UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
TIBA KWA AYA ZA KURUANI TUKUFU
SHOKA LA MAISHA
Matibabu kwa Aya Za Kuruani ni Silaha ya Kwanza katika kuifadhi Nafsi, Mali, Afya, Watoto, Na Kila kinachokuhusu au kumiliki katika Maisha.
Maisha ya Binaadamu yanahitaji Usalama na huu ni Ukweli.
Kuna Aya na Hadithi za Mtume ambazo zinathibitisha Tiba kwa kutumia ya Aya za kuruani.
Kuruani imejaa Tiba mbalimbali.
Kwa Mfano hadithi ifuatayo kutoka katika Sahih Al-Bukhari Namba 3275 inathibitisha faida ya Dua za Aya kutoka katika Kuruani Tukufu.
Hadithi Ya Mtume Mohamad ﷺ inasema kwamba
وَقَالَ عُثْمَانُ بْنُ الْهَيْثَمِ حَدَّثَنَا عَوْفٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ وَكَّلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِحِفْظِ زَكَاةِ رَمَضَانَ، فَأَتَانِي آتٍ، فَجَعَلَ يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ، فَأَخَذْتُهُ فَقُلْتُ لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم. فَذَكَرَ الْحَدِيثَ فَقَالَ إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَةَ الْكُرْسِيِّ لَنْ يَزَالَ عَلَيْكَ مِنَ اللَّهِ حَافِظٌ، وَلاَ يَقْرَبُكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم “ صَدَقَكَ وَهْوَ كَذُوبٌ، ذَاكَ شَيْطَانٌ ”.
TAFSIRI
Abu Huraira Alisema, Mtume Wa Mwenyeezi Mungu ﷺ Alinipa Jukumu la kusimamia Zakati za Mwezi wa ramadhan (Zakat-Ul-Fitr). Kuna mtu ambaye alikuja na kuanza kuchukua chakula hicho kwa mikono yake miwili (bila ya Idhini au ruhusa) basi nikamkamata na kumwambia kwamba nitampeleka kwa Mtume wa mwenyeezi Mungu ﷺ . Baada ya hapo Abu Hurayra akaendelea kuelezea Kisa hicho na akaongezea kwa kusema kwamba Mtu huyo (mwizi) akamjibu kwamba “Unapoenda kulala soma Aya ya Kursiy na Mlinzi wa Mwenyeezi Mungu atakulinda na Shetani hawezi kukusogelea mpaka Alfajiri. Na kuhusu habari hii Mtume ﷺ akasema kwamba “Mtu huyo alisema ukweli ijapokuwa ni muongo, na huyo ni Shetani.
ENGLISH TRANSLATION
Narrated Muhammad bin Sirin: Abu Huraira said, “Allah’s Messenger (ﷺ) put me in charge of the Zakat of Ramadan (i.e. Zakat-ul-Fitr). Someone came to me and started scooping some of the foodstuff of (Zakat) with both hands. I caught him and told him that I would take him to Allah’s Messenger (ﷺ).” Then Abu Huraira told the whole narration and added “He (i.e. the thief) said, ‘Whenever you go to your bed, recite the Verse of “Al-Kursi” (2.255) for then a guardian from Allah will be guarding you, and Satan will not approach you till dawn.’ ” On that the Prophet (ﷺ) said, “He told you the truth, though he is a liar, and he (the thief) himself was the Satan.“
Katika Mlango huu Nitaanza kwa Kuorodhesha baadhi tu za nasiha zilizotolewa na Sheikh kutoka Syria na Nadhani hivi sasa anaishi Egypt. kwa kadiri mwenyeezi Mungu atakavyojaalia. Ikiwezekana tusome kwa pamoja Aya zifuatazo na Mwenyeezi Mungu akipenda Aya hizi zitatupa faida kubwa. Sheikh alisisitiza kwa Uhakika kwamba Aya hizi zimeisha fanyiwa majaribio na faida zilipatikana. Na Baada ya Aya hizi Mwenyeezi Mungu akipenda nitakuwa nikiorodhesha Aya Nyinginezo za Mashekhe mbalimbali ambazo ni Tiba katika Mazingara mbalimbali ya maisha.
DUA ZA KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI
KATIKA KUTIBU NA KUTATUA MATATIZO MBALIMBALI.
Aya chache zifuatazo ingelikuwa bora uzihifadhi lakini kama huwezi kwa sababu ya lugha basi utumie Tafsiri ya kiswahili hapa chini au Tafsiri kwa lugha yeyote ile lakini kwa maana iliyo sahihi bila kubadilisha. Na Inshaallah mwenyeezi Mungu atatakabali maadam nia yako ni safi.
1/Sura Ya Al-Fatiha (Mara Saba Asubuhi na Mara Saba Usiku)
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١) ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢) ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣) مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤) إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥) ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦) صِرَٲطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ (٧)
TAFSIRI
1.Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
2.Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote
3.Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo
4·Mwenye kumiliki siku ya malipo.
5.Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada.
6.Tuongoze njia iliyonyoka.
7. Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale) waliokasirikiwa, wala (ya) wale waliopotea.
2/Aya Ya Al-Kursiy Sura ya Al-Balkarah Namba 2 Aya Namba 255 (Mara Moja Asubuhi na Mara Moja Usiku)
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُۚ لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬ۚ لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِۗ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَۚ وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَاۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ (٢٥٥)
TAFSIRI
l.Mwenyezi Mungu hakuna mola ila Yeye,(na) ndiye Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kilajambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni Vyake(peke yake vyote) vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi. Na nani huyo awezaye kuombea mbele Yake (Mungu) bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yaliyo) nyuma yao; wala(hao viumbe) hawajui chochote katika (yaliyo katika)ilimu Yake (Mwenyezi Mungu) ila kwa alipendalo(Mwenyewe). Enzi yake imeenea mbingu na ardhi;wala kuvilinda hivyo hakumshindi; na Yeye (pekeyake) ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu
3/Sura Ya Al-Bakarah Namba 2 Kipande cha Aya Namba 102. (Mara Saba Asubuhi na Mara saba Usiku)
وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنۡ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ
TAFSIRI
Wala hawakuwa wenye kumdhuru yo yote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
4/Kipande cha Aya kinachomhusu Nabii Musa. Sura Ya Yunus Namba 10 Aya Namba 81 (Mara Saba Asubuhi na Mara Saba Usiku)
مَا جِئۡتُم بِهِ ٱلسِّحۡرُۖ إِنَّ ٱللَّهَ سَيُبۡطِلُهُ
TAFSIRI
Musa alisema: “Mliyoleta ni Uchawi; Mwenyezi Mungu sasa hivi ataubatilisha.
5/Sura Namba 23 Aya namba 97 na 98 (Mara Saba Asubuhi na Mara saba Usiku_
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنۡ هَمَزَٲتِ ٱلشَّيَـٰطِينِ (٩٧) وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحۡضُرُونِ (٩٨)
TAFSIRI
91.Na sema: “Mola wangu! Najikinga kwako (Uniepushe) na wasiwasi wa mashetani” 98.”Na najikinga kwako, Mola wangu, ili wasinihudhurie.”
6/Sura Namba 112 (Mara Tatu Asubuhi Na Mara Tatu Usiku)
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ
TAFSIRI
1.Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja(tu).
2.Mwenyezi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe Vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea).
3.Hakuzaa wala Hakuzaliwa
4·Wala hana anayefanana Naye hata mmoja.
7/Sura Namba 113 (Mara Moja Asubuhi na Mara Moja Usiku)
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢) وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ (٣) وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥)
TAFSIRI
1.Sema “Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote”
2.Na shari ya Alivyoviumba
3.Na shari ya giza Ia usiku liingiapo
4·Na shari ya wale wanaopulizia mafundoni,(wakavunja mashikamano yaliyo baina ya watu)
5·Na shari ya hasidi anapohusudu.
8/Sura Namba 114 (Mara Moja Asubuhi na Mara Moja Usiku)
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (١) مَلِكِ النَّاسِ (٢) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (٣) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (٤) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (٥) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (٦)
TAFSIRI
1.Sema “Ninajikinga kwa bwana mwenye kuwalea”
2.Mfalme wa watu
3.Muabudiwa wa watu
4.Na shari ya mwenye kutia wasiwasi aliyejificha
5.Atiaye wasiwasi nyoyoni mwa watu
6.(Ambaye ni) katika maijini na watu
DUA ZA KURUANI
Dua iliyo nzuri sana ni ile aliyotufundisha Mwenyeezi Mungu katika maneno yake matukufu aliyotuletea Mtume Mohamad ambayo ni Kuruani Tukufu. Kuruani Tukufu imekusanya dua ambazo tukizifuatilia na kuzifahamu tutapata manufaa makubwa sana. Na ingependeza sana tukizifahamu dua hizo ili tunapoomba tuelewe tunaomba kitu gani. Pia kuna masharti ya kufuata ili dua zetu zikubaliwe.
Dua ya kwanza ambayo kubwa sana ni SURA YA AL-HAMDU ambayo pia inajulikana kwa majina na sifa mbalimbali. Kuhusiana na Dua tunaweza kuigawa Sura hii katika sehemu mbili;
Sehemu ya kwanza Inahusiana na kumtukuza Mwenyeezi Mungu na sehemu ya pili ni Dua.
Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu anatufundisha namna ya kuomba dua. kwanza tumtukuze kama ipasavyo na kisha tumuombe.
Tukumbuke kwamba tunayemuomba ndiye aliyetuumba na ndiye aliyeumba mbingu na ardhi na kila kitu katika ulimwengu au malimwengu yote.
Kama tukifuata masharti yote basi matakwa yetu yote yatakubaliwa, shida zetu zote zitatatuliwa, Mitihani duniani itakuwa rahisi kwetu, Makaburini itakuwa salama kwetu na Siku ya kiyama huko akhera itakuwa salama kwetu na pia mwisho mwema katika kila jambo.
Sura hii imepewa majina mengi mbalimbali. Tutachagua baadhi tu ya hayo ambayo yatatusaidia kufahamu zaidi maelekezo ya sura hii.
AL-FATIHA فاتحة الكتاب (UFUNGUZI WA KURUANI TUKUFU)-The opining of the book
AL-QURAN AL’ADHIIM القرآن العظيم (KURUANI TUKUFU)-The Glorious Qur’an.
SURATU AL-HAMD سورة الحمد (SURA YA KUMSIFU MOLA)-Praise of Almighty Allah.
AL-WAFIYA الوافية (ILIYOKAMILIKA NA IMEKUSANYA MAANA YA KURUANI YOTE)-The Comprehensive
AL-KAFIYA الكافية (IMEJITOSHELEZA KATIKA SALA IKIWA HUWEZI KUSOMA SURA NYINGINE BASI INATOSHA KATIKA RAAA ZOTE)-The Sufficient.
UMMULKITAAB / UMMULQURAAN أمُّ الكتاب وأمّ القرآن (MAMA YA KURUANI AU MAMA YA KITABU CHA KURUANI KWANI NI MUHTASARI WA MAFUNDISHO YOTE YA KURUANI)-Mother of the Book and Mother of the Quran.
ASWALAAT الصّلاة (SWALA)-Prayer.
ASHIFAA الشفاء (MATIBABU YA MARADHI MBALIMBALI)-CURE
ASABAALMATHANIY السبع المثاني (AYA SABA ZILIZOKARIRI)
SURA YA DUAA دعاء (SURA YA DUAA). Chapter of Supplication
Kufuatana na majina tuliyoyataja tunaweza kufahamu umuhimu wa sura hii na faida zake.
سُوۡرَةُ الفَاتِحَة
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١)
ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢) ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣) مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤) إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥) ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦) صِرَٲطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ (٧)
Sura hii ina aya saba . Aya tano za mwanzo zinamsifu Mwenyeezi Mungu na Aya Mbili za mwisho ni Dua. Kama tulivyoona Majina ya sura hii yanhusiana na mambo mablimbali kwa mfano mojawapo ya mabo hayo ni Matibabu na ndiyo maana ikaitwa SHIFAA yaani Matibabu na ikaitwa DUA kwa maana kwamba inaweza kutumika katika Dua.
Unapopata shida yeyote katika maisha yako basi soma sura hii kiasi ya kadiri yako yaani kiasi cha uwezo wako, kama huwelewi kuruani basi soma tafsiri yake kwa lugha yeyote na mwenyeezi mungu atakufahamu. Mwenyeezi Mungu ameumba lugha mbalimbali na lugha yeyote unaweza kuitumia katika dua zako kwa hiyo usijilazimishe mpaka ikafikia ukaacha kila kitu.
Ukiniuliza namna ninavyoomba mimi basi mitakuelezea muono wangu ambao siyo lazima ufuate bali ninavyopenda mimi ni kusoma sura hii mara saba katika maombi yeyote ninayotaka. Yaani ninapotaka kuomba mwenyeezi mungu basi husoma sura hii mara saba. Kwa nini nimechagua namba saba na siyo nyingine, jawabu ni kwamba Nimechagu namba hii kwani Kufuatana na utafiti mbalimbali uliofanyika na wataalamu mbalimbali nimesoma umuhimu wa namba hii kwa mfano Hija wanazungukia jengo la Meccca mara saba, Safwa na Marwa wanazunguka mara saba, Kutupia vijiwe mshetani mara saba, mbingu imeumbwa katika matabaka saba na ardhi pia hivyo hivyo, maumbile yetu katika tumbo la mama yamepitia stages au mapitio saba, mwanga wa jua umeumbwa kutokana na rangi saba, viungio tunavyotumia katika sala ni saba (paji la uso, viganja ya mikono miwili, magoti mawili na miguu miwili) kwa hiyo ukichunguza utaona mwenyeezi mungu ameipa namba hii umuhimu sana pia katika kuruani kuna utafiti mbali mbali unaohusiana na namba hii Nimeelezea katika website hii baadhi ya utafiti huo unaohusiana na namba saba. Kama nilivyosema idadi ya kusoma hakuna ulazima wowote ufuate namba saba bali ni njia yangu ninayoifanya ninapotaka kuomba na siyo wajibu ufuate. Ukisoma zaidi ya mara saba ni vizuri zaidi na hata mara moja pia ni vizuri. uchaguzi ni wako. Tumepewa uhuru katika uchaguzi huu.
TAFSIRI YA SURA YA AL-FATIHA
SWAHILI
1.Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
2.Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote
3.Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo
4·Mwenye kumiliki siku ya malipo.
6.Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada.
7.Tuongoze njia iliyonyoka. Njia . ya wale uliowaneemesha; siyo (ya
wale) waliokasirikiwa, wala (ya) wale waliopotea.
ENGLISH
1/In the name of Allah , the Entirely Merciful, the Especially Merciful.
2/ [All] praise is [due] to Allah , Lord of the worlds
3/The Entirely Merciful, the Especially Merciful,
4/Master of the Day of Judgment.
5/It is You we worship and You we ask for help.
6/Guide us to the straight path
7/The path of those upon whom You have bestowed favor, not of those who have evoked [Your] anger or of those who are astray.
MAONI YANGU KATIKA TAFSIRI YA SURA YA AL-FATIHA
Aya namba tano na sita ni Dua. Kwa hiyo baada ya kumtukuza mwenyeezi mungu na kumsifu katika aya nne za mwanzo kama alivyotaka mwenyeezi mungu mtukufu na ndiyo baada yake mwenyeezi mungu anatufunsdisha tumuombe. kwa hiyo ni vizuri na adabu kubwa kwanza kumsifu na kumtukuza mola wako kama alivyotaka na kisha kumuomba haja zako zozote zile. Kwa hiyo kwanza ni kumtukuza aliyekuumba na baadaye tumuombe matakwa yetu.
Katika Aya ya nne tunamuomba atuongoze katika njia iliyonyooka. Hapa maana yake ni kubwa sana. Njia iliyonyooka ambayo haina matatizo, njia iliyonyooka duniani ambayo haina shida au balaa yeyote. Njia ya usalama. Usalama katika kila kitu. Shida za dunia, Mitihani mikubwa na midogo. Misukosuko katika maisha. Matatizo ya kimaisha yanayotokana na shida za kila siku, maradhi yanayosababishwa na kila kitu. Maradhi yanayotokana na mashetani ambao wamemwahidi mwenyeezi mungu kwamba watafanya juhudi sana kuwapotea viumbe na kuwasababishia njaa na khofu na mengineyo ya hatari. Kwa hiyo usalama hapa ni neno kubwa sana. kila mtu anapenda usalama wake na familia yake. hakuna mtu anapenda shida za dunia kama vile ufakiri, mauaji, na mengineyo yote. kwa hiyo aya hii ina maana kubwa sana tena sana na ndiyo maana sura hii ikajulikana kama mama ya kuruani. Njia iliyonyooka ambayo amewapa neema wale waliofanikiwa katika kumtii mwenyeezi mungu. Neema za kheri na baraka katika maisha yetu na familia zetu. Riziki zilizobarikiwa ambazo zinazalisha afya nzuri. Neema katika mapato. Neema katika usalama. Neema katika maisha yetu tuishi bila matatizo na kutuepushia shari zinazotokana na viumbe vinginevyo alivyoviumba, viumbe tunavyovijua na tusivyovijua.
Ukisoma sura hii asubihi na usiku kabla ya kulala kwa maoni yangu itakuwa vizuri sana kwani mchana na usiku utakuwa katika usalama.
Na pia dua hii tunatumia katika sala mara tano kila siku ambayo pia inatosha lakini unaweza kuongeza asubuhi na usiku kwa nia ya dua peke yake na hasa pale unashida yeyote basi tumia kama dawa.
NYONGEZA KATIKA SURA YA AL-FATIHA
MLANGO UNAENDELEA
بسم الله الرحمن الرحيم
الحمد لله رب العلمين
الرحمن الرحيم
ملك يوم الدين
اياك نعبد واياك نستعين
اهدنا الصرط المستقيم
صرط الذين انعمت عليهم غير المغضوب عليهم ولا الضالين
Kuanziamwanzo wa sura hii mpaka kipande cha aya kinachosema
صرط الذين انعمت عليهم Kuna jumala ya herufi 114. Je unaona muashirio wa Sura za Kuruani ambazo jumla yake ni 114? Kuruani imekusanya Sura 114 kwa hekima kubwa sana. Kuruani ni Neema Kubwa sana tena sana. Sura hii imeanzz na Rehema na Sifa za mwenyeezi mungu mtukufu. Yaani kuanzia mwanzo wa sura hii mpaka kipande hiki ni Sifa na neema na mazuri peke yake. Na kwa hiyo kuruani yenye sura 114 ambazo ni neema inawiana na Aya hizo zinazohusu mazuri peke yake. Lakini kile kipande cha mwisho kinachosema غير المغضوب عليهم ولا الضالين Kina sifa mbaya na kwa hiyo hawa walio na sifa mbaya hawatafaidika na hizo sura 114 za kuruani na huenda ndiyo maana herufi hizo 114 zimeishia katika Aya za sura hii ambazo zinazungumzia sifa nzuri tupu. Je unaona Maajabu?
Jambo la pili katika Sura hii ni Dua kubwa ya Kumuomba Mwenyeezi Mungu uongofu. Jambo la kushangaza ni kwamba uongofu huo Mwenyeezi Mungu anatoa jibu lake katika Mwanzo tu wa Sura inyofuata.
ذلك الكتب لا ريب فيه هدي للمتقين
Mwenyeezi Mungu anasema katika Aya hii (Kitabu hicho hakina shaka yeyote kuna uongofu kwa wacha Mungu) KItabu kinachozungumzia hapa na Kuruani tukufu. Katika Sura ya Al-Fatiha tunaomba Uongofu na Baada ya hapo tunapata jibu katika Aya ya pili ya Sura Ya Al-Baqarah. Kwamba Uongofu mnaouomba upo katika Kuruani tukufu basi mfuate. Kuruani ina maajabu makubwa. Tunaona uhusiano baina ya Sura ya Al-Fatiha na Mwanzo wa Sura ya Al-Bakarah. Uongofu ni Ujumbe aliokuja nao Mtume Mohamad basi tuufuate. Dua peke yake haitoshi bali vitendo pia. Na Nasiha nzuri ni ile aliyoitoa Imamu Shafii aliposema kwamba. “Mkitaka uongofu basi mfuate kwa vitendo na je uliona Merikebu ikatembea ardhini?” Yaani Meli ina njia yake na uongofu pia una njia yake. Nadhani imeeleweka.
Sura ya A-lFatiha Ina Aya 7 na ajabu kubwa ni Kwamba katika Herufi 28 za Lugha ya Kiarabu kuna herufi 7 ambazo hazikutumika katika Sura hii!!! Mbona Inshangaza. Sura hii imembatana na Siri kubwa sana. Na Namba 7 ambayo nimeielezea kwingineko katika miujiza ya Mtandao (Website) hii. Namba ya ajabu. Kwa nini herufi hizi hazikutumiwa katika kujenga Sura hii yenye Aya 7? Kwanza kabla ya kuelezea Jawabu ningependelea kudokeza kwamba Kushuka kwa sura hii ni Muujiza mwingine wa kushagaza. Hadithi ifuatayo inahusiana na Muujiza huu.
-وعن ابن عباس رضي الله عنهما قال: بينما جبريل عليه السلام قاعد عند النبي ﷺ سمع نقيضًا من فوقه، فرفع رأسه فقال: “هذا باب من السماء فتح اليوم ولم يفتح قط إلا اليوم، فنزل منه ملك فقال: هذا ملك نزل إلى الأرض لم ينزل قط إلا اليوم، فسلم وقال: أبشر بنورين أوتيتهما، لم يؤتهما نبي قبلك: فاتحة الكتاب، وخواتيم سورة البقرة، لن تقرأ بحرف منها إلا أعطيته” ((رواه مسلم)). النقيض: الصوت.
This hadith explains the importance of Surat Al-Fatihah and the concluding Ayat of Surat Al-Baqarah, which were given to Prophet Muhammad (ﷺ) as two special lights that no other prophet was given before.
Ibn ‘Abbas (May Allah be pleased with them) reported: While Jibril (Gabriel) was sitting with the Messenger of Allah ﷺ, he heard a sound above him. He lifted his head, and said: “This is a gate which has been opened in heaven today. It was never opened before”. Then an angel descended through it, he said: “This is an angel who has come down to earth. He never came down before”. He sent greetings and said: “Rejoice with two lights given to you. Such lights were not given to any Prophet before you. These (lights) are: Fatihah-til-Kitab (Surat Al-Fatihah), and the concluding Ayat of Surat Al-Baqarah. You will never recite a word from them without being given the blessings it contain s”. Muslim.
Tafsiri kwa Kiswahili
Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa: “Jibril (Jibril) alipokuwa amekaa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alisikia sauti juu yake. Akainua kichwa chake, na kusema: “Huu ni mlango ambao umefunguliwa mbinguni leo. Haujawahi kufunguliwa kabla”. Kisha Malaika akashuka kupitia humo, akasema: “Huyu ni Malaika aliyeshuka duniani. Hajawahi kushuka kabla”. Akatuma salamu na kusema: “Furahini kwa nuru mbili ulizopewa. Nuru hizo hakupewa Nabii yeyote kabla yenu. Hizi (nuru) ni: Fatiha-til-Kitab (Surat Al-Fatihah), na Aya ya mwisho ya Suratu. Al-Baqarah”. Hutasoma neno lolote ila utabarikiwa nalo(Neno lolote utakalolisoma katika Sura na Aya hizi basi utabarikiwa) SAHIH MUSLIM
Sasa tuzungumzie zile herufi 7 ambazo hazikutajwa katika Sura hii. Wanvyuoni waliopewa fikra wamejitahidi kutupa undani kwa nini hazikutajwa katika Sura Hii. Wakasema kwamba hazikutajwa kimakusudi na kwa hekima kubwa ka sababu herufi hizo zimeambatana na Adhabu ya Moto wa Jahannam (Kiyama). Hebu tuzielezelee and Kuzichambua. Mwenyeezi mungu anajua zaidi lakini juhudi zao huenda zimelenga sababu inayokubalika.
HERUFI 7 AMBAZO HAZIKUTUMIKA KIHEKIMA KATIKA SURA YA AL-FATIHA NA SABABU YA KUTOKUTUMIWA
Wanasema wanavyuoni hao kwamba Sura ya Al-Fatiha ni sura yenye sifa za Rehema na Herufu hizo zimeambatana na sifa za adhabu kubwa sana za Jahannam (Moto) na ndiyo maana hazikutumiwa.
ظ ف ث ش ز خ ج
Seven letters do not occur in al-Fatiha.
They are the thā’ of al-thubūr (destruction),
the jīm of al-jahīm (Hellfire),
the khā’ of al-khawf (fear),
the zāy of al-zaqqūm (the tree of bitter fruit in Hell),
the shīn of al-Shaqāwa (misfortune) ,
the zā’ of al-Zulma (darkness)and the
fā’ of al-firāq (separation)
Herufi Ya SHIN na ZA ش ز Mwenyeezi Mungu Amezitumia Herufi hizi katika Maneno Mawili ya Aya ifuatayo (ZAFIR na SHAHIYQ)-Makelele na Kwikwi ya hali ya Juu. Maneno haya yanahusu Vilio vikubwa huko Motoni. Angalia Tafsiri hapa chini.
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُواْ فَفِى ٱلنَّارِ لَهُمۡ فِيہَا زَفِيرٌ۬ وَشَهِيقٌ (١٠٦)
Ama wale wenyc hali mbaya (kwa sababu ya kufanya kwao mabaya), wao watakuwa Motoni humo wawe wanapiga makclcle (ya kama milio ya_
punda) na kutoa kwikwi
Those who are wretched shall be in the Fire: There will be for them therein (nothing but) the heaving of sighs and sobs:
Herufi Ya JIYM ج Katika neno JAHANNAM-Moto Wa Kiyama Aya Ifuatayo
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادً۬ا (٢١)
Truly Hell is as a place of ambush,
Na kwa hakika Jahannamu Inawangoja Wabaya
Ijapokuwa Herufi ya JIYM imetumika katika Pepo pia JANNAH lakini wanvyosema ni kwamba Maadamu imetumika katika Moto Pia basi haikutumika katika Sura hii.
Herufi Ya FA ف Katika Neno YATAFARRAQUWN- Watatengana
وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَتَفَرَّقُونَ (١٤)
And the Day the Hour appears – that Day they will become separated
Na siku kitakapotokea Kiama, siku hiyo watafarikiana (viumbe; hawa wende Peponi na hawa wende Motoni).
Herufi Ya KHA خ Katika Neno KHIZY – Fedheha
ثُمَّ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ يُخۡزِيهِمۡ وَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَڪَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تُشَـٰٓقُّونَ فِيہِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ إِنَّ ٱلۡخِزۡىَ ٱلۡيَوۡمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلۡڪَـٰفِرِينَ (٢٧)
Then on the Day of Resurrection He will disgrace them and say, “Where are My ‘partners’ for whom you used to oppose [the believers]?” Those who were given knowledge will say, “Indeed disgrace, this Day, and evil are upon the disbelievers” –
Kisha siku ya Kiama atawafedhehesha na atasema:”Wako wapi wale mliokuwa
mkiwashirikisha na mimi ambao kwa ajili yao mlikuwa mkigombana (na Manabii)?” Watasema wale waliopewa ilimu: “Hakika fedheha na msiba leo utawafika makafiri “
——————————————————————
FUNGUO ZA RIZIKI NA MENGINEYO MAZURI
DUA KUBWA ALIYOBASHIRIWA MTUME (Sala na Amani za Mola Zimfikie) PAMOJA NA SURA YA AL-FATIHA. (AYA HIZI NI FUNGUO ZA RIZIKI) KWA UWEZO WAKE MWENYEEZI MUNGU TUMIA FUNGUO HII UJIONEEE MAAJABU. INSHAALLAH RIZIKI ILIYOBARIKIWA BILA KUKATIKA. TUNALIA DHIKI ZA MAISHA KILA SIKU LAKINI TUNASAHAU KUNA FUNGUO (DAWA) ZAKE.
Malaika alikuja na kumbashiria mtume kuhusu Aya hizi mbili na pia sura ya Al-Fatiha. Soma Hadithi hapa juu katika Sura Ya Al-Fatiha
Hizi Aya Mbili kutoka katika Mwishoni mwa Sura Ya Pili inayojulikana kama Al-Baqarah Aya namba 285 na 286 zimetajwa katika hadithi sahihi iliyopokelewa kuhusu Malaika Aliyembashiria Mtume (Sala na Amani za Mola Zimfikie) kwamba Aya hizi na Sura ya Al-Fatiha ni Nuru Mbili. Ukisoma Aya mbili utaona ni Dua Kubwa sana na Hivo hivyo kama tulivyoelezea hapa juu kuhusu sura ya Al-Fatiha. Aya Mbili hapa chini zinahusu Kumuomba Mwenyeezi Mungu Msamaha (Maghfira) kwa Madhambi yetu yanayotokana na sisi Binaadamu. Ukisoma Aya hizi kila siku asubuhi na usiku inakuwa vizuri sana. Sura Ya Al-Fatiha ni dua ya kuomba Uongofu na Aya hizi zinahusu mambo mbalimbali kama vile Imani na Kumtii Mola na pia Maghfira. Lazima tuelewe kwamba Kuomba Maghfira ni njia mojawapo wa kuzidisha Riziki. Ukiwa una dhiki ya kimaisha basi Dua ya Maghfira ni nzuri sana na Hizi Aya mbili ni mojawapo wa Aya mbali mbali katika Kuruani ambazo ni dua ya kuomba maghfira. Ukiniuliza usia basi usia wangu usome Aya hizi kila siku katika maisha yako kwani kuna faida kubwa.KIsa Kinachofuata Cha Imamu Abu Hanifa ambaye alikuwa imamu wa FIQH miongoni mwa Imamu Wanne wa SUNNI. Kisa hiki nimekinukulu kwa kiingereza na Inshaallah Nitakifasiri kwa Kiswahili nikipata nafasi.
The Curious Story of the Imam and the Baker: Dhikr, Hospitality, and Humility
During his old age, Imam Ahmad bin Hanbal, the renowned scholar of Islam and a famous theologian, was travelling when he stopped by a town. After salah, he wanted to stay for the night in the mosque. Out of humility, he didn’t introduce himself to anyone – he did not want the recognition and adulation that would come with people knowing he was a ‘renowned scholar’. Bearing in mind, these were the days before social media and TV and billboard posters, so people knew of great or notorious individuals from afar without ever knowing what they looked like. So to those in this particular town, Imam Ahmad was just ‘another man’.
Failing to recognise Imam Ahmed, the caretaker of the mosque refused to let him stay there for the night, and ordered him to leave. So, with nowhere else to go, Imam Ahmad made preparations to sleep on the street. A baker, whose shop was nearby, watched this scene play out and took pity on Imam Ahmed – of course, without knowing who he was. He invited the Imam to stay at his bakery for the night. Imam Ahmad agreed.
While the Imam rested, his host remained busy throughout the night preparing bread to sell in the morning. Imam Ahmed watched as the baker mixed and kneaded the dough, tended the fire, and pulled hot loaves from the oven, all the while uttering remembrances of Allah and Istighfar (asking for Allah’s forgiveness).
In the morning, the Imam eagerly asked his host about his continual dhikr and istighfar. The baker told him it had become like second nature, a habit and practice that he had been doing for many years. Imam Ahmad then asked whether the man had experienced any reward from this practice. The baker answered:
“By Allah! There is not a single dua that I made except that it was answered – all apart from one.”
When Ibn Hanbal asked what that unanswered prayer was, the baker responded:
“To see the famed Imam Ahmad ibn Hanbal!”
At this, tears came to the Imam’s eyes and he told the baker:
“I am Ahmed ibn Hanbal! By Allah! I was brought to your place so that you can have your wish come true.”
SubhanAllah!
There are many beautiful lessons from this story.
First, is the power of dhikr and istighfar – it opens doors to blessings and is a means for your du’as to be answered.
Second, there is a connection between the baker’s remembrance of Allah and his service to others – his dhikr didn’t prevent him from fulfilling his (halal) job; and crucially, that dhikr softened his heart so that he was not only mindful of Allah but also mindful of the needs of others.
Third, a general lesson is the profound importance of hospitality, even to strangers – those guests bring with them great blessings, and we should never turn them away.
Fourth, Allah is Al-Lateef! The One who is Subtle in His plans, and Sensitive to people’s unspoken hopes and dreams. Something that at first seemed negative (being refused by the mosque) ended up being the means by which something positive could happen for both the Imam and the baker.
And finally, we learn about the humility of Imam Ahmed – he could easily have utilised his fame to his advantage! He only needed to tell the mosque caretaker, or anyone for that matter, who he was and he would have received the best hospitality imaginable. But instead, he refused to turn his knowledge into a privilege. He refused to have an advantage above other people simply due to his fame, and was willing to be treated the same as everyone else. A further testament to his lack of ego was the way he observed the baker while he worked through the night – the great Imam Ahmed was open to learning from others who were not as learned as him, and realised that truth and wisdom is often preserved and passed down by those who have no name. He constantly sought to learn, even from a humble baker.
We can always learn from others, no matter who they are.
AYA MBILI ZA DUA KUBWA SANA, UKIZIDAWIMU BASI BILA SHAKA UNAJIONGEZEA RIZIKI KWA WINGI
NI FUNGUO ZA RIZIKI NA MAMBO MBALIMBALI MENGINE TUNAYOYAJUA NA MENGINE HATUYAJUI
سُوۡرَةُ البَقَرَة
Sura AlBaqarah
Ayat Number 285
ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓٮِٕكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٍ۬ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ (٢٨٥)
ENGLISH
The Messenger has believed in what was revealed to him from his Lord, and [so have] the believers. All of them have believed in Allah and His angels and His books and His messengers, [saying], “We make no distinction between any of His messengers.” And they say, “We hear and we obey. [We seek] Your forgiveness, our Lord, and to You is the [final] destination.”
SWAHILI
Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hayo): wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake; (nao hao Waislamu na Mtume wao husema), “Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake (wote tunawaamini).” Na husema: “Tumesikia na tumetii. (Tunakuomba) msamaha, Mola wetu! Na marejeo ni kwako.”
Ayat Number 286
لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَعَلَيۡہَا مَا ٱكۡتَسَبَتۡۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذۡنَآ إِن نَّسِينَآ أَوۡ أَخۡطَأۡنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تَحۡمِلۡ عَلَيۡنَآ إِصۡرً۬ا كَمَا حَمَلۡتَهُ ۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلۡنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦۖ وَٱعۡفُ عَنَّا وَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَآۚ أَنتَ مَوۡلَٮٰنَا فَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡڪَـٰفِرِينَ (٢٨٦)
ENGLISH
Allah does not charge a soul except [with that within] its capacity. It will have [the consequence of] what [good] it has gained, and it will bear [the consequence of] what [evil] it has earned. “Our Lord, do not impose blame upon us if we have forgotten or erred. Our Lord, and lay not upon us a burden like that which You laid upon those before us. Our Lord, and burden us not with that which we have no ability to bear. And pardon us; and forgive us; and have mercy upon us. You are our protector, so give us victory over the disbelieving people.”
SWAHILI
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yo yote ila yaliyo sawa na uweza wake. (Faida ya) yale iliyoyachuma (hiyo nafsi) ni yake na hasara ya yale iliyoyachuma ni juu yake. (Husema): “Mola wetu! Usitutese kama tukisahau (tukaacha yaliyo mema) au tukikosa (tukafanya mabaya). Mola wetu! Na usitubebeshe mzigo kama uliowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu! Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya watu makafIri.”
DUA NZURI UNAPOKUWA UNADHULUMIWA NA HUNA NJIA YA KUJIOKOA. KUMBUKA KWAMBA NI DHULUMA AINA NA SURA YEYOTE. DHULUMA KUBWA AU NDOGO. NI SHOKA LENYE KUVUNJA BALAA LOLOTE LINALOKUKABILI POPOTE ULIPO.
Dhuluma zipo mbalimbali ambazo zingine tunaishi nazo na nyingine tunaziona na kuzisikia. Katika maisha kila binaadamu huenda alikumbana na aina mojawapo ya hizi dhuluma.
Soma Aya hiyo nitakayoitaja hapa chini kimoyomoyo unapokumbana na shida ya aina hizi au pia kuombea wengineo ambao wapo katika matatizo ya aina hii.
Dua hii inatokana na kisa cha watu waliokimbilia katika pango na kisa hicho kinajulikana kwa Waislamu na Wakristo pia. Kuruani imetaja kisa hicho kwa urefu na kinaganaga . Mwenyeezi Mungu anatufundisha na sisi pia tuitumie dua hiyo tunapokuwa katika mazingara ya dhuluma.
Watu hao walikimbilia katika Pango (KAHF) kujiepusha na Mfalme katili ambaye alikuwa Kafiri na hawa waliokimbilia katika Pango hilo walikuwa wachamungu wa Kikristo wa hapo awali yaani wafuasi wa nabii Isa. (Sio Wakristo wa hivi sasa bali hapo awali ambao walifuata mafundisho ya Ukweli ya Nabii Isa.
Nimetaja Miujiza mbalimbali (iliyogunduliwa kutoka katika sura hii ya KAHF Namba 18) hivi karibuni katika sehemu nyinginezo za website (Mtandao) hii.
Kuna miujiza mbalimbali inayohusiana na kisa hiki. Na mwenyeezi mungu amesema pia katika Aya namba 9 ya sura ya Al-Kahf (Sura Namba 18) kwamba kisa hiki ni katika miujiza yake mikubwa na ukifikiri utaona maajabu siyo madogo.
أَمۡ حَسِبۡتَ أَنَّ أَصۡحَـٰبَ ٱلۡكَهۡفِ وَٱلرَّقِيمِ كَانُواْ مِنۡ ءَايَـٰتِنَا عَجَبًا (٩)
Or have you thought that the companions of the cave and the inscription were, among Our signs, a wonder?
Nimetoa tafsiri kwa kiingereza na Mwenyeezi Mungu akipenda nitaifasiri kwa Kiswahili hapo baadaye na pia nitadokeza baadhi ya miujiza kutoka katika kisa hiki. Leo Nitataja moja au mbili tu ya miujiza hiyo na nyinginezo hapo baadaye Mungu akipenda. Pia nimetaja moijiza mbalimbali yenye uhusiano na kisa hiki kwingineko katika website (mtandao) hii.
Angalia Maajabu. Kisa hiki kimetajwa katika Aya 18 tu!! na ajabu ni kwamba Sura hii pia ni namba 18!!!
Sura Hii ipo katikati ya Msahafu katika Juzuu ya 15 na tunaelewa kwamba Kuruani imekusanya Juzuu 30!!! Yaani Sura Inayoitwa Pango imewekwa katikati ya Msahafu kiajabu sana tena sana….
Kwa nini mpangilio huu? Nitakudokezea Mola akipenda hivi karibuni katika ukurasa huu huu lakini siyo leo.
DUA NI HII HAPA CHINI—————……..
Sasa Dua ambayo muhimu sana ya Kujiokoa na dhuluma au kuwaombea wengineo ambao wapo chini ya dhuluma ni kama ifuatayo:
إِذۡ أَوَى ٱلۡفِتۡيَةُ إِلَى ٱلۡكَهۡفِ فَقَالُواْ رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةً۬ وَهَيِّئۡ لَنَا مِنۡ أَمۡرِنَا رَشَدً۬ا (١٠)
When the young men fled for refuge to the Cave and said: Our Lord! Give us mercy from Thy presence, and shape for us right conduct in our plight.
Dua ni kipande cha pili katika Aya hii:
رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةً۬ وَهَيِّئۡ لَنَا مِنۡ أَمۡرِنَا رَشَدً۬ا
RABANA AATINA MIN LADDUNKA RAHMATAN WA HAYYI’ LANA MIN AMRINA RASHADAN
Our Lord! Give us mercy from Thy presence, and shape for us right conduct in our plight.
Ndugu yangu soma Dua hii kwa kiasi ya uwezo wako na kwa kweli ninakuhakikishia Utafanikiwa. Lakini fanya subira kwani subira yavuta kheri na usiharakishe kwani mitihani ya Mwenyeezi Mungu ina sura mbalimbali. Kuna mitihani mingine Mwenyeezi Mungu anapima imani zetu.
Inshaallah Dua hii itakuokoa. Tafadhali usidharau nakuhakikishia.
Kuhusu miujiza ya sababu ya kushuka Kisa hiki na mengineyo yaliyopo katika sura hii ya 18 Mola akipenda nitaizungumzia hivi karibuni. Muhimu ni uzima. Inshaallah
TUNATAMANI TUZAE WATOTO WENYE UTUKUFU, WATOTO WAZURI WENYE ADABU NA HEKIMA BASI DUA IFUATAYO NI NZURI SANA. NA SISI TUOMBE DUA YA ZAKARIYA HUENDA TUKAPATA ALIYOYAOMBA MTUKUFU HUYO.
Dua Hii (Aya Namba 38 hapa chini) aliiomba Nabii Zakari. Kisa cha Mama Maryam na Zakariya katika sura ya IMRAN namba 3 Aya 35 mpaka Aya namba 39
إِذۡ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ عِمۡرَٲنَ رَبِّ إِنِّى نَذَرۡتُ لَكَ مَا فِى بَطۡنِى مُحَرَّرً۬ا فَتَقَبَّلۡ مِنِّىٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ (٣٥)
فَلَمَّا وَضَعَتۡہَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّى وَضَعۡتُہَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰۖ وَإِنِّى سَمَّيۡتُہَا مَرۡيَمَ وَإِنِّىٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَـٰنِ ٱلرَّجِيمِ (٣٦)
فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ۬ وَ أَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنً۬ا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّاۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيۡهَا زَكَرِيَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزۡقً۬اۖ قَالَ يَـٰمَرۡيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَاۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ (٣٧)
هُنَالِكَ دَعَا زَڪَرِيَّا رَبَّهُ ۥۖ قَالَ رَبِّ هَبۡ لِى مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً۬ طَيِّبَةًۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ (٣٨)
فَنَادَتۡهُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ وَهُوَ قَآٮِٕمٌ۬ يُصَلِّى فِى ٱلۡمِحۡرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحۡيَىٰ مُصَدِّقَۢا بِكَلِمَةٍ۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدً۬ا وَحَصُورً۬ا وَنَبِيًّ۬ا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ (٣٩)
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى غُلَـٰمٌ۬ وَقَدۡ بَلَغَنِىَ ٱلۡڪِبَرُ وَٱمۡرَأَتِى عَاقِرٌ۬ۖ قَالَ كَذَٲلِكَ ٱللَّهُ يَفۡعَلُ مَا يَشَآءُ (٤٠)
35-(Kumbukeni) aliposema mke wa Imrani (baba yake Maryamu katika kamwomba Mola wake): “Mola wangu! Nimeweka nadhiri kwako
aliyomo tumboni mwangu kuwa wakfu (wakutumikia mambo ya dini); basi nikubalie. Bila shaka Wewe ndiye usikiaye na ujuaye.” .
36-Basi alipomzaa, alisema: “Mola wangu! Nimemzaa mwanamke” – .na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa – “Na mwanamume
(niliyefikiri kuwa nitamzaa) si sawa na mwanamke . (niliyemzaa). Na nimempa jina Maryamu (mtumishi
wa Mungu). Nami namkinga kwako, yeye na kizazi chake, (uwalinde) na Shetani aliyebaidishwa na rehema yako.” yako.”
37-Basi Mola wake akampokea (yule mtoto) kwa kabuli njema na akamkuza kukua kwema, na
akamfanya Zakaria awe mlezi wake. Kila mara Zakaria alipoingia chumbani (kwake) alikuta vyakula pamoja naye (huyo Maryamu). Akasema; “Ewe Maryamu! Unapata wapi hivi?” Akasema: “Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila kuwaza (mwenyewe).”
38-Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake, akasema: “Mola wangu! Nipe kutoka kwako mtoto mwema. Wewe ndiye usikiaye maombi (ya
wanaokuomba)
39-Mara Malaika wakamlingania, bali. amesimama akisali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kuwa utazaa
mtoto; umwite) Yahya, atakayekuwa mwenye kumsadikisha (Mtume atakayezaliwa) kwa neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu (Naye ni Nabii lsa) na atakayekuwa bwana kabisa na mtawa na Nabii
anayetokana na watu wema. (Nao ni nyinyi).
40-Akasema (Zakaria): “Mola wangu! Nitapataje mtoto, na hali uzee umenifikia, na mke wangu ni tasa?” Akasema (Mwenyezi Mungu):
“Ndivyo vivyo hivyo; Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo”
Hizi Aya zinazungumzia kisa hicho na dua ni kipande kutoka katika Aya hizi nacho ni
رَبِّ هَبۡ لِى مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً۬ طَيِّبَةًۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ
“Mola wangu! Nipe kutoka kwako mtoto mwema. Wewe ndiye usikiaye maombi (ya
wanaokuomba)”
Aya Hii ndiyo Dua.
maneno haya machache sana lakini siyo madogo. Basi tutumie dawa hii tunapohitaji mtoto au watoto na Inshaallah Mwenyeezi Mungu atatubariki na kutupa mtoto wa aina hii. Kwa kweli tumepewa funguo zote lakini hizo funguo zina mashari yake tunapotaka dua zikubaliwe. Tunamuomba Mwenyeezi Mungu atupe uwezo wa kufuata masharti hayo na pia funguo hizi zifanye kazi yake. Allahu Akbar.
MARADHI YA MOYO-WASIWASI
Hakuna binaadamu ambaye ameepukana na wasiwasi na hasa huu wakati wa leo tulionao. Dunia ya leo, mazingara ya kisasa yamejaa vishawishi ambavyo yanasababisha wasiwasi. Baada ya mapinduzi ya Viwanda katika nchi za magharibi maisha yamekuwa ya haraka haraka na nchi zetu za Mashariki zinafuata kasi hizo kama bendera. Maradhi ya wasiwasi yamezidi na kupelekea watu kupata dhiki ya nafsi na hii inajulikana kama Stress au Depression. Maradhi ya hatari. Maradhi haya yanapelekea mpaka watu kujiua. Huzuni pia ni mojawapo ya Maradhi haya. Wakati mwingine wasiwasi unakuja kwa vitu vya upuuzi vya duniani, kupapia papia vitu vya anasa vya dunia. Haraka haraka za kupuuzi, kwa mfano unaogopa kufukuzwa kazi na hujui baada ya hapo utawezaje kuishi na hutakuwa na pesa, au una mtihani na unogopa kufeli, au chochote kile cha kidunia ambacho kinasumbua roho yako.
Sisi waislamu tunamshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutup adawa mbalimbali za kuzuia na pia kutibu maradhi haya. Hospitali kuna madawa lakini pia Inategemea iwapo hayo madawa yatalenga maradhi hayo au hata mwili wako kukubali dawa hizo kwa hiyo madawa yote inategemea Mwenyeezi Mungu Mtukufu asaidie ili dawa ifae. Dua ni muhimu kabla ya kwenda hospitali na huenda dua hiyo ikakutibu kabla ya kutumia madawa. Kuna Hadithi za Mtume ambazo zinafundisha Dua mbalimbali za kutibu maradhi haya. Katika Ukurasa huu nitakuelezea dua kutoka katika Kuruani Tukufu na ikiwezekana Dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume Mohamad. (Salamu na Amani za Mola Zimfikie)
Maradhi ya waiswasi hutokana na Meshetani ambao wanatguletea uchafu huo. Kazi yao ni kumuangamiza binaadamu na wapepania kufanya hivyo kama walivyomuahidi Mwenyeezi Mungu kwamba kazi zao ni kumdhuru binaadamu na kumpoteza.
Sura Ifuatayo ni Dua kubwa sana ya kujilinda na kujitibu na maradhi ya aina hii. Weka Nia na Kwa imani ya hali ya juu kisha uisome kwa kadiri ya uwezo wako.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (١) مَلِكِ النَّاسِ (٢) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (٣) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (٤) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (٥) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (٦)
Transliteration:
1/QUL A’UDHU BIRABBI NNASI 2/MALIKI NNASI 3/ILAHI NNASI 4/MIN SHARRI L WASWASI ALKHANNASI 5/ALLLADHIY YUWASWISU FI SUDURI NNASI 6/MINALJINNATI WANNAS
TAFSIRI
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu, kuneemesha neema kubwa kubwa na kuneemesha neema ndogo ndogo.
1. Sema: Ninajikinga kwa Bwana Mwenye Kuwalea
2. Mfalme wa watu
3. Muabudiwa wa watu
4.N a shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma.
5.Atiaye wasiwasi nyoyoni mwa watu
6. (Ambaye ni) katika maiini na watu.
Kwa hiyo hizo Aya ni Dua ya kujilinda na Mashetani hao wa Kijinni na Kibinaadamu. Usidanganyike na Sayansi za kisasa kwamba labda haya mambo siyo ya kweli. Kama kweli Sayansi ndiyo bora kuliko Mwenyeezi Mungu basi Wana Sayansi hao wafufue walikufa au waumbe Kiumbe chochote kile. Hata Nzi hawawezi kuumba wacha binaadamu. Dunia hii imejaa maradhi mablimbali na mengine hayana matibabu kwa hiyo tuombe dua. Kama unashindwa kusoma Kuruani basi Tafsiri yake inatosha. Unaweza kutumia lugha yeyote na siyo lazima Arabic.
Na Pia kuna Dua Nyinginezo ambazo zinafanya kazi ya kutibu maradhi kama haya. Hapa chini nimeorodhesha dua ya Mtume Mohamad (Salamu na Amani ya Mola Zimfikie) na Pia nyinginezo kutoka katika Kuruani Tukufu.
Unaweza pia kutumia Dua zifuatazo:
Du’as for Anxiety, Stress and Depression
DUA NUMBER 1
اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْهَمِّ وَالْحُزْنِ وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ وَالْبُخْلِ وَالْجُبْنِ وَضَلَعِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ
Transliteration: Allahumma inniiy a’uzubika min alhammi wal huzni wal ajzi wal kasli wal bukhli wal jubni wa dala’id dayni wa galabatir rijaal.
Translation: O Allah, I take refuge in you from anxiety and sorrow, weakness and laziness, miserliness and cowardice, the burden of debts and from being overpowered by men.
[Hadith | Sahih Al-Bukhari]
DUA NUMBER 2
حَسْبُنَا ٱللَّهُ وَنِعْمَ ٱلْوَكِيلُ
Transliteration: Hasbunallahu wa ni’mal wakeel.
Translation: Allah is sufficient for us, and He is the best disposer of affairs.
[Qur’an | Surah Ale-Imran | 3:173]
DUA Number 3
اللهم اخرجني من الظلمات إلى النور
Transliteration: Allahumma Akhrijniiy min adhulumaati ilaa annur.
Translation: Oh Allah take me out of darkness and into the light.
[Practiced Du’a]
DUA Number 4
لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِالله
Transliteration: La hawla wa la quwwata illa billah.
Translation: There is no power or strength except with Allah.
[Hadith | Ibn Majah]
DUA Number 5
Anas bin Malik said when the Prophet (PBUH) would be afflicted with a stressful trial, he would say:
Recite the du’a as follows:
يَا حَيُّ يَا قَيُّوْمُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيْث
Transliteration: Yaa Hayyu yaa Qayyum, bi-rahmatika astaghith.
Translation: O Ever-Living, O Self-Subsisting Sustainer of all, I seek help through Your mercy.
[Hadith | Tirmidhi]
——————————————————————————–
TIBA YA MAJI
Wazazi wetu walitumia Kombe na hii inatokana na maji. Hatukuwaamini na tuliwaona wanapoteza wakati. Kumbe tulidanganyika kwani wazee wetu hawakukosea hata kidogo. Walikuwa katika haki. Maji ukiyasomea Kuruani na Dua kisha ukayanywa kwa nia yoyote kama vile Kinga na maradhi au kama una tatizo la afya basi hiyo ni dawa kubwa ambayo bado haileweki. Chukua Maji katika Glassi au Kikombe au chombo chochote and usomee Sura Ya Al-Fatiha au Chapter ya Kwanza ya Kuruani Tukufu, Au hata Aya ya Kwanza “BISMI LLAHI ARRAHMANI ARRAHIYM” Au ikiwezekana Soma Sura Tatu za mwisho wa Kuruani Yaani Sura Ya IKHLAS namba 112, na Sura ya AL-FALAQ namba 113 na Sura Ya ANNASI Namba 114 . Kama huwezi kusoma Kuruani basi uombe dua kwa lugha yeyote ile na huu unamtaja Mwenyeezi Mungu na kisha umwombe Mwenyeezi Mungu akupe Tiba kutokana na maji hayo. Inshaallah Mwenyeezi Mungu atatupa hayo tunayoyatafuta. Tukifanya Asubuhi na Usiku ni nzuri sana. Sayansi pia imethibitisha haya ninayoyazungumza, Sikiliza Video hapa chini ya
Profesa Dr Masaru aligundua maajabu ya Maji yanayoathirika na Mazingara na pia hivyo ndivyo yale Maji ya ZAM ZAM huko Mecca yalivyoathirika na zile Sauti za Mahujaji wanapokuwa wanamtaja Mwenyeezi Mungu hapo katika Kaaba ambayo ndiyo ipo hiyo Chemchem ya Maji. Tulisomea Maji basi tumejitengenezea Kombe au dawa yetu. Ukiwa unaishi Ulaya au nchi yeyote ambayo hakuna Mashekhe wenye kujua kutengeneza Kombe basi tujitengenezee mwenyewe dawa yetu bure bila kumsumbua mtu yeyote. Alhamdulilah. Tufanye hivyo. Na Inshaallah leo hii kabla ya kulala nitajitengenezea Kombe yangu kwa nia ya Kuijenga Afya isivamiwe na Maradhi au chochote kile na Nikiamka salama kwsho Asubuhi Mola akipenda. Video Hapa Chini Inahusu habari ya Profesa Dr Masaru
DUA YA KUJIOKOA UNAPOJIKUTA UMEFANYA MADHAMBI
17/03/2025
Bismillahi Arahman Arahiim
Tunapojidhulumu nafsi zetko kwa madhambi ya aina yeyote au kwa kiwango chochote kama vile madhambi makubwa au madogo basi tujue kwamba dawa yake ni kutubia kwani Mwenyeezi mungu anawapenda sana wenye kutubia. Hatua za kufuata katika toba hiyo ni kujisahihisha na kutokurudia tena kufanya makosa kama hayo, na pia kujutia katika nafsi zetu na kujifundisha yaliyo mazuri na la mwisho kumuomba Mwenyeezi Mungu atusamehe na atusaidie na kutulinda na shari za nafsi zetu na njama za Mashetani. Dua siyo jambo dogo bali kubwa sana, na tutajua umuhimu wa dua wakati tumepatwa na janga katika majanga ya dunia. Misukosuko ya dunia inapotukuta na tukaomba dua na misukosuko hiyo inapoondoka hapo ndiyo tutakumbuka faida za dua.
Alhamdulilah Leo ningependelea kuzungumzia Dua nzuri sana ambayo ni dua kubwa aliyoiomba nabii Yunus.
Kwa kifupi Nabii Yunus ambaye mzaliwa wa NINEVEH ambao ulikuwa mji mkubwa wa dola ya Assirian (Assyrian Empire) ambayo leo hii ni katrika sehemu ya IRAQ. Mtu huyu alipewa utume na Mwenyeezi Mungu na akapewa jukumu la kuwalingania watu wa mji huo wa Nineveh kama kawaida ya Mweyeezi Mungu kutuma wajumbe kwa kila Taifa lao.
Watu wa Nineveh walifanya ukaidi sana na wakaendelea kufanye maasi yote yaliyokatazwa na katika maasi hayo kuabudu Miungu ya Masanamu. Nabii Yunus akafanya juhudi sana kuwakataza lakini alipoona ukaidi wa watu hao umezidi akawakumbusha adhabu iliyowafikia mataifa yaliyopita kama vile AD, THAMUWD na NUHU lakini hawakumtii na kumjibu kwamba wazazi wao walifanya ibada hizo za masanamu na hakuna baya lolote lililowapata, hawakumjali bali walimcheka na kumwambia hawaogopi nasiha hizo kwamwe na anapoteza wakati wake bure. Nabii Yunus akahisi hatari ya adhabu ya Mwenyeezi Mungu ambayo huenda ikatokea wakati wowote basi akaamua akimbie mbali na mji huo. Safari yake aliamua aende Joppa ambaye leo hii inajulikana kama Jaffa huko Pelestina, Mji huu wa Jaffa ni Bandari na Alipofika Joppa (Jaffa) akachukua Meli ambaye ilikuwa ikielekea Mji wa Tarshish ambayo ni Bandari ya huko Spain. (Angalia Picha hapa chini)

Lengo la Mtume huyu ni kukimbia mbali sana na NINEVEH kwani alikuwa anajua adhabu ya mwenyeezi mungu itakuja na alikuwa akijiokoa. Kwa kweli uamuzi huo haukumfurahisha Mwenyeezi Mungu kwani alipewa kazi ya kulingania dini na siyo kujiamulia mambo hovyo hovyo. Ilimbidi asubiri amri ya Mwenyeezi Mungu lakini aliharakisha.
Alipopika Joppa akapanda Meli ambayo ilikuwa ikielekea Tarshish na katika safari hiyo ikaanza Mkasa mwingine Mkubwa sana. Mwenyeezi Mungu akatoa Mtihani usiku ulipoingia, dhoruba iliendelea, na kutikisa meli huku na huko. Inasemekana kwamba Meli hiyo ilikuwa imejaa abiria na Mizigo na Ijapokuwa walipunguza Mizigo kwa kutupa naharini lakini tatizo halikuondoka na ikawa Meli inaendelea kuyumbayumba hovyo hovyo na kufuatana na Itikadi za wakati huo waliamini kwamba huenda kuna Mtu mmojawapo kati yao ambaye analeta Mkosi katika Meli hiyo, katika hali hiyo na kufuatana na uamuzi wa Nahodha na wasimamizi wa Meli hiyo ilibidi wapige Kura na kumtafuta mtu huyo. Kwa kweli Kura ya kutupa Vijiti au Mawe mojawapo ya kura hii ilifanyika mara tatu lakini kila wakipiga kura ilikuwa Vijiti au mawe yalikuwa yakimuamgukia na kumuashiria Nabii Yunus lakini kila mara hawakuamini kwani walimuona Nabii Yunus kuwa ni mtu Muaminifu na Mchamungu na haiwezekani kuwa na mkosi au ubaya wowote. Hatimaye Nabii Yunus alijitambua kwamba hili linalotokea ni Makosa aliyoyatenda kwa kukimbia Kulingania Dini huko NINEVEH na kwa hiyo aliamua na kujitupa Baharini bila ya Ubishani wowote. Angalia Subira na Imani ya Nabii huyu Ilivyokuwa Kubwa. Alipojitupa na Kutua Baharini akakumbana na Samaki Mkubwa (Huenda Nyangumi) na Nabii Jonas Akamezwa.
Baada ya Kumezwa na huenda pia kabla ya hapo alikuwa akiomba dua inayojulikana katika Kuruani tukufu. Dua hiyo aliendelea kuiomba na kwa baraka za Mwenyeezi Mungu baada ya Masiku na Mchana (Wengine wanasema siku tatu na wengine zaidi ya siku tatu) wa Msukosuko ndani ya tumbo la Samaki huyo Mkubwa(Nyangumi au Samaki aina nyingine) Kwa uzezo wake Mwenyeezi Mungu samaki huyo akamtapika Nabii Yunus ufukoni au pwani katika sehemu za nchi hiyo. Na kwa baraka ya Dua hiyo Mwenyeezi alimuoteshea Mti mara tu baada ya kutoka tumboni mwa Samaki na Mti huo ulimfaa kwa Kivuli na Matunda.
Kwa kifupi nimeelezea kisa hiki ili tuone faida ya Dua. Sasa tuielezee dua hiyo aliyoiomba nabii Yunus na tufaidike nayo kwa kuitumia ili na sisi itufae pia.
لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبۡحَـٰنَكَ إِنِّى ڪُنتُ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٨٧)
MATAMSHI
LA ILAHA ILA ANTA SUBHANAKA INIY KUNTU MINADWALIMIN
TAFSIRI
Hakuna aabudiwaye isipokuwa wewe, Mtakatifu; hakika mimi njlikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu
Dua kutoka katika Aya Ifuatayo Sura ya Al-Ambiyaa Aya Namba 87
وَذَا ٱلنُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَـٰضِبً۬ا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقۡدِرَ عَلَيۡهِ فَنَادَىٰ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ أَن لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبۡحَـٰنَكَ إِنِّى ڪُنتُ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٨٧)
TAFSIRI
Na (Mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa, na akadhani ya kwamba hatutamdhikisha. Basi (alipozongwa) aliita katika giza (akasema): “Hakuna aabudiwaye isipokuwa wewe, Mtakatifu; hakika mimi njlikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Unaweza kuisoma dua hii kwa lugha yeyote uiwezayo uchaguzi ni wako.
DUA KUBWA YA MATIBABU KUTOKANA NA MARADHI YASIYO NA DAWA
23/03/2025
Alhamdulilah leo siku ya Ramadhani tukufu na ni siku katika masiku kumi ya mwisho. Namuomba Mwenyeezi Mungu atupe nguvu , afya na subira tufunge katika masiku haya kama ipasavyo kwani hatujui kama Ramadhani ijayo itatukuta tupo hai. Kwa kweli hatujui yajayo. Hakuna kiumbe anayejua cha baadaye isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake. Kila usiku tunapoingia na kulala kitandani tukumbuke kitanda kingine kinachotusubiri ambacho ni udongo na wadudu. Hili jambo linatia wasiwasi sana. Yaani haya ndiyo yanayotusubiri mwisho wetu. huko makaburini sasa hizi nyumba zetu na mali zetu? Na hili siyo huenda bali linakuja tupende au tusipende na jambo la kutisha. Kila mtu peke yake ndani ya tundu la ardhi. Sasa hivi vinono vya dunia? raha za dunia? mapesa na magari na vinginevyo? Kila kitu tutaacha nyuma. Sasa huko makaburini tutakaa muda gani? lini kiyama? huko makaburini tunasubiri kufufuliwa siku ya kiyama ili tusimame mbele ya haki. Kwa kweli inatisha. Hii dunia imejaa marembo ambayo yanatufaa kwa muda mfupi sana. Kwa haya nitaishia hapa namuomba Mola atupe uwezo wa kufanya yale atakayo na atusaidie kwani sisi peke yetu hatuwezi. kwa hiyo leo Inshaallah (Mungu akipenda) Tutasoma dua ya Nabii Ayub ambayo inahusiana na maradhi yasiyotibika.
Tunapoambiwa hospitalini kwamba hakuna dawa yeyote itakayotufaa kutuondolea maradhi au tunapotumia madawa na madawa na hakuna manufaa yeyote yanayopatikana na dawa hizo basi tusikate tamaa kabisa kwani tuelewe kwamba hakuna ugonjwa usiokuwa na dawa. Mtume Mohamad (ﷺ) amesema
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنَا أَبُو أَحْمَدَ الزُّبَيْرِيُّ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ سَعِيدِ بْنِ أَبِي حُسَيْنٍ، قَالَ حَدَّثَنِي عَطَاءُ بْنُ أَبِي رَبَاحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ دَاءً إِلاَّ أَنْزَلَ لَهُ شِفَاءً ”.
Narrated Abu Huraira:
The Prophet (ﷺ) said, “There is no disease that Allah has created, except that He also has created its treatment.” (Sahih al-Bukhari 5678)
Mtume (ﷺ) alisema kwamba hakuna ugonjwa Mwenyeezi Mungu aliyeuumba isipokuwa ameumba pia matibabu yake. (Hadithi hii ni Sahihi kutoka katika Vitabu Vya Imamu Bukhari.)
Yule yule aliyetuumba basi ni yule yule ndiye mwenye uwezo wa kututibi kwa njia mbalimbali kama vile madawa ya hospitali na dua. kwa hiyo tusikate tamaa kabisa. Tukiugua sana na hakuna dawa basi tusiwe na wasiwasi au khofu yeyote kwani ujua Mwenyeezi Mungu yupo na madawa yapo Inshallah (Kwa uwezo wake Mola).
Dua aliyoiomba Nabii Ayub inatufundisha tufuate nhia yake kwani aliugua sana maradhi mabaya na shetani alikuwa akimkatisha tamaa ili asiwe na imani na mwenyeezi mungu na kama kwamba maradhi na ufakiri ulifuata unatokana na Ibada yake kwani nabii ayubu alikuwa mchamungu sana na Mashetani walikuwa wakifanya juhudi kumvurugia imani yake na hivi ndivyo mashetani walivyomuahidi Mwenyeezi Mungu kwa kusema kwamba watafanya juhudi kubwa sana kumharibu na kumharibia binaadamu maisha yake na kila kitu chake lakini Mwenyeezi Mungu akasema hawatamweza Mchamungu kwani Atalindwa na Mola.
Hii ndiyo dua aliyoiomba Nabii Ayubu
أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٲحِمِينَ
INNIY MASSANIYADHURRU WA ANTA ARHAMU ARRAHIMIYN
“Mimi imenipata dhara, nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.”
No Bora uinue mikono kisha useme Ewe Mola Wangu “Mimi imenipata dhara, nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.”
Dua ambayo ipo Katika Aya Namba 83 Sura ya A-Lambiyaa Namba 21
۞ وَأَيُّوبَ إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُ ۥۤ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٲحِمِينَ (٨٣)
Na (Mtaje) Ayyubu, alipomwita Mola wake (akasema) “Mimi imenipata dhara, nawe ndiwe Unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.”
Dua hii unaweza kuisoma kwa lugha yeyote uitakayo kama huelewi Kuruani. Mwenyeezi Mungu atakusikia kwani ametuahidi kwamba yupo karibu sana na sisi na anatusikia na kutuona. Na Mwenyeezi Mungu anampenda Mweney subira. Nabii Ayub alikuwa na subira sana na Mwenyeezi Mungu amemsifu sana na kisa chake kutoka katika Kuruani Sura ya SWAD Namba 38 Aya namba 41 mpaka 44
وَٱذۡكُرۡ عَبۡدَنَآ أَيُّوبَ إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُ ۥۤ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلشَّيۡطَـٰنُ بِنُصۡبٍ۬ وَعَذَابٍ (٤١)
ٱرۡكُضۡ بِرِجۡلِكَۖ هَـٰذَا مُغۡتَسَلُۢ بَارِدٌ۬ وَشَرَابٌ۬ (٤٢)
وَوَهَبۡنَا لَهُ ۥۤ أَهۡلَهُ ۥ وَمِثۡلَهُم مَّعَهُمۡ رَحۡمَةً۬ مِّنَّا وَذِكۡرَىٰ لِأُوْلِى ٱلۡأَلۡبَـٰبِ (٤٣)
وَخُذۡ بِيَدِكَ ضِغۡثً۬ا فَٱضۡرِب بِّهِۦ وَلَا تَحۡنَثۡۗ إِنَّا وَجَدۡنَـٰهُ صَابِرً۬اۚ نِّعۡمَ ٱلۡعَبۡدُۖ إِنَّهُ ۥۤ أَوَّابٌ۬ (٤٤)
41. Na mkumbuke mja wctu Ayubu, alipomwita Mola wake, (akanena): “Kwa yakini Shetani amenifikishia udhia na taabu. (Niondoshee Mola wangu maradhi haya yaliyonishika).”
42. (Mwenyezi Mungu akamwambia):- “Uharikishe mguu wako (patachimbuka chechem chini yake, maji yake yatakuwa dawa yako). Basi haya maji baridi y·a kuogea (koga), na (haya maji baridi) ya kunywa, (yanywe).”
43· Na tukampa watu wake na wengine kama wao pamoja nao, kwa rehema itokayo kwetu, na (ipate kuwa) mawaidha kwa watu wenye akili.
44. “Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, (si funbo); kisha mpige kwacho (mkeo kwa kiapo ulichoapa kuwa utampiga kwa mabaya aliyoyafanya), wala usivunje kiapo., Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira, mja mwema; kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana
Katika Aya namba 44 hakumpiga Mke wake kwa fimbo bali vijiti ili kumuonyesha kosa alililifanya kwani wakati nabii Ayubu alipokuwa amepigwa na balaa na kuugua (Maradhi yaliyosababishwa na Mashetani) Mkewe alikuwa imani yake inayumbayumba na dhaifu kutokana na mashetani waliokuwa wakimfata Mume na Mke ili kuwapoteza na imani ya Nabii Ayubu ilikuwa kubwa sana na Mkewe alikuwa kidogo anatetereka lakini hii ni kawaida na Nabii ayubu hakufurahishwa na udhaifu huo na aliweka nadhiri kwamba atampa mkewe fundisho kumpiga na hapo ilikuwa kiapo alichoapa nabii ayubu na aliwajibika kukitimiza. Kwa hiyo siyo kumpiga bali kumgusa gusa na vijiti ilikutekeleza nadhiri aliyonuia alipokuwa anaugua.
Family Tree Of Prophet Ayyub
Prophet Ayyub (عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ) was a descendant of Prophet Ibrahim (عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ) and believed by some to have a mother who was the daughter of Prophet Lut (عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ). His wife, Rahma, was a descendant of Prophet Yusuf (عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ). They lived in Rome and had fourteen children. Ayyub (عَلَيْهِ ٱلسَّلَامُ) was blessed by Allah (سُبْحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ) with strength, health, large lands, livestock, and a loving family. He was a respected community leader who was humble and always ready to help others, thanking Allah (سُبْحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ) for his blessings.

Surat Al-Anaam Number 6 Ayat Number 82 to 84
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يَلۡبِسُوٓاْ إِيمَـٰنَهُم بِظُلۡمٍ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَهُمُ ٱلۡأَمۡنُ وَهُم مُّهۡتَدُونَ (٨٢)
وَتِلۡكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيۡنَـٰهَآ إِبۡرَٲهِيمَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦۚ نَرۡفَعُ دَرَجَـٰتٍ۬ مَّن نَّشَآءُۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ۬ (٨٣)
وَوَهَبۡنَا لَهُ ۥۤ إِسۡحَـٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ ڪُلاًّ هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُ ۥدَ وَسُلَيۡمَـٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَـٰرُونَۚ وَكَذَٲلِكَ نَجۡزِى ٱلۡمُحۡسِنِينَ (٨٤)
82. “(Hapana shaka kuwa) wale walioamini na hawakuchanganya imani yao na ushirikina kuwa hao ndio watakaopata amani, nao ndio walioongoka.”
83. Na hizi ndizo (baadhi ya) hoja zetu tulizompa lbrahimu iuu ya watu wake. Tunamyanyua katika vyeo yule tumtakaye (kwa kuwa anakwenda mwendo tunaoutaka). Hakika Mola wako ndiye Mwenye hikima(na) ndiye ajuaye.
84. Na tukampa (Ibrahimu mtoto . anayeitwa) lshaqa na (mjukuu anayeitwa) Yaaqubu, wote tukawaongoa. Na Nuhu tulimwongoa zamani (kabla ya kuja Nabii lbrahimu ulimwenguni). Na katika kizazi chake (Nuhu, tulimwongoa) Daudi na Suleimani na Ayyubu na Yusufu na Musa na Haruni. Na hivi ndivyo tuwalipavyo wafanyao merna
——————————
Mwenyeezi Mungu akipenda hivi karibuni nitaendelea na mlango huu kwani kuna mengi mapya katika mlango huu ambao ni muhimu sana.