UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
SIASA ZA DUNIA NA SAYANSI
Alhamdulilah. Leo Tarehe 10 September 2022. Baada ya Kuandika machache katika Mlango wa “Makala ya Sayansi-3” nimeona bora nijipumzishe na kuanza kuandika Mlango huu mpya ambao kulikuwa na Habari zilizokuwa katika Fikra zangu tangu Jana na kwa kuchelea kuzisahau nimeona bora niharakishe katika Mlango huu mpya. Kuna methali inayosema “Kipya kinyemi ingawa Kidonda” kwa hiyo hebu tuanze na Mlango Mpya.
Tulisomeshwa Mashuleni kuhusu Historia ya Ukoloni.,Kwamba baada tu ya Vita kuu ya pili Duniani Mataifa Makubwa wakaa Kitako kupanga mipango ya kugawana Nchi za Dunia. Dunia nzima ikagawanywa vipande vipande, Vinyang’anyiro vikaanza, Mipaka ya Nchi za Dunia Ikachorwa. Mtawala na Mtawaliwa, Vita vya Mapaka na Mapanya. au Papa na Dagaa. Katika Utawala Utamaduni Mpya ukaja na kuenezwa na Huu ndiyo Ukoloni kwa Ufupi. Na ilikuwa Dunia Nzima. Sizungumzii hapa nchi moja bali Dunia Nzima.
Sasa Tuache Vita Vya Dunia hebu turudi Nyuma Hapo zamani sana yaani katika Karne za Nyuma kuanzia Mwaka 711 (8th Century) Uislamu ulienea huko Ulaya. Na baada ya Miaka Mingi waislamu waliishi huko Ulaya. Baadaye Ulaya walipata bahati ya Kusoma Elimu walizokuja nazo Waislamu. Pia Jambo lingine ambalo ningependelea kulitaja ni kwamba Elimu za Waislamu ziliibiwa pia na Majina yao kufutwa katika vitabu vya Historia. Huu ni ukweli. Hapa chini kuna Video ya Historia hiyo ambayo inashangaza sana. Imetengenezwa na Wajerumani. Isikilize Vizuri. Inazungumza kwa lugha ya Kijerumani lakini imefasiriwa kwa Kiingereza na Kiarabu. Wajerumani wenyewe wanasema ukweli kwamba waliiba Uvumbuzi mbali mbali za Waislamu katika Nyanja Mbalimbali. Waislamu walikuwa wamezama katika Uvumbuzi mbalimbali na walikuwa mwenge duniani. Elimu hizo chanzo au msingi ni KURUANI Tukufu. Ndugu zanguni angalia Mambo haya ya kushangaza. KURUANI ndiyo ilikuwa chanzo cha Elimu za Waislamu hawa wa Mwanzo ambao kama siyo wao basi Kusingekuwako na maendeleo tunayoyaona leo hii. Kuruani ndiyo iliyohimiza kufanya juhudi ya Utafiti wa kisayansi Duniani.
Sikiliza Video kwa Maelezo zaidi.
Hii Video imefanywa na Wajerumani wenyewe. Yaani sisi yetu masikio na macho tu. Tuangalie ili tusome Historia za Dunia.
Video-1
Video za Elimu za Waislamu na Wizi uliofanyika kuibiwa Elimu hizo. Video imefanywa na Wajerumani. Kwa lugha ya Kijerumani lakini Maandishi ya Tafsiri kwa Kiingereza na Kiarabu
Video-2
Hii Video ni Namba 1 inahusu Elimu zilizoibiwa. Waislamu waliibiwa Elimu zao. Lugha hapa ni Kijerumani na Kiarabu tu peke yake.
Video-3
Video namba 2 Ineendelea habari ya Elimu za Kiislamu zilizoibiwa. Video kwa lugha kijerumani na Kiarabu tu.