili malipo ya vitendo na imani ya kafiri kwa kuchanganya na elimu ya sayansi ambayo haiwezekani kwa mtume Mohamed (Sala na Amani ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) kujua elimu inayohusiana na bahari katika karne ya saba.

Elimu kwamba ndani ya bahari kuna Giza kubwa linalosababishwa na tabaka la kwanza la Mawimbi (internal waves) na tabaka la pili la Mawimbi Juu ya bahari (surface waves)na Pia tabaka la tatu la Mawingu (clouds) ambayo yanazidisha Giza hilo kwa kuzuia miale ya Jua isifike baharini na kupenya ili kuleta mwanga katika baadhi ya Maili ndani ya Bahari. kwani Elimu hii ni ya hivi karibuni haiwezekani kwa wakati huo (karne ya saba) mtume kujua habari hizi zinazohitaji vyombo vya utafiti wa hali ya juu. Ninaongeza Video Tatu zinazotuelezea habari hizi kwa kinaganaga kwa mfano wa kisayansi.

Video-1

Majaribio Yenye Uhusiano na Mawimbi Ndani Ya Bahari na ajabu kubwa tunasoma habari hizi katika kuruani Tukufu Na Mtume aliishi Jangwani!!! Ushahidi kwamba Aliyetuma Kuruani hii ndoye yule yule aliyeumba ulimwengu!!.

Video-2

Hotuba Inayohusiana na Mawimbi ya ndani Baharini. Je huoni maajabu ya Kuruani kwamba inataja Elimu hii ambayo tunaisoma hivi leo baada ya kutumia viombo vya kisasa katika utafiti. Haiwezekani mtu kuzama baharini hovyo hovyo isipokuwa kwa viombo vya hali ya juu sana tena sana. Je Mtume alisoma wapi?

Video-3

Giza Baharini na maelezo yake. Je unaona Maajabu ya kuruani kwamba inazungumzia Giza la bahari na na hali kwamba hakuna mtu yeyote katika karne hiyo aliyeweza kuzama na kujua haya. Je haishangazi? kwa kweli inatisha sana .
Tumwogope na kumtukuza Mwenyeezi Mungu kila wakati. Alhamdu Lilahi.

KURUANI INATHIBITISHA KWAMBA MILIMA INA MIZIZI

MILIMA INA MIZIZI

Kuruani imeitangulia sayansi kwa muda mrefu. Hata hivi leo wanasayansi wa elimu ya Gelogy bado hawajaielezea habari hii ila kwa uchache sana. Ukichunguza vitabu karibu vyote vya mashuleni na vinginevyo havielezei Elimu hii kama ipasavyo kwani bado ilikuwa haijulikani. Ni Elimu ya Miaka michache iliyopita. Kitabu Kinachojulikana kama Earth (Yaani Ardhi) ni mojawapo ya vitabu vinavyotumiwa katika Vyuo Vikuu (universties)ulimwenguni, na mmoja wa waandishi wa kitabu hiki Ni Profesa Emeritus Frank Press ambaye alikuwa mshauri wa sayansi wa Rais wa Marekani alyestaafu bwana Jimmy Carter na kwa muda wa miaka 12 lalikuwa Rais wa  National Academy ya KIsayansi  huko Washington DC. Kitabu chake kinasema kwamba “Milima ina Mizizi”

Yaani ana maana kwamba imezama ndani ya Ardhi mfano wa Kigingi kinavyoingia ardhini katika ujenzi wowote ule kwa mfano wa  Hema. Unapojenga Hema utatumia Vigingi ili liwe madhubuti na urefu wake ndani ya  ardhi ni mrefu zaidi kuliko juu yake ambo tunauona kwa macho. Huu mfan mzuri ukilinganisha na Milima juu ya ardhi.

Na Kuruani imetaja Elimu hii tangu karne ya saba. Mwenyeezi Mungu anasema karika Kuruani Tukufu Sura Ya Anabaa Namba 78 Aya Namba 6 na 7 

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَـٰدً۬ا (٦) وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادً۬ا (٧)

Tafsiri Ya Aya Hizi

Je! Hatukuifanya ardhi kuwa tandiko (6) Na milima kuwa kama vigingi (vya ardhi) (7)

Sayansi ya wakati huu tulionao inathibitisha kwamba milima ina mizizi mirefu kutoka katika gamba la ardhi na kuingia ndani yake kwa urefu zaidi ya sehemu iliyopo juu ya ardhi (tunayoiona kwa macho) na Neno lililo zuri katika kuelezea habari hii ni  “Vigingi” na ajabu Kuruani uimechagua neno lililo sahihi kwa hali ya juu kuliko sayansi ya sasa. 

Kwa kweli maneno ya kuruani siyo ya Mtume au binaadamu yeyote duniani. Ni manenio yake Mwenyeezi Mungu Mtukufu kwani katika Historia Ya Sayansi Elimu hii imeanza kujulikana katika nusu ya pili ya karne ya 19!!!! na ajbu iliyoje Mtume Mohamed amezipokea Aya hizi katika karnet ya 7!!! (karne kumi na 12 kabla ya Sayansi tunayojigambia nayo kwa ujinga wetu). 

Vigingi (Pegs) Vya Milima  inafanya kazi kubwa katika kulishika au kilidhibiti  Gamba Ardhi  livunjike vunjike (au kumomonyoka). Na Nadharia hii Mpya ya Elimu inayojulikana kama Plate Techtonics inathibitisha kwamba Milima inadhibiti  (stabilize)Ardhi ishikamane. Na Nadahria hizi zimekuja katika miaka iliyofuata  1960. Elimu hii ya hivi karibuni inashughulikiwa na wataalamu wa Elimu ya Ardhi (Geology).

Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani Tukufu kuhusu habari hizi katika Sura Ya Annahl Namba 16 Aya Namba 15

وَأَلۡقَىٰ فِى ٱلۡأَرۡضِ رَوَٲسِىَ أَن تَمِيدَ بِڪُمۡ وَأَنۡہَـٰرً۬ا وَسُبُلاً۬ لَّعَلَّڪُمۡ تَہۡتَدُونَ (١٥)

Tafsiri Ya Aya 

Na na akaweka katika ardhi milima ili (ardhi) isiyumbeyumbe nanyi. Na (akaweka) Mito na Mabarabara ili mpate kuongoza (njia mnazozitaka)

Hatuna zaidi ya kusema isipokuwa Allahu Akbaru (Mungu Mkubwa)!!!

Mlima Juu ya Gamba La Ardhi na Mzizi wake Chini ya Ardhi. Inathibitisha kwamba yule yule aliyeumba milima hii ndiyo yule yule aliyeshusha kuruani tukufu

Baadhi Ya Milima Ulimwenguni (Uingereza, Ugerumani, Ufaransa, Russia) na Mizizi Yake Yake

Video-4

Sherehe Ya Kiutaalamu Juu Ya Utafiti wa Milima Ya Himalayas na Mizizi Yake

CLONING (KUNAKILI) VIUMBE

CLONING AU KUNAKILI

Cloning Ni Mchakato Mgumu (Complex Process) ambao unahusika na kunakili umbile za mnyama. Aina za mifugo ambazo wana sayansi wamefanikiwa kunakili ni Ngombe,Nguruwe, Kondoo, Mbuzi, Panya, Sungura, Paka, Farasi na Mbwa.

Wanasayansi wa leo wanafuata hatua mbalimbali katika kutekeleza kazi hizi lakini Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha kutokufanikiwa kwa juhudi hizi. Kiinitete (Embryo) kinaweza kufeli kukua au hata baada ya kukua kinaweza kufeli kuungika katika ukuta wa tumbo la uzazi au sababu nyingi nyinginezo. Katika kunkili kunahitajika kwa  Seli (Cells) zinazojulikana kama Somatic Cells. Na mara nyingi huchukua Cells za masikio ya Wanyama au sehemu nyinginezo za mwilini.

Na Ajabu kubwa suala hili la kuzalisha kwa njia hii limeshajibiwa katika kuruani tangu karne ya saba!!!  je hatuoni maajabu? kwa kweli fikirini aya inayofuata kwa kweli inashangaza sana tena sana.

وَلَأُضِلَّنَّهُمۡ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمۡ وَلَأَمُرَنَّهُمۡ فَلَيُبَتِّڪُنَّ ءَاذَانَ ٱلۡأَنۡعَـٰمِ وَلَأَمُرَنَّہُمۡ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلۡقَ ٱللَّهِ‌ۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيۡطَـٰنَ وَلِيًّ۬ا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدۡ خَسِرَ خُسۡرَانً۬ا مُّبِينً۬ا (١١٩)

[Surat An-Nisa 4:119]

And I will mislead them, and I will arouse in them [sinful] desires, and I will command them so they will slit the ears of cattle, and I will command them so they will change the creation of Allah.” And whoever takes Satan as an ally instead of Allah has certainly sustained a clear loss.

Yaani Shetani  aliposema Nitawapoteza Binaadamu, Na kisha nitawaamrisha na wataka masikio ya wanyama wa mifugo na nitawaamrisha na watabadili umbile la Mwenyeezi Mungu, Na yule atakayemchukua Shetani kuwa kama ni msaidizi au mwenziwe basi kwa hakika amepata hasara kubwa.

Hii Aya ilishuka karne ya saba wakati ambao Elimu hii ya Cloning ilikuwa haijulikani je huoni maajabu? Hii Aya inatuhusu sisi watu wa sayansi za leo.

VIVULI KATIKA KURUANI NA MAAJABU YAKE

VIVULI KATIKA KURUANI NI MUUJIZA WA AJABU

Kwa kwawaida vivuli vinatokana na Jua. Asubuhi sana vivuli vinakuwa virefu na ikifika katikati ya mchana vivuli hupungua sana na hata kufikia kutoweka, Na jioni Vivuli huongezeka na kurefuka kufuatana na Jua Kwani Jua ndiyo lenye kusababisha Vivuli.

Kwa kawaida ardhi inachukua masaa 24 (siku Moja) kujizunguka na ndiyo maana tunapata Vivuli virefu na vifupi.

Lakini Vivuli vitatoweka iwapo Ardhi itajizunguka kwa spidi ya 1.27 metre kwa sekunde moja (1,27 m /s) Yaani itachukua muda wa mwaka mzima (siku 365.5) katika kujizunguka.

kipimo cha Equatorial Circumference ya ardhi ni 40,075 Kilomita(The equatorial circumference of Earth is about 24,901 miles (40,075 km).  Ukigawa umbali huu kwa masiku ya mwaka mzima 365,5   (365.5 x 24 x 3600 ili tupate mbio za ardhi kwa sekunde moja) Jawabu utalopata ni metre 1.27 m /s  kwa sekunde moja.

Aya Ifuatayo inazungumzia Uwezo Wa Mwenyeezi Mungu katika Kutowesha Vivuli. Na Muujiza katika Aya Hii ni kama Ifuatavyo:

Chapter (25) sūrat l-fur’qān (The Criterion)

أَلَمۡ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيۡفَ مَدَّ ٱلظِّلَّ وَلَوۡ شَآءَ لَجَعَلَهُ ۥ سَاكِنً۬ا ثُمَّ جَعَلۡنَا ٱلشَّمۡسَ عَلَيۡهِ دَلِيلاً۬ (٤٥)

Tafsiri Ya Aya 

Hast thou not turned thy vision to thy Lord?- How He doth prolong the shadow! If He willed, He could make it stationary! then do We make the sun its guide;

Ajabu Ya kwanza katika Aya ya Kuruani hapa juu Sura Namba 25 Aya Namba 45

Neno Sakinan (Utulivu) ni neno la namba 11 Na Neno Jua Ni la namba ya 14 .Yaani Ukihesabu maneno kutoka mwanzo wa Aya mpaka neno Utulivu na Neno Jua (Ashams) Na Ukigawa Utulivu katika Jua yaani 14/11 utapata 1,27 na ni namba inayoashiria spidi (speed)ya 1.27 metre  kwa sekunde moja (1,27 m /s) katika sayansi ya kutowesha Vivuli.

Ajabu Ya Pili ni kwamba ukigawa herufi za Aya Hii ambazo ni 57 kwa namba ya aya hii ambayo ni ya 45 utapata tena hiyo 1.27 m/s maili kwa sekunde moja ambayo inaashiria  spidi (speed)ya 1.27 mita kwa sekunde moja (1,27 m /s) katika sayansi ya kutowesha Vivuli.

Ajabu Ya Tatu Aya za kuruani kuanzia mwanzo mpaka sura ya Alqamar ni Aya 4901 na ukigawa na Aya zote za kuruani ambazo ni 6236 utapata namba 1,27 ambayo inayoashiria spidi (speed) ya 1.27 mita kwa sekunde moja (1,27 m /s) katika sayansi ya kutowesha Vivuli.

Asili ya mwanga ni Jua ambalo linapiga Mwezi kisha Mwanga huu unakuja katika ardhi yetu na kwa hiyo Mwezi Unasaidia kuuongoza Mwanga na kutuletea ardhini. Na huenda ndiyo maana spidi (speed)hii ya 1.27 m/s inapatikana pia katika aya za sura ya Alqamar unapogawa na aya za msahafu. Na Muujiza huu katika Sura Ya Alqamar unashangaza kwani Ukisimama katika Mwezi na kisha kuingalia Ardhi utaiona Imetulia na hakuma mzunguko wowote. (Kwani Ardhi inapozunguka kwa spidi ya 1,27 au inaposimama na kutokujizunguka basi Vivuli Vitatoweka) na watu wa ardhini watakuwa katika Giza la milele au Mwanga wa milele na hapa tunathibitishiwa na Mwenyeezi Mungu katika kuruani anaposema katika Aya Mbili zifuatazo:

Chapter (28) sūrat l-qaṣaṣ (The Stories)

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡڪُمُ ٱلَّيۡلَ سَرۡمَدًا إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَـٰمَةِ مَنۡ إِلَـٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيڪُم بِضِيَآءٍ‌ۖ أَفَلَا تَسۡمَعُونَ (٧١)

Tafsiri Ya Aya

Say, “Have you considered: if Allah should make for you the night continuous until the Day of Resurrection, what deity other than Allah could bring you light? Then will you not hear?

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِن جَعَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡڪُمُ ٱلنَّہَارَ سَرۡمَدًا إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَـٰمَةِ مَنۡ إِلَـٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيڪُم بِلَيۡلٍ۬ تَسۡكُنُونَ فِيهِ‌ۖ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ (٧٢)

Tafsiri Ya Aya 

Say, “Have you considered: if Allah should make for you the day continuous until the Day of Resurrection, what deity other than Allah could bring you a night in which you may rest? Then will you not see?”

Kipimo cha Mita hakikuwapo wakati wa Mtume Mohamed katika karne ya 7 bali kipimo cha wakati huo ni “Cubit”. Kipimo cha Mita kilianza katika karne ya 1791!!!  na pia watu wakati huo hawakujua kwamba ardhi inajizunguka na kupatikana hesabu ya mita katika kuruani ni Muujiza kwani Elimu hii ni Juu ya uwezo wa binaadamu na ndiyo maana tunaita Muujiza.

Jambo lingine la kushangaza ni kwamba tukihesabu maneno katika Sura Ya Alfurkan mpaka Aya namba 45 Sura hii tutapata namba mbalimbali zenye kushangaza.

Kuanzia Neno أَلَمۡ “Alam” ni Namba 533 Mpaka Neno la mwisho دَلِيلاً۬ Daliyla ambalo ni Namba 548 Katika Aya Hii neno وَلَوۡ Walaw ni la Namba 540 ambalo linaashiria Degrees (360 Degrees + 180 Degrees=540) na Degrees 540 kwa kawaida ni sawasawa na Zero kwani Tangent ya namba hizi katika hesabu (tg (540 Degrees)=tg(360 Degrees)=tg (180 Degrees)=tg(0 Degrees)=0) Ni Zero. Neno وَلَوۡ (Walaw) linaashiria Zenith (Jua linapokuwa katikati) yaani wakati kivuli kinapotoweka. Neno hili linajulikana katika elimu ya fasihi kama “Palendrom” yaani unaweza kulisoma kwa kushoto au kulia lakini maana na matamshi hayabadiliki. Na aina ya maneno yanayojulikana kama “Palendrom” yapo katika lugha nyinginezo za ulimwengu pia. Maneno yote katika Aya Hii Ya kushoto na Kulia tunaweza kutafuta Degrees za Angles (pembe) Zake kutoka katika hiyo zero “0” Kwa hiyo tunapata maneno kabla ya Neno “Walaw” -1 Degrees mpaka -7 Degrees za Vivuli (upande wa kushoto)na baada ya Neno “Walaw”kwa upande wa kulia tunapata maneno 1 Degrees mpaka 8 Degrees za Vivuli. Na Pembe au Angles hizi tunaweza kuzitumia katika kupima urefu wa vivuli. Kwa mfano ukijua Degrees unaweza kupata Tangent na Mengineyo. Kwa kifupi kwa kutumia Elimu ya Hesabu Inayojulikana kama Trigonometry unaweza kutafuta vipimo vinginevyo.

Katika Aya hii hatusomi namna ya kutafuta urefu wa Vivuli bali tunaashiriwa Elimu ambayo haikuweko wakati wa Mtume na ajabu kubwa kwamba kuruani inagusia mambo haya kiajabu sana Huu ni Muujiza Mkubwa sana.

Vivuli vina umuhimu sana katika kupima urefu wa majengo au chochote ambacho kirefu sana bila ya kutumia mashine yoyote bali kwa kutumia kitu kama vile fimbo ya kawaida tu na ukijua urefu wake kisha ukienda Juani na kupima urefu wa kivuli chake basi unaweza kutumia vipimo hivi katika kutafuta urefu wa jengo lililorefu sana.

Kwa mfano ikiwa kipimo cha Fimbo ni Mita Mbili na kipimo cha Kivuli chake ni Mita Tatu na ukipima urefu wa Kivuli wa jengo kubwa na ikiwa kivuli hicho ni meter 18 basi utatafuta 2/3 (kipimo cha fimbo)ya 18 (kipimo cha jenngo refu) na jawabu litakuwa ni 12 kwa hiyo urefu wa jengo hilo kubwa ni mita 12. Na pia unaweza kutumia vipimo vya kivuli kwa kutumia Trigonometry Calculator katika kutafuta mengineyo yanayohusiana na hesabu zako kama vile Degrees au Tangent na Mengineyo. 

Elimu hii inathibitisha kwamba yule yule aliyeumba ulimwengi ndiyo yule yule aliyeshusha kuruani. Hii inatuzidishia imani na pia kutusaidia kumcha mwenyeezi mungu kama ipasavyo.

Tusidanganyike na Sayansi kwani ni Elimu ndogo sana katika Elimu zake Mwenyeezi Mungu Mtukufu, Tusitupe dini kwa Ujinga kwani Sayansi ndiyo inatukaribisha na dini kama anavyosema mwana sayansi maarufu Einstein:

“science without religion is lame and  religion without science is blind. He told William Hermanns in an interview that “God is a mystery. But a comprehensible mystery. I have nothing but awe when I observe the laws of nature. 

Sasa Je tufuate fikra za watu wakubwa kama hawa au tufuate wajinga wasiojua chochote? 

MILIMA YENYE RANGI ZA KUSHANGAZA-RAINBOW MOUNTAINS

Hivi karibuni wataalamu wamegundua milima yenye rangi inayojulikana kama “Rainbow Mountains”  Wataalamu wanatuambia kwamba hapo zamani ilifunikwa na barafu na kwa hiyo ilifichika lakini kwa ajili ya joto la mazingara ya sasa barafu hiyo inayayuka na rangi ya milima hiyo imefichuka. Milima hiyo ipo huko China na pia huko Peru.  Angalia picha hapa chini ya milima hiyo. Na linaloshangaza Quruani inazungumzia haya tangu karne ya 7. Je Mtume Mohamed alijua vipi haya?  Alikwenda China na Peru na akafukua barafu juu ya milima hiyo kisha akajua habari hizi? haiwezekani hata kidogo. Angalia Kuruani inavyoshangaza. Ni dalili zake Mwenyeezi Mungu kuthibitisha kwamba Kuruani ni ya ukweli Mtupu  na siyo maneno ya hovyo kama wanavyodai wajinga..

Kuruani Inazuzngumzia Haya Katika Sura Namba 35 Aya Namba 27

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ ثَمَرَٲتٍ۬ مُّخۡتَلِفًا أَلۡوَٲنُہَاۚ وَمِنَ ٱلۡجِبَالِ جُدَدُۢ بِيضٌ۬ وَحُمۡرٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُہَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ۬

Tafsiri Ya Aya:

27. Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji toka mawinguni! Na kwayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana

Milima Ya Rangi Huko China na Peru

NENO MASHARIKI NA MAGHARIBI NA UMBILE LA ARDHI KATIKA KURUANI TUKUFU

MASHARIKI NA MAGHARIBI (MOJA/SINGULAR)

Mashariki na Magharibi zote ni zake Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Jua huchomoza Mashariki. Kuchomoza kwa Jua ni tokeo linalosababishwa na kujizunguka kwa Ardhi (on its own axis). Ardhi inajizunguka kinyume cha mzunguko wa Saa (anticlockwise) na baada ya saa 12 tunalielekea Jua na kuliona linachomoza na baada ya hapo ardhi inaendelea kujizunguka na baada ya saa 12 nyinginezo ardhi inakuwa mbali na Jua na hapo tunaliona linatua. Kwa hiyo kujizunguka kwa ardhi ndiyo sababu inayotupelekea kuona kuchomoza na kutua kwa Jua. Mashariki au Kuchomoza kwa Jua na Magharibi au Kutua kwa Jua zote hizi mbili ni Maumbile na Elimu yake Mwenyeezi Mungu na ndiyo maana anasema katika Aya hii kwamba Mashariki na Magharibi ni miliki yake.

Sura Namba 2 Aya Ya 115

وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُ‌ۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ۬ (١١٥)

Tafsiri Ya Aya

Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi mahala po pote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile)

MASHARIKI NA MAGHARIBI (MBILI/DUAL)

Mwenyeezi Mungu anasema pia katika Aya hii kwamba yeye ndiye Mtawala wa Mashariki mbili na Magharibi Mbili. Kwani tunapoona Kuchomoza kwa Jua katika upande mmoja wa ardhi basi katika upande wa pili (opposite) wa ardhi sehemu inayoelekeana na hiyo Jua litaonekana linatua na hali kadhalika Katika upande wa pili wa ardhi Jua linapoonekana Kuchomoza basi katika upande wa kwanza (opposite) wa ardhi Jua litaonekana linatua. Kwa kifupi Kila upande utakuwa na Kuchomoza na Kutua kwa Jua.na Kwa hivyo tutapata Mashariki mbili (kuchomoza kwa jua) na Magharibi mbili (kutua kwa Jua). Tafsiri Hii inakubaliana na fahamu ya Aya Mwenyeezi Mungu anaposema kwamba Yeye ndiye Mola wa Mashariki Mbili na Magharibi Mbili.

Sura Ya Al-Rahman Ayat Number 17

رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ وَرَبُّ ٱلۡمَغۡرِبَيۡنِ (١٧)

Tafsiri Ya Aya 17.

Mola wa mashariki mbili na Mola wa magharibi mbili.

MASHARIKI NA MAGHARIBI (WINGI/PLURAL)

Kila sehemu katika Ardhi ina saa yake ambayo inatofautiana na nyiniginezo kufuatana na mzunguko wa ardhi. Wakati wa Kuchomoza na Kutua kwa Jua pia kutatofautiana. Kila Mji utakuwa na saa maalum ambayo Jua huchomoza na pia kutua na kwa lugha nyingine kila mji utakuwa na Mashariki/East (kuchomoza kwa Jua) na Magharibi/West (Kutua Kwa Jua) Kwa hiyo Kuna Mashariki/East na Magharibi/West kila pahali na kila sehemu. Yaani zaidi ya Moja. Kuruani haikukosea Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Yeye ndiye mola wa Mashariki zaidi ya Moja na Magharibi zaidi ya moja.

Sura As-safaat Ayat Number 5

رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَہُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَـٰرِقِ (٥)

Tafsiri Ya Aya

Mola wa mbingu na ardhi na yaliyomo kati yake, (yao); na ni Mola wa mashariki zote (na magharibi zake).

ARDHI NI DUARA katika mfano wa yai la mbuni(Spherical)

Kuchomoza kwa Jua na Kutua kwa Jua katika sehemu mbalimbali za ardhi kunathibitisha kwamba ardhi ni Duara (Spherical) na kwamba ipo katika kujizunguka (On it own axis). Ingelikuwa siyo Duara (yaani Flat kama vile sahani) basi tusingepata Mashariki (sunrises)na Magharibi (sunsets) zaidi ya Moja au Plural Easts and Wests.

Aya zifuatazo pia zinathibitisha kwamba ardhi ni Duara (Spherical). Kwani Kujizunguka kwa ardhi na kulielekea Jua kunasababisha Mchana na Kujizunguka kwa ardhi na Kuenda mbali na Jua kunasababisha Usiku. Jua linapochomoza basi miale yake ambayo ni mkusanyiko wa rangi 7 zinapoingiana na chembe za giza linalozunguka ardhi tunapata Mchana na Ardhi inapojizunguka na Kuenda mbali na Jua basi Mwanga ambao una rangi 7 utatoweka na kuliacha Giza la asili linalozunguka ardhi na hili Giza ndilo Usiku. Katika Aya hapa chini Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Usiku Ni Muujiza ambao tunauvua au kuondoa miale ya mwanga wa jua na mara tunakuwa kizani yaani kiza ya usiku.

Sura Namba 3 Aya 190

إِنَّ فِى خَلۡقِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱخۡتِلَـٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّہَارِ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّأُوْلِى ٱلۡأَلۡبَـٰبِ (١٩٠)

Tafsiri Ya Aya

Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwapo Mwenyezi Mungu mmoja), kwa wenye akili

Sura Namba 57 Aya 6

يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِى ٱلنَّہَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّہَارَ فِى ٱلَّيۡلِ‌ۚ وَهُوَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ (٦)

Tafsiri Ya Aya

Anaingiza usiku katika mchana na Anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye Anajua yaliyomo vifuani, (seuze yanayosemwa au kufanywa).

Sura Namba 36 Aya 37

وَءَايَةٌ۬ لَّهُمُ ٱلَّيۡلُ نَسۡلَخُ مِنۡهُ ٱلنَّہَارَ فَإِذَا هُم مُّظۡلِمُونَ (٣٧)

Tafsiri Ya Aya

Na usiku ni alama kwao (vile vile ya neema za Mwenyezi Mungu_ juu ya viumbe vyake); tunauvua humo mchana; mara wao wanakuwa kizani.

————————

Kwa Kweli Kuruani ni Muujiza Usio na Mwisho na haiwezekani Mtume Mohamed (Sala na Amani zake Mola Zimfikie) atunge Elimu kama hii kwani haiwezekani kabisa na wala hata tusiote ndoto kuwaza hayo. Katika Karne ya 7 haiwezekani Mtume kuweza kuelewa Sayansi inayohusiana na Wingi wa Easts and Wests yaani zaidi ya moja na mpaka leo Hakuna vitabu vinavyozungumzia habari hii kwa kirefu. Kuruani hapa imetangulia Elimu zote kwa kutujuulisha Mapya tena kwa lugha rahisi inayoeleweka. Hatukatai historia inasema kwamba Mgiriki anayejulikana kwa jina kama  Aristarchus of Samos (born c. 310 BCE—died c. 230 BCE)  alikuwa wa kwanza kuzungumza Kuhusu  Kujizunguka kwa Ardhi lakini ufafanuzi wa kielimu ya hali ya juu Kuhusu Subject au Topic hii tunapata katika kuruani Tukufu na hii inathibitisha kwamba kuruani ni maneno ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Alhamdu Lilahi tunamshukuru Mola kwa Kutufundisha.

Maelezo Kuhusu Tafsiri Ya Aya Hizi ni Juhudi za binaadamu na huenda tumesibu au tumekosa. Kila mara tunasema “Mungu ndiyo anayejua zaidi” Namuomba Mola atakabali kazi hii katika Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Allahu Akbar, Allahu Akbar.

MUUJIZA WA ELEMENTS (NITROGEN NA CARBON)katika Kuruani Tukufu NITROGEN KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Namba 14 Aya Namba 42-43

وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَـٰفِلاً عَمَّا يَعۡمَلُ ٱلظَّـٰلِمُونَ‌ۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمۡ لِيَوۡمٍ۬ تَشۡخَصُ فِيهِ ٱلۡأَبۡصَـٰرُ (٤٢) مُهۡطِعِينَ مُقۡنِعِى رُءُوسِہِمۡ لَا يَرۡتَدُّ إِلَيۡہِمۡ طَرۡفُهُمۡ‌ۖ وَأَفۡـِٔدَتُہُمۡ هَوَآءٌ۬ (٤٣)

TAFSIRI YA AYA

42-Wala usidhani Mwenyeezi Mungu ameghafilika na (haya) wanayoyafanya madhalimu.Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku ambayo macho (yao) yatakodoka (yatoke nje kwa khofu)

43·(Wawe) wanakwenda mbio, vichwa juu, na macho yao hayapepesi, na nyoyo zao tupu

NITROGEN KATIKA KURUANI SHEREHE YA KISAYANSI

Neno هَوَآءٌ۬ limetajika katika kuruani Tukufu mara moja tu. Nalo lina maana ya “Tupu” yaani hakuna kitu au Hewa.

Nitrogen ni Aina Ya Element au Hewa ambayo ipo karibu asilimia 80 (80%)kuliko Element nyinginezo zote. Nayo ni Madhubuti (Stable) Haiathiriki na chochote.

Hewa tunayotumia katika kupumulia ni 78 % ya Nitrogen na 20.95% ya Oxygen. Na Elements nyinginezo kidogo kama vile Argon, Carbon Dioxide, Neon, Helium na Hydrogen. Nitrogen tunayoitumia haibadiliki wala kuathirika  baadaye tunaipumua nje hivyo hivyo kama mwanzo. Tunatumia Oxygen na kutoa Carbon Dioxide ambayo CO2 ni chakula cha Mimea. Tunapopumua  tunatoa 78 % Ya Nitrogen, 16% ya Oxygen na 4% ya Carbon Dioxide. Hewa hii yaani Nitrogen haiathiriki kwa Photosynthesis au baada ya matumizi ya binaadamu au wanyama kwani ni hewa iliyo madhubuti sana.(Inert)

Katika kuruani neno Hawaa linaashiria Hewa ya Nitrogen ambayo haikujulikana wakati huo wa karne ya 7 wakati kuruani iliposhuka. Bali iligunduliwa na Scottish physician aliyejulikana kwa jina Daniel Rutherford katika mwaka wa 1772

KATIKA KURUANI TUKUFU.

Ukihesabu herufi za هَوَآءٌ۬ “Hewa” katika Aya hii utaona zimetumika kama ifuatavyo:

مُهۡطِعِينَ مُقۡنِعِى رُءُوسِہِمۡ لَا يَرۡتَدُّ إِلَيۡہِمۡ طَرۡفُهُمۡ‌ۖ وَأَفۡـِٔدَتُہُمۡ هَوَآءٌ۬ الدّخان

Haa =6 Waw=3 Alif=2 na Hamzah=3 Na Jumla ni 14

(6 + 3 + 2 + 3=14)

na namba hii 14 katika Chemistry inaashiria  ATOMIC MASS YA NITROGEN ambayo ni 14 (Atomic mass: 14.0067 u)

Jambo lingine la kushangaza ni kwamba namba ya Aya ambayo ni 43 ni PRIME NUMBER ya 14 katika Table au mraba wa Prime Numbers wa Hesabu. Na Pia Aya hii ipo katika sura namba 14!!!

CARBON KATIKA KURUANI SHEREHE KISAYANSI

Muujiza Mwingine ni katika Sura Ya Al-Dukhan nao pia unashangaza kwani namba ya Sura ambayo ni ya 44 ni sawa na Atomic Mass ya Nitrogen ambayo pia ni 44. Namba 44 Sura katika Kuruani ambayo ni ADUKHAN yaani “MOSHI” au “SMOKE” inaashiria Atomic Mass ya Carbon ambayo ni 44

je unaona maajabu ya Kuruani? Tunaona Yule aliyeumba ulimwengu/malimwengu ndiye yule yule aliyeshisha kuruani.

Namba ya Sura Inayojulikana kama AL-DUKHAN (Yaani SMOKE) ni 44 na namba hii ni Atomic mass ya Carbon Dioxide ambayo ni Moshi.

Ukiangalia Sayansi ya Kuungua Vitu utaona Carbon Ndiyo inayohusika zaidi kuliko aina ya hewa nyinginezo. Kwa Mfano kitu kikiungua utaona Nitrogen haiathiriki wala kuungua kwani ni aina ya hewa ambayo madhubuti (inert), Methane na Oxygen zitaathirika na kuzalisha Carbon kwa wingi ambayo ni hewa na Maji kidogo.

N2 (Nitrogen 80%) Isiyoungua+ CH4 (Methane)Carburant + 202 (20% Oxygen)——->Co2 (Fume) + 2H20 (Water)

Atomic Mass 44 ya Carbon inatokana na Atomic Mass ya Carbon kujumlisha Atomic Mass ya Oxygen.

Atomic Mass= 12 (Carbon) + 2 X 16 (Oxygen)

12 + (2 x 16)=44

Katika Mtandao tunapata pia uhakikisho wa  jawabu la Atomic Mass ya Carbon ni 44.01 g/mol

Ndugu Waislamu angalia Kuruani ilivyojaa Maajabu yasiyo mwisho. Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.

JINA LA BWANA “BAKENKHONSU” NDIYE “HAMANA” ALIYETAJWA KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Namba 28 Aya Namba 38

وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ مَا عَلِمۡتُ لَڪُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَيۡرِى فَأَوۡقِدۡ لِى يَـٰهَـٰمَـٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجۡعَل لِّى صَرۡحً۬ا لَّعَلِّىٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّى لَأَظُنُّهُ ۥ مِنَ ٱلۡكَـٰذِبِينَ (٣٨)

SWAHILI

38-Na Firauni akasema: “Enyi wakuu! Simjui aliye mungu wenu mwingine asiyekuwa mimi. Basi ewe Hamana! (Nifanyie matufali). Niwashie moto juu ya udongo (wa matufali hayo mpaka yakauke barabara) unijengee mnara ili nimuone Mungu wa Musa, na mimi namdhani kuwa ni katika waongo (lakini haidhuru twende nikamtazame huyu Mungu wake)

English

38-The Pharaoh said, “My people, I know no one who could be your lord besides myself. Haman, construct for me a tower of baked bricks so that I may climb on it and see the God of Moses; I think he is a liar.”

HISTORIA YA MJENZI MKUU (ARCHITECT) BAKENKHONSU ALIYEITWA HAMANA (Mtumishi wa Mkuu wa miungu ya wakati huo)

Bakenkhosu alikuwa Mmoja wa MaKuhani wakubwa walioajiriwa katika Hekalu ili wasimamie ibada ya mungu (Wakati huo waliamini kwama ni Mkubwa wa Miungu wote na kwamba ndiye aliyeumba ulimwengu)) aliyejulikana kwa jina kama Amun.(Kuna Sanamu la Amun lililomwakilisha mungu huyu huko Ujerumani (Munich) katika Jengo la Makumbusho la Kimisri (Egyptian Museum).

Habari za maisha yake yameandikwa nyuma ya Sanamu hilo.

(“I performed benefactions in the Estate of Amun while I was Chief of Works for my lord. I made for him the Temple of Ramesses II-who-hears-Prayer, at the Upper Portal of the Temple of Amun. I erected obelisks in it, of granite stone, whose beauty reached (up) to the sky)

(Angalia Picha ya Sanamu lake hili hapa Chini).

Historia inasema kwamba Mtu huyu aliajiriwa katika Hekalu hilo maisha yake yote na alipitia vyeo mbalimbali katika ukuhani na Unabii na Mwishowe alichaguliwa na kuwa Nabii wa Kwanza wa Amun. Bwana huyu alikuwa na Elimu kubwa ya Ujenzi (Architect) wakati huo.Alipewa Miradi mbalimbali ya Ujenzi na Mfalme wa Misri (Firauni) aliyejulikana kama Ramesses II (Ramesses the Great who was the most powerful pharaoh of the New Kingdom). Mjenzi (Architect) Huyu ndiye aliyejenga Hekalu linalojulikana kama Karnak Temple huko Cairo. (Hivi leo Karnak Temple inatembelewa na Watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Hekalu hili limejengwa kwa ufundi wa hali ya juu usio mfano, na Gharama Kubwa imetumika katika Ujenzi huu. Na hii inaonyesha Kwamba Ramses II (Firauni) alitilia umuhimu sana Ujenzi wa Majengo makubwa makubwa. Na katika Jengo hili kuna Sanamu kubwa Za Mfalme Ramses II(Firauni).

Historia ya Egypt tunaweza kuigawa katika sehemu tatu. Zamani, Katikati na Mpya (Old, Middle na New Egypt). Bakenkhonsu aliishi katika kipindi cha Egypt Mpya (New Egypt) katika karne ya 19. Mfalme (Firauni) wa wakati huo alijulikana kama .Ramesses II

Maandishi yaliyochambuliwa na Wataalamu huko Cairo (Egypt) yanatufafanulia zaidi Kuhusu asili ya Jina Hamana. HieroGlyphics au Maandishi ya zama za Firauni yanayowakilisha Jina hilo ni “ham nata tapiy amana” Neno “Ham” ni “Servant” au Mtumishi na Neno “Amana” (Kutokana na Matamshi ya Kimisri) linatokana na Jina la huyo mungu “Amun! Kwa hiyo Bakenkhonsu alijulikana kama “Ham Amana” (Mtumishi wa Amun) Na kuruani kwa lugha ya Kiarabu (Arabic Language) inatumia Jina Hamana yaani (Ha +Mana). Kwa kifupi Bakenkhonsu alijulikana kama Hamana yaani Mtumishi wa mkubwa wa miungu huyo Amun na Pia alikuwa Architect Mkubwa kwa wakati huo.

Na lugha hii ya zamani huko Misri yaani “HieroGlyphics” imechambuliwa vizuri zaidi baada ya kufukuliwa kwa Jiwe Maarufu linalojulikana kama Rosetta Stone katika mwaka 1799 lililoandikwa kwa Maandishi ya aina tatu; Kimisri au HieroGlyphics, Kigiriki na Ki Demotic. Na baada ya muda mrefu wa Juhudi za Wataalamu Mbalimbali katika kutafuta njia za kufasiri maandishi haya hatimaye katika mwaka 1820s Mfaransa aliyejulikana kama Jean-François Champollion alikamilisha kufasiri Maandishi yote ya Hieroglyphics.

MUUJIZA WA KIHISTORIA KATIKA KURUANI TUKUFU.

Mtume Mohamed alipata wapi habari kama hizi ambazo hazikuandikwa na kitabu chochote ulimwenguni na wala hakuna aliyejua. Jina hili la “Hamana” lipo katika Kuruani kiajabu sana na tunafahamu zaidi sasa baada ya Machimbuzi ya hivi karibuni Huko Cairo Egypt.Yaani habari hizi ziliandikwa katika Sanamu la Bakenkhonsu lililofukuliwa huko Misri nalililoandikwa kwa Lugha ya HieroGlyphics.

Jina Hamana limetumika katika Biblia Linamuashiria Kiongozi huko Persia (Iran) chini ya Mfalme Ahasuerus. lakini hakuna habari za Hamana aliyekuwa Kuhani na Mtaalamu aliyekuwa Mjenzi mkuu (Architect) huko Misri katika Enzi za Firauni Ramsses II. Kipindi alichotawala Ramesses II ni kuanzia mwaka 1279 mpaka 1213 BC (Before Christ) yaani kabla ya Kuzaliwa Nabii Isa. Muujiza ni kwamba Kuruani imetaja Jina la Hamana ambalo halikujulikana mpaka baada ya Kufukuliwa kwa Sanamu la Bakenkonsu na pia baada ya wataalamu kusoma namna ya kufasiri maandishi ya enzi ya Firauni baada ya Kusoma Lugha ya HieroGlyphics katika Rosetta Stone.(Angalia Picha hapa chini)Hapa Kuruani Inatufichulia yaliyopita. Mambo yalifichika na kufukiwa chini ya Ardhi baada ya Karne na karne. Yaani baada ya Miaka Mingi. Elimu za Kisasa zinafasiri habari hizi zilizoandikwa kwa lugha tusizojua. Leo hii tunaona Muujiza mbele ya macho yetu. Allahu Akbaru. Allahu Akbaru.

UJENZI KWA KUTUMIA UDONGO ULIOUNGUZWA KWA  MOTO.

Muujiza wa Kisayansi katoka katika Aya Hii Ni kutumia Moto na Kupasha moto Matofali ili Kuyageuza Mawe. Wataalamu wamehangaika sana kuelewa Ufundi waliotumia Mafirauni katika Ujenzi wa Majengo kama vile Pyramids huko Egypt.(Angalia Picha hapa Chini) Walidhanu kwamba Mawe waliyotumia yaliletwa kutoka mbali sana na ilibidi watumishi wengi sana katika juhudi hizo. Ufundi wa Ujenzi uliofichikana mpaka mwaka 1981 wakati Mtaalamu alipokuja na Nadharia inayohusiana na Kuchoma Matofali ya Udongo na kuyageuza mfano wa Mawe. Katika Mwaka 2006 Nadharia hii ikakubaliwa na Wataalamu wengineo baada ya Majaribio ya Kisayansi kwa kutumia vyomob vya kisasa vya Hali ya Juu. Katika enzi Ya Mtume Mohamed hawakujua Utaalamu huu. Majengo yaliyojengwa huko Egypt kama vile Pyramids yanatupa mafundisho makubwa sana. Kwani Firauni alidai uungu na alijenga majengo marefu na makubwa sana ambayo yalichukua karibu miaka 4500, na ni muda ambao hakuna sehemu nyingine duniani iliyoweza kushindana na ufundi huu. Leo hii majengo haya yamebaki ili watu wasome na waelewe kwamba Mungu yupo na mwenye uwezo wa kila kitu na waka tusidanganyike na mendeleo ya aina yeyote hapa duniani.

Haya Majengo yaliyobaki kama vile Pyramids na mengineyo ni baadhi tu ili tupate kusoma na kuwa na fundisho lakini mengineyo yamevunjwa vunjwa kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu Mtukufu kama anavyosema katika Aya Ifuatayo:

Sura Namba 7  Ayat Namba 137

وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَـٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَـٰرِبَهَا ٱلَّتِى بَـٰرَكۡنَا فِيہَا‌ۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْ‌ۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُ ۥ وَمَا ڪَانُواْ يَعۡرِشُونَ (١٣٧)

SWAHILI

137-Na tukawarithisha watu waliokuwa wanaonekana madhaifu (waliokuwa wakionewa; nao ndio hao Bani lsraili); (tuliwarithisha miji ya) mashariki ya ardhi na magharibi yake ambayo tuliitia baraka (nyingi miji hiyo). Na likatimia neno jema la Mola wako kwa wana wa Israili; kwa kule kuvumilia kwao. Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na watu wake; na (pia) yale waliyokuwa wakiyajenga.

ENGLISH

137-And We made a people, considered weak (and of no account), inheritors of lands in both east and west, – lands whereon We sent down Our blessings. The fair promise of thy Lord was fulfilled for the Children of Israel, because they had patience and constancy, and We levelled to the ground the great works and fine buildings which Pharaoh and his people erected (with such pride).

Ujuzi huu umejulikana hivi karibuni na ajabu kubwa ni kwamba Kuruani inatuambia ufundi huu uliofichika kwa muda mrefu. Mtume Mohamed alijua vipi Architecture au Ufundi wa Ujenzi wa hali ya juu kama huu. Na Waarabu wa Mecca hawakujenga majumba marefu kama Pyramids na Mengineyo. Huu ni Muujiza siyo mdogo. Kuruani ni Muujiza Mkubwa Sana na Mtume ni wa haki. Haya yote yamekuja kututhibitishia leo hii katika enzi ya Sayansi kuhusu Ufundi huu na mengi mengineyo.

sanamu la Bakenkhonsu (anayejulikana kama Hamana katika Kuruani Tukufu) huko Ujerumani (Munich) Egyptian Museum. Maisha yake yameandikwa nyuma ya sanamu hili

Pyramid Huko Misri Cairo. Dalili la Udongo juu ya Jengo hili linathibitisha kwamba limejengwa kwa matofali ya udongo yaliyochomwa na siyo Mawe kama walivyodai hapo awali. Sasa Mtume mohmaed alijua vipi habari zilizofichikana miaka mingi . Huu Ni Muujiza usiyo mdogo. Allahu Akbar

Hili ndilo Jiwelinalojulikana kama “Rosetta Stone”limeandikwa kwa lugha Tatu. Hieroglyphics (juu), Demotic (katikati) and Greek (chini) na jiwe hili lilisaidia katika kusoma na kuchambua maandishi ya Kimisri ya hapo zama za Firauni. Yaani Maandishi ya Hieroglyphics