UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MATIBABU WAKATI WA KIPINDI CHA DHAHABU; “GOLDEN AGE”
katika Video hii hapa chini kuna habari za maendeleo ya matibabu katika kipindi cha dhahabu “Golden Age”.
Waislamu walikuwa katika kipindi cha elimu kubwa wakati ambao nchi za ulaya zilikuwa bado nyuma sana katika kipindi kinachoitwa “Dark Ages” na Elimu ya Waislamu ilikuja Europe baada ya waislamu kutawala Spain kwa miaka mingi.
Katika kipindi hicho vitabu vya sayansi vilivyoandikwa kwa lugha ya kiarabu vilifasiriwa katika lugha ya kilatini na kisha kufasiriwa katika lugha nyinginezo za Ulaya.
Watafiti wanatueleza habari nyingine kuwa vitabu vingi vilichukuliwa na vingine kuibiwa kutoka kwa waislamu.
Na mpaka leo kitabu maarufu cha Sheikh Ibn Sina kimechapishwa katika lugha mbalimbali na unaweza kupata habari zake katika mtandao kwa wanavyuoni wanaotaka kufanya utafiti zaidi katika elimu ya matibabu.
Bwana Ibn Sina alikuwa wa asili ya Kifarisi, alizaliwa huko Bukhara katikati ya Asia (Uzbekhistan) katika mwaka 980 AD na akafariki mwaka 1037 AD Aliandika vitabu vinginevyo na alikuwa hodari katika elimu nyinginezo kama vile Hesabu na Falsafa.
Alikuwa mtibabu wa magonjwa ya nafsi na pia aliandika mashairi. Alihitimisha kuhifadhi kuruani alipokuwa na umri mdogo.
Ibn Sina alijulikana ulaya kwa jina la Avicenna na kitabu chake maarufu kwa jina “The Cannon of Medicine” kimeelezea elimu mbalimbali ya matibabu yaliyotumika wakati wake.
Mpaka leo elimu yake ni msingi wa matibabu ya kisasa.
Wanavyuoni wengine kama vile Al-Raziy na wengineo pia wametajwa habari zao katika hii Video.
SISIMIZI KATIKA KURUANI
Mwenyeezi Mungu ameashiria habari za sisimizi katika kuruani katika kisa cha Nabii Sulayman. Na pia akajaalia sura kuitwa kwa “sisimizi” au “Annaml”. Kabla ya maendeleo ya kisayansi watu hawakuelewa maisha ya sisimizi na wala umuhimu wa mwenyeezi mungu kutaja katika kuruani habari za sisimizi.
Ni wadudu wanaoishi kwa umoja na kuna speshi (aina au species) zaidi ya 12000 za sisimizi katika dunia. Sisimizi mmoja ana uwezo wa kubeba uzito sawa na mwili wake mara 20. Katika kilka Spishi (Jamii au species) ya sisimizi kwa kawaida hugawanyika katika makundi mbalimbali;
Na kila kundi lina kazi maalum. Kundi lenye kufanya kazi, kundi lenye kumlinda Malika wao , kundi lenye kujenga nyumba zao, Kundi lenye kutafuta chakula, kundi lenye kulea mayai na watoto.
Watafiti wanasema Sisimizi wanatumia njia mbalimbali katika kuwasiliano: Kwa kutumia Sauti kama utakavyoona katika Video, Wanapogusana au Wanapogusa ardhi kwa kutumia miili yao na kusababisha mtetemeko wa ardhi (vibrations) na njia nyingineyo kama vile kutumia kemikali inayojulikana kama “pheromones” ambayo imeelezwa vizuri katika Video. Na pia hutumia Antenna au manyoya mwilini mwao katika kutafsiri habari yoyote inayohusiana na wamasiliano yao na mengi mengineyo ambayo hatujui isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake..
Jambo la kushangaza na ambalo linatuhusu katika mjadala huu sio kumsoma uhai wa sisimizi bali kusoma Aya katika kitabu kitukufu “Kuruani Takatifu” zinazozungumzia wadudu hawa (sisimizi).
Aya katika sura namba 27 ya “Annaml” au “sisimizi” aya kuanzia namba 16-19
وَوَرِثَ سُلَيۡمَـٰنُ دَاوُ ۥدَۖ وَقَالَ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ عُلِّمۡنَا مَنطِقَ ٱلطَّيۡرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَىۡءٍۖ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَضۡلُ ٱلۡمُبِينُ (١٦)
وَحُشِرَ لِسُلَيۡمَـٰنَ جُنُودُهُ ۥ مِنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ وَٱلطَّيۡرِ فَهُمۡ يُوزَعُونَ (١٧)
حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَوۡاْ عَلَىٰ وَادِ ٱلنَّمۡلِ قَالَتۡ نَمۡلَةٌ۬ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّمۡلُ ٱدۡخُلُواْ مَسَـٰكِنَڪُمۡ لَا يَحۡطِمَنَّكُمۡ سُلَيۡمَـٰنُ وَجُنُودُهُ ۥ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ (١٨)
فَتَبَسَّمَ ضَاحِكً۬ا مِّن قَوۡلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوۡزِعۡنِىٓ أَنۡ أَشۡكُرَ نِعۡمَتَكَ ٱلَّتِىٓ أَنۡعَمۡتَ عَلَىَّ وَعَلَىٰ وَٲلِدَىَّ وَأَنۡ أَعۡمَلَ صَـٰلِحً۬ا تَرۡضَٮٰهُ وَأَدۡخِلۡنِى بِرَحۡمَتِكَ فِى عِبَادِكَ ٱلصَّـٰلِحِينَ (١٩)
Tafsiri ya aya hii kwa kiswahili:
16/Na Suleimani alimrithi Daudi na akasema:”Enyi Watu! Tumefundishwa (hata kutambua) usemi wa ndege na tumepewa kila kitu; hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri”.
17/Na akakusanyiwa Suleimani majeshi yake katika majini na watu na ndege, nayo yakapangwa makundi makundi (katika kwenda kwake).
18/Hata walipofika katika bonde la wadudu chungu (aina ya sisimizi), alisema mdudu chungu (wa kike) (kuwaambia wenziwe): “Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Suleimani na majeshi yake, hali ya kuwa hawakuhisini (hawana habari)”.
19/Basi akatabasamu akilichekea neno lake (huyo chungu), na akasema: “Ee Mola wangu! Nipe nguvu nishukuru neema Yako Uliyonineemesha mimii na wazazi wangu, na nipate kufanya vitendo vizuri Uvipendavyo, na Uniingize-kwa rehema Yako-katika waja Wako wema”.
MUUJIZA KUTOKA KATIKA AYA HIZI
Jambo la Kwanza ni kutajwa neno “Bonde” (Valley)Yaani aya hii intufahamisha kwamba wadudu hawa wanaishi kwa pamoja na wana miji yao kama vile “Bondeni” au Hujenga majengo mbalimbali kutegemea aina ya sisimizi. Angalia Video ya kwanza watafiti walipofukua Bonde la wadudu hawa na namma walivyojenga nyumba zao na vyumba mbalimbali na kila chumba kina matumizi yake.
Jambo la pili katika Aya hizi Mwenyeezi Mungu ametumia neno Qalat Annamla” ni mwanamke kuwaambia wenziwe kuwa waingie majumbani mwao. Na kama tunavyoelewa baada ya utafiti wa kisayansi wa hivi karibuni kwamba sisimizi wa kike hawana mabawa na ndiyo maana waliambiwa waingie katika nyumba zao kwani kama wangelikuwa sisimizi wa kiume labda wangeambiwa watumie mbawa kuruka angani(kwani sisimizi wa kiume wana mabawa) Na mwenyeezi Mungu katumia neno “Qalat” na herufi “t” yenye maana anayetamka ni mwanamke akiwaambia wenziwe wajifiche. Angalia Picha hapa chini ya ukurasa huu.
Jambo la tatu katika Aya hizi ni kuonyesha mawasiliano baina wa wadudu hawa, yaani wanapeana habari kwa njia mbalimbali kama katika Video ya pili na ya tatu.
Jambo la nne linaonyesha kuwa wadudu hawa wana hisia, wanaelewa kuwa Suleimani ana huruma na kwamba atakapopita na jeshi lake huenda akawakanyaga bila kujua na sio kukusudia, Suleimani alifurahi sana kumsikia sisimizi huyu na kuelewa kwamba Sisimizi alitambua kuwa Suleimani ni Nabii na Nabii hawezi kufanya ubaya kwa hao sisimizi.
Jambo la tano linaonyesha kuwa wadudu hawa wanaishi kwa umoja na wala hawaishi pekee na ndio maana Sura hii imeitwa “Annaml” kwa Tafsiri ni “Sisimizi” (“Ants”).
Jambo la sita ni kwamba sayansi haiwezi kugundua siri nyinginezo kama vile yaliyo ndani ya nafsi za wadudu hawa. Wanasayansi wanafanya utafiti katika kufasiri lugha kwa kutumia vyombo mbalimbali lakini tafsiri zote ni iza kubuni tu.
Quruani ni Muujiza hata katika majina ya Sura za Kuruani. Uchaguzi na upangaji wa Sura, au Aya, Au Herufi na idadi zake pia zote ni Muujiza. Na huwezi kukuta kosa katika kuruani kwani mwenyeezi Mungu ameahidi kutunza maandishi yake. Ni Elimu zetu zilizo pungufu na Sayansi zilizo bado nyuma zinazosababisha kutokuielewa kuruani.

Picha hii inaonyesha kuwa Sisimizi wa kiume wana mabawa na wakike hawana mabawa
Ukipata Message “Video Unavailable” basi tafadhali Bonyeza hapo juu “Watch on You Tube” ili uione Video hii.
Hili ni Bonde (Valley) ambalo linamilikiwa na sisimizi. Wamejenga nyumba zao chini ya Ardhi. Kuruani inathibitisha nyumba hizi.
Utafiti wa mawasiliano baina ya sisimizi. Kuruani inathibitisha mawasiliano haya.
Mawasiliano mbalimbali lakini hawana masikio bali wana njia nyinginezo mbalimbali.
Sauti za sisimizi zimerikodiwa kwa kutumia vyombo vya kukuza sauti.Wadudu hawana masikio lakini wanasauti zilizorikodiwa ambazo zina matumizi mengine katika jamii yao.
NYUKI
MUUJIZA WA NYUKI KATIKA KURUANI TUKUFU
Mwenyeezi Mungu amesema Katika Kuruani Takatika
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
Tafsiri Ya Sura Namba 16 Aya Nambari 68 na 69
Na mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba: “Jitengenezee majumba (yenu) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayoyajenga (watu)
ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٦٩)
“kisha kuleni (Nyuki wa kike) katika kila matunda, na mpite (Nyuki wa kike) katika njia za Mola wenu zilizofanywa nyepesi (kizipita).” Kunatoka katika matumbo yao kinywaji (asali) chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponyo (poza au dawa) kwa wanaadamu. Hakika katika hayo muna mazingatio kwa watu wenye fikra.
Katika Aya hizi mbili tunasoma elimu mbalimbali zinazohusiana na maisha ya nyuki na faida ya asali
1/Mwenyeezi Mungu amewafundisha kujenga nyumba zao kwa ufundi mkubwa katika miti, milima na pia kutumia mizinga ya asali inayojengwa na watu.
2/Wamefundishwa hapa kutumia njia mbalimbali zilizo nyepesi.
3/Asali yenye rangi mbalimbali na dawa kwa binaadamu
4/Katika kifungu hiki Mwenyeezi Mungu anamuamrisha Nyuki wa kike na sio wa kiume kwani herufi “Y” katika kifungu “Kuliy”na “Faslukiy” ni ya Feminine (Kike) na “ki” katika “rabikki” ni ya Feminine (Kike). Na neno “ha” katika Butuniha ni linaashiria Feminine (Kike).
ُثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا
Sayansi imegundua hivi karibuni kwamba Nyuki wa kike ndio wenye kufanya kazi ya kutafuta chakula na wa kiume wana kazi nyinginezo kama vile kumlinda malikia na kumtia Mbolea za kiume-Fertilization.
Ukizichinguza mafundisho haya utaona kwamba njia mbalimbali nyepesi wanazotumia nyuki katika kutafuta chakula ni zenye ufundi mkubwa sana. kama tunavyoona katika Video hapa chini kwamba nyuki anapogundua chakula (maua) basi ataonja kidogo kisha atarudi kuwajuulisha wenziwe. na wanasayansi watafiti wa uwanja huu wamegundua pia mawasiliano baina ya nyuki kwa kwa njia ya dansi mojawapo inayoitwa kwa kiingereza “waggle dance” nyuki atacheza dansi ambayo itawaonyesha wenziwe njia (direction) katika njia hizo nyepesi alizotaja mwenyeezi mungu. na pia mda wa dansi unaonyesha umbali wa chakula (uwa) hicho, muda mfupi una maana ya umbali sio mrefu na muda mrefu ni umbali ulio mrefu.
Utafiti wa wataalamu mwingine unaonyesha dansi mbalimbali na kila dansi in habari tofauti katika kuwasiliana huko.
Jambo lingine la kushangaza ni muujiza wa Elimu ya Hesabu katika Aya ifuatayo:
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
Aya pekee Katika kuruani inayozungumzia habari za nyuki na yenye neno la nyuki.
Na jambo la kushangaza ni kwamba
1/idadi ya maneno yaliyotumika katika Aya hii ni 16
2/Herufi za kiarabu (Abgadiya) zilizotumika bila kukariri katika Aya hii ni 16
و ا ح ي ر ب ك ل ن ت خ ذ م ج ش ع
3/Sura Ya “Annhl” ni namba 16
4/Sura Ya “Annahl” ina Aya 128 nazo kihesabu zina uhusiano na namba 16 kama vile katika kizidisho (multiple) cha (16 x 8=128)
5/Maneno ya sura hii (ukihesabu herufu Alwaw-Al’atf kama neno) ni 2080 KIzidisho (multiple) ya( 130 x 6=2080)
6/Kifungu (Phrase) وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡل kina herufi 16
7/Maneno ya Kuruani kuanzia mwanzo wa sura mpaka neno رَبُّكَ katika kifungu وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ yaani kabla ya neno ٱلنَّحۡل katika kifungu إِلَى ٱلنَّحۡل ni 992 ambayo ni kizidisho (multiple) ya (62 x 16=992)
8/Na ukihesabu maneno baada ya neno ٱلنَّحۡل mpaka mwisho wa sura utakuta 1088 kizidisho (multiple) ya (68 x 16=1088)
Hekima na Muujiza huu Mwenyeezi Mungu ameujaalia ili uwazidishie imani wachamungu wa leo hii katika wakati wa technologia ya juu na pia iwe hoja kwa wana sayansi wanaojigambia na sayansi.
Namba 16 Mwenyeezi Mungu hakuchagua bure kwani Nyuki katika Elimu ya Jenetiki (Genetics) ameumbwa kama ifuatavyo:
Drone Bee ana chromosomes 16 (Male Bee/Nyuki wa kiume) Haploid=1n
Queen Bee (Malkia) ana chromosomes 32 Diploid=2n
Worker Bee ana Chromosomes 32 (Female Bee/Nyuki wa Kike) diploid=2n
Yaani kila kilichoumbwa na mwenyeezi Mungu kina namba tofauti za Chromosomes, Binaadamu wana Chromosomes 23 na hivyo hivyo Nyuki wana Chromosomes 16 Na Female Bee (Nyuki wa kike) ana Chromosomes 32 ambazo zinazotokana na kuzaliwa kwake kutota katika yai ambalo lilitiwa mbolea na nyuki wakiume na kuchanganyikana. (16 + 16=32)
Na ajabu ni kwamba Katika Aya tulizozitaja hapo juu pia tunakuta kizidisho (multiple) ya namba 32 kama ilivyo katika mfano huu hapa chini:
1/Aya za sura ya “Annahl” ni 2080, kizidisho (multiple) cha(32 x 65)
2/Idadi ya aya za sura ya “Annahl” ni kizidisho (multiple) cha 128=(32 x 4)
3/Maneno ya Kuruani kuanzia mwanzo wa sura mpaka kifungu وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ kabla ya kifungu إِلَى ٱلنَّحۡل ni kizidisho (multiple) ya 992 (32 x 31)
4/Na ukihesabu maneno baada ya neno ٱلنَّحۡل mpaka mwisho wa sura 1088 ,kizidisho (multiple) ya (32 x 34)
Kuna Elimu inayoitwa “BIOMIMETICS” nayo inahusiana na Binaadamu kusomea viumbe na kutumia mfano huo katika Kuendeleza Technologia mbalimbali kama vile watu wamejenga nyumba mbalimbali kufuata mfano wa nyumba zilizojengwa na Nyuki.
Jambo lingine muhimu ni kujua kwamba Sega La Nyuki (Honeycomb) (kama katika picha hapa chini)limejengwa na nyuki kwa ufundi mkubwa sana lina umbile la “Hexagon” (pembe sita) na hili ndilo jengo wanalounda nyuki na kutumia katika kuweka Asali. Wanasayansi wanasema kwamba ni jengo halipotezi wakati wa nyuki katika kuliunda, halipotezi nafasi kwani asali hujaa vizuri na pia natumizi machache ya nta ya nyuki (Wax inayotokana na asali na pollen ya maua) katika ujenzi huo. Umbile lingine lolote kama vile Pembe Nne (Square) au Pembe Tatu (Triangle) au Pembe Tano (Pentagon) na maumbile nyinginezo hayawezi kuwa mazuri kama Pembe Sita (Hexagon) kwani zingepoteza Nta ya nyuki au Wakati wao katika ujenzi au Nafasi Ya Asali au vyote hivi.
Baada ya kuangalia Video hizi na baada ya kupata habari kama hizi je kuna shaka yeyote kwamba kuruani ni kitabu cha ukweli? Sayansi kadiri inavyoendelea na kugundua vitu utakuta habari zake katika kuruani.
Na Ajabu ni kwamba bado kuna mengi ya kusoma katika kuruani na sisi bado hatuna elimu ya kutosha. Kwa sababu elimu zetu ndogo na ndiyo maana tumezidi ujinga. Kuruani imekuja kuinua watu juu lakini wengi wameidharau na kuiacha nyuma na Mwenyeezi Mungu ametuacha tuzidi kuwa nyuma kwa ujinga wetu. Mwenyeezi Mungu anasema:
وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ ڪَثِيرً۬ا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٌ۬ لَّا يَفۡقَهُونَ بِہَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٌ۬ لَّا يُبۡصِرُونَ بِہَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٌ۬ لَّا يَسۡمَعُونَ بِہَآۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ كَٱلۡأَنۡعَـٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡغَـٰفِلُونَ (١٧٩)
Na Bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na wanaadamu (kwa sababu hii) Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo (hawataki kufahamu kwazo), na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama; hali wao ni wapotovu zaido. Hao ndio walioghafilika.
Elimu ya Jenetiki (Genetics) Inatufahamisha Idadi Ya Chromosomes katika Nyuki wa Kike ni 16 (Masculine) Na Nyuki wa Kiume ni 32 (Feminine).
Mawasiliano Baina Ya Nyuki
Mawasiliano Ya nyuki kwa njia ya dansi
Maisha Ya Nyuki na Ufundi waliopewa na Mwenyeezi Mungu

Sega La Nyuki (Honeycomb) ambalo linaonyesha Umbile la Hexagon.
KUNGURU KATIKA KURUANI TUKUFU
Maajabu ya kushangaza ni kwamba Kunguru alitajwa katika kuruani walipokuja kumfundisha Kabil namna na kumzika ndugu yake Habil.kisa hiki kinatuonyesha kwamba Kunguru ni Njiwa mwenye Akili na ufundi ambao umempita Binaadamu. Kabili alipomuua ndugu yake Habili na Mwenyeezi Mungu akatuma Kunguru wawili ambao walipigana na mmoja kamuua mwingine na kisha kumzika mbele ya Kabil ili kumfundisha namna ya Kuzika. Kuruani intuonyesha elimu na ufundi wa kunguru na leo hii tunaona Utafiti wa kisayansi unatuthibitishia haya.
Sura Namba 5 Ayat Namba 31
فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابً۬ا يَبۡحَثُ فِى ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُ ۥ كَيۡفَ يُوَٲرِى سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَـٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَـٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٲرِىَ سَوۡءَةَ أَخِىۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ (٣١)
Tafsiri Ya Aya
Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika ardhi ili amwonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake. Akasema: (yule ndugu aliyeua): “Ole wangu! Nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu?” Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.
Na ajabu ni kwamba leo hii wana Sayansi wamefanya utafiti na kugundua vizuri Maajabu ya Akili ya Kunguru. Angalia Video Hapa Chini Inayohusiana na utafiti Juu Ya Kunguru na Pia Mkusanyiko anapokufa mmoja wao. Je wanakuja Kuzika? Yote haya Yanatufundisha Uwezo wa Mwenyeezi Mungu kama alivyosema katika Kuruani Tukufu Kwamba Njiwa na Viumbe vinginevyo ni kama sisi binaaadamu.
Sura Namba 6 Aya 38
وَمَا مِن دَآبَّةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَـٰٓٮِٕرٍ۬ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِى ٱلۡكِتَـٰبِ مِن شَىۡءٍ۬ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّہِمۡ يُحۡشَرُونَ (٣٨)
Tafsiri Ya AYa
Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake mbili ila ni umati kama nyinyi (tunadhibiti kila walifanyalo).Hatukupuza Kitabuni (mwetu) kitu cho chote. Kisha watakusanywa kwa Mola wao (awalipe)
na Pia Ardhi ni pamoja na viumbe vinginevyo na siyo binaadamu peke yao.
وَٱلۡأَرۡضَ وَضَعَهَا لِلۡأَنَامِ (١٠)
Tafsiri Ya Aya
Na ardhi Ameiweka (Ameitandaza) kwa ajili ya viumbe
Jina La Kunguru (Al-GHURAB) Katika Sura Ya Alfatiha
Na tukifanya kuhasabu Herufi za Jina la Kunguru (AL-Ghurab) tutapata Jumla Ya Herufi 80 (Alif=22 + Lam=22 + Ghain=2 + Raa=8 + Alif=22 + Baa=4=80)
Na Sayansi inatuambia kwamba Chromosomes za Kunguru ni 80, Na Katika aina au Speshi (Species) za Crow 17 kwa mfano Corvus brachyrhynchos au Corvus Corax au Corvus Cornix na speshi (species) nyinginezo. (Hapa tumetaja aina tatu tu lakini kuna zaidi ya hizi) Utakuta Speshi (Species) 11 kutoka hizi 17 wana Chromosomes 80.Na Speshi (Species) chache zilizobaki Kuna zenye Chromosomes 78, 82 na 76 Na tukiendelea na Utafiti wetu tutakuta Kunguru ametajika mara mbili Katika Aya namba 31 Sura namba 5 Na mara moja katika Sura Namba 35 Aya Namba 27 Aya namba 31
Sura namba 5
فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابً۬ا يَبۡحَثُ فِى ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُ ۥ كَيۡفَ يُوَٲرِى سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَـٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَـٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٲرِىَ سَوۡءَةَ أَخِىۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ
(٣١) Tafsiri Ya Aya 31.
Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika ardhi ili amwonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake. Akasema: (yule ndugu aliyeua): “Ole wangu! Nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu?” Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.
Sherehe Ya Aya
Ukihesabu herufi za Neno AlGhurab (kunguru) katika Aya namba 31 Sura namba 5 utapata Alif=9 + Lam=9 + Ghain=2 + Raa=6 + Alif=9 + Baa=5=40 Na 40 namba hii inaashiria idadi ya Chromosome katika Maji ya Uzazi wa Corbeau Na Pia ukujumlisha Herufi hizi bila ya kuzihesabu zilizokariri utapata Jumla ya Herufi 31 na namba hii inaashiria namba ya Aya Hii ya 31
Aya namba 27 Sura namba 35
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً۬ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ ثَمَرَٲتٍ۬ مُّخۡتَلِفًا أَلۡوَٲنُہَاۚ وَمِنَ ٱلۡجِبَالِ جُدَدُۢ بِيضٌ۬ وَحُمۡرٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُہَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ۬ (٢٧)
Tafsiri Ya Aya 27.
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji toka mawinguni! Na kwayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(mfano weusi wa kunguru)
Sherehe Ya Aya
Ukihesabu Herufi za jina Garabiyb Al-Suwd (Kunguru Mweusi) katika Aya namba 27 Sura namba 35 utapata Ghain=1 + Raa=5 + Alif=11 +Baa=5 + Yaa=2 + Baa=5 + Sin=2 + Waw=6 + Dal=3=40 Na namba hii 40 inaashiria idadi ya Chromosome katika Maji ya Uzazi wa Corbeau. Na ukihesabu Herufi hizi bila kukariri utapata namba 35 ambayo ni namba ya Sura Hii hii. Ghain=1 + Raa=5 + Alif=11 +Baa=5 + Yaa=2 + Sin=2 + Waw=6 + Dal=3=35 Aya Zinazohusiana na Kisa Cha Habil Na Kabil (Watoto wa Adam)
Sura Namba 5 (Al-Maidah)
۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡہِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَىۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانً۬ا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأَخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ (٢٧) لَٮِٕنۢ بَسَطتَ إِلَىَّ يَدَكَ لِتَقۡتُلَنِى مَآ أَنَا۟ بِبَاسِطٍ۬ يَدِىَ إِلَيۡكَ لِأَقۡتُلَكَۖ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢٨) إِنِّىٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثۡمِى وَإِثۡمِكَ فَتَكُونَ مِنۡ أَصۡحَـٰبِ ٱلنَّارِۚ وَذَٲلِكَ جَزَٲٓؤُاْ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٢٩) فَطَوَّعَتۡ لَهُ ۥ نَفۡسُهُ ۥ قَتۡلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ ۥ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلۡخَـٰسِرِينَ (٣٠) فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابً۬ا يَبۡحَثُ فِى ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُ ۥ كَيۡفَ يُوَٲرِى سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَـٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَـٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٲرِىَ سَوۡءَةَ أَخِىۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ (٣١)
Tafsiri Ya Aya 27 Mpaka 31
27.Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adamu kwa kweli. Walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao, na ya mwengine haikukubaliwa. Akasema (yule isiyokubaliwa sadaka yake). “Nitakuua, Akasema (yule aliyehadidiwa kuuawa): “Mwenyezi Mungu huwapokelea wamchao tu.”
28.”Kama utanyosha mkono wako kwangu kuniua, mimi sitakunyoshea mkono wangu kukuua. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu.
29.”Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako; na kwa hivyo uwe miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.”
30.Basi nafsi yake ikamwezesha kumwua nduguye; akamwua: na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika.
31.Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anayefukua katika ardhi ili amwonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake. Akasema: (yule ndugu aliyeua): “Ole wangu! Nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu· yangu?” Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.
Sherehe Ya Aya Hizi 5
Na ukihesabu maneno katika kisa cha Adamu na Watoto wake wawili Habil Na kabil kuanzia mwanzo wa kisa hicho Sura Namba 5 Kuanzia Aya Namba 27 mpaka Aya Namba 31 katika neno kabla ya Jina la Kunguru kutajwa (hapa ni hilo jina Ghurab la pili) utapata maneno 80 ambayo namba hii inaashiria Chromosomes katika Celi (Cell) Za Kunguru.
katika Aya hii namba 31 ukihesabu Herufi baina ya Majina ya Kunguru mawili utapata Jumla ya Herufi 57 nayo kihesabu inajulikana kama Composite Number kwani ni sawa na 19 X 3 Namba 57 ukii-multiply mara mbili utapata namba 114 ambayo inaashiria idadi ya sura za kuruani. (Yaani 57 mara mbili kufuatana na idadi ya kunguru kutajika) Katika Elimu ya Hesabu; Tukichunguza Composite Namba 57 utakuta ni ya 40, Na namba hii 40 inaashiria idadi ya Chromosome katika Maji ya Uzazi wa Corbeau Na Composite Number 80 ni ya 57. Na Namba 80 inaashiria idadi ya Chromosomes katika Celi au Cell za Kunguru.
Lingine la kushangaza ni kwamba Sura namba 5 na Sura namba 35 ambazo zimetumia neno Kunguru ukijuumlisha namba hizi mbili utapata 40 (35 + 5=40) Na namba hii 40 inaashiria idadi ya Chromosomes katika Maji ya Uzazi wa Corbeau.
Neno Kunguru ni la 19 katika Sura namba 5 Aya ya 31 na la 21 katika Sura Namba 35 Aya Namba 27 na Jumla ya namba hizi mbili ni 40 (19 + 21=40) Na namba hii 40 inaashiria idadi ya Chromosome katika Maji ya Uzazi wa Corbeau.
Neno (Makr) lenye maana ya Hila au Ujanja Mkubwa limetumika katika Aya namba 10 na 43 Sura namba 35 ambayo imezungumzia habari za kunguru. Ukihesabu Namba za Aya Hizi Tatu; Aya Namba 10 + Aya Namba 27 + Aya namba 43=80 ambayo ni idadi ya Chromosomes katika Celi au Cells za Kunguru.
Na ukihesabu Herufi zisizokariri za neno Kunguru katika Aya namba 10 na 43 ya Sura namba 35 Aya hizi ambazo zimetumia neno Makr au Ujanja (nalo linaashiria kiajabu Ujanza wa Kunguru) .Utapata idadi ya herufi 80 ambazo zinaashiria Chromosomes za Kunguru
Alif=27 + Lam=37 + Ghain=0 + Raa=10 + Baa=6 =80
Hapa Alif zisizokariri ni 27 na hatukuihesabu Alif ya pili katika Jina Alghurab. Na namba hii 80 inaashiria Idadi za Chromosomes katika Celi au Cells za Kunguru.
(Na hekima kubwa ya kutajika neno Makr au Ujanja hapa inatuthibitishia kwamba Ujanja wa Kunguru umetokana na Chromosome aliyeiumba Mwenyeezi Mungu kwani hapo mna habari za kila kiumbe)
Kunguru Ni Njiwa Mwenye Intelligence (Ubongo)ya hali ya Juu. Angalia maajabu namna anavyopasi Mtihani Mgumu.
Hapa Kunguru Mmoja Amekufa na wengineo wamekusanyika katika Mazishi. Yaani Mazishi ya Kunguru.
SALA ZA VIUMBE VINGINEVYO
Njiwa na kila kiumbe Wanasali lakini sisi binaadamu hatujui namna wavyosali Sura Namba 24 Aya Namba 41
أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلطَّيۡرُ صَـٰٓفَّـٰتٍ۬ۖ كُلٌّ۬ قَدۡ عَلِمَ صَلَاتَهُ ۥ وَتَسۡبِيحَهُ ۥۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ (٤١)
Tafsiri Ya Aya
Je huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtukuza (vyote) vilivyomo mbinguni na ardhini, na ndege wakikunjua mbawa zao (na wasipozikunjua)? Kila (mmoja katika wao) amekwishajua sala yake na namna ya kumtukuza kwake (Mwenyezi Mungu wake);na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa (yote) wanayoyafanya.
Angalia Video hapa chini za Njiwa Anasujuduna pia Kufanya Tawafu Huko Mecca Ama kweli Mwemyeezi Mungu Mkubwa. Na kwa Hakika Anayosema katika Kuruani ni Kweli.
Na pia Video inayotuonyesha ujanja wa Njiwa. Hawezi kuenda kuchukua asali mwenyewe kwani ataumwa na nyuki kwa hiyo anamtumia binaadamu ambaye baada ya kupata asali anampa njiwa huyo kidogo yaani ujira wake. Kwa kweli Kuruani haina kosa hata moja. Mwenyeezi Mungu anaposema kwamba Wanyama na Ndege ni Viumbe kama sisi, yaani wan maisha yao na pia njia za kupata riziki na mengi mengineyo ya ajabu sana, na kuna mengi hatuyajui. Allahu Akbar, Allahu Akbar
Njiwa Anasujudu Kuielekea Kaaba Huko Mecca. Je unaona Utukufu Wa Nyumba Ya Mwenyeezi Mungu?
Njiwa Wanafanya Tawafu Huko Mecca. Je Unaona Ya Maajabu!!
Kila Kiumbe Kimepewa Ujanja Katika Kutafuta Riziki Yake. Njiwa anapenda kula asali lakini hawezi kuipata kwani ataumwa na nyuki kwa hiyo anamuongoza Binaadamu mpaka katika sehemu ya Asali kisha anasubiri Ujira wake wa asali Yaani Ni Uhusiano wa kazi Baina Ya Njiwa Na Binaadamu.
MUUJIZA KATIKA HADITHI INAYOHUSIANA NA NZI (FLY)
Katika Video ifuatayo Wajinga wanamcheka Mtume Mohamed aliposema kwamba Nzi anapoangukia katika kinywaji basi usitupe kinywaji hicho bali mtumbukize Nzi huyo kabisa kisha umtupe na kinywaji hicho kitakuwa hakina dhara yeyote kwani katika ubawa mmoja kuna maradhi na katika ubawa wa pili kuna dawa. Wanaomcheka Mtume Mohamed kweli ni wapumbavu kwani Wataalamu hivi karibuni huko Australia wamegundua Anti-Biotics katika Ubawa mmoja wa Wadudu kama vile Nzi. (Flies).Ninawaletea hapa chini Habari za Wataalamu katika News ya Gazeti La Sayansi pamoja na Video Ya Wajinga ujionee mwenyewe. Waislamu Kuweni macho na Mtandao kwani umejaa waongo na walaghai. Someni Dini Vizuri ili Mjilinde na wajinga wasiokuwa na Elimu yeyote. Soma Ushahidi hapa chini kutoka katika habari za Sayansi kisha sikiliza Video Ya wajinga wasiojua chochote. PIcha Ya Nzi (Fly) hapa chini inasema Mdudu huyu ni mbaya hana umbile zuri lakini ni mdudu mwenye manufaa sana. Yaani maneno haya yanatoka kwa wataalamu baada ya ugunduzi wa madawa ya Anti-Biotics. Na ugunduzi huu ni katrika Sayansi mpya za Kileo.
Mtume Anasema Katika Hadithi Iliyopo katika Sahih Bukhari
حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ بِلاَلٍ، قَالَ حَدَّثَنِي عُتْبَةُ بْنُ مُسْلِمٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي عُبَيْدُ بْنُ حُنَيْنٍ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ يَقُولُ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم “ إِذَا وَقَعَ الذُّبَابُ فِي شَرَابِ أَحَدِكُمْ فَلْيَغْمِسْهُ، ثُمَّ لِيَنْزِعْهُ، فَإِنَّ فِي إِحْدَى جَنَاحَيْهِ دَاءً وَالأُخْرَى شِفَاءً ”.
Translation:
Narrated Abu Huraira: The Prophet (ﷺ) said “If a house fly falls in the drink of anyone of you, he should dip it (in the drink) and take it out, for one of its wings has a disease and the other has the cure for the disease.”
MAKALA KUTOKA KATIKA GAZETI LA SAYANSI
News in Science /The new buzz on antibiotics
The surface of flies is the last place you would expect to find antibiotics, yet that is exactly where a team of Australian researchers is concentrating their efforts. Working on the theory that flies must have remarkable antimicrobial defences to survive rotting dung, meat and fruit, the team at the Department of Biological Sciences, Macquarie University, set out to identify those antibacterial properties manifesting at different stages of a fly’s development. “Our research is a small part of a global research effort for new antibiotics, but we are looking where we believe no-one has looked before,” said Ms Joanne Clarke, who presented the group’s findings at the Australian Society for Microbiology Conference in Melbourne this week. The project is part of her PhD thesis.
The scientists tested four different species of fly: a house fly, a sheep blowfly, a vinegar fruit fly and the control, a Queensland fruit fly which lays its eggs in fresh fruit. These larvae do not need as much antibacterial compound because they do not come into contact with as much bacteria. Flies go through the life stages of larvae and pupae before becoming adults. In the pupae stage, the fly is encased in a protective casing and does not feed. “We predicted they would not produce many antibiotics,” said Ms Clarke. They did not. However the larvae all showed antibacterial properties (except that of the Queensland fruit fly control). As did all the adult fly species, including the Queensland fruit fly (which at this point requires antibacterial protection because it has contact with other flies and is mobile). Such properties were present on the fly surface in all four species, although antibacterial properties occur in the gut as well. “You find activity in both places,” said Ms Clarke. “The reason we concentrated on the surface is because it is a simpler extraction.” The antibiotic material is extracted by drowning the flies in ethanol, then running the mixture through a filter to obtain the crude extract. When this was placed in a solution with various bacteria including E.coli, Golden Staph, Candida (a yeast) and a common hospital pathogen, antibiotic action was observed every time. “We are now trying to identify the specific antibacterial compounds,” said Ms Clarke. Ultimately these will be chemically synthesised. Because the compounds are not from bacteria, any genes conferring resistance to them may not be as easily transferred into pathogens. It is hoped this new form of antibiotics will have a longer effective therapeutic life.

Ugly but useful: The sheep blowfly is one of the fly species that might provide humans with new antibiotics. (Pic: BioTrack.)
FINGER PRINT KATIKA KURUANI-MAAJABU YASIYO NA MWISHO
FINGER PRINT KATIKA KURUANI-MAAJABU YASIYO NA MWISHO
Sura Namba 75 Aya Namba 1-4
لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَـٰمَةِ (١) وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ (٢) أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَـٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُ ۥ (٣) بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُ ۥ (٤)
Tafsiri Ya Aya 1-4
1-Naapa kwa siku ya Kiama 2-Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu;(kuwa mtafufuliwa na mtalipwa).3-Anadhani mtu ya kuwa sisi hatutaikusanya mifupa yake? 4-Kwa nini! Sisi tunaweza (hata) kuzisawazisha ncha za vidole vyake (tutakapomfufua mara ya pili,ziwe kama zilivyokuwa duniani). (Ncha za Vidole hapa ndiyo leo hii inajulikana kama Finger Print)
Sherehe Ya Kihesabu (Mathemarical Comment)
Ukihesabu Aya za Kuruani Kuanzia Mwanzo wa kuruani mpaka Aya namba 4 Sura Ya Al-Qiyamah Namba 75 Utapata Aya 5555 hizi zinalingana na Namba za vidole vya mikono na miguu Na kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Qiyamah Mpaka Neno Bananah Ayah Namba 4 Kuna Maneno 20 Na namba 20 ni sawa na 5 X 4 ambayo inaashiria Vidole Vya Mikono na Miguu. Kuanzia Mwanzo wa Kuruani Mpaka Sura Ya Kiyama kuna Sura 74 na ukijuumlisha idadi Ya namba za Sura hizi Kuanzia Sura Ya Al-Fatiha mpaka Sura Ya mwisho kabla ya Sura Ya Al-Qiyamah (Yaani 1 + 2 + 3 mpaka 74=2775) utapata 2775 na namba hii ni sawa na 555 X 5 ambayo pia ina namba 5 ambazo zipo Nne nazo zinaashiria Vidole Vya mikono na Miguu. Maneno Ya Sura Ya Alkiyama ni 165 Nayo ni sawa na 55 + 55 + 55 (Tano hapa pia inaashiria Vidole Vitano vya miguu na mikono) Na Neno Bananah katika Aya Ya Sura Ya Al-Qiyamah Aya namba 4 Limetumia Jumla Ya Herufi 5 (Ba + Nun + Alif + Nun + Haa) nazo zinaashiria Vidole Vitano. Na ukihesabu idadi ya Sura Za Kuruani Mpaka mwisho wa sura ya Alkiyama utapata sura 2850 na namba hii ni sawa na 5 X 5 X 114 Tano hapa inaashiria Vidole Vitano na 114 inaashiria idadi ya Sura zote za kuruani.
Katika Kuruani Yote Kuna Aya Mbili tu Ambazo Kumetajwa Neno Bananah;
Sura Ya Al-Anfal Namba 8 Aya Namba 12
إِذۡ يُوحِى رَبُّكَ إِلَى ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ أَنِّى مَعَكُمۡ فَثَبِّتُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ سَأُلۡقِى فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ فَٱضۡرِبُواْ فَوۡقَ ٱلۡأَعۡنَاقِ وَٱضۡرِبُواْ مِنۡہُمۡ ڪُلَّ بَنَانٍ۬ (١٢)
Tafsiri Ya Aya
12-(Kumbukeni) Mola’ wako alipowafunulia Malaika (akawaambia): “Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini; nitatia woga katika nyoyo za makafiri. Basi wapigeni juu ya shingo (zao) na kateni kila ncha za vidole vyao.
Sura ya Al-Kiyamah Namba 75 Aya namba 4
بَلَىٰ قَـٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّىَ بَنَانَهُ ۥ (٤)
Tafsiri Ya Aya 4
-Kwa nini! Sisi tunaweza (hata) kuzisawazisha ncha za vidole vyake (tutakapomfufua mara ya pili,ziwe kama zilivyokuwa duniani). (Ncha za Vidole hapa ndiyo leo hii inajulikana kama Finger Print)
Sherehe Ya Kihesabu (Mathematical Comment)
Sura Ya Al-Qiyamah Aya Namba 4 kuna Jumla ya herufi 23. Na Sura Ya Al-Anfal Namba 8 Aya Namba 12 kuna Jumla ya maneno 23 Namba 23 inaashiria kwanza Muda wa Miaka iliyoshuka Kuruani Tukufu ambayo ni Miaka 23 Na Pia Jumla Ya Chromosomes za baba na mama (23 + 23=46) ambazo ni 46 Neno Banan katika Aya namba 12 Sura Ya Al-Anfal limetumia Herufi 3 tu zisizokariri nazo ni (Baa + Nun + Alif) Na Jumla Ya Herufi Hizi katika Aya Hizi Mbili ni kama ifuatavyo: BA zimekariri mara 9 + Nun zimekariri mara 13 + Alif zimekariri mara 24 =Jumla 46 Na namba hii inaashiria idadi za Chromosomes za baba na mama. (23 za kiume na 23 za kike). Kama tulivyozungumzia kwa kirefu katika Video za “Sauti za Mwandalizi” kuhusu Chromosomes kwamba ndiyo asili ya kila kiumbe. Kwani mchanganyiko wa Chromosomes za baba na mama ndiyo inayosababisha tofauti baina ya viumbe vyote na ndiyo sababu ya kutofautiana kwa Finger Print tangu kuumbwa dunia mpaka mwisho wa dunia. Saini za vidole zinatumika tangu zamani na huwezi kupata binaadamu wawili wenye Finger Print zenye kufanana na hii inatokana na DNA ya Chromosomes ambazo zipo ndani ya Nucleus Ya Cells za kila kiumbe. Ukijuumlisha Namba Ya Sura Ya Al-Qiyamah 75 + Anfal 8=jawabu ni 83 na ajabu ni kwamba namba hii Ni Prime Number ya 23 katika Hesabu(Tumezungumzia Prime Numbers katika website hii).Na hapa tena tunaona namba 23 inaashiria zile Chromosomes tulizozitaja hapa Juu. Kuna uhusiano baina ya Chromosomes katika Aya hizi mbili na Asili ya Finger Print (Neno Bananah) kwani Umbile la Finger Print linatokana na chembe za Chromosomes za baba na mama zilizopo katika kiinitete (Nucleus) za kila kiumbe. Aya Hizi mbili zimetupa neno بَنَانٍ۬ Banan/ بَنَانَهُ ۥ Bananah ambalo lina maana kubwa.
Aya zimekuja na Ujumbe kuwajibu makafiri lakini hapo hapo kuna sayansi ya hali ya juu ambayo imewekwa na Mwenyeezi Mungu. Sayansi za leo zinagundua haya ili kuthibitisha ukweli kwamba kuruani siyo maneno ya Mtume peke yake bali yanatoka kwake Mwenyeezi Mungu aliyetukuka. Allahu Akbar.
DAWA YA MARADHI YA MACHO (CATARACT) KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU
Kisa cha Nabii Yusufu ni kizuri sana kama alivyosema Mwenyeezi Mungu katika Kuruani (Sura Ya Yusuf Aya Ya Tatu). Ni kisa chenye mawaidha makubwa na ya kushangaza. Katika maandishi haya hatutazungumzia Kisa hiki bali kuna Maajabu Mengineyo katika Aya mbili hapa chini.
Baba Yake Yusufu alisikitika na akalia sana kwa muda mrefu kwa kupotelewa na mtoto wake Nabii Yusufu hatimaye akaugua macho. Maradhi haya bila shaka ni Cararact. Na baada tu ya baba yake Nabii Yusufu kutupiwa Nguo hiyo usoni akapona maradhi hayo.
Na ugonjwa huu unasababisha Lens (lenzi) ya macho kuzungukwa na mabakabaka meupe na kusababisha kutokuona vizuri na ukiachilia huweza kusababisha upofu (Cataracts are when the lens, a small transparent disc inside your eye, develops cloudy patches. Over time these patches usually become bigger causing blurry, misty vision and eventually blindness. When we’re young, our lenses are usually like clear glass, allowing us to see through them).
Mtaalamu Dakitari Wa Kimisri (Egyptian) Bwana Abdul Basit Muhammed alifikiri sana kuhusu Aya mbili hapa chini na akajiuliza sababu gani iliyomponesha macho Nabii Yakub yaani Baba Yake nabii Yusuf.
Na akajiuliza sababu gani nguo hiyo iwe ni dawa ya kumponesha Nabii Yakub macho yake. Baada ya kufikiri sana akapata jawabu kwamba hakuna kingine isipokuwa Jasho katika nguo hiyo. Basi akafanya utafiti wa kuchunguza Jasho na kugundua kwamba Jasho lina Viungo au Elements mbalimbali nazo ndiyo pekee zilizosababisha kuponesha maradhi hayo. Dakitafri huyu akafanya utafiti na akafanya majaribio na kugundua kwamba kweli Jasho ni dawa ya maradhi haya.(Jasho la mtu mwingine kwa sasa kuna hatari ya Coronna lakini unaweza kutumia dawa ya Jasho iliyotengenezwa katika pharmacy zenye kujulikana ulimwenguni )
Baada ya Utafiti na uhakika akafanya makubaliano na kampuni ya madawa (Pharmacy) huko Swiss kutengeneza dawa ya macho yenye kutibu maradhi haya bila ya kufanya Operesheni.
Yaani dawa ya kunyunyiliza matonye katika macho. Aliomba kampuni hiyo kutia Jina la dawa hiyo liwe “Dawa Ya Kuruani”
Wataalamu wanasema kwamba dawa hii imesajiliwa katika nchi za Ulaya na Marekani na ina mafaniko makubwa kiasi cha asilimia 99. (This drug, which was compiled by an Egyptian doctor Abdul Basit Muhammad from the secretion of human sweat glands, has success in 99% of cases without any unwanted consequences. Quran drug is registered in Europe and the United States)
Chapter 12 Aya Namba 84 na 93
وَتَوَلَّىٰ عَنۡہُمۡ وَقَالَ يَـٰٓأَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَٱبۡيَضَّتۡ عَيۡنَاهُ مِنَ ٱلۡحُزۡنِ فَهُوَ كَظِيمٌ۬ (٨٤) 84.
Tafsiri Ya Aya
Na akajitenga nao na akasema: “Oo! Majonzi yangu juu ya Yusufu!” Na macho yake yakawa meupe kwa huzuni (Mboni zimefunikwa na weupe); Naye alikuwa amejaa (huzuni).
93 ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِى هَـٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِى يَأۡتِ بَصِيرً۬ا وَأۡتُونِى بِأَهۡلِڪُمۡ أَجۡمَعِينَ (٩٣) .
Tafsiri Ya Aya
“Nendeni na kanzu yangu hii na muiweke mbele ya uso wa baba yangu: naye atafunuka macho aone .. Na nijieni (nyote) pamoja na watu wenu wote. ”
SHAHIDI WA KIUME WAWE WAWILI LAKINI AKIPUNGUA MMOJA WA KIUME NA HAKUNA MWINGINE ISIPOKUWA WA KIKE BASI SHAHIDI WA KIKE LAZIMA WAWE WAWILI. YAANI MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WAWILI KATIKA WALE WATAKAORIDHIWA KUWA MASHAHIDI
Sura Ya Al-Baqarah Aya Namba 182
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيۡنٍ إِلَىٰٓ أَجَلٍ۬ مُّسَمًّ۬ى فَٱڪۡتُبُوهُۚ وَلۡيَكۡتُب بَّيۡنَكُمۡ ڪَاتِبُۢ بِٱلۡعَدۡلِۚ وَلَا يَأۡبَ كَاتِبٌ أَن يَكۡتُبَ ڪَمَا عَلَّمَهُ ٱللَّهُۚ فَلۡيَڪۡتُبۡ وَلۡيُمۡلِلِ ٱلَّذِى عَلَيۡهِ ٱلۡحَقُّ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُ ۥ وَلَا يَبۡخَسۡ مِنۡهُ شَيۡـًٔ۬اۚ فَإِن كَانَ ٱلَّذِى عَلَيۡهِ ٱلۡحَقُّ سَفِيهًا أَوۡ ضَعِيفًا أَوۡ لَا يَسۡتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلۡيُمۡلِلۡ وَلِيُّهُ ۥ بِٱلۡعَدۡلِۚ وَٱسۡتَشۡہِدُواْ شَہِيدَيۡنِ مِن رِّجَالِڪُمۡۖ فَإِن لَّمۡ يَكُونَا رَجُلَيۡنِ فَرَجُلٌ۬ وَٱمۡرَأَتَانِ مِمَّن تَرۡضَوۡنَ مِنَ ٱلشُّہَدَآءِ أَن تَضِلَّ إِحۡدَٮٰهُمَا فَتُذَڪِّرَ إِحۡدَٮٰهُمَا ٱلۡأُخۡرَىٰۚ وَلَا يَأۡبَ ٱلشُّہَدَآءُ إِذَا مَا دُعُواْۚ وَلَا تَسۡـَٔمُوٓاْ أَن تَكۡتُبُوهُ صَغِيرًا أَوۡ ڪَبِيرًا إِلَىٰٓ أَجَلِهِۦۚ ذَٲلِكُمۡ أَقۡسَطُ عِندَ ٱللَّهِ وَأَقۡوَمُ لِلشَّہَـٰدَةِ وَأَدۡنَىٰٓ أَلَّا تَرۡتَابُوٓاْۖ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَـٰرَةً حَاضِرَةً۬ تُدِيرُونَهَا بَيۡنَڪُمۡ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَلَّا تَكۡتُبُوهَاۗ وَأَشۡهِدُوٓاْ إِذَا تَبَايَعۡتُمۡۚ وَلَا يُضَآرَّ كَاتِبٌ۬ وَلَا شَهِيدٌ۬ۚ وَإِن تَفۡعَلُواْ فَإِنَّهُ ۥ فُسُوقُۢ بِڪُمۡۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ وَيُعَلِّمُڪُمُ ٱللَّهُۗ وَٱللَّهُ بِڪُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمٌ۬ (٢٨٢)
TAFSIRI
282. Enyi mlioamini! Mnapokopeshana deni kwa muda uliowekwa, basi iandikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika; kama alivyomfunza Mwenyezi Mungu hivyo; basi naandike. Na ayatamke (maneno hayo ya kuandikwa hivyo, mkopaji) ambaye juu yake iko haki; ·naye amwogope Mwenyezi Mungu, Mola wake; wala asipunguze cho chote ndani’ yake. Na kama yule ambaye juu yake iko Haki (mkopaji) ni mpumbavu au mnyonge au yeye hawezi kuandikisha mwenyewe basi aandikishe msimamizi wake (yule mtu anayemwendeshea mambo yake) kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika watu wenu wanaume (Waislamu). Lakini ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili (watatosha); katika wale mnaowakubali kuwa mashahidi. IIi kama mmoja wao (katika wale wanawake) akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuiandika (hiyo deni), ikiwa ndogo au kubwa mpaka muda wake; hayo (ya kuandika) ndiyo bora mbele ya Mwenyezi Mungu, na imara zaidi kwa ushahidi, na pia ni ya kupelekea kuwa msiwe na shaka. lla ikiwa ni biashara iliyohudhuria mnayopeana (macho kwa macho) baina yenu, basi si vibaya kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Wala asitiwe taabuni mwandishi wala shahidi. Na kama mkifanya hivyo; basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mwogopeni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyczi Mungu anakuilimisheni; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
SHEREHE KISAYANSI
Aya hii inahusika na Madeni na Biashara. Tunafundishwa namna ya kukopana na pia njia iliyo bora katika Biashara ili kujiepusha Dhuluma. Hakuna katika Kuruani kisicho na maana. Aya zote zina Muujiza. Kuhusiana na Mashahidi Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Ikiwa yule Mkopaji ni mpumbavu au mnyonge au yeye hawezi kuandikisha mwenyewe basi aandikishe msimamizi wake (yule mtu anayemwendeshea mambo yake) kwa uadilifu. wanaume (Waislamu). Lakini ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili (watatosha); katika wale mnaowakubali kuwa mashahidi. IIi kama mmoja wao (katika wale wanawake) akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine.
Jambo la kushangaza ni Hekima ya Mwenyeezi Mungu anaposema kwamba Lakini ikiwa hakuna mashahidi wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili (watatosha); katika wale mnaowakubali kuwa mashahidi. IIi kama mmoja wao (katika wale wanawake) akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine.
Kuhusu Ushahidi wa Mwanaume mmoja lakini Wanawake wawili na sio mmoja inaonyesha kwamba Wanawake wana tabia ya Kusahaukwa hiyo itabidi wawili ili mmoja wao akisahau basi wa pili atamkumbusha mwenzake.
Sayansi Inatuelezea kuhusu maisha ya Mwanamke kwamba baada ya Mwanamke kupita Muda wa Hedhi na kuingia Muda unojulikana kwa Lugha ya kiingereza “Menopause” (yaani hakuna tena kuzaa) basi Hormone ndani ya mwili wa Mwanamke inayojulikana kama Estrogen inpungua na kupungtua huko kunaathiri ubongo katika kuhifadhi habari zilizopita na kusababisha kusahau
(Hormonal imbalance. During menopause, women’s levels of estrogen drop, which has been shown to cause problems with the way the brain stores memories. This will only result in normal memory loss and brain fogginess)
Sayansi inasema pia kwamba Ubongo wa Mwanaume na Mwanamke unatofautiana katika maumbile. (Angalia Picha Hapa Chini) na tofauti hii haitakuwa bure bure bali kuna sababu mbalimbali na mojawapo ni kazi (Functions) ya kila sehemu.
Elimu zetu bado changa na hapa Mwenyeezi Mungu anatufundisha Elimu ambayo hata Sayansi bado ipo nyuma na ndiyo maana ukiuliza wataalamu wanababaika.
Mwenyeezi Mungu anajua zaidi kwa nini Shahidi wa kiume anapokosekana basi angalau Mmoja anatosha na shahidi wa pili watakuwa wanawale wawili na siyo mmoja. Mwenyeezi Mungu ana hekima kubwa.
Allahu Akbar. Allahu Akbar

Tofauti Kati Ya Ubongo wa Kiume na Kike. Kuna Tofauti mbalimbali. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi na kuruani haikukosea. Allahu Akbar
Angalia Neurons (Mishipa Midogo sana) ambayo inaungana kiajabu sana Ubongo wa Mume na Mke unatofautiana na siyo sawa. Kuruani ni Muujiza Mkubwa. Sayansi ipo nyuma. Tofauti hii inathibitisha kwamba Mume Mmoja anatosha kuwa Shahidi bali Wanawake lazima wawe wawili kwani wana tatizo la kusahau sahau. Neurons za Kike zimesambaa na kuungana baina ya Left and Right Hemispheres (widthwise)za Ubongo lakini za kiume hazikusambaa baina ya Hemispheres mbili bali zimeenea na kuungana katika kila Pande Moja Moja yaani lengthwise(Hemisphere). Ubongo wa Mume unaweza kusimamia Hukumu na kutatua matatizo makubwa na Specific. Wa Kike unafuata Emotions na Pia unaweza kutatua Matatizo madog madogo ya Jamii. Kila Mmoja amepewa uwezo wa kazi maalum. Mke na Mume hawako sawa katika kazi hizi. Mungu Anajua Zaidi. Allahu Akbar
MAAJABU YA KURUANI NA UBONGO WA VIUMBE
UMBILE LA UBONGO
Wataalamu wa Elimu ya BIOLOGY wamegawanya ubongo katika sehemu tatu; Cerebrum, Cerebellum na Brainstem.
Cerebrum imegawanyika katika sehemu mbili; Right Cerebral Hemisphere na Left Cerebral Hemisphere.
Cerebrum Hemisphere imagawanyika katika sehemu au lobes nne; Frontal, Temporal, Parietal, na Occipital.
Katika Utafiti huu unaohusiana na Kuruani Tukufu tutazungumzia Sehemu au kipande (Lobe)moja tu nayo ni Frontal Lobe ambayo inahusiana na Utu (Personality), Tabia (Behaviour), Hukumu (Judgement), Kutatua Tatizo (Problem Solving), Mazungumzo (Speech), Harakati Za Mwili, (Body Movement) na Shughuli Nyinginezo Za Mishipa Ya Fahamu (Motor Function).
Kwa hiyo Frontal Lobe ndiyo yenye kuhukumu Utu (Personality) na Pia uwezo wa Kuwasiliana na Wengine katika Jamii.
Na sehemu hii yaani Frontal Lobe ni sehemu au Lobe kubwa kuliko Lobes nyinginezo katika Ubongo. Karibu Thuluthi ya Ubongo ni Celebral Hemispheres zote mbili ni Frontal Lobes. Frontal Lobes zimefunikwa na Prefontral Cortex (PFC).
Wataalamu wanatuambia kwamba Sehemu ya mbele ya Ubongo yaani Frontal Lobes ndiyo sehemu ya Maamuzi ya Binaadamu. Ukiamua kufanya Madhambi au Mazuri basi hiyo ndiyo Mashine yenye kufanyauamuzi huo na ndivyo Mwenyeezi Mungu alivyojaalia.
Ni Sehemu iliyopewa Madaraka kufanya kazi hiyo na tunaweza kuiita Executive Area au Sehemu ya Kutenda.
Yaani kuchagua kati ya Baya na Zuri.
SHEREHE KISAYANSI KUFUATANA NA AYA ZA KURUANI
Sura Ya Al-Alaq Namba 96 Aya Namba 15-16
كَلَّا لَٮِٕن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ (١٥) نَاصِيَةٍ۬ كَـٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ۬ (١٦) 15-
Sivyo hivyo (anavyofanya!) Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za paji la kichwa (mbele ya kichwa) (tumtie Motoni)
———————
16-Paji La kichwa lenye uongo na madhambi. Sura Ya Al-Rahman Namba 55 Aya Namba 41
يُعۡرَفُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ بِسِيمَـٰهُمۡ فَيُؤۡخَذُ بِٱلنَّوَٲصِى وَٱلۡأَقۡدَامِ (٤١) –
41-Watajulikana waovu kwa alama zao; basi watakamatwa kwa nywele za paji la kichwa (mbele ya kichwa) na kwa miguu (watiwe Motoni). –
———————————–
Katika Aya Mbili hapa Juu Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Kama huyo Kafiri hataacha Ukaidi basi atamkokota kwa nywele zake za mbele ya kichwa na kisha atatupwa motoni.
Nywele Mbele ya kichwa katika sehemu ya Frontal Lobe ambayo wana Sayansi wanatuthibitishia kwamba ndiyo sehemu inayohusika na Hukumu (Judgements), Maamuzi (Decision Making) na pia katika Kudhibiti (Control) vitendo kama vile Ukweli na Uongo, Na Haki (Righteousness).
Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Kafiri atachukuliwa kwa kushikwa nywele za meble ya kichwa ambazo zimeota juu ya sehemu inayohusiana na Uongo.
Na Syansi ya leo inatuthibitishia yaliyozungumzwa na Kuruani miaka 1400 iliyopita. Kwa kweli ni Muujiza sio Mdogo. Kuruani inaelezea Sayansi kwa njia tusiyotegemea. Allahu Akbar. Na Katika Aya Ifuatayo Mwenyeezi Mungu anatuambia na hata wanyama sehemu hiyo ya Ubongo imepewa kazi maalum kufuatana na maisha yao. Na wote Binaadamu na Wanyama Mwenyeezi Mungu anasarifu atakavyo.
Sura Ya Hud Namba 11 Aya Namba 56
إِنِّى تَوَكَّلۡتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّى وَرَبِّكُمۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذُۢ بِنَاصِيَتِہَآۚ إِنَّ رَبِّى عَلَىٰ صِرَٲطٍ۬ مُّسۡتَقِيمٍ۬ (٥٦)
6-“Mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe yo yote isipokuwa Nywele za Paji la Uso (Mbele ya kichwa) zipo katika mikono yake Mwenyezi Mungu (anamsarifu atakavyo). Bila shaka Mola wangu yuko juu ya njia liyonyoka.
” HADITHI YA MTUME
Mtume Mohamed (Sala na Amani ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alisema
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: (الْبَرَكَةُ فِي نَوَاصِي الْخَيل)
Baraka Katika Nywele za Mbele ya Kichwa cha Mbunyu( Forelock)
Mbunyu ni Mtoto wa Farasi na Punda
Hadithi Hii ilikusanywa katika Vitabu vya MIshkat Almaswabih na pia Mutafakun (Imekubaliwa) baina ya Imamu Muslim Na Bukhari
Inasema kwamba
“kuna Baraka Katika Nywele za mbele ya kichwa cha Mbunyu”
Na ndiyo sehemu ya Ubongo inayojulikana kama Frontal Celebral.
Sasa Mtume alisoma wapi Sayansi hii ya leo inayohitaji Mashine kubwa kubwa za kisasa za kusomea Ubongo. Hii Inathibitisha Kwamba Kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu na Mtume alikuwa Mjumbe tu. Mtume (Sala na Amani za Mwenyeezi mungu Zimfikie) alifanya kazi yake aliyopewa ya kifikisha Ujumbe. Na Huu sio Muujiza Mdogo. Allahu Akbar.

Sehemu za Ubongo Tulizozitaja katika Sherehe. Forebrain (Cerebrum)ndiyo tuliyoifanyia Utafiti..

Sawa Na Picha Ya Kwanza. Mgawanyiko wa Lobes. Utafiti wetu ulikuwa katika Frontal Lobes

Picha nyingine ya Lobes
MAAJABU YA MIKOJO YA NGAMIA NA MENGINEYO-MUUJIZA WA HADITHI ZA MTUME NA KURUANI TUKUFU
DAWA KUTOKANA NA MWILI WA NGAMIA
Hadithi inayohusiana na Faida za Ngamia
Hadithi ilikusanywa na Imam Ahmad an-Nasa’i (rahimahullah) katika vitabu vyake vinavyojulikana kama Sunan an-Nasa’i Ni Hadithi Sahihi na sikuitaja yote bali kipande tu kitakachohusu Muujiza Wa Kisanayansi ambao tutazungumzia leo.
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَدِمَ أَعْرَابٌ مِنْ عُرَيْنَةَ إِلَى نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَسْلَمُوا فَاجْتَوَوُا الْمَدِينَةَ حَتَّى اصْفَرَّتْ أَلْوَانُهُمْ وَعَظُمَتْ بُطُونُهُمْ فَبَعَثَ بِهِمْ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِلَى لِقَاحٍ لَهُ فَأَمَرَهُمْ أَنْ يَشْرَبُوا مِنْ أَلْبَانِهَا وَأَبْوَالِهَا حَتَّى صَحُّوا
Tafsiri Ya Hadithi
Anas Ibn Malik alisema “Baadhi ya Waarabu kutoka Uraynah (Jina la sehemu au mji au kijiji) Walikuja Kwa Mtume (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) na wakasilimu.(Wakaingia katika dini ya Uislamu). Lakini hali ya hewa ya mji wa Madinnah haikuwafaa; Ngozi zao zikabadilika rangi na kuwa manjano na tumbo zao zikavimba. Mtume Wa Mwenyeezi Mungu (Mohamed) akawapeleka katika sehemu ya ngamia zake ambao walikuwa ngamia wa maziwa na akawaambia wanywe maziwa na mikojo ya ngamia hao mpaka maradhi waliyokuwa nayo yaliwaondoka (yaani wakapona)
Sayansi Kuhusiana Na Faida Za Madawa Mbali Mbali Kutokana Na Ngamia
Katika Hadithi hapa juu tunasoma kwamba Maziwa na Mikojo ya Ngamia ilichangia katika kuwaponyesha hao Waarabu wa wakati huo. La kushangaza katika Hadithi hii ni Sayansi za leo zimefanya utafiti na kutueleza kwamba Maziwa na Mikojo ya Ngamia ina Faida kubwa, kwani Wataalamu wamegundua Njia mbalimbali za kutengeneza Madawa kutokana na Maziwa na Mikojo Ya Ngamia. Allahu Akbar.
Angalia Muujiza Mwingine wa Kushangaza. Sasa Mtume alisoma wapi Elimu hii.WHO (World Health Organisation) wametoa usia wa kutokunywa Mikojo ya Ngami hovyo hovyo kwani huweza kusababisha Maradhi mengineyo kama vile Respiratory Syndrome (MRS) Wataalamu wanatushauri baada ya utafiti mbalimbali kwamba lazima dawa hiyo itengenezwe chini ya uangalizi wa wataalamu wa Madawa Na Katika Madawa yaliyotengenezwa kutokana na Mikojo ya ngamia ni HandCream (Mafuta ya Mikono). Na Dawa za kuponyesha Maini yaliyoharibika kwa ajili ya Ulevi na Dawa Nyinginezo kufuatana na Magonjwa mbalimbali na huenda kuna dawa nyinginezo bado kugunduliwa.
Wataalmu wanasema:
(Camel urine has an unusual and unique biochemical composition that contributes to medicinal values. The chemical composition of camel urine showed the presence of purine bases, hypoxanthine, sodium, potassium, creatinine, urea, uric acid, and phosphates. The nano-particles in the camel’s urine can be used to fight cancer. Camel urine has antimicrobial activity against pathogenic bacteria. Its chemical and organic constituents have also inhibitory properties against fungal growth, human platelets, and parasitic diseases mainly fasciollosis in calves. The healthy status of the liver can be restored through ingestion of diet and minerals in camel urine.)
Katika Faida za Ngamia ni Nyama na Maziwa. Soma Faida hizi hapa chini.
(Camel milk and meat are good source of nutrients for the peoples living especially in the arid and urban areas. Camel milk and meat are unique from other ruminant’s milk and meat in terms of composition as well as claimed health effects. Camel milk has low cholesterol, high minerals (sodium, potassium, iron, copper, zinc and magnesium) and high vitamin C when compared with other ruminant milk. Camel milk contains various fatty acids, enzymes and protective proteins. Camel milk has potential therapeutic effects, such as antibacterial, antiviral, antidiabetic, anti-ageing and anticarcinogenic. The medicinal properties of camel milk can be attributed to the presence of protective proteins, which may possibly play a pivotal role for the enhancement of immune defence mechanism. Not only camel milk, but also camel meat in general, is considered a functional food for cures and remedy for many ailments such as seasonal fever, sciatica, shoulder pain, asthma, removing freckles and for improved performance, in many cultures around the world. Therefore, it is important to illustrate the overview of compositions and medicinal values of camel milk and meat)
Sayansi za Leo zimethibitisha Faida za Matibabu kutokana na Nyama na Maziwa Ya Ngamia. Kilicho muhimu ni Kutafuta njia za Kuchambua Dawa mbali mbali kutoka katika Mikojo ya Ngamia na siyo kunya Mikojo kienyeji kwani kuna hatari zake.
(The biochemical composition of camel urine can be scientifically extracted and formulated as a therapy rather than drinking raw urine)
Historia inasema kwamba Enzi hizo za Mtume Waarabu walikuwa wakitumia Maziwa na Mikojo ya Ngamia kwa Madawa.
Ngamia ana Faida nyinginezo kama vile
-Nwele za Ngamia
(Camel wool is a type of fabric derived from the coats of camels. This type of fabric is more commonly known as camel hair, and it is usually derived from a camel subspecies known as the Bactrian camel)
-Katika Usafiri wa watu na mizigo pia.
(As well as carrying people, camels are used to carry goods. While motorised transportation has, to a certain extent, reduced the role of camels in transportation, they are still one of the best ways for people to move items across desert areas. A camel can walk across terrain that vehicles cannot handle)
Kabla Sijamaliza ningependelea kusema kwamba Kuna mengi na yasiyo na mwisho kuhusiana na Ngamia.
Itahitajia Vitabu na Vitabu ili kuelezea Ngamia. Na hatuwezi kuelezea yote katika Website au sehemu ndogo ya Website kama hii. Bali tumegusia tu Muujiza wa Utibabu kutokana na Mikojo, Nyama na Maziwa Ya Ngamia.
Hii Inasadikisha Maneno ya Mweyeezi Mungu aliposema katika Kuruani Tukufu kwamba Tumsome Ngamia Vizuri ili tupate kumwogopa aliyemuumba.
Leo hii tunasoma habari ndogo sana inayohusiana na Mikojo tu na Inatushangaza.
Yako mengi zaidi ya kushangaza kuhusiana na Mnyama huyu laiti tungejua Yote? Allahu Akbar. Allahu Akbar.
Na Ndiyo maana Mwenyeezi Mungu alisema katika Kuruani Tukufu Sura Namba 88 Aya Namba 17
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ ڪَيۡفَ خُلِقَتۡ (١٧)
Tafsiri
Je Hawamuangalii Ngamia Namna
Tulivyomuumba?
MARADHI YA NAFSI NA MATIBABU KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU
Ian Osborn ni Dakitari Wa Magonjwa Ya Akili ambaye ni mtaalamu katika utibabu wa maradhi yanayojulikana kama (OCD) obsessive-compulsive disorder. Ugonjwa huu una alama zake zifuatazo:
1/Shida na Mvurugo bila Utulivu Unaofanyika Ndani Ya Nafsi Ya Binaadamu wa kusababisha Mtu Kufanya Mabaya na Kujidhuru au Kudhuru Wengine. 2/Kuilazimisha nafsi itende Madhambi yenye uhusiano na Uasherati wa aina yeyote ile
3/Kuilazimisha nafsi kuchukia Dini. Kutukana Dini na Mungu.
Kwa Kifupi Maisha ya Dakitari Ian Osborne
(Ian Osborn is a psychiatrist who specializes in the treatment of obsessive-compulsive disorder. He started as a physician at Centre Community Hospital in State College, Pennsylvania, United States in 1980. He has taught psychiatry as a faculty member at Penn State University.Ian Osborn is an American board certified psychiatrist who has specialized in the treatment of OCD for more than 20 years. He is also the author of two books on the subject: “Tormenting Thoughts and Secret Rituals”)
Katika Vitabu vyake Maarufu kuna ambacho kinajulikana kwa jina “Tormenting Thoughts and Secret Rituals” ambacho kinahusu Utafiti wetu wa leo.Inashangaza sana kwani maradhi aliyoyataja katika kitabu chake yanalingana na maradhi yanayosababishwa na Shetani kama tutakavyoona katika Kuruani Tukufu.
Anasema katika kitabu chake kwamba hivi sasa tunaweza kuuelewa Ugonjwa huu angalau kidogo kuhusu Maradhi haya Ya OCD kwa kuchunguza mishipa ya Fahamu (kufuatana na Elimu ya Neurobioloy) lakini bado kueleweka kwa ukamilifu. Na anatoa ushaidi wa Mtaalamu Mwingine Maarufu wa Magonjwa ya Nafsi na Vichaa (Psychiatrist) anayejulikana kama Sir Aubrey Lewis
Dakitari (Aubrey Lewis) anashangaa sana kuhusu maradhi ya OCD na anasema kwamba maradhi haya yanachanganya Huruma na Ukatili, Fikira Nzuri na Mbaya, Woga na Matamanio, na Matatizo Mengineyo mbalimbali ambayo hayafahamiki.
Dakitari Ian Osborne anaendelea Kukiri katika kitabu chake kwamba yeye mwenyewe aliteseka sana na ugonjwa huu alipokuwa katika Medical Training (Mafunzo ya Utibabu).
Katika Mlango wa Kwanza wa Kitabu chake anazungumzia Vipengele Vya Maradhi Haya vilivyoandaliwa hapo awali na Dakitari Tuliyemtaja hapa Juu ambaye alikuwa maarufu sana katika karne ya Ishirini alijulikana kwa jina Sir Aubrey Lewis.
VIPENGELE VYA MARADHI YA NAFSI (Filth, Harm, Lust and Blasphemy)
1/Filth na Lust zina maana ya Maasi / Uchafu / Uasherati
2/Harm lina maana ya Dhara au Kudhuru. Yaani Kujidhuru au kudhuru wengineo
3/Blasphemy ni kutukana Dini au Kutumia Maneno yeyote ambayo yanamtukana Mwenyeezi Mungu.
Muujiza wa Kuruani ni kwamba Leo hii wataalamu wanasoma haya lakini
-katika Kuruani kuna Aya ambazo zinazungumzia habari hizi kwa ukamilifu na pia kutufundisha namna ya kujiepusha na Maradhi haya kwa vizuri zaidi kuliko sayansi.
-Wataalamu wa Kisayansi bado hawajajua sababu ya maradhi haya na kwa hiyo hawajui namna ya kuutibu ugonjwa huu kikamilifu. Wanajitahidi kwa Njia mbalimbali za matibabu na kuna madawa lakini hayaondoi maradhi haya kikamilifu.
-Kuruani inatuelezea sababu ya maradhi haya na kutuelezea namna ya kujikinga na pia kutibu. -Wana Sayansi wanatumia madawa mbali mbali ya kisasa na Pia kuna aina mbali mbali za Matibabu ili kutibu ugonjwa huu. Madawa na mengineyo yanasadia kidogo lakini madawa haya hayana Uwezo mkubwa.
-Kuruani imeelezea dawa hii kama utakavyoona katika Aya hapa chini.
AYA ZA MAFUNDISHO KUTOKA KWA MWENYEEZI MUNGU ILI KUTULINDA NA NJAMA ZA SHETANI
Matibabu ya Kuruani Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu na njama za Sheitani zinafichuliwa na Mwenyeezi Mungu ili tuwe macho
Bakarah Namba 2 Aya Namba 168-169
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُواْ مِمَّا فِى ٱلۡأَرۡضِ حَلَـٰلاً۬ طَيِّبً۬ا وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ إِنَّهُ ۥ لَكُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ (١٦٨) إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ وَٱلۡفَحۡشَآءِ وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ (١٦٩)
TAFSIRI
168.Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shetani (yale anayokuamrisheni). Bila shaka yeye kwenu ni adui dhahiri.
I69.Yeye anakuamrisheni mfanye mabaya (yenye dhara) na (kufanya) mambo mabaya na machafu, na mumsingizie Mwenyezi Mungu msiyoyajua
Mlinganisho wa Maneno Ya Mtaalamu wa Maradhi Ya Nafsi na Kuruani katika Surah ya Al-Bakarah Namba 2 Aya Namba 169
1/Sayansi inatumia Maneno Filth na Lust = Kuruani Inasema وَٱلۡفَحۡشَآءِ
2/Sayansi Inatumia Neno Harm= Kuruani Inasema إِنَّمَا يَأۡمُرُكُم بِٱلسُّوٓءِ
3/Sayansi Inatumia Neno Blasphemy=Kuruani Inasema وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Katika Aya hizi mbili tunapewa dawa ya maradhi haya ya Nafsi yaani tule vya halali na tujiepushe na kufuata njia ya Shetani.
Israa Namba 17 Aya Namba 64
وَٱسۡتَفۡزِزۡ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتَ مِنۡہُم بِصَوۡتِكَ وَأَجۡلِبۡ عَلَيۡہِم بِخَيۡلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكۡهُمۡ فِى ٱلۡأَمۡوَٲلِ وَٱلۡأَوۡلَـٰدِ وَعِدۡهُمۡۚ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ إِلَّا غُرُورًا (٦٤)
TAFSIRI
64.”Na wavute uwawezao ·miongoni mwao kwa sauti yako, na uwakusanyie (jeshi lako la) wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali (yao) na watoto (wao), na waahidi (ahadi za uwongo). Lakini
Shetani hawapi waadi ila wa udanganyifu (kwani hana lake jambo). Shetani Anatumia Ujanja mbalimbali ili kutupoteza. Katika Hila Zake anaiga sauti zetu na kunong’ona ndani ya nafsi zetu bila sisi kujijua. Utafikiri ni sauti yako lakini anatumia sauti yako mwenyewe kukuhimiza utende vitendo kinyume na maamrisho ya Mweyeezi Mungu. Na kama Tunavyoelewa katika Sayansi kwamba tunapozungumza Sauti inasababisha mawimbi ya hewa (kama vile mawimbi ya Baharini) ambayo yanabeba Mazungumzo yetu kwa msikilizaji. Na
Shetani anapokungonona anasababisha Mawimbi ya hewa ambayo yanagonga sehemu za Ubongo. Sehemu Hizo zinawasiliana na viungo vya Miili yetu kwa kupitia Mishipa ya Fahamu na kuvihimiza vitende vitendo vya kishetani.
Mwenyeezi Mungu anasema Katika Sura Ya Al-Falaq Namba 113 Aya Namba 4
وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤)
Baadhi ya Tafsiri zinasema wenye kupulizia ni wachawi na tafsiri nyinginezo zinasema kuhusu wenye kupulizia tu lakini hazisemi ni nani wenye kupulizia na kuna Mtaalamu Muislamu ambaye anatupa Fikira Mpya kuhusu Tafsiri Ya Aya Hii kwamba Ni Sauti / Mazungumzo au Mapulizio ya Shetani katika Mafundo (Concentrated Cell Bodies) ya Ubongo Kwani Mafundo Ya Ubongo ndiyo yenye Kuhukumu Viungo Vya Mwili. Na Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi Tafsiri Ipi iliyo Sahihi. Ukichunguza utaona Zote zineleta maana Kwani kila Moja ina sababu zenye kuridhisha. Kwa Maoni Yangu Tafsiri zote mbili ni sahihi.
Wenye kunong’ona au kupulizia wanafanya haya kwa njia ya kudhuru na kwa hiyo Kama ni Uchawi ni sawa na kama ni Mashetani pia ni sawa. Kwa hiyo neno ِ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ ni neno limekusanya vikundi vyote hivi. Allahu Akbar.
Ewe Binaadamu Kuwa macho. Jilinge na Mawinbi ya Sauti za Shari kwa Mumcha Mwenyeezi Mungu. Muombe Akulinde.
Wataalamu wa Elimu ya Ubongo walifanya Utafiti na wakagundua kwamba Hata unapokuwa usingizini Ubongo unafanya kazi katika zile sehemu za Mazungumzo sasa haya mawasiliano yanatoka wapi? Basi kaa ukielewa kwamba Huenda ni Minon’gono ya Sheitan. (Devil’s Whispers) Wewe hujijui lakini anazungumza kwa lugha yako hali ukidhani ni fikra zako kumbe siyo. Allahu Akbar
Al-Araf Namba 7 Aya Namba 200-201
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَـٰنِ نَزۡغٌ۬ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُ ۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ (٢٠٠) إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّہُمۡ طَـٰٓٮِٕفٌ۬ مِّنَ ٱلشَّيۡطَـٰنِ تَذَڪَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ (٢٠١)
TAFSIRI
200-Na kama wasiwasi wa Shetani ukikusumbua (kuona kwa nini nisiwajibu masaflhi hawa) basI (sema Audhu Billahi) jikinge kwa Mwenyezi Mungu (na kuchezewa na Shetani, ukaacha wasia wake Mwenyezi Mungu): Bila shaka Yeye ndiye asikiaye na ajuaye.
201-Wale wanaomuogopa (Mwenyezi Mungu)zinapowagusa pepesi za Shetani (wakaasi; kama hivyo kujibizana na masafihi) mara hukumbuka, tahamaki wamekwishaona njia.
Tunapewa dawa ya kinga tunapojikuta tunaanza kupotea. Tukihisi tu tunaanza kwenda mrama basi Tumuombe Mweyeezi Mungu atukinge na shari za Shetani
MWENYEEZI MUNGU ANATUPA NASIHA TUWE MACHO
Al-Imran Sura Namba 3 Aya Namba 175
إِنَّمَا ذَٲلِكُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ يُخَوِّفُ أَوۡلِيَآءَهُ ۥ فَلَا تَخَافُوهُمۡ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ (١٧٥)
TAFSIRI
175-Huyo (aliyekutieni khofu ile) ni Shetani ambaye anakuogopesheni marafiki zake, basi msiwaogope; bali niogopeni Mimi mkiwa Waislamu (kweli).
Mwenyeezi Mungu anatuambia Tusimwogope Shetani na Marafiki zake bali Tumwogope yeye mwenyewe aliyetuumba
Sura Ya Al-Bakarah Namba 2 Aya Namba 268
ٱلشَّيۡطَـٰنُ يَعِدُكُمُ ٱلۡفَقۡرَ وَيَأۡمُرُڪُم بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ وَٱللَّهُ يَعِدُكُم مَّغۡفِرَةً۬ مِّنۡهُ وَفَضۡلاً۬ۗ وَٱللَّهُ وَٲسِعٌ عَلِيمٌ۬ (٢٦٨)
TAFSIRI
268.Shetani anakuogopesheni ufukara na anakuamrisheni ubakhili; na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha utokao kwake na ihsani (kubwa pindi mkitoa); na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa mkubwa na Mwenye kujua.
Unapopata Shida yeyote basi Shetani anakuja kukudangan’ya kwa hila zake atakuahidi kukusaidia lakini uongo mtupu.
Kwa mfano huna pesa na una deni basi Shetani atakunong’ona ndani ya nafsi yako udhulumu au uibe ili ulipe deni lako au uondoe shida zako lakiki uongo mtupu. Shetani hatakusaidia chochote bali atakuongoza uwe Fakiri na kutenda yasio mazuri. Mche Mungu tu peke yake na umuombe usiogope tatizo lolote na wala usikate tamaa bali fanya subira. Na hivyo hivyo unapokuwa na Mali. Shetani atakudanganya ufanye Ubahili kwa kukutishia kwamba ukitoa utakuwa Fakiri au utapata Matatizo.
Mshangao ni kwamba Sayansi Bado ipo Nyuma kwani mpaka sasa Imefeli kutambua chanzo cha Maradhi haya. Na maadamu asili ya maradhi haijulikani inakuwa siyo rahisi kuutibu. Lakini Alhamdulilahi Kuruani Imetangulia. Imeelezea Asili ya Ugonjwa huu ni Dhara inayotokana na Shetani na Pia imetupa Madawa ya kujikinga nayo na pia kututibu. Na Madawa ya Kuruani hayataki pesa. Madawa ya Bure. Alahu Akbar.
Aya za Kuruani Hapa Juu zinafafanua Njia mbali mbali za kijikinga na Shetani na Dhara Yake. Alhamdulilah. Waganga wengi ni Watapeli kwani lengo lao ni kutafuta Pesa .Mwenyeezi Mungu anasema Umuombe tu yeye akukinge na Shari za Shetani. Aya hizi zinaeleweka na wala usidanganyike. Kwenda Hospitali ni Vizuri sana lakini pia tumuombe Mungu yaani tufuate Dawa zote Mbili na Inshaallah tutapona.
La kushangaza pia ni kwamba hawa Madakitari Wataalamu Maarufu walifanya utafiti na hawakuwa Waislamu. Lakini maajabu ni kwamba Matatizo Waliyotatua Ni yale yale yaliyotatuliwa na Kuruani Tukufu na hata Misamiati waliyochagua inalingana kimiujiza sana. Alhamdulilah. Allahu Akbar.

Maana Ya Maradhi ya OCD na Ajabu Ni kwamba Kila Neno au Ibara za Maana Hii zinalingana na Aya za Kuruani utafikiri Wanasayansi walikuwa wanaijua Kuruani. Allahu Akbar

MIshipa Ya Fahamu. Viungio Vya MIshipa Hii ina Mafundo. Tumezungumzia Tafsiri ya Aya Ya Kuruani kutoka Katika Sura Ya Alfalaq.Huenda Aya وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) Hii ina maana ya Haya Mafundo ambayo Shetani Hunongo’na kututia wasiwasi . Mungu anajua zaidi. Wafasiri wengine wanasema Aya hii inahusiana na Wachawi kwani Mtume alifanyiwa Uchawi Pia. Kwa Kweli Mungu anajua Zaidi.

Kutoka Katika Kitabu Cha Ian Osborne.( “Tormenting Thoughts and Secret Rituals”) Hapa anasema kwamba Ugonjwa Ni “MYSTERIOUS” yaani Haujulikani na kwa kweli bado kujulikana vizuri. Maneno haya Hapa Juu ni yale yale yaliyopo katrika Kuruani Tukufu.Allahu Akbar.
MUUJIZA WA MANYANI KATIKA KURUANI
Katika Kuruani Yote Kuna Aya 3 pekee ambazo zinataja Jina la Nyani au Kima (Monkey)
Sura Namba 2, Sura Ya Al-Baqara Aya Namba 65
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِى ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ (٦٥)
TAFSIRI
65.Na kwa yakini mmekwisha kujua (khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya kuihishimu) Jumaamosi. Basi Tukawaambia: “Kuweni manyani wadhalilifu.”
Sura Namba 5 Sura Ya Al-Maida Aya Namba 60
قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ۬ مِّن ذَٲلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡہُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ شَرٌّ۬ مَّكَانً۬ا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ (٦٠)
TAFSIRI
6o.Sema:”Je! Nikwambieni yule ambaye ni mwenye malipo mabaya zaidi kuliko haya mbele ya Mwenyezi Mungu? Ni ambao Mwenyezi Mungu amewalani na kuwakasirikia na kuwafanya wengine kuwa nyani na nguruwe, na wakamwabudu shetani. Hao ndio wenye mahali pabaya na wapotofu (wapotevu) sana (ambao wako mbali) na njia iliyo sawa.”
Sura Namba 7 Sura Ya Al-Araf Aya Namba 166
فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُہُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ (١٦٦)
TAFSIRI
166.Na walipotakabari wasiache waliyokatazwa, tuliwaambia: “Kuweni manyani madhalilifu.”
SHEREHE YA AYA HIZI TATU NA MIUJIZA MBALI MBALI
MUUJIZA WA KWANZA
Katika Sura Namba 2 Sura Ya Al-Baqara Aya Namba 65
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِى ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ (٦٥)
Ukihesabu Herufi Kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka Neno قِرَدَةً utapata Jumla ya herufi ni 48 na hii inaashiria set mbili za Chromosomes zilizoungana baina ya mbegu za baba na mama. Katika Genetics inajulikana kama Diploid yaani ni Muunganisho wa Chromosomes 24 za mama na 24 za baba na jumla ni Chromosomes 48.
MUUJIZA WA PILI
Na Ukihesabu Kutumika na Kukariri kwa Herufi za neno القِرَدَةً (Hapa Alif na Lam ni Definite Articles) katika Aya Hii utapata kama ifuatavyo; Herufi Alif mara 7 + Lam mara 6 + Qaf mara 3 + Ra mara 1 + Dal mara 3 + Ta mara 4 Jumla ni herufi 24 ambayo katika Genetics inajulikana kama Haploid, Ni Set moja ya Upande mmoja wa baba au mama. Herufi 24 hapa inaashiria Haploid yaani Mbegu za Baba peke yake au Mama peke yake.
————————–
MUUJIZA WA TATU
Sura Namba 2, Sura Ya Al-Baqara Aya Namba 65
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعۡتَدَوۡاْ مِنكُمۡ فِى ٱلسَّبۡتِ فَقُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ (٦٥)
Sura Namba 5 Sura Ya Al-Maida Aya Namba 60
قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ۬ مِّن ذَٲلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡہُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ شَرٌّ۬ مَّكَانً۬ا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ (٦٠)
Sura Namba 7 Sura Ya Al-Araf Aya Namba 166
فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُہُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ (١٦٦
(1)Sasa tukichunguza Kutumika na Kukariri kwa Herufi za Jina قِرَدَةً (yaani Bila ya Alif na Lam Mwanzoni) katika Aya Hizi 3 Hapa juu utapata kama ifuatavyo: Herufi Qaf mara 7 + Ra mara 6 + Dal mara 7 + Ta mara 4=24 Tunapata Tena namba 24 ambayo ni Haploid Chromosomes za Nyani (Monkey)
(2)Na tukichunguza Herufi za Jina القِرَدَةً (kwa kuongeza Alif na Lam Mwanzoni)katika Aya 3 tulizizitaja hapa juu utapata kama ifuatavyo: Herufi Alif mara 22 + Lam mara 26 + Qaf mara 7 + Ra mara 6 + Dal mara 7 + Ta mara 4=72 Na namba hii 72 Ni sawa na 24 X 3 Yaani Aya hizi Tatu Kumetajika Jina قِرَدَةً jumla mara 3. La kushangaza ni kwamba Kila Nyani (Monkey) anayo Mbegu za Chromosomes 24 na kwa vile wapo nyani watatu basi 24 X 3=71. Hapa 24 ni Haploid Chromosomes
(3)Sasa tukihesabu Maneno Kuanzia Neno la kwanza, Mwanzo wa Aya Ya kwanza namba 65 Al-Bakarah , Kisha Aya Ya Pili namba 60 Sura Namba 5 na Aya Ya Tatu Namba 177 Sura Ya Al-Araf namba 7 mpaka Jina قِرَدَةً Utapata Jumla ya Maneno Jumla ni 48 ambayo inalingana na Chromosomes za Monkey (Nyani) Diploid Chromosomes.
MUUJIZA WA NNE
Na ukihesabu Herufi TA kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Maidah mpaka Herufi Ta ya neno قِرَدَةً katika Aya Hii Namba 60 utapata Jumla ya Herufi “Ta” ni 48.Na huenda kwa vile Herufi Hii “Ta” Katika Grammar ina maana ya Wingi (قِرَدَةً Neno Hili ni Plural ya neno قِرَدَ ) kwa hiyo katika Genetics inaashiria Chromosomes 48 ambazo asili yake ni nyani mmoja na baadaye kuzalisha wengineo kwa njia ya Chromosomes. Kama tunavyosoma kwamba asili ya Viumbe wote ni Chromosomes.
MUUJIZA WA TANO
Na ukihesabu Herufi Kuanzia Mwisho wa Aya Namba 60 Sura Ya Maidah Kwa kurudi Nyuma mpaka Herufi Ta utapata jumla ya herufi 48
قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ۬ مِّن ذَٲلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡہُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ شَرٌّ۬ مَّكَانً۬ا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ (٦٠)
Jambo la kushangaza ni kwamba Chromosomes ziligunduliwa mwaka 1882 na Mwana Sayansi aliyekuwa Mjerumani anayejulikana kwa Jina kama Walther Flemming. (The Science Channel named Flemming’s discovery of mitosis and chromosomes as one of the 100 most important scientific discoveries of all time, and one of the 10 most important discoveries in cell biology.Flemming’s name is honoured by a medal awarded by the German Society for Cell Biology (Deutsche Gesellschaft für Zellbiologie).
Ugunduzi huu katika karne ya 19 unatuthibitishia kwamba Kuruani ni Maneno Ya Mwenyeezi Mungu kwani Kuruani ilishuka Kwa Mtume (Sana na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) katika karne ya 7 na kutajika kwa Habari za Chromosomes katika Kitabu cha Kuruani ni Muujiza miongoni mwa Miujiza Mikubwa. Allahu Akbar.
Angalia Picha hapa chini ya Utafiti katika Mtandao kuhusiana na Chromosomes 48 za Nyani (Monkeys au Speshi- Species-Nyinginezo katika Jamii Ya Manyani)

Chromosomes 48 Za Nyani kutoka katika Mtandao (Internet) Unaweza Kutafuta Menyewe kwa kutumia Vyombo vya utafiti kama vile nilivyofanya. Nimetumia Google Search Engine.