UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
SAYANSI ZA DUNIA
SAFARI ISIYO NA MWISHO KATIKA UNIVERSITY YA KURUANI TUKUFU
Alhamdulilah nashukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupa Uzima na Afya ya kuweza kuandika haya machache. Kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu leo nitaanza Safari ndefu na Ninawakaribisha wote tusafiri pamoja katika Safari hii Kubwa ya Kuchambua Elimu za Sayansi za Duniani.
Baada ya Kuandika Suala la Pili la Tarehe ya leo 25/09/2022 katika Mlango wa “DARASA LA KILA SIKU” Nimehisi kwamba bado nina nguvu za kutosha za kuendelea kuandika mengineyo yaliyo na uhusiano na Kuruani Tukufu.
Kama ulivyoona kila mlango wa Website Hii haujamalizika. Na hii inatokana na Kwamba Elimu ya Kuruani haina Mwisho.
Nimejiuliza je Niendelee na Milango Miongoni mwa Milango niliyokwishaanza? au Nifungue Mlango Mpya?
Nikajiambia “Kwa nini Nisifungue Mlango Mpya?”
Nikaona Bora Nichague Topic au Kiini Kikubwa ambacho Kinalingana na Nguvu za leo. Nikasema nitachambua “Sayansi Za Dunia”
Ni Kiini siyo Kirahisi na ambacho Hakina Mwisho. Je Itawezekana Hivyo?
Tatizo la Kuelezea Ni La Kwanza na La Pili Utafiti katika Kuruanilazima Kuwe na Uhakika Kwani Haya ni Maneno ya Mwenyeezi Mungu na lazima iwe Sahihi kwa Asilimia 100%. Hakuna Kubuni.
Nimeona Bora Kwanza Nianze moja kwa moja Na Sayansi na kisha Kuhusu Kuruani ambayo ndilo Lengo la Makala Hii nitalishughulikia Mara kwa Mara
Sisi wote ni wanafunzi au kwa lugha safi “Wanavyuoni” na kwa hiyo Nitafanya Jitihada zangu zote kwani Nimepania.
Kwa leo Nawakaribisha katika Mlango huu kwa Salaam za mwenyeezi Mungu zinazosema
“Asalaam Alaykum Watrahmatullahi Wabarakatuh”
Kisha Ninamuomba Mwenyeezi Mungu ambaye ameumba kila kitu ajaalie kila NInachoandika hapa kiwe kwa ajili yake tu na siyo kingine. Isiwe Ujira au Cheo bali Akhera.
Tafadhali Sana Wasomaji ningependelea kuwajuulisha kwamba Mlango huu hautakwisha kwa siku moja na kwa hiyo kutakuwa na nyongeza kila mara na kwa hiyo ukipendelea Utafiti wa malngo huu basi itabidi urudi kila mara unapopata nafasi.
Sasa Nitaanza Kwa Kujiuliza Suali:
Ni Nini Sayansi?
Jawabu:
Sayansi Ni Njia Ya Kuendeleza Elimu zetu na Kufahamu Ulimwengu Baada ya Kukusanya Ushahidi wa Maono na Baada ya Itafiti wa Ushahidi Huo.
Kwa hiyo Siyo Rahisi Kuelezea Neno Sayansi lakini Jawabu Hili siyo Baya na lipo karibu na Sahihi. Ni Definition iliyo Karibu na Ukweli.
‘Science is a means of improving our knowledge and understanding of the universe based on the collection of observation-based evidence.’
Wanasayansi wanatumia Mbinu nne katika Utafiti wa Kisayansi na Mbinu hizo tunaweza kuzipanga kama ifuatavyo:
1/Observation (Yaani Kuona au Kuhisi)
2/Hypotheses (Kufikiri Sababu Kwa kile ulichoona au kuhisi).
3/Prediction (Kukisia Jawabu la Suala Lako)
4/Experiment (Jaribio La Suala)
5/Fact (Baada ya Majaribio Mbalimbali-Several Positive Experiments)
Hizo Ndizo Njia (Method Nne ambazo Wanasayansi Wanatumia Katika Utafiti) Na Baada Ya Experiment jawabu litathibitisha Suala La Utafiti. Ikiwa Experiment mbalimbali zinathibitisha Jawabu Hilo basi Jawabu la Utafiti litakuwa ni La Ukweli na Litaitwa “Scientific Fact”
Ndugu zanguni Waislamu Sayansi zilizopo katika Kuruani Ni “FACTS” tupu na hii inathibitisha Kwamba Maneno ya Kuruani siyo ya Binaadamu. Allahu Akbar. Na pia Inathibitisha kwamba Mtume Mohamad ﷺ ni Mtume wa kweli.
Sayansi Imegawanywa na Wanasayansi katika Mafungu au Matawi Matatu:
A/Natural Sciences
B/Social Sciences
C/Formal Sciences
Sasa Tuchambue Matawi Haya Matatu:
A/Natural Sciences
Mlango wa Sayansi Hii Pia Umegawanywa katika Mafungu Matatu Yafuatayo:
1/Physical Sciences
2/Life Sciences
3/Earth Sciences
Kila Fungu katika Mafungu Haya Matatu Yamekusanya Matawi MbaliMbali:
1/Physical Sciences
Physics
Mechanics
Electromagnetics
Thermodynamics
Kinetics
Chemistry
Inorganic Chemistry
Electrochemistry
Analytical Chemistry
Earth Sciences
Planetary Science
Oceanography
Geology
Astrophysics
Polymer Science
Meteorology
etc.
2/Life Sciences
Anatomy
Botany
Biology
Zoology
Neurobiology
Marine Biology
Embryology
Ecology
Palaeontology
Genetics
Cell Biology
Ethology
NeuroScience
BioChemistry
Taxonomy
Morphology
Microbiology
Marine Biology
Biotechnology
Entomology
etc.
3/Earth Sciences
Astronomy
Meteorology
Atmospheric Sciences
Glaciology
Climatology
Structural Geology
etc.
Tuanze Kuchambua Kipengele cha pili cha Sayansi. Nacho ni Social Sciences
B/SOCIAL SCIENCES
Social Sciences pia zimegawanyika katika Mafungu mbalimbali yafuatayo:
Anthropology
History
Archaeology
Human Geography
Economics
Law
Development Studies
Education
Criminology
Political Science
Translation Studies
Media Studies
Business and Management
Philosophy
Health
International Relations
Linguistics
Custural Studies
Sociology
Physiology
etc.
C/FORMAL SCIENCES
Tuanze Kuchambue Kipengele cha Tatu cha Sayansi. Nacho ni Formal Sciences
Mathematics
Logic
Computer Science
Data Science
Statistics
Systems Science
Artificial Intelligence
Information Technology
etc.
Tuendelee na Safari Yetu isiyo na Mwisho.
Kuna Matawi Mengine Yameungana na Kuzalisha Tawi za Elimu Mpya.
Physics + Chemistry=Physical Chemistry
Astronomy + Physics=Astrophysics
Biology + Chemistry=BioChemisty/Organic Chemistry
Biology + Physics=BioPhysics
Biology +Geology=Palentology
Geology + Chemistry=GeoChemistry
Geology + Physics=Geophysics
Astonomy + Geology=AstroGeology
Sherehe Za kazi za baadhi ya Matawi Ya Elimu Mbalimbali yaliyozozuka hivi karibuni nazo ni kama zifuatazo:
Agronomy: Crop plants
Anthropology: Human past, behaviours, and cultures
Aeronautics: Airplanes and flights
Astronomy: Celestial Objects
Astrophysics: Understanding the working of the universe
Biotechnology: Creating/developing products using microorganisms
Cytology: Cell study
Engineering: Scientific principles and their applications
Exobiology: Extraterrestrial life
Forensic Science: Application of Science in legal process/criminal investigations
Materials Science: Study of properties of solid materials
Mycology: Study on Fungi
Ornithology: Study of birds
Psychology: Understanding the human mind and behaviour
Petrology: Rocks, origin, and characteristics
Radiology: Diagnosing and treating various diseases
Toxicology: Chemical components and their effects on living organisms
Virology: Study of Virus
Hapa Juu nimeelezea Orodha kubwa ya Elimu Mbalimbali za Kisasa ambazo hazikuwapo katika karne za Nyuma. Hizi ni Elimu za Kisasa ambazo zimezuka Kwa ajili ya Kuusoma Ulimwengu. Binaadamu tangu zamani anajitahidi kuusoma Ulimwengu na Dunia ili apate Kuishi Vizuri.
Matawi mbalimbali ya Elimu yamezuka Baada ya maendeleo ya Kisayansi. Elimu hizi zimekuja ili kutatua Matatizo ya Binaadamu na Kumsaidia aishi kwa salama na amani na pia katika kutafuta maisha yaliyo bora zaidi ya haya tunayoishi. Nadhani Katika Mlango huu sikutaja Matawi yote yaliyozuka kwa hiyo huenda kuna mengineyo zaidi ya haya lakini nina uhakika yaliyobaki siyo Mengi na kwa hakika yanatosha kwa kuendelea na utafiti wetu wa Kuruani na hadithi za Mtume.
Hebu Tuangalie Ufupisho wa Uhusiano baina ya Matawi tuliyokusanya hapa juu:
SCIENCE
Tunaweza Kugawa Sayansi Katika Mafungu Makubwa Matatu Makubwa.
A/Formal Science
Empirical Sciences
B/Natural Science
C/Formal Science
Kila Moja Ya haya matawi matatu tunaweza kuyagawa katika Foundation na Application. Yaani Msingi na Matumizi ya Elimu Hizi.
A/FORMAL SCIENCE
1/FOUNDATION YA FORMAL SCIENCE
Logic, Mathematics, Statistics
2/APPLICATION YA FORMAL SCIENCE
Matumizi ya Elimu hizi zimeweza Kutumika katika Computer Science etc.
Empirical Sciences
Empirical Sciences zimegawanyika katika Mafungu Mawili.
1/Natural Sciences
2/Social Sciences
Sasa Tuangalie Foundation na Application ya Matawi haya Mawili.
B/NATURAL SCIENCE
1/FOUNDATION YA NATURAL SCIENCE
Physics; Chemistry; Biology; Earth science; Astronomy
2/APPLICATION YA NATURAL SCIENCE
Engineering; Agricultural science; Medicine; Dentistry; Pharmacy
C/SOCIAL SCIENCE
1/FOUNDATION YA SOCIAL SCIENCES
Economics; Political science; Sociology; Psychology; Cultural anthropology
2/APPLICATION YA SOCIAL SCIENCES
Business administration; Jurisprudence; Pedagogy
KURUANI TUKUFU NA ULIMWENGU/MALIMWENGU
Elimu zote tulizozitaja hapa juu na nyinginezo ambazo hatukuzitaja na zile ambazo bado kuzuka yaani za siku za mbele zinashuhudia kwamba Mwenyeezi Mungu ni mkubwa sana tena sana. Kwa kweli Binaadamu bado wanahangaika Kuusoma Ulimwengu na kwa kweli tupo mwanzoni. Mpaka Leo kuna Mengi ambayo hatujui juu ya ujanja wetu wote tulionao.
Elimu za Mwenyeezi Mungu hazina Mwisho kama alivyosema katika kuruani tukufu kwamba Bahari zingelikuwa Wino na miti kalamu basi Wino ungelikwisha lakini Elimu zake hazina Mwisho. Tunaambiwa na Wataalamu kwamba Kuna Zillions na Zillions ya Galaxies. Huko hakuna ajuaye isipokuwa Mwenyeezi Mung tu peke yake. Ikiwa Hatujaisoma Galaxy yetu (inajuklikana kama Milky Way) je zinginezo? Kwa kweli hizo itabaki ndoto tu yaani haiwezekani hata kufikiria kwani zipo mbali sana. Leo hii wacha Galaxy bali Ardhi tu bado Hatujaimaliza. Hakuna Nchi iliyoweza Kufikia Planets zilizo mbali na sisi. Wanasayansi wameweza kufika katika Mwezi lakini hata huo Mwezi Bado hakuna aliyeweza kuisoma kila kitu. Kwa kweli Binaadamu bado tupo nyuma sana na hakuna Anayeweza Kujigamba. Allahu Akbar.
AYA ZA KURUANI ZINASHUHIDIA UKUBWA WA MWENYEEZI MUNGU MTUKUFU
Tumechambua hapa juu Elimu za Kisayansi na Mwono wa Wanasayansi Duniani kuhusu Matawi Mbalimbali. Sasa imefika wakati tufanye Utafiti katika Kuruani Tukufu kwa kupima Matawi tuliyoorodhesha hapa Juu na Maneno ya Kuruani ili tuone Picha Kamili. Nina imani kwamba Safari hii itatupa faida kubwa sana kwani Elimu hizi zote ni zake Mwenyeezi Mungu na Kuruani ni maneno yake.
Kwa hiyo lengo ni kusoma Elimu hizi kwa Msaada wa Kuruani Tukufu. Nadhani Umenifahamu. Nina imani kubwa kwamba Kuruani itatupa Msaada Kusoma Ulimwengu vizuri zaidi kuliko juhudi zetu. Tutafanya Utafiti kwa mifano. Na Pia Elimu hizi zitatufafanulia zaidi Ufahamu wa Aya za Kuruani. Nina imani kubwa kwamba Kuruani ni Ulimwengu tunaousoma na Ulimwengu ni Kuruani tunayoiona. Kwa hiyo twende mbele na tuanze kazi ambayo siyo ndogo lakini nzuri sana.
Katika Kuruani Sura Ya Al-Bayyina Namba 98 Aya Namba 2 na 3 Insema
رَسُولٌ۬ مِّنَ ٱللَّهِ يَتۡلُواْ صُحُفً۬ا مُّطَهَّرَةً۬ (٢) فِيہَا كُتُبٌ۬ قَيِّمَةٌ۬ (٣)
2. Mtume kutoka kwa Mwenyeezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakwaswa.
3. Ndani yake humo kuna Vitabu Madhubuti (Vya Hali Ya Juu)
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anasema kwamba kuruani imekusanya Kurasa zilizotakaswa yaani zimetoharishwa. Hakuna Upuuzi ndani yake. Na kisha anaendelea kutuambia kwamba Katika Kuruani utakuta Vitabu Madhubuti au Vitabu Vya Hali ya Juu, Au Sheria Madhubuti yaani Za Hali ya Juu. Neno linalokaribia zaidi ni Vitabu kutokana na neno Kutubun na siyo Sheria peke yake kama wanavyosema baadhi ya Wafasiri wa Kuruani Tukufu.
Suali ni “Vitabu Gani ambavyo vimekusanywa katika Kurasa za Kuruani Tukufu?”
Ukifanya Uchunguzi utaona ni kila Mafundisho waliyokuja nayo Manabii na Mitume wote waliopita. Mafundisho hayo au Ujumbe huo umekusanywa kwa njia ya Ufupisho na kwa hali ya Kimuujiza kwani imekusanya ujumbe wa Mitume wote tuliyoambiwa katika Hadithi za Mtume Jumla yao ni 124000 Ujumbe huo umekusanywa katika Kitabu hiki cha kuruani. Ukichunguza zaidi utakuta Kuna mafundisho au Vitabu mbalimbali vya nyanja mbalimbali za Elimu kama vile Kitabu cha FIqh, Kitabu cha Ndoa au Mafundisho ya Ndoa, Kuna kitabu Cha Hija, Kuna Kitabu Cha Tohara, Kuna kitabu cha Namna Ya Kufanya Biashara, Kuna kitabu cha Sala, Kuna Kitabu cha Zaka, Kuna kitabu cha Imani, Kuna kitabu cha Zakati, Kuna kitabu cha Elimu za Dunia yaani Kumetajwa kimuujiza Aya zinazozungumzia Elimu mbalimbali za Dunia na Vitabu Vinginevyo ambavyo tunavovijua na vile ambavyo hatuvijui na ambavyo vitahusu mambo ya baadaye.
KURUANI IMEKUSANYA ELIMU TUKUFU NA ZA HALI YA JUU
Kuruani Siyo kitabu cha Sayansi lakini ni Maneno ya Mwenyezi Mungu na maneno haya ni Tohara yaani Safi. Maneno haya ni mkusanyiko wa Vitabu vyenye Elimu za hali ya Juu sana.
Ukifanya utafiti utakuta Kuruani imekusanya Aya ambazo zinaashiria MIlango yote Mitatu Ya Sayansi za hali ya Juu. kuna Natural Sciences, Social Sciences na Formal Sciences. Kuruani Imekusanya Elimu za Sayansi za hali ya Juu. Ukisoma Kuruani kwa fahamu nzuri utaona ikekusanya Elimu za Ulimwengu wote na hakuna kilichobakia lakini kwa njia ya ufupisho na hekima ya hali ya juu. Hakuna Binaadamu anayeweza kufanya hivi. Kitabu cha Kuruani ni Muujiza mkubwa sana.
Inaendelea katika Mpango wa pili
UNIVERSITY/KURUANI-2