SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Sayansi Za Maji

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

VIDEO-1

Moto unatokana na Lava inayovuja kutoka katika nyufa za kitanda cha bahari.
Moto haukaushi Maji na wala Maji hayazimi Moto kama kawaida tunavyojua. Kuruani ilitaja jambo hili kabla ya ugunduzi wa sanyasi hivi karibuni Tazama Video hii uone maajabu hayo.

ELIMU MBALIMBALI ZA ARDHI KATIKA KURUANI

MOTO NA MAJI

Moto na Maji havikai pamoja. Moto hukausha Maji na Maji huzima Moto. Lakini katika Video hapa juu  utaona maajabu ya Moto katika Bahari za ulimwenguni. 

Lava (Volcano) ambayo inavuja kutoka katika ardhi ya bahari kwa ajili ya uzito mkubwa juu yake inapenya katika Bahari kupitia katika Nyufa za kitanda cha Bahari.

Lava ambayo ina moto mkubwa inachemsha maji karibu yake na pia Maji yanajitahidi kuuzima moto huo  na hali iyo inaendelea mara kwa mara kutoka  karne na karne.

Habari hizi zimegunduliwa na kuthibitishwa na wanasayansi wa Bahari (oceanographers) miaka michache iliyopita.

Lakini habari hizi zimetajwa katika kuruani tangu miaka elfu moja na mia nne iliyopita. Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani Tukufu Sura Ya namba 52 Aya ya 1 mpaka 6:

وَٱلطُّورِ (١) وَكِتَـٰبٍ۬ مَّسۡطُورٍ۬ (٢) فِى رَقٍّ۬ مَّنشُورٍ۬ (٣) وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ (٤)

وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ (٥) وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ (٦)

Tafsiri ya aya hii:

1/Naapa kwa mlima (huoo aliosemezwa Musa

2/Naapa kwa kitabu kilichoandikwa (kila aliyotaka mwenyeezi mungu yaandikwe)

3/(Kilichandikwa) kwa karatasi ya ngozi (iliyosafi na)kikakunjuliwa (kisomwe)

4/Na kwa (hiyo)Nyumba inayozuriwa (daima) (Tafsiri nyingine inasema Kaaba hiyo ni “Bait-ul-Ma’mur” ambayo ipo mbinguni mfano wa kaaba (mecca) ipo sambamba na juu ya Kaaba ya Mecca ambayo inazuriwa daima na  malaika. Na Tafsiri nyingine inasema ni Kaaba ya Mecca).

5/Na kwa sakafu (mbingu) zilizonyanyuliwa juu.

6/Na kwa bahari zilizojazwa (maji) (au kuwaka moto siku ya kiama)

Aya hii namba ya sita ilifasiriwa na wafasiri hapo awali kama tunavyoona hapa katika tafsiri hii kwamba bahari kujazwa maji au itawaka moto katika siku ya kiama.

Lakini leo hii sayansi imegundua habari za Moto katika Maji na hivyo inaturudisha katika tafsiri ya aya hii ambayo tutaifasiri hapa kama ifuatavyo:

6/Na kwa bahari zilizojaa Moto.

Na hii ndiyo tafsiri inayokubaliana na mashekhe wetu wa sasa ambao wamesoma elimu za Bahari kwani maswahaba au waliofuatia wasingekubali moto na maji kukaa pamoja kwani haingii akilini na mwenyeezi Mungu ameshusha Aya hii ili iwe hoja kwa watu wa leo wanaojigambia elimu ya sayansi na kudharau dini ya kiislamu na kuruani.

Neno  “Sujirat”  lipo katika Aya nyinigine sura namba 81 aya ya 6

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ (٦)

Tafsiri

“Na bahari zitakapowashwa moto”  (siku ya kiama)

Pia lina maana ya Bahari zitakapowashwa moto (yaani siku ya kiama) kwa hiyo aya hii inathibitisha aya tuliyotaja hapo juu ina maana ya moto baharini. Neno hili limetumika kwa maana mbalimbali kama vile Masjur au Sujiraj kufuatana na Elimu ya Arabic Morphology (Swarfa) lakini maneno yote yanayotokana na asili ya neno “Sajjara” linaashiria maana ya “Moto” jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba katika lugha ya kiarabu neno moja hubeba maana zaidi ya moja na ndiyo maana kuna tafsiri za kuruani mbalimbali. Lakini Alhamdulilahi yote hiyo ni neema yake mwenyeezi mungu kama alivyosema Mtume Mohamed (Amani na sala zimfikie) “Kukhitilafiana kwa Umma ni Neema” na ukichinguza utakutaTafsiri zote hazipingani. Na huo ndiyo muujiza wa Kuruani. Tafsiri inakubaliwa wakati fulani na baada ya miaka kadhaa tafsiri nyingine inakuja na kutugundulia siri ya kisayansi na mengineyo. Huu ndiyo muujiza mkubwa wa maneno yake mwenyeezi mungu.

Na Hadithi ya Mtume Mohamed pia inathibitisha habari hii ni ile ambayo imehesabiwa kuwa ni “Dhaifu” iliyopo katika hadithi za Sunan Abi Dawuud inayosema: 

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ زَكَرِيَّا، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ بِشْرٍ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ بَشِيرِ بْنِ مُسْلِمٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏……………………….. فَإِنَّ تَحْتَ الْبَحْرِ نَارًا وَتَحْتَ النَّارِ بَحْرًا ‏”‏ ‏.‏

ضعيف (الألباني) حكم :

Tafsiri ya Hadithi hii kuanzia hapo nilipopigia mstari:

Inatokana (alizungumzia) na  Abdullah Ibn Amr : Mtume (Amani na sala zimfikie) “…………………………………….  kwani chini ya Bahari kuna Moto na chini ya Moto kuna Bahari.

Linalotukhusu hapa ni kipande hiki nilichokipigia mstari kwani sehemu nyingine ya hadithi nimeziondoa kwani haihusu mjadala huu wa kisayansi.

Hadithi Hii ni Dhaifu kwani huenda habari za Moto na Maji hazikukubalika hapo zamani lakini sasa baada ya sayansi huenda hadithi hizi zikawa sio dhaifu kama zilivyochukuliwa hapo awali.

Kwa kweli Kuruani ni Muujiza mkubwa na kama alivyosema mwenyeezi mungu kwamba kuruani imezingatia kila kitu na hakuna kisichotajwa.

MAJI MATAMU NA YA CHUMVI

KUHUSU AYA INAYOZUNGUMZIA AINA ZA MAJI MATAMU NA YA CHUMVI

Mwenyeezi mungu anasema katika kuruani tukufu Sura ya Alfurkan namba 25 na Aya namba 53 kuwa;

“Ni yeye ndiye aliyeziunganisha bahari mbili; mojawapo ni yenye kunywika na ni matamu na nyingineyo ni yenye chumvi kali, na akajaalia kinga kati yao ili zisichanganyikane na zisiharibiane”

وَهُوَ ٱلَّذِى مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَـٰذَا عَذۡبٌ۬ فُرَاتٌ۬ وَهَـٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٌ۬ وَجَعَلَ بَيۡنَہُمَا بَرۡزَخً۬ا وَحِجۡرً۬ا مَّحۡجُورً۬ا

Huu ni muujiza katika miujiza yake mwenyeezi mungu.

Katika Video hapa chini  wataalamu wanatueleza  kwamba inataka utaalamu mkubwa sana ili kuweza kuona tofauti ya maji haya, kama katika makutaniko ya maji baina ya mito na bahari, baina ya bahari na bahari au mito na mito. Na katika Video hii tuna mfano mzuri wa bahari kubwa huko Ghuba Ya Alaska (Gulf of Alaska) ambapo bahari mbili zimekutana; maji ya chumvi na matamu  (maji haya matamu ambayo yanayayuka kutoka katika milima hiyo ya barafu kwa ajili ya hali ya joto ulimwenguni na maji hayo yanayayukia tangu miaka na miaka katika upande mmoja wa bahari ya maji ya chumvi) Na Upande huu wa bahari wenye maji matamu unakutana na maji ya chumvi katika bahari hiyo hiyo mbali na milima hiyo.

Lakini ajabu kubwa sana mwenyeezi mungu anatufundisha elimu ambazo zimegundulikana hivi karibuni baada ya utafiti wa wanasayansi wakubwa ulimwenguni kwa kutumia vyombo vya kitaalamu.

Mtume Mohamed (Mwenyeezi Mungu Ampe Amani na Amsalie) hakuandika Kuruani yeye mwenyewe wala kuchukua elimu hii popote kwan Elimu hii haikuwapo wakati huo. Aliyeumba dunia hii ndiyo huyo huyo aliyeshusha elimu hii katika kuruani tukufu, na leo hii inatusaidia kujenga imani zetu na pia kuwa shahidi kwa watu wote ulimwenguni kuwa kuruani ni kitabu chake mwenyeezi mungu.

TAFSIRI YA BAADHI YA MANENO KATIKA AYA HII

Neno مَرَجَ (Maraja) lina maana zaidi ya moja.

Maana ya kwanza ni Kuchanganya (English Mix). 

Maana ya pili ni Mchafuko (English Disturbance). 

Maana ya tatu ni Uzito wa maji (English Density). 

Tafsiri za maana zote tatu zinakubaliana na Elimu za Bahari.

Neno فُرَاتٌ۬ (Furatun)lina maana ya (chumvi kidogo sana au minerals nyinginezo) ambazo huwezi kuhisi unapokunywa maji.

Jambo la kushangaza ni kwamba wanasayansi wa Kemia (Chemistry) wamefanya utafiti na kuona minerals hizo katika maji kwa kutumia elimu na vyombo vya kisasa.

Je Mtume Mohamed alikuwa mjuzi wa elimu ya Kemia au alikuwa na vyombo vya kisayansi na akafanya utafiti huo kisha akaandika kuruani?

kila aya katika kuruani ni muujiza mkubwa, Hakuna mfano wowote katika ulimwengu mzima wa kitabu chochote kama hiki. Hizi ndizo nyenzo ambazo zinatubidi kuzifahamu ili kuzidisha imani yetu katika uislamu na pia kuwafundisha wasiojua elimu hizi.

Hapa Juu Nimeelezea Mkutaniko wa maji Ya Chumvi na Tamu. Na hapa chini nitaendelea Na Aya Nyingineyo inayohusu Mkutaniko wa Bahari mbili yenye maji Ya  Chumvi. Alhamdulilah. Allahu Akbar.

VIDEO-2

Maji Matamu na ya chumvi hayachanganyikani kama alivyotuambia mwenyeezi Mungu katika kuruan. Wanasayansi wamegundua hivi karibuni.

VIDEO-3

Sherehe Kuhusu Maji ya Bahari mbili zinapokutana na kuwepo kwa Transit Area (Barzakh au Kizuizi) baina ya Maji ya aina mbili hizi. Je unaona Maajabu Ya Kuruani Tukufu. Ukibabaika Na maelezo ya wasiyo na Elimu basi sikiliza Video Hii Vizuri. Muujiza Mkubwa Katika Kuruani. Je Mtume walisoma wapi? Kwani Elimu na Utafiti ni wa kisasa.

The Arabian/Persian Gulf water salinity near the bottom decreases from 40 psu in the Gulf to 38.5 psu at the head of the Gulf of Oman. In the Strait of Hormuz The salinity increases from approximately 37 to 38.5 psu. Sehemu Hii yenye kiwango cha chumvi 38.5 ndiyo Barzakh. Wataalamu wamepima na wakakuta Kiwango hiki ambacho ni Average ya Viwango viwili vya Ghuba Ya Oman na Arabian/Persian. Allahu Akbar. Sasa Mtume Mohamed (Sala na Amani kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Alisoma wapi habari kama hizi ambazo zinahitaji vyombo vya kitaalamu vya kisasa ambavyo vya hali ya Juu sana. Kwa kweli Hii inathibitisha Kwamba Kuruani ni Maneno ya Mwenyeezi Muungu na Mtume alikuwa Mjumbe tu. Hakujua habari hizi. Allahu Akbar

PICHA YA RAMANI (MAJI YA CHUMVI BAINA YA GHUBA MBILI NI KATIKATI NAYO NI (STRAIGHT OF HORMUZ) AMBAYO NI BARZAKH. KIWANG CHA CHUMVI NI 38.5

Kuna mkutaniko wa maji ya chumvi kali na yale ambayo yana chumvi siyo kali na mfano ni bahari mbili zinapokutana. Mfano wa kaji matamu na Maji chumvi ni kama vile Mto unapokutana na bahari kama vile Nile na Mediterranean Sea. Aya inayozungumzia Maji matamu na Chumvi imeongeza maneno  وَحِجۡرً۬ا مَّحۡجُورً۬ا  yenye maana ya Sehemu iliyotengwa. Kinachoingia hapo(Visamaki na viumbe vinginevyo vinavyoishi humo) hakiwezi kuendelea sehemu ingine ambayo hatari kwake. Kwa hiyo ni kama vile chumba cha usalama. Maneno haya mawili hayakutumiwa katika Bahari mbili zinapokuata kwani hatari haipo kubwa sana na hakuna haja ya kuweko kwa sehemu iliyotengwa. Kuna Barzakh tu peke yake ambayo ni Transit Area na baadaye kiumbe chochote kinapozoea mazinagar ya upande wowote basi kinaweza kuhama baada ya muda. Nimeelezea vizuri sana karika Video ambayo nimeiandika kwa lugha mbalimbali. Video hiyo ipo katika Website hii chini ya mlango wa Video.

Kama tulivyoelezea hapa juu Tofauti ya Maji Matamu na Chumvi ni kubwa sana kama vile Oil na Maji na kwa hiyo haichanganyiki kwani kuna Kizuizi baina ya maji matamu na ya chumvi na ndiyo maana Aya ikamalizia kwa kusema وَحِجۡرً۬ا مَّحۡجُورً۬ا yaani kuna kizuizi ambacho kinazuia yasichanganyikane. Kutokuchanganyikana kwa Maji haya ni Usalama mkubwa wa Vinavyoishi katika aina Ya Maji ya Chumvi na Tamu.

Katika Aya ifuatayo kutoka katika Sura Ya Al-Rahman tunasoma kwamba kuna uwezekano wa maji haya mawili kuchanganyikana kwani  Aya hii haina kile kipande tulichosoma katika Aya iliyopita ambacho ni      وَحِجۡرً۬ا مَّحۡجُورً۬ا   

Kwa hiyo tunafahamu kuweko uwezekano wa maji haya kuchanganyikana. Na hii inatokana na tofauti ya sifa baina ya aina ya Bahari hizi mbili ambazo siyo kubwa sana yaani Bahari moja ina Chumvi zaidi kuliko nyingine lakini kwa kiwango sicho kikubwa kama vile maji matamu na Chumvi katika Aya Hapo Juu. Ukifikiri utaona hivyo. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi.

Sasa Tushereheshe Aya ifuatayo ambayo inatuelezea kwamba Bahari Mbili (Zenye Kufanana lakini kuna tofauti ndogo) huweza kuchanganyikana bila tatizo lolote.

Sura Ya Al-Rahman Namba 55 Aya Namba 19 na 20

مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ يَلۡتَقِيَانِ (١٩) بَيۡنَہُمَا بَرۡزَخٌ۬ لَّا يَبۡغِيَانِ (٢٠)

TAFSIRI

19.Ni yeye ndiye aliyeziunganisha bahari mbili 20.na akajaalia kinga kati yao ili zisichanganyikane na zisiharibiane.

Aya Hii inahusu Maji Ya Aina Mbili au Bahari Mbili zenye Tofauti ndogo (kuliko Maji Matamu tuliyosoma katika Sura Ya Al-Furqan Namba 25 Aya namba 53) Katika Aya Hizi namba 19 na 20 Tunasoma kwamba Maji yanachanganyikana lakini baada ya muda na kwa kupitia BARZAKH ambayo tunaweza kufananisha na TRANSIT AREA. Tutatumia Mfano wa Ghulf Ya Arabian/Persian na Gulf Ya Oman katika maelezo haya.

Gulf of Oman kipimo cha chumvi ni 37 PSU (Practical Salinity Unit) Gulf of Arabian/Persia kipimo cha chumvi ni 40 PSU (Practical Salinity Unit)

Kipimo cha chumvi kinajulikana kama PSU ni sawa na per thousand or (o/00) au to g/kg.

Strait of Hurmuz ni baina ya Arabian/Persian Gulf na Gulf of Oman (Ghuba Ya Iran na Oman)

Eneo hili lipo katikati na Hapa tunakuta Sehemu inayokutanisha Maji haya ya aina mbili. Kipimo cha maji ya Chumvi katika sehemu hii ni PSU 38.5 Na kipimo hiki ni Average ya Vipimo viwili tulivyovitaja hapa Juu. Yaani Ghuba ya Arabian/Persian ambayo ni 37 PSU na Ghuba ya Oman ambayo ni 40 PSU. Kipimo hiki kimepimwa na Wataalamu wa Elimu ya Bahari (Oceanologists) lakini Jambo la kushangaza ni kwamba Ukitafuta Average ya Vipimo hivi viwili utapata 38.5. (37 + 40=77 ukigawa na 2 = 38.8) .

Kipimo hiki cha 38.8 kinaashiria sehemu ya BARZAKH iliyopo katika kuruani Tukufu. Kwani Ni maji yenye Chumvi zaidi kidogo ya Arabian/Persian Gulf ambayo ni 37 PSU na Chini kidogo ya Omanian Gulf ambayo ni PSU 40.

Na AVERAGE maana yake ni namba inayowiana na namba nyinginezo.

Ukifikiri utaona Kwamba Viumbe kama vile samaki na vinginevyo vinaweza kuhamia katika sehemu ya chumvi ya katikati kwa muda na baada ya kuzoea mazingara hayo viumbe hivyo vinaweza kuhama tena katika Ghuba Arabia/Persia yenye Maji ya Chumvi yaliyo na kiwango cha chini ya Maji Ya Chumvi yaliyopo upande wa Ghuba Ya Oman.

Sehemu hii ya katikati ambayo inajulikana kama BARZAKH ni kama TRANSIT ya sehemu ya Usalama. Kwani Viumbe haviwezi kuhamia kutoka katika Maji ya Chumvi yenye kiwango cha  40 PSU na Kwenda moja kwa moja na kuishi katika Maji yenye Chumvi yenye PSU 37.Ni lazima vihamie katika BARZAKH kwa muda mpaka vizoee katika Maji ya Chumvi iliyo katikati na kisha kuhamia katika Maji Yenye Chumvi ya Chini.

Kwa lugha nyingine Vinavyoishi katika Maji haya vitahama kutoka katika Maji ya Ghuba ya OMAN yaliyo na chumvi ya PSU 40 kwenda katika BARZAKH yenye Chumvi PSU 38.5 na Baada ya kuzoea mazingara hayo Vitahamia katika Maji ya Arabian/Persian yenye Chumvi PSU 37.

Kwa hiyo BARZAKH ni kama sehemu ya TRANSIT ya Maji kabla ya maji hayo kuchanganyika na Maji yenye sifa Nyinginezo.

Kwani Maji ya Ghuba Ya Oman na Arabian/Persian yana sifa mbalimbali zilizotofautiana kama vile Density, Temperature na Mengi mengineyo na lazima kuwe na Sehemu ya katikati au TRANSIT AREA Ili kuleta usalama kwa vinavyoishi katika aina ya Maji haya Mawili.

Na ndiyo maana Kuruani imetumia Neno “BAHRAYNI” lenye maana ya Bahari Mbili. Duality (Muthanna au Mbili) hapa inaashiria Maji yaliyo na sifa Tofauti na hayalingani.

Huu ni Muujiza Mkubwa. Mtume Mohamad (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alijua Vipi Vipimo vya Chumvi vya Baharini na Hasa Kipimo cha BARZAKH kama hapa tulivyoona katika sehemu ya Straight of Hurmuz.

Inabidi vyombo vya Utaalamu vya hali ya juu sana kuweza kujua Elimu kubwa kama hii.

La kushangaza ni kwamba WAHYI ulikua katika karne ya 7 na leo tupo katika karne ya 21. Allahu Akbar. Ni wakaidi na wajinga tu ndiyo wanapinga Uislamu.

Angalia Picha hapa Juu  ya Gulf au Ghuba Ya Oman na Arabian/Persian na maelezo yake yenye kushangaza. Kiwango  cha Chumvi PSU 38.5 ni sehemu ya BARZAKH.

Mwenyeezi Mungu anajua zaidi ikiwa siyo sehemu hiyo lakini vipimo tulivyoviona vya kitaalamu vinathibitisha habari hizi. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

MUUJIZA WA MZUNGUKO WA MAJI -“WATER CYCLE”

MZUNGUKO WA MAJI -WATER CYCLE

Kwa kawaida Maji ya mvua yanatoka ardhini kwa elimu inayojulikana kama “water cycle” Kuna daraja Nne katika mzunguko huu:

Evaporation-Jua linapopiga katika mabahari, maziwa, na mito baadhi ya maji hugeuka na kuwa mvuke (water vapour) na kuchanganyika na hewa. Hewa ilyopata joto hupanda angani na kubeba mvuke wa maji pia.

Condensation-Na jua linapopungua ukali na hewa kubaridika na kuwa baridi basi maji hugeuka na kuwa matonye na haya hukusanyika na kuwa mawingu.

Precipitation-matonye matonye ya maji katika mawingu hujikusanya, kuvutana na kujiunga baina yake na kuendelea kukua na hatimaye kuwa kubwa na nzito nayo hushuka chini kama MVUA. na iwapo hewa ikiwa baridi sana basi mmatonye yatabakia yameganda na kuanguka kama theluji au mvua ya mawe.

Kwa kifupi hizi ndiyo njia tatu ambazo zinajulikana kama “water cycle” au “mzunguko wa maji” Elimu hii iligunduliwa mwaka 1546 Na Bernard Palissy. Historia inasema kwamba huyu ndiye wa kwanza kuja na fikra hii ya mzunguko wa maji. Alipokwenda pwani aliona maji ya chumvi na matamu na akawaza kwamba haya maji matamu yamekuja kwa njia ya mvua.

Huyu asili yake ni Mfaransa alizaliwa mwaka 1509 na kufariki mwaka 1590 huko Paris.

Kabla ya Elimu hii kugunduliwa watu walikuwa nanafikiri kwamba mvua asili yake inakuja kutoka mbinguni na hakuna mtu aliweza kujua kwamba asili ya maji ni ardhini na hakuna aliyejua kwamba haya maji ya ardhi yanapopigwa na jua basi hupanda juu kwa njia ya mvuke kisha yanajikusanya na kurudi tena kama mvua na huu ndio mzunguko unaojulikana kama “water cycle”

Habari hizi zimeelezwa katika kuruani kwa neno moja tu.!!!!! nalo ni مَاءَكِ

kwa maana ya “maji yako”

Mwenyeezi mungu anaiambia ardhi “ardhi kunywa maji yako”.

Mwenyeezi Mungu angeiambia “kunywa maji ya mbinguni” lakini aliiambia “maji yako” Kwa kweli huu ni muujiza mkubwa katika kuruani kama pia miujiza mingineyo kwani.

Angalia hapa kahuna makosa kwani maji asili yake yanatoka ardhini na kuiambia ardhi “kunywa maji yako”; yaani yametoka ardhini au kwa lugha nyingine ni miliki ya ardhi na sio mbingu. Kwa kweli kuruani haikosei na wala haitakosea, maajabu makubwa sana na muujiza ambao unathibitisha kwamba kuruani ni maneno yake mwenyeezi mungu.

Mtume Mohamed angewezaje kujua habari za “water Cycle” kwani maji ya mvua asili yake yanatoka katika maji ya ardhini na sio mbinguni. Habari hizi zipo katika kuruani kuanzia karne ya 7 yaani karne 16 kabla ya ugunduzi.

Huu ni uthibitisho kwamba maneno haya siyo ya mtume bali yule yule aliyeumba ulimwengu ndiye yuleyule aliyeshusha kuruani hii:

Chapter (11) sūrat hūd (Hud)

وَقِيلَ يَـٰٓأَرۡضُ ٱبۡلَعِى مَآءَكِ وَيَـٰسَمَآءُ أَقۡلِعِى وَغِيضَ ٱلۡمَآءُ وَقُضِىَ ٱلۡأَمۡرُ وَٱسۡتَوَتۡ عَلَى ٱلۡجُودِىِّ‌ۖ وَقِيلَ بُعۡدً۬ا لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٤٤)

And it was said, “O earth, swallow your water, and O sky, withhold [your rain].” And the water subsided, and the matter was accomplished, and the ship came to rest on the [mountain of] Judiyy. And it was said, “Away with the wrongdoing people.”

Aya hii inahusu mwisho wa mafuriko ya Nabii Nuhu na Mwenyeezi Mungu aniamrisha ardhi imeze maji yake na Mbingu isimamishe mvua. Kwa kweli Mwenyeezi Mungu ni wa kuogopa.

Na Aya nyingineyo yenye kutuelezea sayansi hii ni ya sura ya AlHijr Aya namba 22

٢٢ وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنْتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ

And We send the fecundating winds, then cause the rain to descend from the sky, therewith providing you with water (in abundance), though ye are not the retainers of its stores. Surah Hijr 15:22

aya hii inaelezea namna ya hewa inavyofanya kazi yake katika kubeba mvuke wa maji hapa ardhini na kupeleka angani na mwenyeezi Mungu ametuamia neno  لَوَاقِحَ  ambayo ni sawa na kutia mbolea au ku  fertilize hewa hiyo. 

Aya zifuatazo  pia zinatuelezea hii elimu ya Hydrology 

٢١ أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَلَكَهُ يَنَابِيعَ فِي الْأَرْضِ

Do you not see that Allah sends down rain from the sky and makes it flow as springs….

Surah Zumar 39:21

١٨ وَأَنْزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّاهُ فِي الْأَرْضِ ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍ بِهِ لَقَادِرُونَ

And We send down water from the sky according to (due) measure, and We cause it to soak in the soil; and We certainly are able to drain it off (with ease).

Surah Muminun 23:18

Aya hizi mbili zinatuelezea zaidi kuhusu mvua inapopiga basi maji hutunzika kwa uwezo wake mwenyeezi mungu.

Kwa kweli tumshukuru sana mwenyeezi mungu kwa neema hii kubwa.

Allahu Akbar, Allahu Akbar. 

Mzunguko wa Maji ambao unajulikana kwa kiingereza kama

Mzunguko wa Maji ambao unajulikana kwa kiingereza kama “water cycle” Muujiza huu umeashiriwa katika kuruani kwa hekima kubwa sana.

UGUNDUZI WA MOTO CHINI YA ARDHI NA KISHA MAJI MENGI CHINI YA MOTO HUO KWA KIPIMO MARA TATU YA MABAHARI YOTE MAKUBWA DUNIANI UNATHBITISHA MANENO YA KURUANI NA HADITHI YA MTUME MOHAMED (Sala Na Amani Zake Mola Zimfikie)

MAJI CHINI YA ARDHI BAADA YA MOTO

Baada ya Utafiti wa muda mrefu wataalamu wamegundia kwamba asili ya Maji katika ardhi yote (Bahari, Mito na Maziwa) Kutoka katika Maji yaliyohifadhiwa ndani ya ardhi yetu. Maji yaliyopo ndani ya ardhi ni mengi sana mara tatu kwa ukubwa kuliko maji yaliyopo juu ya ardhi. Na Maji hayo yanapenya na kuja Juu katika Mito, Mabahari na Maziwa tunayoyanona kila siku. Maji Hayo yamehifadhika katika Miamba ya Rangi ya Blue yanayojulikana kama RINGWOODITE ambayo ipo chini ya ardhi yetu katika tabaka linalojulikana kama MANTLE sehemu ambayo umbali wake kutoka katika Gamba la Ardhi ni kilometer 700. . Miamba Ya RINGWOODITE Yana Joto Kubwa. Wataalamu wanasema kwamba Maji hayo ni kama BUFFER au STORAGE au RESERVOIR (kwa kiswahili ni HIFADHI) ambayo ndiyo sababu Bahari, Mito na Maziwa juu ya ardhi hayabadiliki wala kupungua miaka na miaka. Maji hayo kutoka katika RINGWOODITE hupanda Juu kwa njia ya Nyufa ambazo zimeungana Kuanzia tabaka la MANTLE mpaka Juu katika Gamba la Ardhi katika Maji ya Mabahari, Mito na Maziwa. Yaani Maji yanapozidi kwa njia ya Mvua basi hupenya chini na pia hivyo hivyo hupanda juu inapohitajika. Utafiti ulifanywa na wataalamu na vyuo vikuu duniani. Angalia Picha hapa chini inayohusiana na Habari hizi.

New Scientists

Massive ‘ocean’ discovered towards Earth’s core. A reservoir of water three times the volume of all the oceans has been discovered deep beneath the Earth’s surface. The finding could help explain where Earth’s seas came from.The water is hidden inside a blue rock called ringwoodite that lies 700 kilometres underground in the mantle, the layer of hot rock between Earth’s surface and its core.The huge size of the reservoir throws new light on the origin of Earth’s water. Some geologists think water arrived in comets as they struck the planet, but the new discovery supports an alternative idea that the oceans gradually oozed out of the interior of the early Earth. “It’s good evidence the Earth’s water came from within,” says Steven Jacobsen of Northwestern University in Evanston, Illinois. The hidden water could also act as a buffer for the oceans on the surface, explaining why they have stayed the same size for millions of years.

MUUJIZA WA KURUANI TUKUFU NA HADITHI ZA MTUME

Kuruani ilisema haya yote kabla ya Wataalamu Kugundia haya. Yaani Utafiti huu ni hivi karibuni. Mtume pia alisema katika hadithi kiajabu sana.Katika Hadithi ambayo ni Dhaifu iliyokusanywa na Abu Dawuud inayosema kwamba:

Alisimulia Abdullah ibn Amr ibn al-‘As kwamba Mtume alisema (Sala na Amani Zake Mola Zimfikie) “Chini ya Bahari kuna Moto na Chini ya Moto kuna Bahari

” قال النبي صلى الله عليه وسلم: (إن تحت البحر ناراً وتحت النار بحراً) [رواه أبوداود].

Na Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani Tukufu katika Aya Mbali mbali. La kushangaza ni kwamba Mtume alipata wapi elimu hii na yeye alikuwa akiishi Jangwani. Elimu za bahari zinataka Mashine kubwa kubwa ilikuweza kuzama na pi Vyomobo mbali mbali vya Utafiti. na Enzi Ya Mtume walikuwa hawaya jui haya kabisa. Hakuna aliyeweza kufikiri kwamba Maji na Moto yanaweza kukaa pamoja. Leo hii Sayansi inatuthibitishia kwamba Chini ya Bahari kuna Moto na Chini ya Moto kuna Bahari. Uamini au usiamini hivi ndivyo tunavyoambiwa na Wanasayansi na Wataalamu wa Leo hii katika wakati wa Elimu ya Hali Ya juu.

Al-Muuminuun-Sura Namba 23 Aya Namba 18

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٍ۬ فَأَسۡكَنَّـٰهُ فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابِۭ بِهِۦ لَقَـٰدِرُونَ (١٨)

18-Na tumeteremsha kutoka mawinguni maji kwa kiasi, na tukayatuliza ardhini, (tukayahifadhi ndani ya ardhi). Na hila shaka sisi ni wenye uwezo wa kuyaondoa

Al-Hijr-Sura Namba 15 Aya Namba 22

وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَـٰحَ لَوَٲقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَأَسۡقَيۡنَـٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُ ۥ بِخَـٰزِنِينَ (٢٢)

22-Na tunazileta pepo zimejaa umande (wa kufanya mawingu) na tunateremsha maii (ya mvua) kutoka katika mawingu hayo (yanayochungwachungwa na hizo pepo pia), kisha tunakunywesheni maji hayo (na wanyama wenu na miti yenu na mengineyo). Wala si nyinyi muyawekao (katika ardhi yakawa mito, · maziwa, mifereji, visima

Al-Naziaat-Sura Namba 79 Aya Namba 33

وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٲلِكَ دَحَٮٰهَآ (٣٠) أَخۡرَجَ مِنۡہَا مَآءَهَا وَمَرۡعَٮٰهَا (٣١) وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَٮٰهَا (٣٢) مَتَـٰعً۬ا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَـٰمِكُمۡ (٣٣)

30-Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza. 31-Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake 32-Na milima akaisimamisha 33·(Kafanya haya yote) kwa ajili ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu. (Basi aliyefanya yote haya si muweza wa kufufua?)

A-Raad-Sura Namba 13 Aya Namba 3

وَهُوَ ٱلَّذِى مَدَّ ٱلۡأَرۡضَ وَجَعَلَ فِيہَا رَوَٲسِىَ وَأَنۡہَـٰرً۬ا‌ۖ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ جَعَلَ فِيہَا زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ‌ۖ يُغۡشِى ٱلَّيۡلَ ٱلنَّہَارَ‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٣)

3-Na radi inamsabihi Mwenyezi Mungu kwa kumshukuru na (pia) Malaika (husabihi) kwa kumuogopa. Na (Mwenyezi Mungu) hupeleka mapigo ya radi na kumpiga nayo amtakaye.Na hao (makafiri) wanabishana juu ya Mwenyezi Mungu (kuwa yuko kweli au hayuko), na bali (ya kuwa yuko na) yeye ni Mkali wa kuadbibu

Al-Luqman-Sura Namba 31 Aya Namba 10

خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ بِغَيۡرِ عَمَدٍ۬ تَرَوۡنَہَا‌ۖ وَأَلۡقَىٰ فِى ٱلۡأَرۡضِ رَوَٲسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَبَثَّ فِيہَا مِن كُلِّ دَآبَّةٍ۬‌ۚ وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَأَنۢبَتۡنَا فِيہَا مِن ڪُلِّ زَوۡجٍ۬ كَرِيمٍ (١٠)

10-Ameziumba mbingu pasipo nguzo, (mihimili) mzionazo, na Ameiweka milima katika ardhi iii (ardhi) isikusukenisukeni; naye Ametawanya humo wanyama wa kila namna, na Tumeyateremsha maji kutoka mawinguni, na humo Tumeotesha (mimea) mizuri ya kila aina.

Aya Za Kuruani zinatufafanulia vizuri kwamba Mwenyeezi Mungu ameumba yote haya. Utaaalamu wa hali ya Juu ambao unhusiana na Mzunguko wa maji kiajabu sana tena sana. Sayansi ipo nyuma na mpaka leo bado Sayansi inasita. Ijakuwa kuna utaalamu wa hali ya juu lakini Bado wataalamu wa leo hawana uhakika kwamba Chini ya Bahari kuna Moto na Chini ya Moto kuna Bahari. Mtume alishasema hayo katika Karne ya saba!!! miaka 1400 iliyopita. Allahu Akbar, Allahu Akbar. Kwa Kweli Muwenyeezi Mungu Mkubwa sana. Angalia Mpangilio huu wa ajabu. Bahari mbili na katikati Moto. Bahari tuzazozijua na Zlipo chini ya Ardhi na katikati Moto. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

Gazeti La New Scientists Linathibitisha Mabahari Chini ya Gamba La Ardhi. Allahu Akbar

Picha inaonyesha kuweko kwa maji chini ya Gamba La Ardhi yaani chini ya Earth Crust. . Allahu Akbar.

MUUJIZA WA MAJI ZAMZAM NA MAJI MENGINEYO DUNIANI.

Kuna Hadithi mbalimbali za Mtume Mohamed (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) zilizokusanywa na Imamu Bukhari, Muslim na Wataalamu Wa Hadithi Wengineo Mashuhuru waliopita na ambazo zinahimiza Kutamka بسم الله الرحمن الرحيم “Bismillahi Arahmani Arahiym” katika vitendo vyetu vyote kama vile kuingia nyumbani na kutoka, kula chakula na kunywa maji. Kwa kifupi ni vizuri kutamka maneno haya katika vitendo vyetu vyote. Ukitamka kimoyomoyo ni sawa na kutamka kwa sauti na uchaguzi ni wako mwenyewe.

Leo sitazungumzia Historia Ya Aya hii lakini Muujiza unaotokana na Faida Ya Kusoma Kuruani au Kutaja Majina Ya Mwenyeezi Mungu katika Vyakula Maji Ya Kunywa. Sababu kubwa iliyonipelekea kuchagua Habari hii ni Utafiti Uliofanywa huko Japan Na Ugerumani ambao unashangaza sana.

UTAFITI ULIOFANYWA NA MWANA SAYANSI ANAYEJULIKANA KWA JINA MASARU EMOTO HUKO JAPAN UNASHANGAZA SANA

Utafiti wake unashangaza sana na kilichosababisha kufanya utafiti ni habari alizosoma kwamba kila kipande cha theluji Kinachoanguka kutoka angani kinakuwa na sifa za pekee tofauti na nyinginezo. Hakuridhika na fikra hii kwani Sayansi inasema kwamba Kila tonye la maji dogo au Molecule Ya Maji inaundwa na Atom Mbili za Hydrogen na Atom Moja ya Oxygen na inaandikwa kwa Herufi Mbili H (Hydrogen) na O (Oxygen) na huandikwa “H2O” na kwa hiyo Mtafiti huyu akafikiri kwamba haiwezekani kwa vipande vya theluji kuwa na sifa mbali mbali kwani maadamu asili yake ni moja basi muundo wa Vipande vya theluji vyote vitakuwa na muundo mmoja pia. Suala hili likamhamasisha afanye Utafiti na kuchunguza habari aliyosoma ambazo yeye aliona ni uongo.

Akaunda Maabara (Laboratory) ambayo ilikusanya Freezer yenye Regulator ili Utafiti wake uwe katika mazingara kama yale ya Mvua Inapopiga. kusiwe na Chochote ambacho kitaathiri na kuharibu Majaribio Hayo. Chumba alichofanyia utafiti aliweka Air Condition ili kiwe na Baridi kiasi cha -7 Degrees Centigrade. Akaweka katika Chumba hicho Hadubini (Microscopes) ambazo zina Kamera (Cameras).Na lengo lilikuwa kupiga picha Vipande vya Theluji kabla ya Kuyayuka na kuwa Maji. Na WanaSayansi katika Chumba hicho walivaa Nguo Za Joto kwani hali ya Hewa ni Baridi. Katika Utrafiti huo Alichukua Sampuli ya Maji yaliyotoka Katika Visima Viwili, Mito Miwili na Maziwa Mawili Mbalimbali.Alipogandisha Maji Hayo katika Freezer akashangaa sana kukuta kwamba Kila Kipande Kiliganda kwa Umbile tofauti na Nyingine kulingana na Habari aliyosoma.

Katika Wakati huo kulikuwa na Mwanafunzi aliyekuwa katika University ya Tokyo (Japan) ambaye alimwuliza Mwanasayansi Huyu kuhusu Utafiti huo na Tatizo alilolipata alipojibiwa Tatizo la Utafiti Mwanafunzi wa Kutoka Saudi Arabia akampa habari ya Maji Ya ZamZam na Akampa Bwana Masaru Ili afanye Utafiti kwa kutumia maji hayo pia.

Alipofanya Utafiti wa maji ya ZamZam akashangaa sana tena sana kukuta kwamba Maji hayo hayakuganda (crystallize) katika Freezer ya Utafiti.Lakini akichanganya (Dilute) na Maji ya kawaida kwa kiasi cha Mara 10000 basi maji hayo yataganda lakini anapata Vipande Vya Theluji Viwili Moja juu ya Nyingine. Akamweleza Kijana Kutoka Saudi Arabia habari hizo na Akajibiwa kwamba Huenda Sababu ya kupata Vipande Viwili vya Theluji ni Kutokana na Maneno Ya ZamZam yapo Mawili pia kwani ni Zam na Zam na ndiyo maana akigandisha anapata Vipande Viwili.

Kijana Wa Kutoka Saudi Arabia akaomba Ayasomee Kuruani katika Maji Ya kawaida na kisha Bwana Masaru Agandishe tena. Kwa hiyo kijana huyo akaleta Tape-Recorder na Kuruani ikasomwa. Lengo ni kuyasomea Maji. Bwana Masaru alipogandisha akashangaa kuona kwamba Maumbile ya Theluji ni Safi sana na na kupendeza sana. (The most perfectly-shaped crystals). Na baada ya Hapo akaachia Tape- Recorder itaje majina 99 ya Mwenyeezi Mungu. Mshangao ni kwamba Maji yalipogandishwa kila Jina la Mwenyeezi Mungu likasababisha Theluji kuganda kufuatana na Jina. Yaani Kila Jina Lilizalisha Umbile la Theluji ambalo ni zuri sana na Unique.Bwana Masaru alifanya Utafiti huu kwa muda wa miaka 15 na baadaye aliandika Vitabu Vikubwa Vitano (Five-Volume Book) na Jina La Vitabu hivyo aliviita “Messages From Water” Alielezea Kwamba Amehakikisha Kwamba Maji ni Pekee kwa sifa kwani Yanaweza kufikiri, Kuhisi na Kujielezea. (“I have proven that water, that peculiar liquid, is capable of thinking, fathoming, feeling, getting excited, and expressing itself.”) Na aliendelea kuelezea humo kwamba Maji Ya Zam Zam ni safi (Pure) sana na huwezi kupata kwingine duniani na ni maji ya pekee.

Katika Utafiti wake alitumia Uwanja wa Sayansi unaojulikana kama NANO TECHNOLOGY” alifanya utafiti kwa muda mrefu sana katika Maji ya ZamZam na kagundua kwamba Ukichanganya Tonye Moja La Maji Ya ZamZam katika Matonye 10000 ya Maji Ya Kawaida basi hayo ya kawaida yatageuka na kuwa Sawasawa (Same Quality) kama Maji Ya ZamZam.

Aligundu pia kwamba Mineral (Madini) katika Tonye moja la Maji ya ZamZam ina umuhimu Maalum na Huwezi kupata katika Maji ya aina yeyote duniani.

Akagundua pia kwamba Sifa (Quality) au Viungo vya Maji Ya ZamZam hayawezi kubadilika na Sayansi bado haijapata Jawabu kwa nini sifa hizo hazibadiliki na hata ukiyachakata chakata sifa hizo hazibadiliki au kuharibika.

Masaru Akagundua kwamba Waislamu wanataja BISMILLAHI ARAHMANI ARAHIYM kabla ya kula na kunywa. Akasema kwamba Baada ya Kutaja Aya Hii katika Maji Ya Kawaida basi Kuna Mabadiliko ya Kiajabu ambayo yanatokea katika Sifa (Qualtity) Ya Maji. Yaani Maji Yanakuwa Mazuri.

HABARI ZA KUSHANGAZA KUHUSU MAJI YA ZAMZAM

ZamZam water level is around 10.6 feet below the surface. It is the miracle of Allah that when ZamZam was pumped continuously for more than 24 hours with a pumping rate of 8,000 liters per second, water level dropped to almost 44 feet below the surface, BUT WHEN THE PUMPING WAS STOPPED, the level immediately elevated again to 13 feet after 11 minutes. 8,000 liters per second means that 8,000 x 60 = 480,000 liters per minute 480,000 liters per minutes means that 480,000 x 60 = 28.8 Million liters per hour And 28.8 Million liters per hour means that 28,800,000 x 24 = 691.2 Million liters per day So they pumped 690 Millions liters of Zamzam in 24 hours, but it was re-supplied in 11 minutes only. There are 2 miracles here, the first that Zamzam was re-filled immediately, & the second is that Allah Holds the extra-ordinarily powerful Aquifer for not throwing extra Zamzam out of the well, otherwise the world will SINK. Allah says in the Holy Quran; “We will soon show them Our signs in the Universe and in their own souls, until it will become quite clear to them that it is the truth.

Ayat Quran From Sura 41 Aya Namba 53

Is it not sufficient as regards your Lord that He is a witness over all things?” (41:53)

UTAFITI ULIOFANYWA UGERUMANI

Kama utakavyoona Video hapa chini Ya Mtafiti huko Ugerumani ambaye alichukua Maji kutoka katika sehemu mbalimbali na kisha akapima pH ya maji (kipimo kinachuhusu Kiwango cha Acid katika Maji). Wataalamu wanasema Maji ya ALKALINE ni mazuri kwani yanasaidia Kuondoa ACID mwilini. Maji yenye pH 7 ni maji yaliyo NEUTRAL yanakuwa hayana ACID na chini ya hapo yanakuwa na ACID. Maji Ya ZAMZAM kutoka Mecca kama utakavyoona Video hapa chini yamepimwa na huyu Mtafiti na Kukuta yana pH 8 (kwa hiyo ni maji yanayojulikana kama ALKALINE)kwa kulinganisha na maji kutoka sehemu nyinginezo za Dunia.

KIPIMO CHA pH

pH is a measure of how acidic/basic water is. The range goes from 0 to 14, with 7 being neutral. pHs of less than 7 indicate acidity, whereas a pH of greater than 7 indicates a base. pH is really a measure of the relative amount of free hydrogen and hydroxyl ions in the water. The lower the number, the more acidic. Healthline reveals that “normal drinking water generally has a neutral pH of 7; alkaline water typically has a pH of 8 or 9.” Results show that alkaline water is more beneficial by being able to effectively neutralize the acid in your body compared to other waters

MAONI

Kufuatana Na Hadithi za Mtume na Utafiti Mbalimbali Duniani Nina Imani kwamba Ukisomea Kuruani Maji, Chakula au Kitendo Chochote kile kwa kusoma Aya Ya بسم الله الرحمن الرحيم “Bismillahi Arahmani Arahiym” au Kutaja Jina au Sifa Za Mwenyeezi Mungu basi Kila unachofanya kitafanyika Vizuri. Na Chakula na Maji Vitakuwa Vizuri katika mwili wako.Yaani Mwenyeezi Mungu atavitilia Baraka Kabla ya Kuingia Matumboni.

VIDEO-1

Video Hii inazungumzia Utafiti wa Maji ya ZAMZAM na Habari nyinginezo zinazohusu Aya na Majina Ya Mwenyeezi Mungu yanaposomwa katika Maji na Mengineyo. Allahu Akbar

VIdeo-2

Utafiti Wa Maji Ya ZAMZAM huko Ugerumani. Kwa kweli Inashangaza. Ni Maji Safi yenye pH 8 ambayo inajulikana kama ALKALINE WATER. Ni Maji Mazuri Sana Mwilini

Utafiti Wa Maji Uliofanywa Na Bwana MASARU EMOTO Huko Japan. Kwa kweli inashangaza. Maji Ya ZAMZAM ni Maji yenye sifa pekee Duniani. Na Pia Maji yeyote mengineyo ukisomea Aya ya Kuruani na Pia Kutaja Majina au Sifa za Mwenyeezi Mungu basi Yanakuwa na Mfumo au Structure nzuri. Soma habari hizi hapa juu na pi asikiliza Video niliyoambatanisha hapa.