UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MFUMO/STRUCTURE YA KURUANI
Kwa kadiri tunavyosoisoma kuruani ndiyo kadiri tunavyojikuta kwamba Elimu tuzijuazo hapa Duniani ni tonye tu katika mengi ambayo hatujui. Kuruani inathibitisha kwamba Maneno yake siyo ya Kibinaadamu hata kidogo. Haya ni maneno yake Mwenyeezi Mungu mtukufu. Mwenyeezi Mungu akipenda katika Mlango huu nitagusia tonye tu katika bahari ya Elimu iliyokusanywa katika Kuruani.
Ni yale nitakayogusia unaweza pia kuhakikisha mwenyewe. kwani Hakuna kilichofichika. Allahu Akbar.
Hapa chini nitaelezea Mishangao mblai mbali:
MSHANGAO WA KWANZA
Sura ya Yasin ina herufi 2988
La kushangaza ni kwamba Sura hiyo ni ya 36 na Aya zake ni 83 na ukifanya hesabu ya Multiplication namba hizi mbili yaani 83 mara 36 basi utapata kama ifuatavyo:
83 X 36 yaani Namba ya Sura na Aya zake utapata
2988 ambazo ni idadi ya herufi ya Sura hii. Angalia Mpnagilio wa Kiajabu. Angalia Mfumo au Structure na Kuruani. Je Mtume ﷺ alikuwa akihesabu na kupanga yote haya? huoni kwamba huu ni Kamuujiza miongoni mwa Miujiza mikubwa mingineyo katika Kuruani. Hizi Hesabu zinatisha. Aliyepanga hivi ndiyo aliyeumba ulimwengu huu na Kuruani ni Hotuba yake. Haya siyo manenp ya Kibinaadamu hata kidogo.
MSHANGAO WA PILI
Huu mshangao wa pili unahusu Mwaka Ambao Mtume ﷺ na Majeshi ya Maswahaba walipoiteka Mji wa Mecca kutoka kwa Makafiri. Ilikuwa mwaka 630 Katika Miaka ya Calendar Ya Kiislamu. Yaani Mwaka 630 wa Hijria ambao ni sawa na Mwaka wa 1233 katika Calendar zetu za Ensi ya Kikristo au Gregorian Calendar.
Kwa hiyo Mwaka wa Kiislamu ni 630 H amabo sawa na Mwaka wa Kikristo wa 1233 C.E. (Christian Era).
Sasa hebu tuchunguze na tuendelee na Miujiza ya kiajabu.
Kwanza Ningependelea kuwajuulisha kwamba Waarabu na Mataifa Mengineyo ya wakati huo wa karne ya 7 yaani katika Enzi ya Mtume ﷺ walikuwa wakitumia Herufi kama Namba. Kwa Mfano
Herufi Alif iliwakilisha namba 1
Herufi Baa ilwakilisha namba 3
Herufi Jim iliwakilisha namba 3
Na hivyo hivyo Herufi Zote zilizobaki ziliwakilisha Namba kwani Wakati huo kulikuwa hakuna Namba .
Katika Enzi ya Mtume ﷺ kulikuwa hakuna hizi namba tunazotumia leo hii bali walitumia Herufi katika maisha ya kila siku.
Sasa tuchunguze Maneno Mawili yafuatayo
عام الفتح (AAM ALFATH) yaani “The Year of the Conquest” Kwa lugha za kileo ni “Siku ya Uhuru” Tukibadili maneno haya mawili katika Namba zinazowakilishwa na Herufu hapa juu utashagaa kuona kwamba unapata namba 630 na kama tilivyoona hapa kuu kwamba Namba hii 630 ndiyo siku ambayo Waislamu waliiteka Makca. Hebu tujumlishe Herufi hizi ili tuone Ushahidi:
Herufi Ya Ain inawakilishwa na namba =70
Herufi Alif inawakilishwa na namba= 1
Herufi Mim inawakilishwa na namba=40
Herufi Alif inawakilishwa na namba=1
Herufi Lam inawakilishwa na namba=30
Herufi Faa inawakilishwa na namba=80
Herufi Taa inawakilishwa na namba=400
Herufi Haa inawakilishwa na namba=8
Jumla ya Namba hizi ni =
70 +1 + 40 +1 + 30 + 80 + 400 + 8=630
Kwa hiyo inashangaza kuona Maneno Haya mawili yanatupati namba 630 ambao ni mwaka wa Kuiteka Makca.
Tukizidi utafiti utaona maajabu Mengineyo ya kushangaza. Tukigeuza Namba 630 kutoka katika Mwaka huu wa Kiislamu wa Hijriya kwenza katika Mwaka wa Kikristo utakuta Ilikuwa mwaka 1233
kwa hiyo mwaka wa kiislamu wa 630 ni sawa na mwaka wa kikristo wa Hijriya wa 1233
Mshangao mwingine ni kwamba Aya inayozungumzia Kutekwa kwa Mecca au Conguest of Mecca au Uhuru wa Mecca Ukigeuza Herufi zake basi utashagaa unapozijumlisha kwani namba utakatopata ni 1233 tulioisoma hapa juu.
Aya hiyo ni katika Sura ya Al-Fath Namba 48 Aya Ya Kwanza.
إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحً۬ا مُّبِينً۬ا
Tafsiri ya Aya ni “Tumekufunulia Mfunuo Ulio wazi” yaani Tumekupa Mfunuo wa Uhuru wa Mji wa Mecca.
Aya hii Inazungumzia Uhuru au Conquest ya Mecca. upapogeuza herufi zake katika namba na kuzijumlisha namba hizo utapata Jumla namba 1233.
Na kama tulivyyona namba hii ni mwaka wa Kikristo (Calendar ya Ardhi kuizunguka Jua) ambao unalingana na mwaka wa Kiislamu wa 630 (Calendar ya Mwezi Kuizunguka Ardhi) wa Uhuru au Kutekwa kwa Mecca. Unaona Maajabu wa Namba zinavyozungumza? Je unaonaje haya Maneno ya Kuruani? Ninavyoona haya siyo maneno ya kawaida. Ikiwa mfumo wa Maandishi tu unatushangaza sasa je Maana ya Aya hizi? Kila kitu kinatushangaza, Mpangilio wake, Herufi zake, Maneno yake, Maana Yake na mengineyo tunayoyajua na tusiyoyajua. Allahu Akbar. Allahu Akbar.,
MSHANGAO WA TATU
Tuendelee na safari yetu ya Mshangao wa Tatu.
Kuruani haina mwisho. Itakuwaje na mwisho na Haya ni maneno ya Mwenyeezi Mungu aliyeumba kula kitu. Amesema mwenyewe katika kuruani kwamba Bahari zinegkuwa Wino na Miti kalamu basi Wino ungekisha lakini maneno yake hayataisha. Je huoni Maajabu.
Hebu tuchunguze Sura Ya Al-Naml namba 27. Tuchunguze Neno “KURUANI” ambalo ni la pekee katika Ukurasa huo namba 383 na lipo katika Aya namba 76.
Jambo linalonishangaza sana ni kwamba Neno “KURUANI” yaani الْقُرْءَانَ ukiligeuza Herufi za neno hili katika namba za Hesabu kama tulivyofanya katika Mshangao Namba 2 hapa juu basi utachagaa kuona Kwamba Jumla ya Herufi ni namba 383 na namba hii ndiyo namba ya Ukurasa huo.
Alif=1
Lam=30
Qaf=100
Raa=200
Hamzah=1
Alif=1
Nun=50
1 + 30 + 100 +200 + 1 + 1 + 50=383
Je unaona Maajabu. Baada ya Kujumlisha Namba zilizotumika hapo zamani ambazo zilikuwa zikiwakilishwa na Herufi tunapata Namba 383 ambayo ni Jumla ya Herufi za neno الْقُرْءَانَ Yaani “KURUANI”.
na namba hii ni Namba ya Kurasa ambayo Lipo neno hilo KURUANI katika Aya Namba 76.
Sasa linalojitokeza na kutushangaza zaidi ni kwamba namba 383 ni Prime Number namba 76, Je unaona Maajabu. Katika Elimu ya Hesabu Kuna Prime na Common Numbers. Na Namba 383 ni Prime Number ya 76 yaani ukihesabu Prime Numbers zote kuanzia ya kwanza mpaka ya 76 utapata namba 383. Je onaona ya maajabu. Na 76 ni Aya ambayo ina neno الْقُرْءَانَ “KURUANI”.
Hebu tuchunguze zaidi. Hebu tuhesabu Herufi kuanzia mwanzo wa Ukurasa huu mpaka mwisho wa neno KURUANI na kisha Tuhesabu MANENO kuanzia mwanzo wa Ukurasa huu mpaka Mwisho wa neno “KURUAN” katika Aya Namba 76.
Tukifanya hivyo tutapata mengine ya kushangaza.
Jumla ya Maneno kuanzia mwanzo wa ukurasa huu maka neno KURUANI ni 133
Na Jumla ya herufi kuanzia mwanzo wa Ukurasa huu mpaka mwisho wa Neno KURUANI ni 516
Hebu tutoe Maneno katika Herufi yaani tutoe namba 133 kutoka katika namba 133
516-133= 383 Angalia Mshangao wa kiajabu. tukifanya hivyo tunapata Thamani ya Neno “KURUANI” tuliyoizungumzia hapa juu na Pia Namba ya Ukurasa ambao ni 383. Angalia Maajabu. Ndugu Zanguni Waislamu. Mnaona Maajabu. Haya siyo maneno ya Kibinaadamu hata kidogo. Nakuhakikishia kwa Asilikia 100 yaani 100% kwamba Haya ni maneno ya MUUMBA. Allahu Akbar. Angalia Mpangilio wa Kimuujiza usio na Mwisho. Na bado tupo Mwanzoni. Kuruani imejaa tusiyoyajua. Kuna SIri kubwa kubwa za Maajabu Makubwa. Kuruani ni Ya Binaadamu na Majini pia. Allahu Akbar. Tumche Mungu. Je huoni haya tunayozungumza. Je huogopi?
MSHANGAO WA NNE
Tuendelee na Mshangao wa Nne. Kwa kweli inashangaza sana.
Sura Ya Al-Naml Namba 27 Aya namba 6
وانك لتلقي القران من لدن حكيم عليم
Mwenyeezi Mungu anamwambia Mtume ﷺ kwamba
“Kwa hakika umepewa au umefundishwa kuruani kutoka kwa mwenye Hekima na Elimu”
Sherehe ya Aya hii ni kwamba Mtume ﷺ ameipokea kuruani kutoka kwa Mola mwenye Hekima na Elimu Kubwa.
Hebu Tuifanyie Utafiti Aya hii.
Neno لتلقي yaani Umepokea au Kufundishwa. Neno hili ni la pekee katika Kuruani Yote. Limetumika mara moja tu katika Aya hii.
Neno hili ni la 40 ukihesabu maneno kuanzia mwanzo wa Sura hii mpaka mwisho wa nenp hili. Je unaona ya maajabu. Mtume ﷺ alipewa WAHYI au Revalation au Ufunuo wa kwanza alipokuwa na umri wa miaka 40.
Je unaona ya kushagaza. Hebu tuendelee kuchambua ndugu waislamu hatujamaliza na hatutamaliza kwamwe. Miujiza isiyo na mwisho. Hebu tusonge mbele.
Hebu tujumlishe Namba Ya Sura na Namba ya Aya na Idadi ya Maneno ya Aya hii namba 6
Yaani Namba ya Sura ni 27
Aya namba 6
Jumla ya Idadi ya Maneno ya Aya hii ni 7
27 + 6 + 7=40
Unaona Maajabu. Tunapata tena Umri aliokuwa nao Mtume ﷺ alipopokea Wahyi kwa mara ya Kwanza yaani alipokluwa katika Pango la HIRA na mara ya kwanza alipokutana na Malaika JIBRIL. Je unaona Mara ya pili tunapata Unri wa Mtume ﷺ Allahu Akbar.
Bado hatujamaliza Hebu tuchunguze zaidi ili tuone ya kushangaza.
Neno لتلقي ambalo tumeshalielezea hapa juu tukiligeuza katika namba. yaani kutumia namba za herufi kama tulivyoelezea katika maelezo ya mishangao mingine hapa juu utapata namba ya kushangaza zaidi.
hebu tufanye hivyo.
Herufi Lam=30
Herufi Taa=400
Herufi Lam-30
Herufi Qaf=100
Herufi Yaa=10
Tujumlishe Namba za herufi hizi
30 + 400 + 30 + 100 + 10=570
Ajabu Kubwa. Namba 570 ni Mwaka aliozaliwa Mtume Mohamad. ﷺ Je unaona maajabu. Yaani Mwaka aliozaliwa Mtume ni sawa na thamani ya Herufi za neno hili la LATULAQAA yaani Kupokea au Kufundishwa. Haya siyo mambo madogo. Ni Miashirio ya kiajabu kiajabu. Ni miashirio ya kushangaza. Hebu fikiri. Allahu Akbar.