SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Shaaban 2022

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MWEZI WA SHAABAN MWAKA 2022

Baada ya siku chache tutaingia katika Mwezi Wa Ramadhan. Mungu akipenda itakuwa Mwanzoni mwa mwezi ujao. Naomba Mwenyeezi Mungu atupe uhai Mwezi Huu utukute katika hali ya Uzima na afya nzuri. Pia Namuomba Mwenyeezi Mungu aniwezeshe Kuwaletea Habari mbalimbali zinazohusu Kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad ﷺ

Je Kuna Mazungumzo mengine yaliyo bora kuliko Maneno Ya Muumbaji?

Kwa kweli Hakuna.

Nia yangu kila siku niandike  habari moja na itakuwa fupi ili nisiwachokeshe wasomaji. Kwa hiyo Mlango huu utakuwa na Habari iliyokusanya masiku yaliyobaki katika Mwezi wa Shaaban.

11/March/2022 = Islamic Calendar 08/Shaaban/1443

MUUJIZA WA JUMLA YA AYA ZA KURUANI NA JUMLA YA SURA ZA KURUANI AMBAO UKIJUMLISHA UNAPATA KIPINDI CHA WAHYI (REVELATION).

Ningependelea Kufungua Mlango Huu wa Mwezi Wa Shaaban na Muujiza Ufuatao

Kuruani Ina Sura  114

Kuruani Ina Aya 6236  (Kwa kutohesabu Aya Ya Basmallah katika Sura zote 113 isipokuwa Sura Ya Al-Fatiha.

Angalia Muujiza Ufuatao ambao Unashangaza sana. 

Hebu tupange hizi Namba Mbili za Idadi ya Sura Na Aya kisha Tujumlishe kama ifuatavyo:

114 (Idadi Ya Sura)  6236  (Idadi Za Aya)

1 + 1 + 4 + 6 + 2 + 3 + 6=23

Je unaona Muujiza wa kushagaza. Baada ya Kujumlisha Idadi Ya Sura Na Aya  tunapata Miaka  23 ya Wahyi.

Kuruani ilishuka Kwa Mtume Mohamad ﷺ alipokuwa na Umri wa miaka 40 na akafariki alipokuwa na umri wa miaka 63. Kwa hiyo jumla ya Muda aliokuwa akiletewa Wahyi na Jibril ni miaka 23!!!!!

Je unaona Miujiza isiyo na Mwisho. Allahu Akbar Mola anajua zaidi iwapo tumesibu.

12/March/2022 = Islamic Calendar 09/Shaaban/1443

MUUJIZA WA HERUFI ZA MANENO YALIYOTUMIKA KATIKA MAKUTANO YA KWANZA BAINA YA MTUME NA MALAIKA JIBRIL

Ili kuelezea Muujiza huu wa Mazungumzo baina ya Mtume na Malaika Jibril ningependelea Kuwaletea Hadithi kamili Inayohusu habari hizi.

Hadithi ifuatayo kutoka katika Sahih Al-Bukhari inazungumzia Kuhusu  Habari za Wahyi  au Revelation, Kwa Mtume Mohamad ﷺ Mara ya kwanza alipojiwa na Malaika Jibril katika Pango alilokuwa amejitenga peke yake kwa ajili ya ibada. Alifanya haya kabla ya Uislamu, yaani kabla Ya kushushiwa Aya Za Kuruani. Hivi ndivyo Mwenyeezi Mungu alivyomjaalia kwa kumpa hamu ya  Kumtukuza Mwenyeezi Mungu kabla ya  Wahyi (Revelation).

Sahih al-Bukhari Book 1, Hadith 3

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ ـ وَهُوَ التَّعَبُّدُ ـ اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ الْعَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ، فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الْحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ الْمَلَكُ فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قَالَ ‏”‏ مَا أَنَا بِقَارِئٍ ‏”‏‏.‏ قَالَ ‏”‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ فَقُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ ‏{‏اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ‏}‏ ‏”‏‏.‏ فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رضى الله عنها فَقَالَ ‏”‏ زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي ‏”‏‏.‏ فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الْخَبَرَ ‏”‏ لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي ‏”‏‏.‏ فَقَالَتْ خَدِيجَةُ كَلاَّ وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الْكَلَّ، وَتَكْسِبُ الْمَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الْحَقِّ‏.‏ فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ ـ وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الْكِتَابَ الْعِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالْعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ ـ فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ يَا ابْنَ عَمِّ اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ يَا ابْنَ أَخِي مَاذَا تَرَى فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَبَرَ مَا رَأَى‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى صلى الله عليه وسلم يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏”‏ أَوَمُخْرِجِيَّ هُمْ ‏”‏‏.‏ قَالَ نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلاَّ عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا‏.‏ ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ وَفَتَرَ الْوَحْىُ‏.‏

TAFSIRI  KWA LUGHA YA KIINGEREZA

Narrated ‘Aisha (the mother of the faithful believers): The commencement of the Divine Inspiration to Allah’s Messenger (ﷺ) was in the form of good dreams which came true like bright daylight, and then the love of seclusion was bestowed upon him. He used to go in seclusion in the cave of Hira where he used to worship (Allah alone) continuously for many days before his desire to see his family. He used to take with him the journey food for the stay and then come back to (his wife) Khadija to take his food likewise again till suddenly the Truth descended upon him while he was in the cave of Hira. The angel came to him and asked him to read (By Saying “Read“)  The Prophet (ﷺ) replied, “I do not know how to read.” The Prophet (ﷺ) added, “The angel caught me (forcefully) and pressed me so hard that I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read and I replied, ‘I do not know how to read.’ Thereupon he caught me again and pressed me a second time till I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read but again I replied, ‘I do not know how to read (or what shall I read)?’ Thereupon he caught me for the third time and pressed me, and then released me and said, ‘Read in the name of your Lord, who has created (all that exists), created man from a clot. Read! And your Lord is the Most Generous.” (96.1, 96.2, 96.3) Then Allah’s Messenger (ﷺ) returned with the Inspiration and with his heart beating severely. Then he went to Khadija bint Khuwailid and said, “Cover me! Cover me!” They covered him till his fear was over and after that he told her everything that had happened and said, “I fear that something may happen to me.” Khadija replied, “Never! By Allah, Allah will never disgrace you. You keep good relations with your kith and kin, help the poor and the destitute, serve your guests generously and assist the deserving calamity-afflicted ones.” Khadija then accompanied him to her cousin Waraqa bin Naufal bin Asad bin ‘Abdul ‘Uzza, who, during the pre-Islamic Period became a Christian and used to write the writing with Hebrew letters. He would write from the Gospel in Hebrew as much as Allah wished him to write. He was an old man and had lost his eyesight. Khadija said to Waraqa, “Listen to the story of your nephew, O my cousin!” Waraqa asked, “O my nephew! What have you seen?” Allah’s Messenger (ﷺ) described whatever he had seen. Waraqa said, “This is the same one who keeps the secrets (angel Gabriel) whom Allah had sent to Moses. I wish I were young and could live up to the time when your people would turn you out.” Allah’s Messenger (ﷺ) asked, “Will they drive me out?” Waraqa replied in the affirmative and said, “Anyone (man) who came with something similar to what you have brought was treated with hostility; and if I should remain alive till the day when you will be turned out then I would support you strongly.” But after a few days Waraqa died and the Divine Inspiration was also paused for a while.

Mara ya Kwanza Mtume ﷺ alipokutana na Jibril katika pango la HIRAA huko Mecca akaambiwa  “soma” na katika hali ya kutetemeka na khofu akajibu “Mimi sijui kusoma”. Hadithi nitaifasiri kwa kiswahili Mwenyeezi Mungu akipenda mara tu nitakapopata nafasi.

MUUJIZA 

اقْرَأْ    (Neno La Malaika Jibril kumwambia Mtume Mohamad  yaani “SOMA”)

‏ مَا أَنَا بِقَارِئٍ(Ibara Aliyojibu Mtume Mohamad Kumjibu Malaika Jibril. “MIMI SIJUI KUSOMA”  au “MIMI SIYO MSOMI”)

Herufi za Neno  اقْرَأْ  na Ibara مَا أَنَا بِقَارِئٍ  Ukizigeuza katika Thamani za Namba kufuatana na Hesabu za Mpangilio wa Herufi za Kiarabu ambazo ni 28. (Kwa mfano Herufi Alif Thamani yake ni Moja. Herufi Ba ni Mbili mpaka Mwisho Yaani herufi  Ya ni ya  28). Utapata Namba Zifuatazo:

اقْرَأْ= 1 +19 + 20 + 1=41

مَا أَنَا بِقَارِئٍ=13 + 1 + 1 + 14+ 1 + 2 + 19+1 + 20 + 1=73

اقْرَأْ-Jumla ya Thamani Za Herufi Za Neno IKRAA ni 41

مَا أَنَا بِقَارِئٍ-Jumla Ya Herufi za Ibara “MA ANA BIQARII” ni 73

Ukijumlisha Namba hizi Mbili  73 + 41=114

Unaona Maajabu. Tunapata  idadi ya Sura Za Kuruani. Mazungumzo ya kwanza baina Ya Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa Mtume wake yalikuwa Baina ya neno  “SOMA”  na Ibara  “MIMI SIJUI KUSOMA” au “MIMI SIYO MSOMI”  maneno haya tumeyafasiri katika Thamani za Namba kufuatana na mpangilio wa Herufi (Alphabet za Kiarabu) na Ajabu ni kwamba Kuna Muashirio wa Sura 114 za Kuruani Tukufu.  Allahu Akbar. Je unaona Muujiza wa kushangaza?  Na hata Mtume Mohamad  ﷺ Hakujua Siri iliyobebwa na Herufi Hizi. Utafikiri Malaika Jibril alikuwa akimwambia Soma Sura 114. Na mtume akamjibu kwa kusema “mimi sijui kusoma”. Allahu Akbar.

13/March/2022 = Islamic Calendar 10/Shaaban/1443

JINA LA الْقُرْءَانُ NA MAAJABU YAKE

Katika Enzi Ya Mtume Mohamad ﷺ Waarabu na Mataifa mengineyo katika wakati huo walikuwa wakitumia Herufi kuwakilisha namba. Kwa Mfano Herufi  “Alif” ilipewa Thamani ya Namba 1, Herufi  “Baa” ilipewa Thamani ya Namba 2. Na hivyo hivyo Herufi  nyinginezo zilitumika kuwakilisha namba.  kwani Namba zilikuwa bado hazijulikani. 

Kwa Kutumia Thamani Hizo katika kufasiri Neno  الْقُرْءَانُ  Yaani “Kuruani”  utapata namba  383  (Alif 1 + Lam 30 + Qaf 100 + Raa 200 +  Hamzah 1 + Alif 1 + Nun 50)

Namba  383 Inashangaza sana kwani  ukifanya hesabu (Multiply) Namba Mbili za mwanzo na Ya Ya Tatu Yaani 38 Mara  3 utapata Namba 114  (38  X 3=114) Na Namba Hii ni Jumla ya  idadi ya Sura zote Za Kuruani.

La kushangaza zaidi  Ni Utafiti kwa kulinganisha Sura Mbili:Ya kwanza (Al-Fatiha) Na Ya Mwisho  (Al-Nnasi) utapata Thamani ya Namba 383.

Hebu tuchunguze haya tunayoyazungumza.

Sura Ya Al-Fatiha Ni Ya Kwanza  na kwa hiyo ni namba   1

Na Idadi Ya Maneno yake ni 29

Jumla Ya Herufi Zake ni 139

Sura Ya Al-Nnasi Ni Ya Mwisho na kwa hiyo ni Ya 114

Na Idadi Ya Maneno yake ni 20

Jumla Ya herufi zake ni 80 

Tukujumlisha Namba Hizi Tuatona Ya kushangaza sasa hebu tujumlishe

1 + 29 + 139 + 114 + 20 + 80=383

Unaona Maajabu. Tukijumlisha Namba za Sura Ya kwanza na Ya mwisho. Na kisha Tujumlishe Idadi ya Maneno na Herufi za Sura Ya Mwanzo na Ya Mwisho. Tunapata Thamani Ya neno  “KURUANI” ambayo ni  383

Muashirio huu unasema kwamba. Thamani Ya Sura Ya Mwanzo na Ya mwisho  ni sawa na Kuruani.Tusisahau kwamba Sura ya Alfatiha imekusanya Maana Ya Kuruani Yote. Sura Ya Al-Fatiha Na Annasi zote mbili zinazungumzia Mwenyeezi Mungu na Viumbe  Vyake. Na viwili hivi vinawakilisha Kuruani Yote.

Kuruani Ina Miujiza Isiyo na Mwisho

Tukichunguza Sura Ya Alfatiha Utakuta Aya Zifuatazo zina herufi  114 . Namba 114  inaashiria  Jumla ya Sura za Kuruani

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَٰلَمِينَ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ مَٰلِكِ يَوْمِ الدِّينِ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ اهْدِنَا الصِّرَٰطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَٰطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ

Aya Hizi za Al-fatiha zina herufi  114

hatukuhesabu Herufi ya Aya ya Mwisho  yaani Aya Inayosema

غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ

Kwani Aya Hii inazungumzia  Walioghadhibikiwa na Waliopotea.  Kuruani ni Neema kwa Wachamungu Wenye Kumtii Mwenyeezi Mungu na siyo walioghadhibikiwa na Wakaidi.

Muashirio wa Namba 114 katika Aya Za Al-Fatiha unahusu  Jumla za Sura 114 za  Kuruani .

Unahusu Watiifu peke yao. Kwani Ndio waliokusudiwa katika Aya Zifuatazo.  Wanaomuabudu, na Kumtegemea Mwenyeezi Mungu, Na wale ambao Wanamuomba Mwenyeezi Mungu awaruzuku Uongofu katika Njia iliyonyooka, Ile Njia ambayo wameneemeshwa Na Mwenyeezi Mungu

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَٰلَمِينَ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ مَٰلِكِ يَوْمِ الدِّينِ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ اهْدِنَا الصِّرَٰطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَٰطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ

Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi iwapo tumesibu utafiti huu. Allahu Akbar.  

14/March/2022 = Islamic Calendar 11/Shaaban/1443

MUUJIZA WA HERUFI ZA NENO الْقُرْءَانُ (Kuruani)

Sura Ya Al-Bakarah Namba 2  Aya Namba 185

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْءَانُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

TAFSIRI

185.(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi)huo hii Qurani Ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uwongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga) katika siku nyingine.Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito,na pia (anakutakieni) mtimize hisabu hiyo, na (anakutakieni) kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru.

SHEREHE YA AYA- MUUJIZA WA HERUFI ZA NENO

الْقُرْءَانُ “KURUANI”

Mara ya kwanza kutajika Jina الْقُرْءَانُ “Kuruani” ni Aya ya 185  katika Sura Ya Al-Bakarah. Muujiza Unaoshangaza ni kwamba Herufi za Neno الْقُرْءَانُ kuanzia Mwanzo wa Msahafu (Sura Ya All-Fatiha) mpaka Aya hii zimekariri kwa idadi sawa sawa na Jumla ya Idadi za Aya zote za kuruani Tukufu.

Angalia Muujiza wa Kushangaza. Allahu Akbar. Hebu Tuchunguze Jina au  Neno hili “Kuruani”

الْقُرْءَانُ =

Herufi Alif imetumika mara 2346 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Herufi Lam imetumika mara 1727 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Herufi Qaf imetumika mara 329 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Herufi Raa imetumika mara 484 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Herufi Hamzah imetumika mara 170 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Herufi Nun imetumika mara 1180 Kuanzia Sura Ya Al-fatiha mpaka mwisho wa Aya hii namba 185 katika Sura Ya Al-Bakarah.

Ukijumlisha kukariri kwa Herufi Hizi Utapata namba ya Kushangaza;

2346 + 1727 + 329 + 484 + 170 + 1180=6236

na Namba 6236 ni Jumla ya Aya za Kuruani Tukufu.

Je unaona Ya kushagaza?

Yaani mara ya kwanza kutajika neno “Kuruani” ni katika Aya namba 185 Sura Ya Bakarah na ukihesabu jumla ya Herufi zilizotumika na kukariri za neno hili kuanzia mwanzo wa Msahafu (sura Ya Al-fatiha) mpaka Aya Namba 185 Sura Ya Al-Bakarah ambayo inazungumzia kushushwa kwa Kuruani katika mwezi wa Ramadhan tunapata Idadi ya Aya za Kuruani Tukufu ambazo ni 6236.

Allahu Akbar. Muujiza sio mdogo. Angalia Kuruani Ilivyopangwa kwa ufundi wa hali ya juu. Kila herufi imehesabiwa.

Elimu ya Mwenyeezi Mungu ni kubwa sana lakini Binaadamu Hatufikiri kama ipasavyo na pia hatumpi Mwenyeezi Mungu haki anayostahiki. Hatumwogopi na kumtii kama ipasavyo. Tumeghururika na Mapambo ya Dunia. 

15/March/2022 = Islamic Calendar 12/Shaaban/1443

MAAJABU YA NENO الْقُرْآنُ  (Kuruani)KATIKA MSAHAFU

Mpangilio Wa Herufi, Maneno na Aya za Kuruani ni wa kushangaza sana. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Utafiti wa leo unahusiana na Namba za Sura Na Aya.

Neno الْقُرْآنُ (Kuruani) Limetajika katika Kuruani Tukufu mara 50

Na mara ya kwanza Kutajika ni katika Sura Ya Al-Bakarah  Namba 2 Aya Namba 185 katika Aya Ifuatayo

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

TAFSIRI

185. (Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo hii Qurani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uwongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha kufunga) katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, ·na pia (anakutakieni) mtimize hisabu hiyo, na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru.

Aya Ya Mwisho Kutajika ni Katika Sura Ya Al-Inshiqaq Namba 84 ِAya Namba 21 ifuatayo:

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ

TAFSIRI

21.Na wanaposomewa Qurani hawanyenyekei

SHEREHE

Na Baina Ya Aya Hizi mbili  kuna Aya  48  ambazo zimetaja Neno الْقُرْآنُ  (Kuruani)

Sasa Angalia Yafuatayo ambayo Yananishangaza sana tena sana.

Aya Ya kwanza= 2:185  (Yaani Sura Ya Pili Aya Namba 185

Aya Ya Pili=84:21  (Yaani Sura Namba 84  Aya Namba 21

Angalia Sasa Maajabu yanayofuata:

8421-2185=6236  (Ukitoa Namba za Aya Ya Kwanza katika Namba za mwisho unapata Namba 6236  ambayo ni Idadi za Aya Za Kuruani)

Tusisahau kwamba Namba za Sura Na Aya ziliongezwa baada Ya Mtume Mohamad ﷺ Kufariki Dunia. Namba hizi ziliongezwa ili kuwasaidia Wasomaji.

Kwa kweli ni katika Miujiza mikubwa kwani Mwenyeezi Mungu ameahidi kuihifadhi Kuruani isiharibiwe. Na kwa hiyo Nyongeza Za Namba hazikuwa bure bure bali Mwenyeezi Mungu ndiye aliyewapa fikra ya kuongeza Namba hizi na kisha Yeye Mwenyewe ndiye alijaalia kufanyike Miujiza kama hii. 

Je unaona Ya kushagaza.  Ukitoa Namba za Aya Ya kwanza iliyotaja neno Kuruani  kutoka katika Namba za Aya Ya Mwisho iliyotaja Neno kuruani unapata  jawabu ni 6236 ambayo ni Idadi ya Aya Za Kuruani ambazo ni 6236. Allahu Akbar. Kwa kweli Mwenyeezi Mungu Mkubwa na Kuruani ni Muujiza mkubwa sana tena sana.

16/March/2022 = Islamic Calendar 13/Shaaban/1443

REVERSE TOPICS AU REVERSE SYMMETRY/MADA ZINAZOFANANA KWA NJIA YA REVERSE AU KINYUME

Alhamdulilah leo ningependelea tufanye Utafiti kwa ufupi unaohusu mpangilio wa Mada katika kuruani. Ningependelea kuanza na Mlinganisho wa Mada katika Sura Moja na siku sijazo tufanye darasa katika Mlango Mwingine  Mpya litakalohusu Mlinganisho wa Maneno katika Aya, Mlinganisho wa Mada baina ya Sura Mbili Na Mlinganisho wa Mada baina ya Sura zaidi ya Mbili. 

Mwenyeezi Mungu akipenda nitaufungulia mlango mpya kwa maelezo zaidi lakini katika Mwezi huu wa Shaaban nitajitahidi kugusia machache.

Mlinganisho wa Mada katika Sura Moja   

Mwenyeezi Mungu amejaalia Aya Namba 143 katika Sura Ya Al-Bakarah kuwa ya Katikati ni Muujiza Mkubwa. Hapo Mwanzoni Kuruani haikuwa na Namba yeyote kwani Namba za Sura Na Aya ziliongezwa baadaye. Muujiza unaoshangaza ni kuwa Aya Hii inazungumzia kwamba  Waislamu ni Taifa ambalo lipo katikati Ya Dini zote na Kibla Ni Jengo ambalo pia lipo katikati ya taifa la kiislamu. Ni Muujiza kwani Aya za Sura hii ni 286 na Aya hii ipo katikati. Mtume Mohamad ﷺ hakushughulika na Muujiza huu bali tumewekewa sisi bila yeye mwenyewe kujua. Maajabu mengineyo ni kwamba Mada Za sura hii pia zinashangaza sana. Ukilinganisha Mada za Aya  kabla Ya Aya namba 143 na Mada za Aya  baada ya Aya hii utaona Zimepangwa kiajabu sana.

Na kila Mtafiti atapata Muujiza kufuatana na Mtizamo wake.

Na huu ndiyo Muujiza kwani Kuruani imejaa Maajabu yasiyo na Mwisho. Kila Mtafiti anapata Ya Kushangaza. Allahu Akbar.

Ukichunguza Sura Hii ya Al-Bakarah utapata Mada Mbalimbali. Hapa chini nitaorozesha Baadhi na kisha tutalinganisha Baina Ya Mada za Mwanzo na Mwisho wa Sura.

MADA KATIKA AYA  ZA MWANZO KABLA YA AYA NAMBA 143

1/WAUMINI, WASIOKUWA NA IMANI NA WANAFIKI

2/KUUMBA 

3/SHERIA WALIZOPEWA WAISRAELI

4/MTIHANI ALIOPEWA NABII IBRAHIM

——————————————————————————

Aya Namba 143 ambayo ipo katikati

و كذلك جعلنكم امه وسطا لتكونوا شهدا علي الناس و يكون الرسول عليكم شهيدا و ما جعلنا القبله التي كنت عليها الا لنعلم من يتبع الرسول ممن ينقلب علي عقبيه و ان كانت لكبيره الا علي الذين هدي الله و ما كان الله ليضيع ايمنكم ان الله بالناس لروف رحيم

TAFSIRI

Na vivyo hivyo tumekufanyeni umati katikati (kama kibla chenu tulivyokifanya katikati) ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume ﷺ awe shahidi juu yenu. Na hatukukifanya kibla ulichokuwa nacho.(mara ya kwanza kuwa ndiyo kibla chako sasa na mpaka mwisho wa ulimwengu) ita tupate kumjulisha (atambulikane) yule anayemfuata Mtume na yule anayegeuka akarejea nyuma. Na kwa yakini lilikuwa jambo gumu isipokuwa kwa wale aliowaongoza Mwenyezi Mungu. Na Mwcnyezi Mungu hakuwa mwenye kuipoteza imani yenu. Kwani Mwenyezi Mungu kwa watu ni Mpole sana (na) mwenye rehema.

—————————————————————————

MADA KATIKA AYA  ZA MWISHO BAADA YA AYA NAMBA 143

5/MTIHANI WALIOPEWA WAISLAMU

6/SHERIA WALIZOPEWA WAISLAMU

7/KUUMBA

8/WAUMINI, WASIOKUWA NA IMANI NA WANAFIKI

Hizi Mada 8  zimepangwa kiajabu.

Mada Ya Kwanza  katika Sura Ya Al-Bakarah imezungumziwa tena Mwishoni katika Sura Hii ya Al-Bakarah, Yaani Mada namba 1 Katika Sura Ya Al-Bakarah imezungumziwa tena Katika Mada namba 8

Mada Namba 2  Katika Sura Ya Al-Bakarah imezungumziwa tena Katika Mada namba 7

Mada namba 3  Katika Sura Ya Al-Bakarah imezungumziwa tena Katika Mada namba 6

Mada namba 4 Katika Sura Ya Al-Bakarah imezungumziwa tena Katika Mada namba 5

Mada zinafanana kwa njia ya Reverse.  Na ijapokuwa kila Mada inatofautiana na Nyingine katika Habari zake lakini  zinafanana katika Malengo yake.

Mpangilio huu wa kiajabu ni saini yake Mwenyeei Mungu kwamba binaadamu hawezi kuandika kitabu kama hiki. Ni Uthibitisho kwamba aliyeleta Kuruani ni Mwenyeezi Mungu. Mpangilio wa kiajabu sana.

17/March/2022 = Islamic Calendar 14/Shaaban/1443

MUUJIZA WA MATUMIZI YA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MTUKUFU “ALLAH”

Jina La Mwenyeezi Mungu  “ALLAH”  limetajika katika Kuruani katika Mifumo Mbalimbali  (Kwa Kiarabu inajulikana kama Mushtaqaat Na kwa Kiingereza Derivatives)

Jumla Ya  idadi ya Kutajika kwa Jina “ALLAH” katika mifumo mbalimbali ni  Mara 2699. 

Kwa hiyo Jina La Mwenyeezi Mungu Mtukufu limetajika katika Msahafu Mara  2699. 

Jambo la kushangaza ni kwamba Namba Hii inajulikana kama Prime Number, Na Ni Namba isiyogawanyika Na namba Yeyote isipokuwa na Namba yenyewe yaani 2699 au Namba 1.

Namba hii inajulikana katika Hesabu kama x2 Factor Number. Yaani haigawanyiki na Namba yeyote isipokuwa na Yenyewe au Moja tu. 

Sasa angalia Ya kushangaza. Namba hii inathibitisha Kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mmoja tu peke yakena hana mshirika.  Angalia Muujiza wa kushagaza.

Namba Hii imepangwa kimakusudi na siyo bure bure. Muujiza Mkubwa mbele ya macho yetu. Allahu Akbar.

Jina اللَّهِ Limetajwa katika Kuruani Mara 829

Jina  لِلَّهِ Limetajwa katika KUruani Mara 129

Jina اللَّهُ Limetajwa katika Kuruani Mara  972

Jina بِاللَّهِ Limetajwa katika Kuruani Mara 139

Jina اللَّهَ Limetajwa Katika Kuruani Mara 592

Jina لِّلَّهِ Limetajika Katika Kuruani Mara 14

Jina فَاللَّهُ Limetajika Katika Kuruani Mara 6

Jina فَلِلَّهِ Limatajika Katika Kuruani Mara 6

Jina أَبِاللَّهِ LImetajika Katika Kuruani Mara 1

Jina ءَاللَّهُ  Limatajika Katika Kuruani Mara 2

Jina تَاللَّهِ Limatajika Katika Kuruani Mara 9

Jumla ni  829 + 129 + 972 + 139 + 592 + 14 + 6 + 6 + 1 + 2 + 9=2966

18/March/2022 = Islamic Calendar 15/Shaaban/1443

MUUJIZA WA MIAKA YA WAHYI NA MPANGILIO WA AYA KATIKA MSAHAFU

Aya ifuatayo Namba 23 Katika Sura Ya Zumar  Namba 39  Ni Muujiza katika Miujiza isiyo na Mwisho. Namba Ya Aya Ni ya 23 na inazungumzia Kuja kwa Wahyi  yaani Kushushwa kwa Kuruani. Na Maajabu ni Kwamba muda wa kushuka Kwa Kuruani Kwa Mtume Mohamad ﷺ ilichukua Muda wa miaka 23. Angalia Muujiza. Aya Hii ni ya 23 katika Sura Ya Zumar. Namba Ya Aya inalingana na muda wa Wahyi  (Revelation) kwa Mtume ﷺ  

Allahu Akbar. Muujiza mbele ya macho yetu.

اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُتَشَابِهًا مَثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ ذَلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَنْ يَشَاءُ وَمَنْ يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ [الزمر: 23].

TAFSIRI

Mwenyezi Mungu amereremsha hadithi nzuri kabisa (kwa kuteremsha) kitabu chenye maneno yanayowafikiana, (yasiyopingana) (na) yanayokaririwa (bila kuchosha); husisimka kwayo ngozi (miili) za wale wanaomwogopa Mola wao … Kisha ngozi zao na nyoyo zao huwa laini kwa kumkumbuka Mola wao. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu; kwa huo humuongoa amtakaye. Na anayeachiwa na Mwenyezi Mungu kuwa amepotea, basi hakuna wa kumuongoa.

19/March/2022 = Islamic Calendar 16/Shaaban/1443

Muujiza Wa Neno  “KURUANI” katika Aya namba  114 Sura Ya Twaha Namba 20. 

Kuruani Ni Muujiza mkubwa sana tena sana.

Kila siku tunasoma Mapya na hakuna Mwisho  Kuruani Ni Mabahari yasiyo kauka. 

Allahu Akbar.  Aya ifuatayo imejaa Miujiza ya kushangaza.

فَتَعَالَى اللَّهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآَنِ مِنْ قَبْلِ أَنْ يُقْضَى إِلَيْكَ وَحْيُهُ وَقُلْ رَبِّ زِدْنِي عِلْمًا [طه: 114

TAFSIRI

14.Ametukuka Mwenyezi Mungu. Mfalme wa haki. Wala usiifanyie haraka (hii) Qurani (kwa kusoma), kabla haujamalizika Wahyi (ufunuo) wake. Na (uombe) useme: “Mola wangu, · nizidishie ilimu.”

SHEREHE

Mwenyeezi Mungu  anampa nasiha Mtume Mohamad ﷺ katika kusoma Kuruani.

Mtume Mohamad ﷺ alipokuwa analetewa Wahyi na Jibril na kufundishwa Kuruani alikuwa na haraka ya kuhifadhi na alikuwa akihofia kusahau lakini  Mwenyeezi Mungu akamwambia asifanye hivyo. Bali asome na kuihifadhi bila pupa na wasiwasi. Na katika Aya hii Mwenyeezi Mungu anamfundisha Mtume ﷺ Dua Nzuri sana inayosema 

“Sema Ewe Mola Nizidishie Elimu”

Dua hii inatoka Kwa Mwenyeezi Mungu na Ni nzuri kuitumia. 

MUUJIZA 

Muujiza Wa kwanza

Ukiangalia Aya utaona ni ya namba 114 na Aya hii inzungumzia WAHYI (Revelation) na Mtume ﷺ anapewa nasika kwamba asiharakishe bali asome pole pole kwa kuelewa na pia aombe dua. Na afanye hivyo hivyo mpaka mwisho wa WAHYI (Revelation). Yaani kuruani yote yenye Sura zote ambazo ni jumla ya Sura 114.  Sasa angalia Muujiza Mwingine. Aya hii katika Sura Ya Twaha ni Ya Namba 114 na Jumla ya Sura Za Kuruani Zote ni 114 Pia!!!

Allahu Akbar. Unaona Maajabu ya Mpangilio wa kushangaza. Aya inazungumzia Revelation (Wahyi) ya Kuruani ambayo ina Jumla ya Sura  114 na Namba Ya Aya hii ni ya  114 pia!!! Je Mtume ﷺ alipanga Aya Hizi?  Haiwezekani kwani Namba zote ziliongezwa baadaye yaani baada ya kufariki Mtume ﷺ na huu ndiyo muujiza.

La kushangaza zaidi ni  Neno  بِالْقُرْآَنِ “Kuruani” katika Aya Hii. Neno  hili  ni la  41154  kuanzia mwanzo wa kuruani. Yaani idadi ya maneno kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Fatiha Mpaka Neno بِالْقُرْآَنِ “Kuruani”  ni  maneno  41154

Tunapofanya utafiti wa namba hii tunaona mengine ya kushagaza sana. Namba hii ni sawa na kusema 

19 x 19 114=41154

Sasa Angalia Ya Maajabu. Namba 114 ni idadi ya Sura Za Kuruani. Namba 19 ya kwanza  ni Idadi ya Herufi za Aya Ya Kwanza بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ na Namba 19 ya pili ni Idadi ya Malaika wa Moto wa Jahannam. Kama tunavyosoma katika Sura Ya Al-Mudathir kuhusu Idadi Ya Malaika Wa moto wa Jahannam ni 19  na pia  Kuna Miujiza isiyo na mwisho ambayo ina uhusiano na namba 19.  Hizi namba  19 X 19 X 114 ni namba za miujiza mikubwa. Namba 19  nimeigusia katika Milango mingine ya website hii.  Allahu Akbar.  Kwa kweli Tumche Mwenyeezi Mungu kwani huko tunapokwenda kunatisha. Makaburi yanatisha. Allahu Akbar.

20/March/2022 = Islamic Calendar 17/Shaaban/1443

MAAJABU YA KUKARIRI KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU  “ALLAH” NA IDADI HIYO KULINGANA NA RAKAA NA SUJUDU. 

Kuna Aya Katika Kuruani ambazo zimeanziwa na Jina La Mwenyeezi Mungu Mtukufu “ALLAH” kwa Mifumo  au Mushtaqaat (Derivatives) mbalimbali kama ifuatavyo:

1/Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina  الله   ni  34

2/Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina و لله  ni  17

3/ Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina تالله  Ni  2

4/Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina لله   ni 4

5/Jumla ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina هو الله  ni  3

6/Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina فلله  ni 2

7/Jumla Ya Aya ambazo zimeanziwa na Jina و الله ni 20

Kuna Maajabu makubwa ya Idadi ya kukariri huku na siyo bure bure.

Lakini Mwenyeezi Mungu anajua zaidi na sisi tunabahatisha kwa kufasiri kwa kutumia neno  “Labda” . Na mimi nitafanya hivi kwa kusema huenda namba hizi zinatupa maana ifuatayo:

1/Namba 34 huenda    inaashiria SUJUDU  za Sala zetu 5 kwani jumla ya Sujudu  ni 34 

2/Namba  17 huenda   inaashiria Idadi ya Jumla za Rakaa za Sala 5

5/Namba 2 huenda inaashiria Jumla ya Rakaa 2  za Sala ya Asubuhi

6/Namba 4 huenda   inaashiria Jumla ya Rakaa 4 za Sala ya Dhuhuri, Al-Asr na Ishaa

7/Namba  3  huenda inaashiria Jumla ya Rakaa za Sala ya Maghrib

8/ Namba  2 huenda  inaashiria ibada mbili;   KURUKUU na KUSUJUDU

9/Namba  20 huenda inaashiria   Thawabu  10 za KURUKUU na 10 za KUSUJUDU kama Mwenyeezi Mungu alivyosema katika Sura Ya Al-Anam Aya namba 160 hapa chini.

kwamba Mtu akifanya Wema atalipwa Mara 10 na akifanya ubaya basi atalipwa Dhambi Moja tu peke yake.  (Angalia Huruma Ya Mwenyeezi Mungu. Ukifanya Wema unalipwa 10 lakini ubaya hulipwi 10 bali Moja tu peke yake) Allahu Akbar

﴿ من جاء بالحسنة فله عشر أمثالها ومن جاء بالسيئة فلا يجزى إلا مثلها وهم لا يظلمون ﴾ [ الأنعام: 160]

Kama tulivyoona kwamba Kurukuu, Kusujusu katika Sala zote 5 huwa  tunamtukuza Mwenyeezi Mungu yaani  ALLAH  na kama tulivyosema Aya ambazo zimetanguliwa na Jina La Mwenyeezi Mungu zimekariri na kuashiria Ibada hii ambayo tunamtukuza ALLAH

25/March/2022 = Islamic Calendar 22/Shaaban/1443

MAAJABU MAKUBWA KATIKA AYA YA MTIHANI ULIOTOLEWA NA MWENYEEZI MUNGU KWETU NA KWA MAJINI WOTE

Allahu Akbar, Allahu Akbar. Huu siyo mtihani mdogo. Naapa kwamba huu siyo myihani mdogo. Allahu Akbar. Ndugu wasomaji.  Sikiliza Mwenyeezi Mungu anavyosema katika Aya ifuatayo kisha tufikiri maajbu ya Mfumo wa Aya hii. Ni Aya Siyo Ndogo. Mtihani siyo mdogo.

Mwenyeezi Mungu anasema katika Sura Ya Asraa  Aya Namba 88

قُل لَّٮِٕنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْبِمِثۡلِ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُہُمۡ لِبَعۡضٍ۬ ظَهِيرً۬ا (٨٨)

Hebu  Tuichunguza Aya Hii Yenye maajabu. Kabla ya uchunguzi tusome  Tafsiri ya Aya. 

TAFSIRI

88. Sema “Hata wakijikusanya watu (wote) na majinni ill kuleta mfano wa hii Qurani basi hawangaliweza kuleta mfano wake; hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao.,

Huu Ni Mtihani  anatoa Aliyetuumba na aliyeumba kila kitu. Anamwambia Mtume ﷺ atuambie kwamba 

Wakikusanyika Binaadamu wote na Majini yote kisha wasaidiane katika kuandaa Mfano wa Kuruani basi hakuna angelieweza. 

Tunaambiwa hapa siyo tuandike kitabu chetu cha  kuruani bali tuigize  mfano wa kuruani.  Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba ikiwa kuigiza haiwezekani basi kuandika upya ndiyo haiwezekani kabisa. 

Hapa Mwenyeezi Mungu anatupa mtihani kwa kutuhurumia yaani tuandike kitabu kama kuruani kwa kuchukua mfano huu. 

Sasa tujiulize suali  “ikiwa mtihani huu ambao tunasaidiwa kwa mfano wa kuigiza  tumefeli basi kuandika bila ya mfano ndiyo hata tusiwaze yaani tutafeli na tutafeli na tutafeli na tutafeli.

Mwenyeezi Mungu baada ya kusema haya kaongezea Muujiza katika Aya hii ambao unatisha. Kwa kweli unashangaza. Lakini pia unatisha. hebu tuone muujiza huo.

MUUJIZA MKUBWA SANA WA MFUMO WA AYA HII YA 88 KATIKA SURA YA AL-ISRAA

Hebu niilete tena Aya hii kisha tuichambue Vipande Vipande. Allahu Akbar.

قُل لَّٮِٕنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْبِمِثۡلِ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُہُمۡ لِبَعۡضٍ۬ ظَهِيرً۬ا (٨٨)

Ndugu wasomaji angalieni vizuri Aya hii utaona maajabu ya kushangaza.

Aya Namba 88

Kiini cha Aya Hii Ni “KURUANI”  (Nimetia Rangi Ya Buluu)

Upande wa Kushoto Kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka Herufi BA  ya Neno  بِمِثۡلِ  Yaani kipande cha Aya kufuatacho

قُل لَّٮِٕنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ     بِ

Kipande hiki kinasema

“Sema Wakikusanyika Binaadamu na Majini ili walete”

na Upande wa Kulia Kuanzia  

لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُہُمۡ لِبَعۡضٍ۬ ظَهِيرً۬ا

Kipande hiki kinasema

“Hawataweza Kuleta Mfano huu (Kuruani) na hata wakisaidiana”

Yaani Vipande hivi viwili vimeizunguka  Ibara inayosema

مِثۡلِ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ

Ibara hii inasema   “Mfano wa Kuruani”

Kwa hiyo  Kipande cha kwanza na cha pili kinazungumzia Kuruani ambayo  ibara hiyo ipo katikati ya Aya.

Ukichunguza sana kwa kufikiri utaona Hivi vipande viwili yaani Ibara ya Kwanza na Ya mwisho ni kama majiwe ya mizani na Katikati ni Mizani yenyewe.

—————————

1/ قُل لَّٮِٕنِ ٱجۡتَمَعَتِ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَىٰٓ أَن يَأۡتُواْ بِ

Ibara Ya Kulia (Majiwe Ya Mizani)

——————————-

2/ مِثۡلِ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ   (MIZANI YENYEWE)

————————–

لَا يَأۡتُونَ بِمِثۡلِهِۦ وَلَوۡ كَانَ بَعۡضُہُمۡ لِبَعۡضٍ۬ ظَهِيرً۬ا

Ibara Ya Kushoto (Majiwe Ya Mizani)

—————————————–

Sasa tuchunguze zaidi tuone Vipimo  hivi vya kushangaza

IBARA YA UPANDE WA KUSHOTO 

1/Ibara hii ina Herufi   32

2/Ibara hii ina Herufi  zisizokuwa na NUQTA  20

3/Ibara hii ina Herufi ambazo zina NUQTA 12

4/Jumla Ya NUQTA katika Herufi ni  17

5/Herufi Za Kasrah  ni 7

Jumla ya Namba hizi ni   88 (32 + 20 + 12 + 17 + 7=88)

IBARA UPANDE WA KULIA

Ndugu waislamu  Ibara ya Upande wa Kulia una Idadi ya Viungio sawa sawa na Upande wa kushoto!!!!!!!!

1/Ibara hii ina Herufi 32

2/Ibara hii ina Herufi zisizokuwa na NUQTA 20

3/Ibara hii ina Herufi ambazo zina NUQTA 12

4/Jumla Ya NUQTA katika Herufi ni 17

5/Herufi Za Kasrah ni 7

Jumla ya Namba hizi ni 88 (32 + 20 + 12 + 17 + 7=88)

Angalia Maajabu.  Ibara mbili  zimegawanywa sawa sawa kila kitu.  NUQTA, Herufi. Na HARAKATI!!!!

Na Katikati Ni  “KURUANI” mfano wa Mezani Yenyewe.

Angalia Vipimo Allahu Akbar.  Vipimo vya Kiajabu. 

NUQTA, Na Harakati ziliongezwa baada ya Kufariki Mtume na yeye hakujua nyongeza hizi. Iliongezwa ili kuwasaidia wasomaji wa lugha Ya Kuruani ili kuwaepushia na Makosa.  Sasa angalia Mwenyeezi Mungu alikuwa Anachunga yote haya. Aliyajua Yatakayoongezwa. Alijua Vipimo hivi ambavyo leo hii itakuwa muujiza kwetu. Allahu Akbar.  Je unaona Haya. Yaani Muujiza mpaka katika  NUQTA  (English: Dots)

Aya hii ni Changamoto kwetu na Pia Aya hi hii imebeba Miujiza isiyo na mwisho.

Hebu tufikiri. Ibara Mbili katika Aya Hii zinafanana katika NUQTA, Herufi  Na Harakati.

Sasa la kushangaza Zaidi ni Namba Ya Aya.  Hebu Angalia. Aya Hii ni Namba 88!!!!!  sawa sawa na Jumla ya Muujiza tuliouona hapa juu!!!

Hebu angalia. Tumejumlisha NUQTA, Herufi na Harakati  yaani  Kasrah na tukapata  88  na sasa tuanona Aya namba 88

Unaona Ya kushangaza?????
Allahu Akbar. Kwa wale wanaojua Lugha Ya Kiarabu inawashagaza pia kwani siyo kawaida katika lugha hiii kuhesabiwa  viungio vidogo vidogo kama hivi. NUQTA, Harakati na Herufi kwa kawaida havihesabiwi kwa hiyo siyo kawaida. Na hata lugha zetu nani anahesabu Herufi? je huoni Maajabu?  Ndugu Waislamu Hii siyo lugha ya Binaadamu. Ni saini yake Mwenyeezi Mungu Mkubwa aliyetukuka. Hii ni onyo  kwetu turudi katika Kuruani na ibada. Kwa kweli inatisha. Inatisha sana. Hebu tufikiri   na tukumbuke Nyumba zetu za baadaye yaani Makaburi. Sasa Kuruani hii tuisome na kuifuata kabla haijachukuliwa na Mwenyewe aliyeileta. Itakapoondolewa itakuwa majuto. Allahu Akbar.

26/March/2022 = Islamic Calendar 23/Shaaban/1443

MIAKA  300 NA 309   YA WACHAMUNGU WALIOLAZWA  PANGONI NA KUSHUKA KWA SURA YA AL-KAHF. MUUJIZA WA HESABU ZA MANENO YA AYA

Sura Ya Al-Kahf Namba 18 Aya Namba 25

وَلَبِثُواْ فِى كَهۡفِهِمۡ ثَلَـٰثَ مِاْئَةٍ۬ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعً۬ا (٢٥)

TAFSIRI

25.Na walikaa katika pango Lao mIaka mia tatu, na wakazidisha (miaka) tisa.

SHEREHE YA AYA

Kisa cha Maajabu. Watu wachamungu waliokimbilia katika Pango na Kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu akawalaza Miaka 300 ya Hesabu za Calendar za Kileo.  Yaani Gregorian Calendar. Calendar hii inahesabu Kuzunguka kwa Ardhi katika Jua kwa muda wa siku 365. 

Kwa Calendar ya Kiislamu ambayo inajulikana kama Hijriy Calendar (Ilianzishwa kwa kuhesabu mara ya kwanza Mtume Mohamad Kuhama Madina alipokimbilia huko kwa ajili ya kutafuta Usalama kutokana na Hatari ya Makafiri wa Mecca)  inakuwa ni Miaka  309  kwa hesabu ya Mwezi kuizunguka Ardhi. Nimezungumzia kwa urefu na pia Kuna Video katika Website hii ambayo inayohusu tofauti ya Calendar hizi mbili na kwa hiyo nitagusia kwa ufupi tu hapa. 

Kwa kifupi Calendar ya kiislamu ambayo inatumia Mwezi inabidi tuongeze Miaka 9  ili ilingane na Miaka 300.

kwani Hesabu za masiku ya Kiislamu ni pungufu. Kila Mwezi wa Kiislamu una siku 29.5  na ndiyo maana ya kuongeza Miaka 9 kama ilivyo katika Tafsiri ya Aya hii.

Kwa kweli Calendar zote mbili ni sahihi kwani ni zake Mwenyeezi Mungu. Jua na Mwezi ameziumba Ili kutusaidia tupate kuhesabu masiku, miezi na miaka.

Aya hii inatupa habari kwamba wachamungu hao walilazwa katika pangi kwa mida wa miaka  300 kwa hesabu za Jua na Wakazidisha miaka 9 ni kwa hesabu za HIjri  yaani hesabu za kutumia  Mwezi.

Na hii ndiyo  Tafsiri ya Ibn Kathir ambayo inakubaliana na Sayansi.

Lakini kuna Tafsiri Nyinginezo ambazo zinasema vinginevyo kwamba  Kutajwa kwa miaka 300 na 309  ni Kauli za Watu kwani kauli hizo ni kudhania dhania tu. Dhana hizi zinaungana na Dhana za Aya Kabla ya Aya hii wakati watu walipokuwa wakijadiliana kuhusu idadi ya wachamungu hao waliolazwa pangoni  na Mbwa  wao. Tafsiri hii pia imetiliwa mkazo na Abdullah bin Abbas ambaye alikuwa Mmojawapo wa Maswahaba wa Mtume Mohamad ﷺ ambao walikuwa na Elimu kubwa katika wakati huo.

MUUJIZA WA KUSHANGAZA

Sasa tufanye utafiti wetu ambao utahusu idadi ya Maneno, Herufi na Nuqta za Aya hii na tuone tunapata Kitu gani?

وَلَبِثُواْ فِى كَهۡفِهِمۡ ثَلَـٰثَ مِاْئَةٍ۬ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعً۬ا

Jumla ya Idadi ya Maneno Ya Aya  hii ni   8

Jumla ya Idadi ya Herufi Ya Aya Hii ni 36

Na Jumla Ya idadi ya Nuqta za Aya hii ni 21  (ukihesabu Nuqta mbili za Herufi  YA   katika فِى utapata Jumla ya herufi ni 23 lakini hatukuzihesabu kwani wataalamu wa lugha wanasema kwamba Nuqta za Herufi “Ya”  siyo lazima kuziandika ikiwa herufi hii ipo Mwishoni mwa Neno kama hapa katika Neno فِى)

Sasa angalia Maajabu   yanayofuata

Maneno  8  X  Herufi  36= 288  ujumlisha Nuqta 21=309

Angalia Ya kushangaza tunapata  Hiyo Miaka  309 ambayo Aya hii inazungumzia.

Je unaona Ya kushangaza.  Hii ni saini yake Mwenyeezi Mungu. Anathibitisha Muujiza huu kwamba Kisa hiki ni cha kweli. Na sio uongo. 

Muujiza mwingine  tumezungumzia katika sehemu nyingine ya Website hii kwamba

Ukihesabu Maneno ya Kisa hiki chote kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa Kisa hiki unapata Jumla ya maneno ni 309 pia  na Pia ukihesabu Kurasa za Kuruani Kuanzia Aya Hii mpaka mwisho  wa Msahafu  utapata  Jumla ya Kurasa (Pages) Ni 309  pia.  Allahu Akbar.  Hizi ni Saini zake Mwenyeezi Mungu kututhibitishia Muujiza Huu kwamba ulifanyika bila uongo.

Pia tuelewe kwamba Kisa hiki kilijulikana sio kwa ukamilifu kabla ya kushuka sura ya Al-Kahf kwani Wakristo na Mayahudi wakati huo walikuwa hawana uhakika kuhusu idadi ya watu hao na miaka waliolazwa hapo pangoni. Mayahudi  walikuja kumuuliza Mtume Mohamad ﷺ kuhusu habari ya kisa hiki. Walitaka kumchunguza kama alikuwa Mtume wa haki. Na hii ndiyo sababu ya kushushwa Sura Hii ya Al-Kahf ambayo imeelezea kisa hiki kwa kirefu kwa kutumia maneno  309.

Allahu Akbar. Miujiza isiyo na mwisho.

28/March/2022 = Islamic Calendar 25/Shaaban/1443

MUUJIZA WA KIWANGO CHA DHAHABU KATIKA SURA YA AL-ZUKHRUF.

GOLDEN RATIO  FORMULA “a + b/a na pia a/b”

Tulizungumza katika sehemu nyingine ya Webiste hii kuhusu Kiwango cha Kupimia Uzuri  wa Kila umbile Ulimenguni. Kiwango  hilki kinajulikana kama “Golden Ratio”  au Kwa KIswahli  “KIwango Cha Dhahabu”  na kiwango hiki kinawakilishwa na Namba  au Ratio  1.618

Wataalamu wanasema kwamba Kitu chochote kinachokua Kizuri sana kwa umbile  basi vipimo vitatupa namba hii.  Leo ningependelea kuwakumbusha niliyoyaelezea katika  Mlango wa Website hii kuhusu  Mji wa Mecca ambao  Location au Sehemu ya Mji huo  ukifanya hesabu kutafuta  Golden Ratio kwa kutumia umbali wa  Latitudes  baina Ya Mecca na Kusini na Kisha Mecca na Kaskazini ya Dunia na Pia Longitudes Baina ya Mecca na Mashariki na Kisha Mecca na Magharibi ya Dunia  utapata  Kiwango cha Dhahabu 1.618  na pia ukifanya hesabu utaipata namba hii katika Aya Za Kuruani katika sehemu mbali mbali. Nilielezea Sehemu hizo katika Milango ta Website hii na kwa hiyo sitarudia tena.

Alhamdulilah Leo Nitagusia Muujiza Mpya wa Golden Ratio  “Kiwango Cha Dhahabu” katika Sura Ya Al-Zukhruf Namba  43 Allahu Akbar. Kwa kweli Kuruani Ni Muujiza Mkubwa. Hebu  Tuanze na Safari hiyo ili tuone ya Kushangaza.

Kwanza Tufasiri Aya Tatu Kutoka Katika Sura Ya Al-Zukhruf na  kisha Tushereheshe Mambo Ya Kushangaza.  Allahu Akbar na Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi.

Sura Ya Az-Zukhruf  Kuanzia Aya Namba 33 mpaka Aya namba 53

وَلَوۡلَآ أَن يَكُونَ ٱلنَّاسُ أُمَّةً۬ وَٲحِدَةً۬ لَّجَعَلۡنَا لِمَن يَكۡفُرُ بِٱلرَّحۡمَـٰنِ لِبُيُوتِہِمۡ سُقُفً۬ا مِّن فِضَّةٍ۬ وَمَعَارِجَ عَلَيۡہَا يَظۡهَرُونَ (٣٣) وَلِبُيُوتِہِمۡ أَبۡوَٲبً۬ا وَسُرُرًا عَلَيۡہَا يَتَّكِـُٔونَ (٣٤) وَزُخۡرُفً۬ا‌ۚ وَإِن ڪُلُّ ذَٲلِكَ لَمَّا مَتَـٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا‌ۚ وَٱلۡأَخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُتَّقِينَ (٣٥) وَمَن يَعۡشُ عَن ذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ نُقَيِّضۡ لَهُ ۥ شَيۡطَـٰنً۬ا فَهُوَ لَهُ ۥ قَرِينٌ۬ (٣٦) وَإِنَّہُمۡ لَيَصُدُّونَہُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّہُم مُّهۡتَدُونَ (٣٧) حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَنَا قَالَ يَـٰلَيۡتَ بَيۡنِى وَبَيۡنَكَ بُعۡدَ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ فَبِئۡسَ ٱلۡقَرِينُ (٣٨) وَلَن يَنفَعَڪُمُ ٱلۡيَوۡمَ إِذ ظَّلَمۡتُمۡ أَنَّكُمۡ فِى ٱلۡعَذَابِ مُشۡتَرِكُونَ (٣٩) أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ أَوۡ تَہۡدِى ٱلۡعُمۡىَ وَمَن كَانَ فِى ضَلَـٰلٍ۬ مُّبِينٍ۬ (٤٠) فَإِمَّا نَذۡهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنۡہُم مُّنتَقِمُونَ (٤١) أَوۡ نُرِيَنَّكَ ٱلَّذِى وَعَدۡنَـٰهُمۡ فَإِنَّا عَلَيۡہِم مُّقۡتَدِرُونَ (٤٢) فَٱسۡتَمۡسِكۡ بِٱلَّذِىٓ أُوحِىَ إِلَيۡكَ‌ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَٲطٍ۬ مُّسۡتَقِيمٍ۬ (٤٣) وَإِنَّهُ ۥ لَذِكۡرٌ۬ لَّكَ وَلِقَوۡمِكَ‌ۖ وَسَوۡفَ تُسۡـَٔلُونَ (٤٤) وَسۡـَٔلۡ مَنۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ مِن رُّسُلِنَآ أَجَعَلۡنَا مِن دُونِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ءَالِهَةً۬ يُعۡبَدُونَ (٤٥) وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَقَالَ إِنِّى رَسُولُ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٤٦) فَلَمَّا جَآءَهُم بِـَٔايَـٰتِنَآ إِذَا هُم مِّنۡہَا يَضۡحَكُونَ (٤٧) وَمَا نُرِيهِم مِّنۡ ءَايَةٍ إِلَّا هِىَ أَڪۡبَرُ مِنۡ أُخۡتِهَا‌ۖ وَأَخَذۡنَـٰهُم بِٱلۡعَذَابِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ (٤٨) وَقَالُواْ يَـٰٓأَيُّهَ ٱلسَّاحِرُ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهۡتَدُونَ (٤٩) فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡہُمُ ٱلۡعَذَابَ إِذَا هُمۡ يَنكُثُونَ (٥٠) وَنَادَىٰ فِرۡعَوۡنُ فِى قَوۡمِهِۦ قَالَ يَـٰقَوۡمِ أَلَيۡسَ لِى مُلۡكُ مِصۡرَ وَهَـٰذِهِ ٱلۡأَنۡهَـٰرُ تَجۡرِى مِن تَحۡتِىٓ‌ۖ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ (٥١) أَمۡ أَنَا۟ خَيۡرٌ۬ مِّنۡ هَـٰذَا ٱلَّذِى هُوَ مَهِينٌ۬ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ (٥٢) فَلَوۡلَآ أُلۡقِىَ عَلَيۡهِ أَسۡوِرَةٌ۬ مِّن ذَهَبٍ أَوۡ جَآءَ مَعَهُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕڪَةُ مُقۡتَرِنِينَ (٥٣)

Kwanza Ingekuwa Bora  Kufasiri Aya Tatu  kutoka katika Sura Hii na kisha kufuatia na sherehesho na kisha Muujiza wa  Kiwango Cha Uzuri  au “Golden Ratio”

Tafsiri Aya Namba 33

33.Na kama isingekuwa watu watakuwa kundi moja wote, bila shaka Tungalifanya dari za nyumba za watu wanaomkufuru Mwingi wa rehema kuwa za fedha, na ngazi wanazopandia (pia za fedha).

Tafsiri Aya Namba 35

35.Bali na Marembo (pia); lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyo kwa Mola wako ni ya wenye kumcha Mwenyezi Mungu.

Tafsiri Aya Namba 53

53· “Basi mbona hakuvishwa vikuku vya dhahabu, au kuja Malaika pamoja naye wakimuandama (wakimfuata kila mahala kama kweli Mtume)?”

Sherehe Ya Aya Hizi

Katika Aya Namba 33 Kuna Khabari za  Majengo Mazuri ambayo Dari  zake ni za fedha ambayo ni madini yenye Thamani Kubwa na pia na Hayo yote watapewa Wanaomkufuru Mwenyeezi Mungu kwani wametaka haya ya dunia tu basi watapata haya wanayoyatamani na zaidi ya hayo kama inavyoelezwa katika Aya Namba 35 kwamba Watapewa Vingine Vilivyo Na Urembo lakini watu hao ambao wanasifika kwa Ukafiri watapata haya tu katika dunia hii ya maisha mafupi lakini huko Akhera hawatapata haya tena bali adhabu kali. Na Wachamungu watapewa kila kizuri na kila cha urembo na wapapewa hayo milele hakuna mwisho kwani walimtii na kuncha Mwenyeezi Mungu. Na Aya Namba 53 Mwenyeezi Mungu anatufahamisha Kauli ya Firauni alivyowaambia watu wake kwamba Kama Nabii Musa ni Mkweli basi Mwenyeezi Mungu angempa Mabangili ya Dhahabu na Angeliandamana na Malaika kuthibitisha Utume wake.

MUUJIZA WA KIWANGO CHA DHAHABU  AU GOLDEN RATIO

Ukihesabu Herufi Za Sura Hii kuanzia Mwanzo mpaka mwisho  utapata Jumla ya herufi ni  3553

Ukichunguza zaidi utaona Namba hii 3553  inaashiria Aya Namba 35  na 53  kwani Katika Aya Namba 35  Kumetajwa neno  “MAREMBO”  au ZUKHRUF  na Neno hili ndiyo Jina La Sura Hii  Al-Zukhfuf.  Na Katika Aya Namba 53  Kumetajwa “DHAHABU”  

Hebu  Tutumie Elimu ya “Kiwango Cha Dhahabu”  au “Golden Ratio”  ambayo inatumiwa na Wataalamu katika kupimia  Uzuri. Tutumie katika Kupimia  Maneno  haya Mawili:  La kwanza “Zukhruf”  na La Pili  “Dhahabu”

Kama tulivyosema Jumla Ya Herufi za Aya Hii ni 3553.

Tukihesabu Herufi Kuanzia Mwanzo  wa Sura Ya Al-Zukhruf mpaka Neno  DHAHABU  katika Aya Namba 53  utapata Jumla Ya Herufi  ni 2196  sasa tugawe na Herufi za Sura yote . 

3553  kugawa kwa 2196=1.618   

Angalia Maajabu  ya kushangaza. Baada ya Kugawa herufi hizi tunapata Kiwango cha Namba Ya Uzuri.  Yaani Uzuri wa Dhahabu. Allahu Akbar. 

Mtu  akidai kwamba hii ni bahati nasibu tu basi tuendelee na Utafiti wa pili tuone je tunapata Kiwango hiki cha uzuri?  yaani  1.618 ?

Ikiwa Jumla ya Herufi kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Zukhruf mpaka neno  DHAHABU  ni 2196  basi  herufi  kuanzia  Baada ya neno  DHAHABU mpaka mwisho wa Sura Ya Al-Zukhruf ni  1357  (ukijuumlisha  2196 na 1357  utapata Jumla ya Herufi  ni 3553) 

Sasa tugawe  baina ya Namba 2196  (Jumla Ya Herufi za Upande wa Neno  DHAHABU)

na  1357  (Upande wa Jumla za Herufi zote Baada ya Neno  Dhahabu mpaka Mwisho wa Sura Utapata Jawabu  1.618  ambayo  ni  “Kiwango Cha Dhahabu”   Golden Ratio.

Kwa kweli hatugawi  bila mpango  bali kwa kutumia FORMULA za kitaalamu  za kutafutia Golden Ratio  ambayo inasema:     a + b/a  na pia  a/b

Huu ni uthibitisho  kwamba Kuruani haikuguswa kwa kupunguzwa au kuzidishwa  chochote (herufi, Neno, Aya, Au Nuqta). Kwani ingelikuwa hivyo basi  Mpangilio huu tusingeliupata kabisa. Ukiondoa Herufi au kuzidiasha tu basi hatupati “Golden Ratio” kama tulivyoona katika Utafiti Huu. Allahu Akbar. Angalia Muujiza wa Kuruani. Allahu Akbar.

Ili kuthibitisha zaidi Habari hii hebu tuchunguze Idadi ya Maneno kama tilivyofanya katika kuhesabu Herufi.

Tukihesabu Idadi ya Aya Kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Zukhruf Mpaka neno ZUKHRUF katika Aya Namba 35 utapata Jumla Ya Aya  ni 34  na Jumla ya Aya Kuanzia Baada ya Aya Namba 35 yenye neno  ZUKHRUF Yaani Kuanzia Aya Namba 36 mpaka mwisho wa Sura utapata jumla ya Aya ni 55  (Sura Hii Ya Al-Zukhruf ina Aya 89). Sasa Tuitumie ile Formula tulitosoma hapa Juu yaani:

a + b/a na pia a/b

a + b =  55 + 35=89 kugawa kwa  “a” ambayo ni 55=1.618 

———————————

a/b= 55 kugawa kwa 34= utapata jawabu  1.618 

——————————

Je Unaona Ya kushangaza. Tunapata tene na tena na tena KIwango cha Uzuri  au Kiwango cha Dhahabu. Baina ya maneno haya mawili katika Kuruani. (ZUKHRUF na DHAHABU) Je unaona. Allahu Akbar.

Kuruani sicho kitabu cha mchezo. Hakuna Binaadamu yeyote hata wenye  PHD’s mbalimbali za ulimwenguni au hata Maprofesa wote wenye kujigamba wana Elimu hawafikii Ufundi wowote uliopo katika Mfumo wa Kuruani. Licha  Binaadamu na hata Majini pia wote. hakuna ujanja mbele ya kuruani. 

UTABIRI WA LIFT ZA KUPANDA  KATIKA NYUMBA ZA GHOROFA

Katika Aya namba 33 tuliyoifasiri hapa juu. Tunaona Pia  Utabiri  wa Mtume  Mohamad ﷺ kama tunavyoona leo. Katika Aya hii kuna kipande kinachosema.

وَمَعَارِجَ عَلَيۡہَا يَظۡهَرُونَ  ukikichunguza utaona tafsiri yake ni Lift  za Ghorofa za Nyumba za kisasa wakati ambapo katika enzi ya Mtume Mohamad ﷺ kulikuwa hakuna Majengo ya aina hii. Sasa Mtume ﷺ

alijua vipi kama sio muujiza. Hebu  fikiri. Neno Maarij  ni  Kupanda Juu na neno hili pia limetumika katika  ISRAA  WALMIIRAJ   katika safari ya Mtume kwenda Jerusalem na kisha kupandishwa Angani. Neno  MIIRAJ  ni  Elevation. yaani Kupanda  na Neno  YADHHARUUNA  yaani Kupanda Juu ya kipandio chochote kama vile farasi, Ngamia au Merikebu na vipandio vinginevyo na katika Aya hii ina maana ya  kupanda LIFT ya Ghorofa: kupanda LIFT katika Majumba ya Kisasa. Aya hii inatuambia kwamba Makafiri watapewa kila kitu duniani kama tulivyosema katika sherehe yetu hapa juu. Enzi ya Karne ya Saba kulikuwa hakuna Magorofa yenye kutumia LIFT!!!!!

Je unaona Maajabu?  Allahu Akbar.  Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi iwapo sivyo. Ninasema huenda na sisemi ndivyo hivi. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi  iwapo nimesibu. Jambo hili linashangaza. sana.

Allahu Akbar. Mwenyeezi Mungu Mkubwa.