UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
NAFAKA (CEREAL) NA MENGINEYO YA ARDHI KATIKA KURUANI TUKUFU
Mwenyeezi Mungu akipenda nitaufungua mlango huu Kwa habari ya Nafaka (Cereal) katika Elimu ya kilimo Agriculture Kisha nitafuatia na Habari za Elimu ya Ardhi (Geology) Kwa Ujumla Namuomba Mwenyeezi Mungu nisiende Mrama na ikiwa hivyo namuomba msamaha kwani siyo lengo langu. Mambo haya ya Utafiti ni jitihada za Kibinaadamu na kwa hiyo kuna Kupata na Kukosa. Soma habari hizi kisha ufikiri kwa makini na uchague yanayokubaliana na fikra zako kwani sikulazimishi kunisikiliza na uelewe kwamba Kuruani haikosei bali mengine yote ni juhudi za Binaadamu ambaye ni Dhaifu.
SEHEMU YA KWANZA-NAFAKA-CEREAL
UTAFITI NA MUUJIZA WA NAFAKA (CEREALE) KATIKA KURUANI
Sura Ya Al-Bakarah Namba 1 Aya Namba 261
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٲلَهُمۡ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِى كُلِّ سُنۢبُلَةٍ۬ مِّاْئَةُ حَبَّةٍ۬ۗ وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ (٢٦١)
TAFSIRI
261.Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyotoa mashuke saba; ikawa katika kila shuke pana punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, (zaidi kuliko hivi), na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa mkubwa (na) Mwenye kujua.
Sura Ya Yussuf Namba 12 Aya Namba 43, 46 na 47
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬ۖ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِى فِى رُءۡيَـٰىَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ (٤٣)
TAFSIRI
43·Na (siku moja) mfalme (Firauni aliota)akasema (kuwaambia mawaziri wake). “Hakika mimi nimeona (Nimeota Ndoto) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba ving’onda. Na nimeona mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka. Enyi wakubwa! Nifasirieni ndoto yangu ikiwa nyinyi mnaweza kufasiri ndoto.
يُوسُفُ أَيُّہَا ٱلصِّدِّيقُ أَفۡتِنَا فِى سَبۡعِ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعِ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬ لَّعَلِّىٓ أَرۡجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَعۡلَمُونَ (٤٦)
TAFSIRI
46.(Akenda gerezani akamtaka msamaha Nabii Yusufu kwa kule kusahau kwake na akamwambia):”Yusufu! Ewe mkweli! Tueleze hakika ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba dhaifu. Na mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka, ili nirejee kwa watu wapate kujua.”
قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبً۬ا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦۤ إِلَّا قَلِيلاً۬ مِّمَّا تَأۡكُلُونَ (٤٧)
TAFSIRI
47.Akasema:·”Mtalima myaka saba mfululizo kwa juhudi (yaani limeni miaka saba kwa juhudi kwani itaingia njaa kubwa baada ya myaka saba). Na mtakavyovivuna viacheni katika mashuke yake,isipokuwa kidogo mnavyokula (ili hivyo mnavyoviacha mule katika myaka ya njaa itakayokuja).”
SHEREHE YA AYA
Katika Kuruani Tukufu Neno سُنۢبُلَةٍ۬ “SUMBULA” yaani “Mashuke” Limetajika katika Aya Nne peke yake. Aya ya kwanza katika Sura Ya Al-Bakarah na Aya Tatu nyinginezo katika Sura Ya Nabii Yusuf. Kuna Ushahidi Tatu unaotupa tafsiri kwamba Mashuke yaliyokusudiwa katika Aya hizi ni Ngano na siyo Mahindi kama ilivyofasiriwa katika Baadhi ya Tafsiri za Kuruani.
USHAHIDI WA KILIMO
Aya Ya kwanza namba 261 kutoka katika Sura Ya Al-Bakarah inatupa mfano wa Kila Shuke lenye Punje 100 Shuke la mahindi kwa kawaida linabeba Punje zaidi ya Mia Moja. Na Ngano kwa kutumia kilimo cha kisasa huweza kubeba punje Mia na siyo kwa wingi kama vile Shuke la Mahindi. Kwa hiyo huu ni Ushahidi wa kwanza kwamba Mashuke yaliyokusudiwa katika Aya hizi Nne ni Ya Ngano na siyo Mahindi. Mtaalamu wa Elimu ya Kilimo kutoka Russia alielezea habari hizi kama ifuatavyo
Average number of grains per ear in optimal conditions can be about 70, but some modern wheat cultivars have 80 or more. Average number of spikes per plant in field in optimal conditions can be from 6 to 9 depending on cultivar (bread wheat). A single grown cereal plant can produce up to 90 ears)
Kwa hiyo anatuthibitishia kwamba Shuke Moja la Ngano katika Kilimo cha kisasa linaweza kubeba Mbegu 80 au zaidi na kwa hiyo kuruani imetaja mbegu 100 haikukosea. Na akaendelea kusema kwamba Mashuke ya Ngano katika wakati wa Hewa Nzuri yaweza kuwa baina ya 6 na 9 na Kuruani katika Aya imetolewa mfani wa Mashuke 7 na kwa hiyo 7 X 100=700 na hii ndivyo tunavyosoma katika Aya namba 261 ya Sura Ya Al-Bakarah. Kwamba Ukitoa Sadaka moja basi utapata Thawabu nyingi mfano wa Ngano ambayo Mbegu moja utakayopanda ikizaa Mashuke 7 na kila Shuke likiwa na Mbegu 100 moja basi utapata Jumla ya Mbegu 700. Na hivyo hivyo Sadaka yako itakavyozaa. Ulitoa Sadaka Moja utapata thawabu mara mia 700 pia. Allahu Akbar.
USHAHIDI WA HISTORIA
Historia inatuambia kwamba Mahindi duniani asili yake ni kutoka Mexico na ililimwa huko mara ya kwanza karibu miaka Elfu Tisa iliyopita na haiwezekani kutajika katika kuruani katika Enzi ya Nabii Yusuf Miaka karibu 16000 iliyopita na katika wakati huo Mahindi yalikuwa bado kugundulikana.
USHAHIDI WA KIHESABU
Hebu sasa tuchambue Aya Hizi nne kihesabu ili tupate kujua Vizuri zaidi iwapo Aya hizi zinazungumzia Ngano au Mahindi.
Huu utakuwa ushahidi wa Tatu.
Kwanza inabidi tuelewe kwamba Chromosomes za Nafaka kama vile Wheat (Ngano), Rye, Barley, Oats. ni Namba inayogawanyika na namba 7.
Nimezungumzia Chromosomes katika website hii kwa hiyo sitarudia tena kuisherehesha lakini nitaigusia tu kwamba Asili ya kila kilicho na Uhai ni Mbegu ya Kike na Kiume ambayo inaunda Chromosomes. Na Chromosomes ndizo zenye kubeba Genes zenye habari ya Maumbile ya kila kitu.
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٲلَهُمۡ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِى كُلِّ سُنۢبُلَةٍ۬ مِّاْئَةُ حَبَّةٍ۬ۗ وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ (٢٦١)
Ukihesabu Maneno ya Aya hii kuanzia ibara سَبۡعَ سَنَابِلَ yenye maana ya “Mashuke Saba” mpaka mwisho wa Aya utapata Jumla ya maneno ni 14 (yaani 7 X 2=14).
Na Chromosome za kia nafaka Karibu zote tulizozitaja hapa (Wheat (Ngano), Rye, Barley, Oats) ni Jumla ya Namba inayogawanyika na namba 7.
Kwa Mfano:
Chromosomes za Barley na Rye (Kama sikosei kwa Kiswahili ni Shayiri) ni Diploids yaani Saba mara mbili (7×2=14 ).
Chromosomes za Ngano ya Durum au Durum Wheat ni Tetraploids (7 x 4=28) yaani Saba mara nne.
Chromosome za Ngano Nyepesi au Soft Wheat ni Hexaploids (7×6=42 ) au Saba mara sita.
Aya ya Pili Inayofuatia pia inashangaza kwani tunapata Jumla ya Maneno yake Namba 14 kama ifuatavyo:
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬ۖ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِى فِى رُءۡيَـٰىَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ (٤٣)
Ukihesabu Maneno ya Aya hii kuanzia ibara سَبۡعَ سَنَابِلَ yenye maana ya “Mashuke Saba” mpaka mwisho wa Aya utapata Jumla ya maneno ni 14 (yaani 7 X 2=14)
Aya hii pia inaashiria namba 7 ambayo ni asili ya Chromosome zote za Nafaka zinginezo tulizozitaja hapa juu na kama tulivyosema kwamba Diploid, Tetraploid na Hexaploids ni Namba iliyojengeka kwa namba 7.
Aya ya Tatu Inayofuatia pia inashangaza kwani tunapata jumla ya meneno yake ni Namba 14 kama ifuatavyo:
قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبً۬ا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦۤ إِلَّا قَلِيلاً۬ مِّمَّا تَأۡكُلُونَ (٤٧)
Ukihesabu Maneno ya Aya Hii yote jumla yake ni 14 pia. Angalia Maajabu na hii ni Namba Diploid. Yaani 7 x 2=14. Yaani 14 inagawanyika kwa namba 7
Huu Muashirio unashangaza kwani Namba 14 imekariri katika Aya Hizi tatu ambazo zinazungumzia Nafaka ya Ngano. Na Kama tulivyoona Chromosomes za Nafaka ni namba Inayogawanyika na namba 7. Au ni namba iliyojengeka kwa Msingi wa namba 7.
Hebu tuendelee na Safari yetu na tuchunguze zaidi. Kwa kweli haya siyo mambo madogo. Hizi ni siri kubwa. Kuna mengi katika Aya cheche. Hebu tuchunguze zaidi. Allahu Akbar. Mbona namba 7 imekaririkariri hivi? ni siri ambazo zimebeba makubwa.
Sasa tuhesabu maneno Ya Aya zote nne na tukifanya hivyo tutapata jawabu pia la kushangaza.
Aya Ya Kwanza Jumla ya maneno ni 24
Aya Ya Pili jumla ya maneno ni 24
Aya Ya Tatu jumla ya maneno ni 22
Aya Ya Nne Jumla ya maneno ni 14
Sasa tujumlishe Namba hizi Nne. 24 + 24 + 22 + 14= 84 na namba hii ni sawa na 12 X 7
Je unaona tunapata tena namba 7. Yaani Jumla ya Maneno katika Aya hizi nne ni 84 na namba hii msingi wake ni namba 7.
Kama sikosei Huu ni muashirio wa Chromosomes za Nafaka. Kwani kama tulivyosema kwamba Chromosomes za nafaka ni Diploid 7 (7 x2), Tetraploid ya 7 ( 7 x 4) na Hexaploid ya 7 (7 x 6).
Je Unaona Msingi wa Chromosomes Namba 7 inavyojitokeza. Allahu Akbar. Huu siyo Muujiza mdogo hata kidogo.
Haiwezekani Namba 7 kukariri kariri bure bure bila mpango bali imepangwa na yule yule aliyeumba ulimwengu na ndiye yeye tu aliyeshusha kuruani hii na ni message au ujumbe au hotuba yake.
Na heiwezekani Ujumbe wake kuwa na Upuuzi. Bali ni Miujiza isiyo na mwisho.
Huu ni Muujiza siyo mdogo kwani wakati kuruani iliposhushwa hakuna aliyekuwa akijua Elimu inayohusiana na Chromosomes.
Elimu hii imeanzishwa karne ya 19 katika mwaka 1888.
Hebu tuendelee na Safari ya Uchunguzi yenye maajabu.
Sasa tuzinukulu Aya hizi tena mara ya pili na tuhesabu Maneno ya Aya hizi kuanzia Neno سُنۢبُلَةٍ۬ katika Aya ya kwanza mpaka neno سُنۢبُلِهِۦۤ Aya ya mwisho.
مَّثَلُ ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٲلَهُمۡ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنۢبَتَتۡ سَبۡعَ سَنَابِلَ فِى كُلِّ سُنۢبُلَةٍ۬ مِّاْئَةُ حَبَّةٍ۬ۗ وَٱللَّهُ يُضَـٰعِفُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ (٢٦١)
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬ۖ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِى فِى رُءۡيَـٰىَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ (٤٣)
يُوسُفُ أَيُّہَا ٱلصِّدِّيقُ أَفۡتِنَا فِى سَبۡعِ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعِ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬ لَّعَلِّىٓ أَرۡجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَعۡلَمُونَ (٤٦)
قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبً۬ا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦۤ إِلَّا قَلِيلاً۬ مِّمَّا تَأۡكُلُونَ (٤٧)
Ukihesabu Maneno haya kuanzia Neno la kwanza سُنۢبُلِهِۦۤ “MASHUKE” (Aya ya Kwanza) mpaka neno سُنۢبُلِهِۦۤ “MASHUKE”la mwisho wa Aya ya mwisho (Aya ya Nne) utapata jumla ni maneno 70 na namba hii ni sawa na 10 x 7
Je unaona namba 7 invyojitokeza kiajabu?
Sitarudia kuielezea kwani inaeleweka.
Sasa tuhesabu Herufi za Neno سُنۢبُلَ lenye maana ya “SHUKE” katika Aya Hizi nne. Tukifanya hivyo tutapata Jumla ya herufi hizi kama ifuatavyo:
Herufi SIN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 22 Herufi NUN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 26 Herufi BAA imetumika katika Aya Hizi Nne mara 23 Herufi LAM imetumika katika Aya Hizi Nne mara 41 Ukijumlisha 22 + 26 + 23 + 41= 112 na namba hii ni sawa na 12 X 7
Mara nyingine tena tunapata Namba 7 kwani Namba 112 inagawanyika kwa namba 7. Angalia Namba 7 inavyojitokeza. Allahu Akbar.
Sasa tuhesabu Herufi za Neno السنبل kwa kuongeza Alif na Lam (Definite Article).
Kwa kuongeza Alif na Lam maana inakuwa kwa kiingereza “The Spike” na bila ya Herufi Alif na Lam inakuwa “Spike”
Ukihesabu herufi za Neno السنبل utapata Jumla ya Herufi ni kama ifuatavyo:
Herufi Alif imetumika katika Aya Hizi Nne mara 29
Herufi Lam imetumika katika Aya Hizi Nne mara 41 Herufi SIN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 22 Herufi NUN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 26 Herufi BAA imetumika katika Aya Hizi Nne mara 23 Herufi LAM imetumika katika Aya Hizi Nne mara 41
Hebu Tujumlishe Namba hizi:
29 + 41 + 22 + 26 + 23 + 41=182
na namba hii ni sawa na 26 X 7=182 Je unaona namba 7 Inavyojitokeza mara nyingine.
Je huoni Kwamba huu ni Muujiza Mkubwa. Na la kushangaza zaidi ni utafiti ufuatao wa herufi katika Aya zote.
ukihesabu Herufi zote kuanzia Aya kwanza yaani Aya namba 261 Sura Ya Albakarah tuliyoitaja hapa Juu mpaka Aya Namba 47 Sura Ya Yusuf Aya namba 47 utapata ya kushangaza zaidi.
Herufi utakazozipata ni kama ifuatavyo
Herufi SIN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 1910 Herufi NUN imetumika katika Aya Hizi Nne mara 9006 Herufi BAA imetumika katika Aya Hizi Nne mara 3710 Herufi LAM imetumika katika Aya Hizi Nne mara 12660
Jumla ya herufi zote hizi nne za neno SUMBUL yaani “SHUKE” au “SPIKE” ni
1910 + 9006 + 3710 + 12660= 27286
Sasa la kushangaza zaidi ni namba 27286 ambayo pia inagawanyika kwa namba 7 yaani ni sawa na kusema 3898 x7 =27286
Na kama tulivyoona namba 7 ndiyo msingi wa Chromosomes za Nafaka.
Allahu Akbar. Je Unaonaje? Sina Mengi ya Kukueleza isipokuwa kujishika Tama.
Hata mimi ninayeandika haya Nipo katika Mshangao. Hili siyo dogo. Allahu Akbar
Nimeweka picha hapa chini za Mfano wa Ngano na Barley peke yake. Ya kwanza ni idadi ya Chromosomes ya baadhi ya Nafaka tulizozotaja na ya pili ni Chromospmes zenyewe katika chembe ndogo ya ngano (Cell au Celi) ambazo huwezi kuona kwa macho bali Inabidi Utumie Chombo ya Kuonea vitu vodogo sana kama vile Microscope.

Chromosome za Ngano ni Haxaploid yaani 6 x 7 na Barley ni Diploid Yaani 2 x7 Allahu Akbar.