UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD

KAMA TUNAVYOONA KATIKA PICHA HAPA JUU-SAYANSI YA MAISHA YA NYOTA (LIFE CYCLE OF THE STAR)
Kwa kifupi Kama tunavyoona katika picha hii kwamba Maisha Ya Nyota huanzia na Kung’ara kwake mpaka inapokufa na kutokutoa mwanga tena, na katika hali hii inapitia daraja mbali mbali kwa majina mbalimbali kufuatana na ukubwa wake.
Kwa Mfano Average Star (Nyota ya katikati) huishia na kuwa White Dwarf na mwishowe Black Dwarf. Lakini Massive Star (Nyota Kubwa) huishia na kuwa Neutron Star au Black Hole.
Maisha ya nyota zote zinaanzia katika Mawingu ya Gesi(Hydrogen, Helium na Plasma na Vumbi) Angani linayojulikana kama “Stellar Nebulae” Na Mwingiliano wa Nuclear (Nuclear Reaction) Katika Nyota unasababisha Nyota zing’are kwa muda mrefu. Umri wa Nyota unategemea ukubwa wake, kwani Nyota zilizo kubwa sana zinatumia Hydrogen yake (Mafuta Yake) kwa haraka zaidi kuliko Nyota Ndogo Na Maisha yake yanakuwa Mafupi (Mamia Ya Miaka) ukilinganisha na Nyota ndogo ambazo huishi kwa muda mrefu zaidi kutokana na matumizi madogo ya hydrogen yake (Mafuta Yake) Na kuishi kwa (Mabilioni Ya Miaka)
Hydrogen(Mafuta Ya Nyota)ambayo inasababisha Nuclear Reactions(Mwingiliano Ndani ya Nuclear)katika Nyota inapoanza kwisha basi itaingia katika hatua ya mwisho (final stage) ya maisha yake na baada ya muda itavimba, kubaridika na kubadilika rangi na kuwa Umbile Kubwa lenye rangi Nyekundu (Red Giants).
Njia zitakazofuata hizo Nyota zinategemea Ukubwa wa Nyota. (Mass of the Star).
Nyota Ndogo kama vile Jua letu litapita katika njia ya utulivu na Baada ya kwisha mafuta yake (Hydrogen) na Kwisha nguvu (Tabaka lake la kwanza kupasuka)litaingia katika Stage inayojulikana kama “Planetary Nebula” kwani umbile hili linafanana na Planet na hatimaye kuwa na Umbile lenye kung’aa kwa jina la White Dwarf na baada ya muda kubaridika na kutokung’aa na hapa tutalipa jina lingine la Black Dwarf.
Nyota kubwa huishia Na Kuwa Na Nguvu Kubwa (Energetic and Violent), Na kisha kupasuka na kusambaa angani na Nyota hiyo inajulikana kwa jina la Supernova.
Na mara baada ya Vumbi la anga kuondoka itabaki Nyota iliyojijaa(dense Star) inayojulikana kama “Neutron Star” Nayo hujizunguka kwa mbio sana na hujulikana kwa jina la Pulsars.
Nyota Yeyote Inayopasuka kama ni kubwa sana basi husababisha kuzuka Tundu La Giza Huko Angani linalojulkana kama “Black Hole”.
MUUJIZA KATIKA KURUANI
Kufuatana na Picha Hapa Juu Tutazungumzia na Kutoa Uthibitisho kutoka katika kuruani kwa Milango Mitatu:
(1) Nebulla (2)Neutron Star (3)Black Holes.
Nebulla (Stellar or Planetary)
Chapter (55) sūrat l-raḥmān Aya Namba 37(The Most Gracious)
Na Mbingu Itakapopasuliwa Na kuwa Nyekundu (au Uwa la Waridi) kama Vile Ngozi Nyekundu
Then when the heaven is rent asunder, and it becomes rosy or red like red-oil, or red hide.
فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ وَرۡدَةً۬ كَٱلدِّهَانِ (٣٧)
Aya Hii inatuelezea Mawingu Haya mfano wa Uwa la Waridi (Angalia Rangi Ya Mawingu katika Picha) Na Hivyo ndivyo siku ya kiama tutakavyoonyeshwa Mbingu itakapopasuka. Na mfano mdogo tu kwetu leo hii ni hii Nebula ambayo wana sayansi wamepiga picha kwa kutumia vyombo kama vile Telescope za kisasa.Na siku ya kiama tunaona zaidi ya hii.
———————————
Neutron Star “Pulsars”
Chapter (86) sūrat l-ṭāriq Aya Namba 1-3 (The Night-Comer)
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ (١) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ (٢) ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ (٣)
Naapa Kwa Mbingu na Kinachogonga (The Knocker)
Je kipi kinachokujuulisha kinachogonga?(The Knocker) Ni Nyota Ipenyezayo ( kwa nguvu/ukali wake)-It is the piercing star.
Katika Aya Hizi Tunaelezwa kuhusu Neutron Star (Nyota Zinazogonga kama nyundo) zinazojulikana kama “Pulsars” Ni Nyota yenye uwezo wa kupenya kila kitu (inayosababisha kuweko kwa Tundu katika Anga)
————————————-
Black Holes (Mashimo Ya Giza Angani)
Chapter (53) sūrat l-najm Aya Namba 1(The Star)
وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ (١)
Naapa Kwa Nyota Inapojizamia Yenyewe-By the star when it goes down, (or vanishes).
Aya Hii Inazungumzia Nyota inapokufa na kusababisha kuwa Shimo la Giza Angani
Chapter (81) sūrat l-takwīr Aya Namba 16(The Overthrowing)
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ (١٥) ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ (١٦)
Naapa kwa kisichoonekana au kinachojificha, Kinachotembea na Kufagia (Kusafisha)-So, verily I swear of that invisibles * that running and sweep”
Aya Hizi mbili zinatupa habari zaidi ya Matundu ya Giza huko Angani ambayo yamejificha (Invisible), Hayana Utulivu Yaani Yana Movement (Running) na yanavuta (sweep)kila kinachokaribia karibu yao kama vile mashine za kufyonza taka.
Mbele ya Macho Yetu tunaona Maajabu Ya kuruani. Wataalamu Wametuchorea Picha hapa Juu ya Maisha Ya Nyota “Life Cycle” Sasa Mtume aliishi huko Jangwani katika karne ya saba. Alijua vipi Elimu hizi ambazo leo hii kumetumika Vyombo Mbalimbali kuvisoma. Ni Elimu za kisasa na siyo enzi ya Ugiriki. Tufungue Macho. Maajabu na Inatisha Kwani Yule Yule Aliyeumba Ulimwengu Ndiyo Yule yule Aliyeshusha Kuruani ambayo Ni Muujiza miongoni mwa miujiza mikubwa isiyo na mfano. Tumche na Tumwogope Mungu!!!
UCHAGUZI WA KUZALIWA MTOTO WA KIKE AU KIUME UNATEGEMEA MBEGU YA BABA NA SIYO YAI LA MAMA/SEX DETERMINATION DEPENDS ON THE SPERM OF THE MALE
MBEGU YA MUME NDIYO INAYOFANYA UAMUZI WA ATAKAYEZALIWA NI WA KIUME AU WA KIKE/SEX DETERMINATION DEPENDS ON MALE SPERM
Katika Mwaka 1905, Nettie Maria Stevens (1861-1912) na Edmund Beecher Wilson (1856-1939) Waliokuwa wataalamu wa Elimu Ya Genetics (Geneticists) Walifanya Utafiti na kugundua Asili yetu kwamba tunatokana na Mbegu Ya Baba, Na kwamba Mbegu hiyo Ndiyo inayohukumu Uchaguzi wa Kuzaa Mtoto wa Kike au Kiume.
Hawa Wataalamu Wa Kimareekani walipata heshima kubwa baada ya kufanya uvumbuzi katika mwaka 1905 kwamba Mbegu ya baba ina (XY) Sex Chromosomes/Gamets na Yai la Mama lina (XX) Sex Chromosomes/Gametes. Kwa hiyo Mbegu ya Baba ndiyo yenye kufanya uchaguzi wa kuzaliwa Mtoto wa kiume au wa kike. Yaani Mbegu ya Baba ina (XY) X ya Uke Na Y ya Ume Sex Chromosomes au Gametes Na Yai la Mama lina XX (Uke) Sex Chromosomes au Gametes peke yake.
Mbegu ya Baba inapoingia katika Yai na ikiwa mbegu hiyo itakafanikiwa kuingia Yai Hilo na hiyo Mbegu ni (X) Sex Chromosome basi mtoto atazaliwa wa Kike kwani Mama ana mbegu ya (XX) Chromosome na zikikutana (XX) Mbili Mtoto atazaliwa wa Kike. na ikiwa Mbegu Ya Baba ambayo itafanikiwa kuingia katika Yai ni (Y)sex Chromosome na Kwa vile Mbegu Ya Mama Ni (XX) Chromosome basi zitakutana Mbegu za aina Mbili (XY) yaani (Y) Ya baba na (XX) ya Mama basi Mtoto atakayezaliwa atakuwa ni Wa Kiume.
Kwa hiyo Baba ndiye anayohukumu atakayezaliwa katika uchaguzi yaani Mtoto atazaliwa wa kike au wa kiume. Yaani Mbegu ya kiume au (Sperm) Ndiyo yenye kuhukumu uchaguzi wa kike au kiume. Hivi ndivyo Sayansi Inavyotuambia baada ya utafiti mrefu.
Lakini Miaka 1400 iliyopita huko Arabuni Katika Mji wa Mecca Mtume Mohamed alishushiwa Kuruani na habari hizi.
Aya zinazofuata zinaelezea kwa njia nzuri sana kupita lugha za sayansi.
Mwenyeezi Mungu anasema katika Sura zifuatazo:
Sura Namba (76) sūrat l-insān (Man) Aya Namba 2
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا
Kwa hakika Tumemuumba Binaadamu kutoka katika Tonye la Baba lenye X na Y Gametes au Semen. Ili tumpe mtihani na Kisha tukamjaalia mwenye kusikia na Kuona
Sura Namba (32) sūrat l-sajdah (The Prostration) Aya Namba 8
ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ مَاءٍ مَهِينٍ
Kisha Tukajaalia Kizazi Chake kutokana na Mbegu ya Baba (X au Y) au Semen ambayo Inatokana na maji Yaliyo dhalili
Sura Namba (75) sūrat l-qiyāmah (The Resurrection)
أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةً۬ مِّن مَّنِىٍّ۬ يُمۡنَىٰ (٣٧) ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً۬ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ (٣٨) فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ (٣٩)
Je hakuwa Mbegu X au Y (Ya Baba) kutokana na Mchanganyiko wa asili yaani X na Y Chromosomes au Gametes au Semen Kisha akawa kipande cha Nyama (Blastocyst) na Tukakiumba na Kusawazisha na Kutokana na hicho tukaumba Mume na Mke (male and Female)
Katika Aya Hapa Juu tunapata maneno matatu kwa maana moja
نُطْفَةٍ أَمْشَاجٍ
سُلَالَةٍ
مَّنِىٍّ۬ يُمۡنَىٰ
maneno haya matatu kwa kiingereza au lugha ya sayansi yana maana moja ya “Semen” kwa maana ya Mbegu Ya Baba ilichanganyika (X na Y Chromosomes/Gametes)
Na neno نُطۡفَةً۬ katika Aya namba 39 sura ya Alkiyamah namba 75 lina maana ya Mbegu Moja Ya Baba (Yaanni X au Y) katika Aya Hii Mwenyeezi Mungu anasema Kwamba asili Yetu ni Mbegu ya Baba (Yaani X au Y Gamete). kabla Ya Fertilization Kufanyika katika yai la Mama na kuwa XX au XY (XX atazaliwa mtoto wa Kike na XY atazaliwa mtotowa Kiume).
ELEMENT YA CARBON KATIKA UTAFITI WA UMRI WA VIUMBE
MATUMIZI YA CARBON YANATHIBITISHA NENO “NGAMIA” KATIKA KURUANI NI “PUNDA” SIYO NGAMIA NA PIA KURUANI ILIYOGUNDULIWA UINGEREZA NI ILE ILE TANGU ENZI YA MTUME MOHAMED BILA KUGUSWA
Kwa kutumia Elimu hii ya “Carbon Dating” Wataalamu wamechunguza Mifupa ya Ngamia huko Palestine kwa kutumia elimu ya Carbon Dating au Absolute Dating. na wakakuta Ngamia wa mwanzo kuja huko Arabuni ilikuwa mwaka Elfu Moja kabla ya Enzi ya Ukristo yaani 930 BC Wanasema katika Magazine ya National Georaphic kwamba “Domesticated Camels Came to Israel in 930 B.C.”
Hivi ndivyo Gazeti linalosema . Kwa hiyo utafiti unathibitisha kwamba Katika wakati wa Nabii Youssef kulikuwa hakuna Ngamia na usafiri wao walitumia Punda. Tukija katika kuruani tunakuta muujiza huu
Chapter (12) sūrat yūsuf (Joseph) Ayat 94 and Ayat 72
وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّى لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ -٩٤
Katika Aya Hii Neno ٱلۡعِيرُ limefasiriwa kama Ngamia na wafasiri. Lakini Leo hii kwa kutumia Carbon Wanasayansi wamegundua baada ya utafiti uliofanya wa Mifupa wa Ngamia ya muda mrefu sana huko Palestini. Mifupa hiyo inaonyesha kwamba Ngamia wa kwanza kuja Palestini ilikuwa mwaka 930 kabla ya enzi ya Ukristo yaani BC. Tafsiri iliyo sahihi ni Punda.
Ushahidi hapa chini ni Tafsiri ya Tabariy Na Kurtubiy na Pia Kamusi Ya Lisan Alarab wanasema kwamba neno hili la ٱلۡعِيرُ lina maana ya Punda
الطبري: “حدثنا القاسم قال، حدثنا الحسين قال، حدثني حجاج عن ابن جريج عن مجاهد قال، قوله: (حمل بعير) قال، حمل حمار”. طبعاً بعض المفسرين نقلوا معنى آخر من الإسرائيليات حيث اعتبروا أن البعير هي الإبل.
ففي تفسير القرطبي: ولمن جاء به حمل بعير وأنا به زعيم: البعير هنا الجمل في قول أكثر المفسرين وقيل : إنه الحمار، وهي لغة لبعض العرب; قاله مجاهد واختاره.
Utafiti huu unathibitisha Kwamba njia ya usafiri katika enzi za Nabii Yusuf/Yakoub ilikuwa ni Punda na hapa juu Aya hii inazungumzia Kisa cha Nabii Yusuf hapo zamani sana kabla ya Ngamia kuja hapo Palestini.
Muujiza ni kwamba Neno hili lina maana mbili; ya “Punda” Na “Ngamia” na ndiyo maana wafasiri walichukua “Ngamia” lakini baada ya utafiti wa sayansi sasa tunaelewa kwamba wakati wa Mtume Mohamed (sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu zimfikie) Neno hili lilipokelewa kwa maana ya Punda na siyo Ngamia. Na Mtume Pia alijua kwamba Ni Punda.
Na Mwenyeezi Mungu alichagua neno Hili lenye maana mbili ya Ngamia na Punda ili iwe Muujiza kwetu katika kipindi cha Sayansi. Mwenyeezi Mungu angelitaka angechagua Neno la Himar (Punda) au Gamal (Ngamia) na angefanya hivyo kusingepatikana Muuujiza tunaopata leo hii. Na hii inaonyesha Muujiza mkubwa kwani Mtume Hakuigusa kuruani kwa kubadilisha chochote.
Neno hili lilibaki hivi hivi na wafasiri walifasiri kufuatana na Elimu zao za wakati wao. Hawakukosa bali walifanya jitihada kubwa katika kazi hiyo.
Kuruani ya hapo awali iliyogunduliwa huko Uingereza na ambayo imewekwa hapo Birmingham Library ni kithibitisho kikubwa kwamba kutabu hiki hakikuguswa. Utaalamu wa Carbon Dating Ulitumika katika utafiti huu.
(The tests, carried out by the Oxford University Radiocarbon Accelerator Unit, showed that the fragments, written on sheep or goat skin, were among the very oldest surviving texts of the Koran. These tests provide a range of dates, showing that, with a probability of more than 95%, the parchment was from between 568 and 645). Kwa Kweli haya yote yanathibitisha kwamba kuruani ni Maneno Yake Mwenyeezi Mungu na Pia Haikuguswa kama Message zilizopita. Mwenyeezi Mungu amesema kwamba atahifadhi Kuruani na hivyo ndivyo ilivyokuwa na itakavyokua.
ANGALIA MLINGANISHO WA KUSHANGAZA BAINA YA CHUMA KATIKA ARDHI NA SURA YA CHUMA KATIKA KURUANI TUKUFU
Sayansi na Sura ya Alhadiyd- ٱلۡحَدِيدَ Sura Namba 57
Nimeelezea kwa kirefu Katika Video Namba 11 (Sauti Za Mwandalizi)
1- Chuma Ipo Katikati Ya Ardhi /Sura Ya Al-Hadiyd ipo katikati ya kuruani
2-Protons za Chuma (iron) Ni 26 / Katika Sura Ya Al-Hadiyd Aya ya 25 inazungumzia chuma na ukiongeza Basmala inakuwa Aya ya 26. Na Ukihesabu ABJAD au Gematrical Values za herufi HADIYD pia unapata jumla ni 26.
3-Isotope za Chuma zipo 7 tu na mojawapo ni aina ya 57 ambayo ipo katikati ya aina hizo / Mojawapo ya aina 7 za Iron ni Namba 57 na hiyo ni ya katikati. Na pia Chuma Ipo katikati ya ardhi. Na Kithibitisho kingine. Neno Nazala limetajika katika sura ya Hadiyd mara 5 na Neno Samaa limetajika mara 7 nazo ukiziunga unapata 57 kuashiria namba ya sura.
4/Umbali kutoka katika Gamba la ardhi mpaka katika chuma ambayo ipo katikati ya ardhi ni kilomita 5100 / Ukihesabu Aya za kuruani kuanzia mwanzo mpaka sura ya Alhadiyd Aya namba 25 utapata jumla ni aya 5100!!!!
5-Umbali wa Mantle Ni 2885 Kilomita / Ukihesabu ABJAD au Gematrical Values za herufi ya aya namba 25 kuanzia mwanzo mpaka neno la mwisho kabla ya neno “hadiyd” yaani chuma utapata 2885!!!
6-Specific Heat Ya Chuma Ni 450 J/Kg / Ukihesabu herufi kuanzia mwanzo wa sura ya Alhadiyd mpaka kabla ya aya inayotaja Hadiyd utapata herufi 450!!!!
7-Melting Point ya Chuma ni 1538 Degrees Celcius / Kuanzia sura namba 17 aya namba 50 (solid iron)mpaka sura namba 34 aya namba 10 (molten iron) kuna aya 1538!!!!!
8-Boiling Point ya Chuma ni 2862 Degrees Celcius / Soft Iron katika kuruani ni aya namba 10 Sura namba 34 na ajabu ni kwamba kutoka katika neno “soft iron” mpaka mwisho wa sura hii kuna herufi 2862 (Gaseous Stage) Inafanana na Herufi.!!!!!
9-Melting Temperature Ya IronCore ni zaidi ya 6200 Degrees Kelvin / Sawasawa na ABJAD au Gematrical Values ya herufi zote katika Aya ya IRON (aya namba 25)ambayo ukihesabu utapata idadi ya 6205!!!
10-Chuma Ni Element ya 6 katika Elements za Milky Way Galaxy / Iron (Chuma) Imetajwa katika kuruani mara 6 tu!!!
11-Kuna Karibu 0.6 % ya Chuma katika Ulimwengu / Iron (Chuma) Imetajwa katika kuruani mara 6 tu!!!
12-Chuma Imekuja ardhini kutoka katika Nyota kubwa zinazojulikana kama red super-giants. Wakati wa Supernova (kupasuka kwa nyota iliyofikia mwisho wa uhai)Unapotokea vipande vya chuma husambazwa angani na vingine kuja duniani. Na hivi ndivyo Chuma ilivyokuja ulimwenguni mamilioni ya miaka iliyopita. Ardhi haina joto la kutosha kuweza kusababisha kuweko kwa chuma bali Nyota kubwa nyinginezo zina joto kali ambalo lina uwezo wa kuunda chuma (kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu yeye ndiyo Muumba) / Sura Ya HadIyd Aya Namba 25 Inasema kwamba Tumeleta Chuma na wala haikuumbwa katika ardhi.
13-Chuma Ina Ugumu / Na Aya Namba 25 Sura Ya Hadiyd Inasema kwamba Chuma ina Ugumu.
14-Chuma Ina Manufaa Makubwa Katika Maisha / Na Aya Namba 25 Sura Ya Hadiyd Inasema kwamba Chuma ina Manufaa Makubwa.
Je Ndugu Waislamu Haya Mambo yanashangaza sana. Je huu mlinganisho umekuja vipi? je Kibahati bahati tu? au imepangwa? Kwa kweli sisi hatuna la kusema isipokuwa Allahu Akbar. Alhamdu lilahi aliyeumba ndiyo yule yule aliyeshusha kuruani hii. Kwa kweli elimu yake ni kubwa sana tena sana. Kwa kweli inatisha.
BAADHI YA PICHA HAPA CHINI ZINATUELEZEA ZAIDI KUHUSU CHUMA NA PIA USHAHIDI WA KISAYANSI.

Aina 7 za Chuma. Chuma Namba 57 ipo katikati. Katika Kuruani sura ya 57 ni ya chuma nayo ipo katikati

Kutoka Katika Gamba La Ardhi Mpaka katika Outer Core yaani kabla ya Chuma iliyoganda ni Kilomita 5100 sawasawa na aya za kuruani kuanzia mwanzo wa sura ya Alfatiha mpaka mwisho wa aya namba 25 ya sura ya alhadiyd

Iron ni Element Ya 6 katika Milky Way Galaxy sawasawa na Aya 6 tu zilizoshuka na zinazozungumzia Chuma katika kuruani.
VIPIMO MBALIMBALI KATIKA KURUANI
Vipimo vya kisasa vimeashiriwa katika kitabu kitukufu cha Kuruani kwa njia ya ajabu sana. Kwa kweki inashangaza.
MITA (Meter)
Chapter (69) sūrat l-ḥāqah (The Inevitable) Aya Namba 32
ثُمَّ فِى سِلۡسِلَةٍ۬ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعً۬ا فَٱسۡلُكُوهُ (٣٢)
Tafsiri Ya Aya
32. “Tena katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini muingizeni, (mtatizeni).”
Sherehe Ya Aya
Maajabu ni kwamba urefu huu uliokuwa unatumiwa tangu hapo zamani unajulikana kama Cubit na katika Aya ya kuruani ni ذَرۡعُهَا ni urefu huu wa Cubit. Ukienda katika Mtandao na ukatumia Calculator na kubadili kipimo hiki cha Cubit 70 katika kipimo cha kisasa cha Mita utapata Mita 32 ambayo inalingana na namba ya Aya hii hii!!!! katika Msahafu Jambo hili kwa kweli linashangaza. na wala sio kwa bahati kwani kuruani ina mengi ya mfano huu na haiwezekani bahati kurudia rudia kila mara.
Kilomita (Kilometres)
Kama tulivyoona katika maelezo kuhusu Chuma. Tumeona kipimo cha Kilometer 5100 kutoka katika Gamba la Ardhi (Earth Crust) mpaka katika Chuma ambayo ipo katikati ya ardhi. Na ajabu ni kwamba Ukihesabu Aya za Kuruani kuanzia mwanzo wa Sura ya Alfatiha mpaka Aya inayozungumzia Chuma katika sura ya Alhadiyd utapata Aya 5100!!! kwa kweli hii inaonyesha kwamba kuruani imepangwa na ni muujiza sio mdogo.
MAILI (Miles)
Katika Kuruani tunakuta pia Maili imeashiriwa pia kiajabu ajabu kwa njia za kushangaza sana.
Chapter (9) sūrat l-tawbah (The Repentance) Aya Namba 28
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡمُشۡرِكُونَ نَجَسٌ۬ فَلَا يَقۡرَبُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ بَعۡدَ عَامِهِمۡ هَـٰذَاۚ وَإِنۡ خِفۡتُمۡ عَيۡلَةً۬ فَسَوۡفَ يُغۡنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۤ إِن شَآءَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَڪِيمٌ۬ (٢٨)
Tafsiri Ya Aya
28. Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie huo Msikiti Mtukufu baada ya mwaka wao huu. Na kama mkikhofia umasikini, basi karibuni hivi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kwa fadhila zake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Chapter (17) sūrat l-isrā (The Night Journey) Aya Namba 1
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ (١)
Tafsiri Ya Aya
1-Utukufu ni wake yeye ambaye alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa Baytul Muqaddas-Falastini) ambao (tumeubariki na) tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake (Tulimpeleka hivyo) iii tumuonyeshe baadhi ya Alama zetu. Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kuona.
Sherehe Za Aya
Baina ya Aya hizi mbili kuna Aya 767. Ukitafuta Umbali wa Misikiti hii miwili mikubwa kwa kutumia Hesabu kwa njia Ya Coordinate Distance Calculator kutoka Katika Masjid Alharam Mpaka Masjid Alaqsa utapata Maili 767!!! ambazo sawasawa na idadi ya Aya katika kuruani baina ya Misikiti hii miwili. Umbali Kwa Hesabu Ya Maili (Geographical Distance) . Ukitafuta katika chombo chochote cha utafiti kama vile Google.
Coordinates za kaaba na Aqsa utapata vipimo vifuatavyo:
Kaaba 21.4225° N, 39.8262° E (Coordinates)
Aqsa 31.7761° N, 35.2358° E (Coordinates)
Miaka kwa kutumia Mwanga (Light Years)
Maumbile angani yametengana kwa umbali mkubwa sana na vipimo vya umbali vinavyotumika ni Light Years na siyo Maili au Kilomita kwani tunavyotumia katika ardhi yetu ambavyo ni vipimo vya umbali mdogo.
Chapter (53) sūrat l-najm (The Star)
Aya Namba 49
وَأَنَّهُ ۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ (٤٩)
Tafsiri Ya Aya
49. Na kwamba Yeye ndiye Mola wa (nyota) ya Shiira (Sirius wanayoiabudu. Hiyo imeumbwa na Mwenyezi Mungu kama viumbwa vingine vyote)
Sherehe Ya Aya
Nyota hii “Sirius” ina umbali wa 8.61 Miaka ya Mwanga (Light Years) kutoka katika ardhi. Na ajabu ni kwamba sura hii inajulikana kwa Jina la “Nyota” na Aya ya mwanzo inatujuulisha kuhusu Nyota.
Aya Namba 1
وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ (١)
Tafsiri Ya Aya
Naapa kwa nyota zinapoanguka. (zinapokuchwa) au Kisayansi Nyota Inayojifia (kusababisha Black Hole ambalo ni tundi la Kiza)
Aya Namba 32
ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَـٰٓٮِٕرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٲحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٲسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٌ۬ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ (٣٢)
Tafsiri Ya Aya
32.Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu; isipokuwa makosa hafifu, (hakuna aliyesalimika nayo); bila shaka Mola wako ndiye Mwenye maghufira mengi. Yeye ndiye Anayekujueni sana tangu Alipokuumbeni katika ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase (msizisifu) nafsi zenu; Yeye Anamjua sana aliyetakasika (na asiyetakasika).
Sherehe Za Aya
Ukihesabu kuanzia herufi ya mwisho kutoka Neno Najm katika Aya ya Kwanza ya Sura hii nayo ni herufi Mim mpaka mwanzoni mwa neno Ardhi Aya namba 32 ya sura hii utapata herufi jumla ni 861 ambazo zinalingana na umbali wa ardhi na nyota Sirius wa 8.61 light years unapogeuza katika centi light-years kwa kutumia Calculator. Yaani ukigeuza 8.61 light years katoka Centi Light Years utapata umbali baina ya Ardhi na Nyota Sirius ni 861 Centi Light Years na ambao unalingana na idadi ya herufi baina ya Aya tulizozitaja hapa. Na Centi ambayo ni chembe ndogo ya Light Years ni sawa na Herufi ambazo ni ndogo ukilinganisha na maneno.
Kuruani n iMuujiza wa miujiza mikubwa sana. hapa tunaona muashirio wa kiajabu na kushangaza. Haiwezekani kubahatisha au kuzuka kienyeji kwani maajabu kama haya yanarudiarudia mara kwa mara. Tukikosea katika maoni haya Mwenyeezi Mungu atusamehe lakini je hatuoni maajabu haya ambayo yanashangaza. Hii ni dalili kwamba yule yule aliyeumba ulimwengu ndiyo yule yule aliyeshusha kuruani tukufu. Hivi Vipimo vya kisasa havikuwapo katika enzi ya Mtume Mohamed. Sasa Mtume Mohamed (Sala na Amani za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alivisoma wapi katika karne hiyo ya saba? Je huoni dalili kwamba Kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu Mtukufu? Kuruani ni maneno yalio hai yake mwenyewe Mola na siyo mchezo. Ni maneno yanayotisha sana.
Muujiza Wa Kushangaza kuhusiana na Vipimo Mbalimbali Vya Jua Ardhi na Mwezi
1/Kipenyo (Diameter) cha Jua Katika Kuruani Tukufu
Hesabu zinatufahamisha kwamba:
Kunatakikana Jumla ya Ardhi 109 uzipange pamoja ili kusawazisha na urefu wa Kipenyo (Diameter) cha Jua
Ukigawa Diameter (Kipenyo) Ya Ardhi katika Diameter (Kipenyo) ya Jua (Vipimo vinavyojulikana Duniani Na Vyombo mbalimbali Duniani kama vile NASA-National Aeronautics and Space Administration huko America) utapata idadi ya Ardhi 109 kama hapa chini.
Sun Diameter (kipenyo)/Earth Diameter (Kipenyo)
1,391.400 Kilometres Kugawa kwa 12,742 Kilometres =109 Kilometres
Na ajabu ni kwamba katika Kuruani Kuanzia neno Ardhi وَٱلۡأَرۡضَۖ (Earth) mpaka neno Shams (Sun) بِٱلشَّمۡسِ tunapata maneno 109 sawa sawa na kipimo cha Wanasayansi Duniani baada ya kugawa Diameters (Vipenyo) hapa juu.
سُوۡرَةُ البَقَرَة
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ (٢٥٥) لَآ إِكۡرَاهَ فِى ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَىِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّـٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (٢٥٦) ٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِۗ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ (٢٥٧) أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبۡرَٲهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦۤ أَنۡ ءَاتَٮٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحۡىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۟ أُحۡىِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِى بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِہَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٢٥٨)
2/Umbali (Distance) Baina Ya Jua na Ardhi katika Kuruani Tukufu
Sun’s Diameter (Kipenyo Cha Jua) kugawa na umbali (Distance) baina ya Ardhi na Jua kwa kutumia Vipimo Vinavyojulikana na Wanasayansi Duniani kama vile Chombo cha NASA huko America.
1391,400 Kilometres Kugawa kwa 149,597,890 Kilometrres =107 Kilometres
Yaani Kwa Umbali Zinatakiwa Idadi ya Jua 107 uzipange katika Mstari Mmoja baina ya Ardhi na Jua na ajabu ni kwamba katika Kuruani idadi ya maneno baina ya neno Ardhi ٱلۡأَرۡضِۗ katika Aya Namba 255 Mpaka neno Jua بِٱلشَّمۡسِ katika Aya namba 258 Ya Sura Ya Albakarah kuna maneno 107.
سُوۡرَةُ البَقَرَة
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ (٢٥٥) لَآ إِكۡرَاهَ فِى ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَىِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّـٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (٢٥٦) ٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِۗ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ (٢٥٧) أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبۡرَٲهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦۤ أَنۡ ءَاتَٮٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحۡىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۟ أُحۡىِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِى بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِہَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٢٥٨)
3/ Kipenyo (Diameter) Cha Ardhi katika Kuruani Tukufu
(Hivi ni Vipimo Maarufu Vinavyokubaliwa na Vyombo mbalimbali Duniani kama vile NASA)
Diameter (Kipenyo) ya Mwezi= 3,474 Kilometres Diameter (Kipenyo) ya Ardhi=12,742 Kilometres
Ukigawa 12,742 Kilometres Kwa 3,474 Kilometres =3.7 Kilometres (Yaani 3 Moons ( وَٱلۡقَمَرِ ) + 0.7 Moon= Sehemu ya Moon وَٱلۡقَمَرِ )
Katika Kuruani Tunakuta Muujiza Mkubwa kwani tunapata katika Sura Ya Al-Qamar baina ya Aya Namba 2 na 5 (Yaani Baina ya Neno Qamar na Ardhi) Namba hii 3.7 .
Tukihesabu katika Sura Ya Al-Qamar Baina Ya Neno Qamar na Ardhi tunapata Aya 3 na Herufi 7 za neno إِذَا تَلَٮٰهَا
سُوۡرَةُ الشّمس
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَٮٰهَا (١) وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَٮٰهَا (٢) وَٱلنَّہَارِ إِذَا جَلَّٮٰهَا (٣) وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَٮٰهَا (٤) وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَٮٰهَا (٥) وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَٮٰهَا (٦) وَنَفۡسٍ۬ وَمَا سَوَّٮٰهَا (٧) فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَٮٰهَا (٨) قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّٮٰهَا (٩) وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّٮٰهَا (١٠) كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَٮٰهَآ (١١) إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَٮٰهَا (١٢) فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَـٰهَا (١٣) فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّٮٰهَا (١٤) وَلَا يَخَافُ عُقۡبَـٰهَا (١٥)
4/Umbali (Distance) Baina Ya Ardhi na Mwezi Katika Kuruani Tukufu
(Hivi ni Vipimo Maarufu Vinavyokubaliwa na Vyombo mbalimbali Duniani kama vile NASA)
Umbali baina ya Ardhi na mwezi=356,400 Kilometers
Diameter (Kipenyo) Ya Mwezi=3,474.2 Kilometres
356,400 Kilometres Kugawa Kwa 3,474.2 Kilometres =102.58 Kilometres .
Moons ٱلۡقَمَرُ 102 zinatakikana ukizipanga katika Mstari mmoja baina ya Mwezi na Ardhi
Katika Kuruani tunapata Muujiza Mwingine wa Kushangaza;
Herufi baina ya maneno haya mawili “Moon ٱلۡقَمَرُ na Ardhi ٱلۡأَرۡضَ ” ni 308 (Namba hii inawakikilisha Distance kwa Kilometres)na Ukigawa na herufi za neno ٱلۡقَمَرُ Qamar ambazo ni 3 (hapa inawakilisha Diameter ya Qamar) utapata Herufi 102.66 Baina Ya Maneno Mawili Qamar na Ardhi
308/3=102.66 Namba hii ni sawa sawa na Jawabu tulilopata hapa Juu za Hesabu za Wanasayansi Duniani. Baada ya kugawa Diameter (kipenyo ) na Distance (Umbali)
سُوۡرَةُ القَمَر
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ (١) وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةً۬ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٌ۬ مُّسۡتَمِرٌّ۬ (٢) وَڪَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَڪُلُّ أَمۡرٍ۬ مُّسۡتَقِرٌّ۬ (٣) وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ (٤) حِڪۡمَةُۢ بَـٰلِغَةٌ۬ۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ (٥) فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَىۡءٍ۬ نُّڪُرٍ (٦) خُشَّعًا أَبۡصَـٰرُهُمۡ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ كَأَنَّہُمۡ جَرَادٌ۬ مُّنتَشِرٌ۬ (٧) مُّهۡطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِۖ يَقُولُ ٱلۡكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا يَوۡمٌ عَسِرٌ۬ (٨) ۞ كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٍ۬ فَكَذَّبُواْ عَبۡدَنَا وَقَالُواْ مَجۡنُونٌ۬ وَٱزۡدُجِرَ (٩) فَدَعَا رَبَّهُ ۥۤ أَنِّى مَغۡلُوبٌ۬ فَٱنتَصِرۡ (١٠) فَفَتَحۡنَآ أَبۡوَٲبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٍ۬ مُّنۡہَمِرٍ۬ (١١) وَفَجَّرۡنَا ٱلۡأَرۡضَ عُيُونً۬ا فَٱلۡتَقَى ٱلۡمَآءُ عَلَىٰٓ أَمۡرٍ۬ قَدۡ قُدِرَ (١٢)