SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Sayansi Za Dunia-3

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MUUJIZA KATIKA KURUANI TUKUFU AMBAO UNA UHUSIANO NA UZITO WA MOLE MOJA YA MAJI

Nimeelezea Kwa Kirefu Maana ya Mole hapa chini lakini kwanza ningependelea kudokeza kwamba Aya Namba 18 InakarirI kiajabu sana Katika Kuruani Tukufu katika Aya Zinazozungumzia maji, Sasa tuichunguze Aya Ifuatayo kutoka katika Sura Ya Al-Bakarah Namba 2 Aya namba 22 Nimechagua Aya hii kwani Neno Maji yaani مَآءً۬ limetajika Kwa mara Ya kwanza Katika Aya hii Namba 22 Ya Sura Namba 2 Al-Bakarah.

ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فِرَٰشً۬ا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءً۬ وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَأَخۡرَجَ بِهِۦ مِنَ ٱلثَّمَرَٲتِ رِزۡقً۬ا لَّكُمۡ‌ۖ فَلَا تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ أَندَادً۬ا وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ (٢٢)

TAFSIRI

22-(Mwenyezi Mungu) Ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama busati (mliotandikiwa mstarehe), na mbingu kuwa kama paa, na akateremsha maji kutoka mawinguni; na kwa hayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua(kuwa hana mshirika).

Neno مَآءً۬ Yaani Maji lina Herufi 3 Tukihesabu Herufi hizi kuanzia Mwanzo wa Aya Hii mpaka neno مَآءً۬ lenye maana ya Maji tutapata kama ifuatavyo=

مُ Mim Herufi 5 + ٱ Alif Herufi 9 + ءً۬ Hamzah Herufi 4 Na Ukijumlisha utapata Jumla Herufi 18 yaani (5 + 9 + 4=18).

Hebu Tuendelee na Utafiti tuone maajabu ya kushangaza. Allahu Akbar.

Sasa tukihesabu kukariri kwa Herufi za neno مَآءً۬ Kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Bakarah mpaka Mwisho wa neno Maji yaani مَآءً۬ katika Aya Namba 22 utapata kama ifuatavyo

(مُ Mim Herufi 120 + ٱ Alif Herufi 139 + ءً۬ Hamzah Herufi 24=283)

Tutapata Jumla Herufi 283 na namba hii ni Ya 61 katika Prime Numbers  Na Jambo lingine la kushangaza ni kwamba Namba Hii 61 Ni ya 18 katika Prime Numbers. Na Hii ni mara ya Pili Kutajika na kukariri kwa Namba 18 . (Angalia Picha Ya Prime Number hapa chini).Allahu Akbar. Allahu Akbar

Hebu tuendelee na uchunguzi zaidi wa maajabu haya yasiyo na mwisho.

Katika Kuruani Tunakuta Pia Neno Maji مَآءً۬ limetumika Katika Sura Namba 23 ya Al-Muuminuun, Aya Namba 18 Ajabu Ni Kwamba Namba Ya Aya Pia ni 18!!!!

Hebu tuendelee na Utafiti.

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٍ۬ فَأَسۡكَنَّـٰهُ فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابِۭ بِهِۦ لَقَـٰدِرُونَ (١٨)

TAFSIRI YA AYA 

Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi, na tukayatuliza ardhini, (tukayahifadhi ndani ya ardhi). Na hila shaka sisi ni wenye uwezo wa kuyaondoa. Aya Hii Inazungumzia Maji Pia. Ukihesabu Herufi Za Aya Hii kuanzia Mwanzo Mpaka Neno Maji وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ Utapata Herufi 18 Pia!!!

Angalia Ya Kushangaza. Namba 18 Inakariri tena kiajabu.

Jambo la kushangaza ni kwamba Katika Elimu ya Chemistry Tunakuta Grams 18 Za Maji Ni sawa na MOLE moja.

Hiki Kipimo cha MOLE ni muhimu sana katika Kazi za zinazohitaji vipimo vya madawa kama vile Pharmacy na Hospitalini.

Sasa Hii Namba 18 Mbona Inakariri katika Aya hizi?

Je Namba hii Inaashiria Kitu gani?

Katika Sayansi Ya Chemistry tunafundishwa kwamba Uzito wa Mole Moja Ya Maji ni Grams 18.

Kwa Hiyo huenda Hii Namba ins uhusiano na Uzito Huu.

Hebu tuendelee na Kuelezea zaidi Maana ya MOLE katika Elimu ya Chemistry.

KIPIMO CHA MOLE KATIKA ELIMU YA CHEMISTRY NA UHUSIANO NA KURUANI TUKUFU

Kila Element ina Kipimo Chake na utapata Vipimo hivi katika Periodic Table Ya Chemistry.

Kwa Mfano Mole Moja Ya Sodium ni sawa na 22.990 Grams au Mole Moja Ya Magnesium ni sawa na 24.305 Grams.Na Mole Moja Ya Maji ni 18.01528 Grams.

Kipimo cha MOLE kilichaguliwa na mashirika makubwa ya vipimo duniani Kuingizwa katika Vipimo vya International System of Units (SI) Kuanzia May 20, 2019 Yaani Hivi Karibuni

(The mole designates an extremely large number of units, 6.02214076 × 1023. The General Conference on Weights and Measures defined the mole as this number for the International System of Units (SI) effective from May 20, 2019)

katika Elimu ya Chemistry Molar Mass ya maji katika Periodic Table ni uzito wa Grams 18.01528

katika kila Mole Moja Ya Maji kuna Atoms za Hydrogen Mbili na Atom ya Oxygen Moja

(H2O = 2 Hydrogen Atoms Grams =1.008 X 2 + 1 Oxygen Atom Grams 15.999= Grams 18.01528 Kwa Kila Mole Moja Ya Maji.)

Kwa Hiyo kuna Kiasi Cha Maji Gram 18.01528 katika Kila Mole Moja.

Kipimo Cha Moles Kinasadia sana Katika shughuli za Vipimo vya Madawa.

Katika Utafiti Wetu wa leo tunasoma kwamba Tunapohitaji Kuelewa Uzito wa Mole Moja Ya Maji basi uhesabu Molecule Moja Ya Maji Yaani Inaandikwa katika ChemisrtyH2O na Itabidi Ujumlishe Grams za Atom za Hydrogen Mbili na Atom Moja Ya Maji. Jumla Utapata Gram 18.01528 ambacho ni kiwango Katika kila Mole Moja.

Fikra Ya Mole iligunduliwa na Lorenzo Romano Amedeo Carlo Avogadro,(Alizaliwa Mwaka August 9, 1776, Turin, Huko Italy na Kufariki Mwaka July 9, 1856.Turin), Alikuwa Mtaalamu wa Elimu ya Hesabu na Physics (Italian mathematical physicist).

Wanasayansi Wanaelezea Neno “Mole” kama ifuatavyo:

(The mole is the unit for amount of substance. It is abbreviated to mol. 1 mol is the amount of substance that contains the same number of particles as there are atoms in 12.0 g of carbon-12.The Avogadro constant = 6.022 × 10 23 atoms per mole).

Angalia hapa chini Picha ambazo zina uhusiano na MOLE Nimeziambatanisha hapa chini. Allahu Akbar.

Hii Inathibitisha kwamba kuruani haikuandikwa bila mpango Ni ushahidi kwamba Mwenyeezi Mungu Mkubwa ndite aliyepanga haya. Na siyo Mchezo. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

Kuruani Ni Ya Karne Ya 7 na Sayansi katika Elimu ya Chemistry Inayohusika Na Molar Mass Elements ni ya Mwanzoni mwa karne ya 20!!!! Allahu Akbar.

Angalia Uhakika Kwamba Mtume alibebeshwa Ujumbe atufikishie na siyo Ujumbe Mdogo. Na ndiyo Maana Mwenyeezi Mungu akasema Kwamba Angelishusha hii Kuruani Katika Mlima ungaliuona ukinyenyekea (na) kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi Mungu.

Sura Namba 59 Aya Namba 21

لَوۡ أَنزَلۡنَا هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍ۬ لَّرَأَيۡتَهُ ۥ خَـٰشِعً۬ا مُّتَصَدِّعً۬ا مِّنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِ‌ۚ وَتِلۡكَ ٱلۡأَمۡثَـٰلُ نَضۡرِبُہَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ (٢١)

TAFSIRI

21-Lau kama tungaliteremsha hii Qurani juu ya mlima, ungaliuona ukinyenyekea (na) kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi Mungu.Na hii ni mifano tunawapigia (tunawaeleza) watu ili wafikiri.

Kwa Kweli haya siyo maneno ya Binaadamu. Sasa tujiulize Swali. Je Mtume alijua Vipi Elimu hii ambayo imekubaliwa miaka miwili iliyopita? Je huu sio Muujiza?

Mwenyeezi Mungu alijua Ugunduzi Huu wa leo katika wakati wa sayansi. Na bado mengi Hatujui. Allahu Akbar.

Kwa kweli Sayansi bado ipo Nyuma. Kuruani ni Maneno Yake Yule aliyeumba Kila Kitu. Ushahidi Tumeuona Hapa Na Kwingineko.

HISTORIA FUPI YA MOLE.

Maelezo yafuatayo yana husiana na Mkataba wa Mashirika Makubwa Ya Vipimo Duniani kama vile IUPAP, IUPAC,International Organization for Standardization (ISO),na CIPM ambayo yalikubaliana Kutumia na kuingiza Kipimo Cha MOLE kiwe mojawapo wa Vipimo Vinginevyo Duniani.

Following the discovery of the fundamental laws of chemistry, units called, for example, “gram-atom” and “gram-molecule,” were used to specify amounts of chemical elements or compounds. These units had a direct connection with “atomic weights” and “molecular weights,” which were in fact relative masses. “Atomic weights” were originally referred to the atomic weight of oxygen, by general agreement taken as 16. But whereas physicists separated isotopes in the mass spectrograph and attributed the value 16 to one of the isotopes of oxygen, chemists attributed that same value to the (slightly variable) mixture of isotopes 16, 17, and 18, which was for them the naturally occurring element oxygen. Finally, an agreement between the International Union of Pure and Applied Physics (IUPAP) and the International Union of Pure and Applied Chemistry (IUPAC) brought this duality to an end in 1959/60. Physicists and chemists have ever since agreed to assign the value 12, exactly, to the “atomic weight,” correctly the relative atomic mass, of the isotope of carbon with mass number 12 (carbon 12, 12C). The unified scale thus obtained gives values of relative atomic mass. It remained to define the unit of amount of substance by fixing the corresponding mass of carbon 12; by international agreement, this mass has been fixed at 0.012 kg, and the unit of the quantity “amount of substance” was given the name mole (symbol mol). Following proposals of IUPAP, IUPAC, and the International Organization for Standardization (ISO), the CIPM gave in 1967, and confirmed in 1969, a definition of the mole, eventually adopted by the 14th CGPM (1971): 1.The mole is the amount of substance of a system which contains as many elementary entities as there are atoms in 0.012 kilogram of carbon 12; its symbol is “mol.” 2.When the mole is used, the elementary entities must be specified and may be atoms, molecules, ions, electrons, other particles, or specified groups of such particles. At its 1980 meeting, the CIPM approved the 1980 proposal by the Consultive Committee on Units of the CIPM specifying that in this definition, it is understood that unbound atoms of carbon 12, at rest and in their ground state, are referred to.

Kipimo Cha Mole Moja Ya Maji ni karibu (aprox) Kiasi Cha 18 Grams

Tumeona Sherehe Ya Aya Hapa Juu Namba 283 ni Zile herufi zilizokariri na Namba hii position yake ni Prime Number Namba 61, Na la kushangaza hii 61 position yake ni Prime Number namba 18

Sherehe Maana Ya MOLE na Vipimo Vya Maji na Mada Nyinignezo kwa Kutumia MOLE

MUUJIZA WA MAELEKEZO YA MTUME KATIKA UJENZI WA MSIKITI HUKO SANA’A (Yemen)

Hapo mwanzo Wasilamu walikuwa wakisali kuelekea BAYT AL-MAQDIS iliyopo Palestina. lakini Katika Mwaka wa Pili baada ya Hijra ya Mtume (sala na Amani Yake Mola Zimfikie) kwenda Medinna aliamrishwa na Mwenyeezi Mungu abadilishe Kibla na Kuelekea Kaabah ambayo ipo Mecca Al-Mukaramah(Saudi Arabia).Na ndiyo ikawa Kibla mpaka leo. Na wakati huo Uislamu ulikuwa ukienea na wengi kuingia katika dini ya kiislamu.

Habari nitakayozungumza leo inahusika na Nchi ya Yemen.Mtume(sala na Amani Yake Mola Zimfikie) aliwapeleka  huko Yemen Walimu ili kuwafundisha dini. Miongoni mwa wale waliopelekwa na Mtume(Sala na Amani Yake Mola Zimfikie) Yemen ni Ali Ibn Abi Talib, Muadh Ibn Jabel Na Wabr Ibn Yuanas Al-Khozaee na huyu Wabr Ibn Yuanas Al-Khozaee aliamrishwa na Mtume (sala na Amani Yake Mola Zimfikie) Ajenge Msikiti huko Sanaa (Yemen) na akamuelekeza namna ya kujenga msikiti huo kama ilivyo katika Hadithi ambayo ipo Katika kitabu kinachojulikana kama Al-Mu’jam al-Awsat (Arabic: المعجم الأوسط للطبراني‎- kitabu cha kwanza, Hadithi Namba 831) Kilichoandaliwa na Mwanachuoni wa Hadithi za Mtume(Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Ambaye anajulikana kwa jina la Al-Tabarani (kazaliwa mwaka 874 na kufariki mwaka 971 CE, Ambayo ni sawa na Mwaka wa Hijriya 260–360 AH).(Kitabu hiki kina Hadithi 9500 na ni miongoni mwa Vitabu mbalimbali ambavyo aliviandika Mwanachuoni huyu. Kitabu hiki alikigawanya baina ya Hadithi Sahihi, Dhaifu na Zile ambazo siyo sahihi yaani za uwongo na ambazo zinajulikana kama Hadith kama Hadith Maudhu’u)

Tunasoma kwamba Wabr Ibn I’Saa Alkhuzai’i alisema kwamba Mtume (Sala na Amani yake Mwenyeezi Mungu zimfikie) alimwambia Ajenge Msikiti hapo Sana’a (yaani katika mji wa Sanaa uliyopo Yemen) na kufanya Kiblah ya msikiti huo ielekee katika upande wa kulia wa Mlima unaojulikana kama DHIYN.

Kwa kweli Huu Ni Muujiza sio mdogo kwani Mtume anatoa Fundisho wajenge msikiti na wafanye Kibla ya Msikiti huo ielekee upande wa kulia wa Mlima unaojulikana kama DHIYN ambao upo karibu kilometer 30 kutoka Sanaa (Yemen)na Ajabu ni kwamba Leo hii Sayansi imetuletea Vyombo mbali mbali kama vile Satellites zinazoweza kupaa angani na kuchukua picha mbali mbali za ardhi tunayoishi. Satellites imesaidia kuchunguza zaidi na kukuta mlima huo upande mmoja unaelekea KIBLA ya Mecca na upande wa pili unaelekea Msikiti wa Mji wa Sanaa (yemen)Kwa kweli inashangaza sana. Allahu Akbar. Kwani Mtume aliamrisha bila ya yeye kutumia ufundi na vyombo vya kisasa.

Je amewezaje kujua kwamba Mlima huo kwa upande wake wa Kulia unaelekea KIBLAH ya Msikiti huo utakaojengwa na kwa upande wa kushoto wa Mlima huo unaelekea KAABAH huko Mecca (Saudi Arabia).

Kipimo hicho ni sahihi bila ya kosa hata Centimeter moja.

Angalia Muujiza mbele ya macho yako Allahu Akbar.

Miujiza na Miujiza isiyo na Mwisho.

Walipopima muelekeo (Direction) wa Msikiti huko SANAA (Yemen) kuelekea Mlima Huo unaoitwa DHIYN wakakuta asilimia 100% ni Sahihi na Kutoka Upande wa kushoto wa mlima huo unaelekea KIBLA ya KAABAH huko Mecca .

Huu ni muujiza mmojawapo katika miujiza Yake Mtume (Sala na Amani za Mola Zimfikie).

Umbali baina ya Sanaa (Yemen) na Mecca ni Kilometer 81.5 na Umbali baina ya Sanaa na Mlima Dhayn ni 30 Kilometers.

Je Mtume alikuwa Architect? je alikuwa Civil Engineer wakati huo? alisomea Chuo gani Elimu ya Ujenzi?

Kwa kweli ni Muujiza siyo mdogo.

Mwenyeezi Mungu anasema katika Aya zifuatazo kutoka Katika Sura Ya Annajm Namba 53 Aya Namba 3-4

وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ (٣) إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡىٌ۬ يُوحَىٰ (٤)

Aya Hii inasema kwamba Kila alichozungumza Mtume siyo chake bali ni WAHYI kutoka kwa Mola wake.

ili tuelewe vizuri zaidi kisa hiki angalia Video ifuatayo ambayo nzuri sana na ambayo imeandaliwa kwa lugha ya kiarabu na maelezo kwa Lugha ya Kiingereza.

VIDEO-1

Ushauri wa Mtume (S.A.W.) kwa Wabr Ibn Yuanas Al-Khozaee kuhusiana na Ujenzi wa Msikiti huko Sanaa (Yemen) Ulikuwa Muujiza. Alitoa Ushauri Kiblah ya Msikiti Ielekee Upande wa Kulia wa Mlima Unaoitwa Dhiyn. Sayansi za leo kwa kutumia Satellite Inathibitisha upande huo unaelekea Kiblah ya Mecca.