UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
PHILOSOPHY AU FALSAFA فلسفة
Alhamdulilah leo Tarehe 27/09/2022 na Mwenyeezi Mungu akipenda nitaendelea na safari ndefu ya kuelezea Baadhi ya Masomo tuliyoyataja katika Mlango ulipita University/Kuruani-1. Tutaanza na Somo la Msingi wa Elimu za Sayansi Duniani. Somo hili ni Philosophy. Lengo ni kuielezea Elimu hii kwa kifupi na Kisha Tuangalie Uhusiano wake na Kuruani Tukufu.
Kwanza kabisa ningependelea kusema kwamba Jina Philosophy lisikutishe. Kwa kweli Misamiati hutisha na utafikiri ni Elimu kubwa sana na ambayo inawahusu watu wa Vyuo vikuu tu peke yao. Hata Kidogo. Tusibabaike. Ni Elimu kama Elimu nyinginezo na kila mtu anahaki ya kusoma. Elimu sizizoeleweka siyo Elimu nzuri. Elimu nzuri ni ile yenye kueleweka na yenye faida katika Maisha. Huu ni mwono wangu.
Katika Mlango huu mdogo nitajitahidi kufupisha Na kwa njia ya Kueleweka ili tunayosoma yatufaidikie.
Ukisoma Historia ya Elimu hii utakuta ilianzia Miaka Mingi iliyopita katika Nchi mbalimbali za Dunia kama vile Egypt karibu miaka 4000 kabla ya Enzi za Ukristo (BCE au Before Christian Era).Na katika Enzi hiyo hiyo kuna Nchi nyinginezo kama vile Mesopotamia (Iraq) Mwaka 2150 B.C.E. India 1500-500 B.C.E. Persia 1500 B.C.E. China c. 1046-256 B.C.E. Greece c. 585-322 B.C.E. Rome c. 155 BCE.
Kihistoria Sayansi na Jina pia Limebadilika. Hapo Zamani Lilileta maana Nyingine na Huko Ugiriki Elimu hii iliitwa Jina la “PHILOSOPHY” Na Jina hili asili yake ni Kigiriki. Philo ina maana ya “Kupenda” na “Sophia” maana yake ni “”Busara” Na Ukiunga Philo na Sophia Maana inakuwa “Love of Wisdom” yaani “Kupenda Ubusara” Hii Ndiyo Asili ya Maana ya neno hili.
The word philosophy comes from the Greek philo (love) and sophia (wisdom) and so is literally defined as “the love of wisdom”
Elimu hii ilizuka hapo zamani ili kujibu masuala magumu. Na mpaka hivi sasa Elimu hii inatumika na inafundishwa mashuleni. Tatizo ni kwamba Watu bado wanahangaika kutafuta Majibu ya Masuali kama vile Dunia Imezuka Vipi. Akili ni kitu gani? Fikra ni Nini? Mungu ni Nani? Mungu alizuka Vipi? Je Ulimwengu Ulizuka Vipi? Na Masuali Mbalimbali Mengineyo. Haya ndiyo Masuali ya Falsafa. Binaadamu anataka kujua Baada ya Kufariki tunakwenda wapi? Je Mwenyeezi Mungu alizuka Vipi?
Elimu Hii siyo mbaya kwani ina mazuri yake pia. Elimu hii ndiyo imealisha Sayansi. Kwani Enzi hizo kulikuwa Hakuna Sayansi kama leo. Kulikuwa Philosophy au Falsafa na baadaye Ikazaliwa Natural Philosophy yaani Kabla Ya Sayansi.
Inategemea namna Tunavyoitumia. Ukitumia Elimu yeyote kwa njia nzuri utapata faida na ukitumia Elimu yeyote kwa nia mbaya utapata Hasara.
Ajabu ni kwamba Majawabu ya Masuala haya yalikwisha Kujibiwa Na Mwenyeezi Mungu katika Ujumbe wa Manabii wote kuanzia Kiumbe wa kwanza Kuumbwa yaani Nabii Adam. Uislamu haukuanzia Na Mtume Mohamad bali Tangu Kuumbwa Dunia. Mwenyeezi Mungu alituma Manabii 124000 na hawa walitumwa katika Nyakati mbalimbali na Kila mmoja alikuja Na Mfundisho.
Kwa kawaida Binaadamu ana Masuali mengi sana. Majibu yapo lakini watajitahidi kutafuta kwingineko. Na ndiyo maana Elimu hii ya Philosophy ilizuka.
Alhamdulilah Neema Kubwa Ya Uislamu na Pia Dini ya Mbinguni ambazo Mwenyeezi Mungu ametuma Manabii kutoka Kuumba Dunia. Dini hizi za Mbinguni zilikuja Kujibu Masuala haya Magumu yasiyoweza kujibika kwa kutumia Akili.
Katika Kuruani Kuna Philosophy ya Hali ya Juu ambayo tutaizungumza baadaye na Ndiyo maana nikasema Elimu hii siyo mbaya iwapo utaitumia vizuri.
Sasa ni nini Tofauti baina ya Sayansi na Philosophy?
Jawabu rahisi ni kwamba Katika Utafiti Sayansi Inahitaji Kuona na Majaribio (Experiment) Lakini Philosophy inahitaji Utrafiti kwa Kutumia Fikra au Ubongo peke yake (Reasoning). Kwa hiyo Philosopher anafanya utafiti kwa kufikiri na Mwana Sayansi anafanya Utafiti kwa Kutumia Vifaa mbalimbali vya utafiti yaani Kwa Kuona. Na Hii inajulikana Kama Empirical Data.
Philosopher waliojulikana duniani kupitia katika Karne Mbalimbali ni wengi duniani. Ningepedelea kuwataja wachache nao ni:
Greece:Aristotle/Epicurus/Heraclitus/Plato/Pythagoras Socrates. Na Wengineo
Asian/Eastern philosophers:Avicenna/Confucius/ Gautama (the Gautama Buddha)/Omar Khayyám. Na Wengineo ambao Sikuwataja.
Later European/western philosophers: Sikuwataja kwani Wengi
Modern European and American philosophers:
Sikuwataja kwani Wengi
MAANA YA PHILOSOPHY فلسفة KATIKA KIWANGO CHA KITAALUMA (ACADEMIC LEVEL)NA MGAWANYIKO WA MASOMO YAKE
Kufuatana Na Masuala mbalimbali Philosophy inafanya Utafiti katika Nyanja Zifuatazo:
1/Metaphysics
Uwanja huu umeganyika katika Nyanja Zingine Tatu:
1/Ontology. Uwanja huu unauliza maswali kama vile “Dunia ni Kitu Gani?” au “Uhakika Ni Kitu Gani?” na Masuala Mengineyo Mbalimbali
2/Falsafa ya Fikra (Mind)
Masuala yanyohusu Fikra Na Masuala Mengineyo Mbalimbali
3/Falsafa Ya Dini.
Masuala Ya Kidini na Masuala Mengineyo Mbalimbali
2/Epistemology
Uwanja Huu unahusu masuala kama vile. “Elimu ni kitu gani?” au “Sayansi Ni Kitu Gani?” au “Ukweli ni nini? Na Masuala Mengineyo Mbalimbali
3/Ethics
Uwanja Huu unahusu masuala kama vile ” Ni nini Zuri Na Baya” au “Haki Ni Nini” au “Kosa na Sahihi ni Nini?” Na Masuala Mengineyo Mbalimbali.
4/Aesthetics
Uwanja Huu unahusu masuala kama vile. “Ni nini Uzuri?” “Je vitu Vizuri vinapendeza?” au ” Je vitu vya Ukweli Vizuri?” Na Masuala Mengineyo Mbalimbali.
5/Logic
Uwanja Huu unahusu masuala kama vile.”Maneno Tunayotumia Yana Maana Gani?” au “Je mawazo yanaweza Kuwakilishwa na Lugha?” au Je kwa vipi tunaweza Kufikiri kwa usahihi”? Na Masuala Mengineyo Mbalimbali.
6/Axiology
Uwanja Huu unahusu masuala kama vile. “Je wakati ni Pesa au ni sisi tuliyofanya iwe hivyo?” au “Kitu gani Kina Thamani? Na Masuala Mengineyo Mbalimbali.
PHILOSOPHY NA KURUANI TUKUFU
Naona Wakati umefika wa Kuanza Kuielezea Kuruani. Nadhani Maelezo hapa Juu yanatosha kutoa Mwanga wa Elimu ya Philosophy kwa ufupi.
Tumeona Milango mbalimbali Ya Utafiti wa Elimu ya Philosophy na Kwa hiyo Sasa tutachagua Mlango mmoja tu ambao ndiyo tutautumia Katika Utafiti Wa Kuruani. Kwa kweli Kuruani ndiyo itatufundisha Falsafa na siyo Kinyume. Kuruani siyo Kitabu cha Sayansi bali Ni Muujiza ambao umegusia kila kitu Ulimwenguni kwa hiyo siyo mbaya Kuisoma kwani Mwenyeezi Mungu amehimiza Tufanye Hivyo. Amesema mara kwa mara Katika Kuruani Tufikiri Aya Zake ili tuone ukubwa na Utukufu wake.
Uwanja Nitakaotumia ni Elimu Ya LOGIC na Itabidi pia Tuisome Elimu hii kabla ya Kuruani Tukufu. Tuisome Kwani Ni Elimu kubwa Sana. Kila Uwanja hapa Juu ni Mkubwa kwani kuna Nyenzo mbalimblai zinazotumiwa na Nyanja Hizi kufuatana na Mazingara yake.
LOGIC المنطق
Kwa kifupi Elimu ya Logic ni mojawapo ya Nyanja za Falsafa au Philosophy.
Logic Ni Sayansi ambayo inashughulika na Kutathmini (Evaluate) Hoja (Argument). au Kwa Lugha ya Kiingereza tutasema:
Logic is the Science used to evaluate an Argument
Ni Elimu ambayo itakulinda wewe katika Kujiepusha na Fikra Mbaya, au Uwongo.
Hoja au Argument ni Maneno ambayo Yanatumika katika Kuthibitisha Fikra.
Hoja Zimegawanyika katika Sehemu Mbili:
1/Ushahidi wa Kuthibitisha Fikra zako (Premises)
2/Na Hitimisho au Jawabu la Ushahidi. (Conclusion)
Kuna Viashirio (Indicators) vya Kimaneno katika Ushahidi na Pia Hitimisho.
Wakati Mwingine Hakuna Viashirio. Na Ikiwa Hakuna Basi Itabidi Uchunguze Hja Hiyo kwa kufikiri.
Viashirio Vinasaidia Kuelewa Aina Ya hoja Iwapo ni Deductive au Inductive. Kwa kiswahili Viashirio husaidia katika kuelewa aina Ya Hoja iwapo ina uhakika (Deductive) au Hakuna Uhakika(Inductive).
Maneno Yanayotumika katika aina Ya hoja Deductive au Hoja Inayokubalika kiakili ni kama vile:
“Kwa hakika” na Maneno mengineyo ya aina hii.
Maneno Yanayotumika katika aina Ya hoja Inductive au Hoja Isiyo na Uhakika ni kama vile:
“Labda” au “Huenda”
Na Iwapo Indicators au Viashirio havipo basi unaweza kuelewa kwa kuchunguza maana ya Hoja hiyo. Ufikiri vizuri hoja mwelekeo au Mfumo wa hoja hiyo,
Nadhani Tumepata Picha Ya somo la LOGIC
Sasa Tuanze Kuisoma kuruani Na Tuchunguze Elimu hii ya Philosophy na Uwanja huu wa Logic ili tupate Kuelewa Elimu hii kwa uzuri zaidi. Inshaallah hata kama Hapa Juu haikueleweka Nina Uhakika Kuruani itatupa Mwanga Vizuri Zaidi kwani Unapotatanika Katika Jambo Lolote utapata Jawabu katika Kuruani. Kuruani ni Mwalimu Mkubwa Kuliko wote.
PHILOSOPHY-LOGIC (علم المنطق) (YA KURUANI TUKUFU
Logic Kwa Kiswahili safi ni “BUSARA” au “HEKIMA” kwa kiingereza “WISDOM” au “LOGIC”
Sasa hebu tuchunguze Aya za Kuruani Zifuatazo tuangalie Busara aliyotumia Nabii Ibrahim katika Mazungmzo yake Na Mjomba wake “Azar” Katika Aya Hizi tutaona Nabii Ibrahim anatumia LOGIC au “Wisdom” katika Klingania Dini ya Mungu mmoja. Hebu Tuzichunguze kisha Tufanye Uchambuzi wa Ki Logic.
Sura Namba 6 Aya Namba 75 Mpaka 80 Sura Ya Al-Anaam
سُوۡرَةُ الاٴنعَام
وَكَذَٲلِكَ نُرِىٓ إِبۡرَٲهِيمَ مَلَكُوتَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلِيَكُونَ مِنَ ٱلۡمُوقِنِينَ (٧٥) فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبً۬اۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّىۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأَفِلِينَ (٧٦) فَلَمَّا رَءَا ٱلۡقَمَرَ بَازِغً۬ا قَالَ هَـٰذَا رَبِّىۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَٮِٕن لَّمۡ يَہۡدِنِى رَبِّى لَأَڪُونَنَّ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلضَّآلِّينَ (٧٧) فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمۡسَ بَازِغَةً۬ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى هَـٰذَآ أَڪۡبَرُۖ فَلَمَّآ أَفَلَتۡ قَالَ يَـٰقَوۡمِ إِنِّى بَرِىٓءٌ۬ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ (٧٨) إِنِّى وَجَّهۡتُ وَجۡهِىَ لِلَّذِى فَطَرَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ حَنِيفً۬اۖ وَمَآ أَنَا۟ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ (٧٩) وَحَآجَّهُ ۥ قَوۡمُهُ ۥۚ قَالَ أَتُحَـٰٓجُّوٓنِّى فِى ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَٮٰنِۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشۡرِكُونَ بِهِۦۤ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّى شَيۡـًٔ۬اۗ وَسِعَ رَبِّى ڪُلَّ شَىۡءٍ عِلۡمًاۗ أَفَلَا تَتَذَڪَّرُونَ (٨٠)
TAFSIRI
75. Na namna hivi tulimwonyesha lbrahimu ufalme wa mbingu na ardhi (kuwa ni wa Mungu), na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
76. Na usiku ulipomwingilia (lbrahimu na hali kakaa na makafiri), akaona nyota, alinena (makusudi kutaka kuwavuta watumie fikira zao): “(Nyota) hii ni Mola wangu.” Ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia wale makafiri kama kwamba yu pamoja nao katika ibada ile): “Sipendi wale wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).”
77. Na (usiku wa pili) alipouona mwezi unachomoza alisema (kuwaambia wale maraftki zake wa kikafiri): “Huu (mwezi) ndio Mola wangu.” Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotofu (wapotevu). (Na mola huyu hawezi kuniongoza kwani anakuwa hayupo wakati mwengine).”
78. Na (siku ya tatu) alipoliona jua linachomoza alisema (kuwaambia): “Hili (jua) ndilo Mola wangu. Huyu Mola mkubwa kabisa.” Lilipotua alisema: “Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha (na Mungu).,
79. “Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu) si miongoni mwa washirikina.”
8o. Na watu wake wakajadiliana naye (kwa kumwambia Unaacha ibada ya wazee! Utadhurika)! Akasema: “Je, Mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali yeye ameniongoa? Wala siogopi wale mnaowashirikisha naye. Isipokuwa Mola wangu akipenda jambo (kuwa, basi litakuwa). Mola wangu anakijua vyema kila kitu. Basi je, hamshiki mauidha (Hamzindukani)?”
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu alimpa Nabii Ibrahim Elimu ya Mantiq au Logic au Philosophy ya hali ya Juu. Aliruzukiwa Imani Kubwa sana. Katika Tafsiri Hapa Juu angalia Namna alivyokuwa akihojiana na Makafiri. Hii ndiyo Philosophy na Logic tuliyoizungumza hapa juu.
Ametoa Hoja Tatu katika Siku Tatu. Kila Siku anawapa Hoja Moja bila ya Haraka. Kidogo kidogo. Kawapa Ushahidi kwa Hekima na Busara. Hatua kwa Hatua.
Siku ya kwanza akawapa Hoja au Ushahidi wa kwanza ili kuthibitisha Imani yake aliyoificha mbele ya wale Makafiri kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mkubwa na yeye ndiye aliyeumba kila kitu. Akawaonyesha Nyota na akawaambia Makafiri waliokuwa naye kwamba huyu ndiyo Mungu Wake. Na Nyota hiyo ilipotua akawaambia kwamba Yeye hapendi Miungu inayopotea. (Kwani Kupotea kwao kunaonyesha udhaifu na kwamba Imeumbwa na haina faida wakati huo inapopotea)
Siku ya Pili akawapa Hoja au Ushahidi wa Pili ili kuthibitisha Imani yake aliyoificha mbele ya wale Makafiri kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mkubwa na yeye ndiye aliyeumba kila kitu. Akawaonyesha Mwezi ulipochomoza akasema tena maneno yale yale kama alivyosema siku ya Kwanza Kwamba Huyu ndiye Mungu wake. Na mwezi Ulipotua akasema Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotofu (wapotevu). (Na mola huyu hawezi kuniongoza kwani anakuwa hayupo wakati mwengine).”
Na Siku ya Jua akawapa Hoja au Ushahidi wa Tatu ili kuthibitisha Imani yake aliyoificha mbele ya wale Makafiri kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mkubwa na yeye ndiye aliyeumba kila kitu. Akawaonyesha Jua Lilipochomoza akasema tena maneno yale yale kama alivyosema siku ya Kwanza Kwamba Huyu ndiye Mungu wake. : “Hili (jua) ndilo Mola wangu. Huyu Mola mkubwa kabisa.” Lilipotua alisema: “Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo Mnayoyashirikisha na Mwenyeezi Mungu.
Na hapo akaendelea kufichua ukweli bila khofu yeyote na kuwaambia “Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu) si miongoni mwa washirikina.” Na watu wake wakajadiliana naye (kwa kumwambia Unaacha ibada ya wazee! Utadhurika)! Akasema: “Je, Mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali yeye ameniongoa? Wala siogopi wale mnaowashirikisha naye. Isipokuwa Mola wangu akipenda jambo (kuwa, basi litakuwa). Mola wangu anakijua vyema kila kitu. Basi je, hamshiki mauidha (Hamzindukani)?”
Hii ndiyo Logic ya Mazungumzo.
Kwa hiyo tukitumia Elimu ya Logic katika kuchambua Aya hii utaona kama ifuatavyo:
1/Siku ya Kwanza (Argument aju Hoja inayojulikana kama Premises au Ushahidi wa Kwanza)
2/Siku ya Pili ((Argument au Hoja inayojulikana kama Premises au Ushahidi wa Pili)
3/Siku ya Tatu((Argument au Hoja inayojulikana kama Premises au Ushahidi wa Tatu).
Aya namba 79 ndiyo inajulikana katika Elimu ya Logic kama Conclusion. Kwani ndilo Linalohitaji Ushahidi. Ushahidi mara 3 ili kuthibitisha yaliyopo katika Aya namba 79 ambayo inasema:
“Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu) si miongoni mwa washirikina.”
Na ukichunguza Aya hapa juu utaona ni Deductive kwani Ushahidi wote ulitolewa Unakubalika bila Shaka Yeyote. Kwani Hakuna Badili. Nyota, Mwezi na Jua zote ni Viumbe ambavyo havipo Milele bali huja na kupotea na Siku ya kiyama vitapotea kabisa na hata Sayansi inasema hivyo na siyo Kuruani peke yake. Na Conclusion pia ni Sahihi bila Shaka Yeyote. Kwa hiyo Ninavyoona mimi huu ni Mfano Mmojawapo Mzuri sana wa Logic katika Kuruani Tukufu.Kuruani inatufundisha Elimu ya Logic katika Madakika Machache na kwa lugha Rahisi kueleweka. Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi iwapo nimesibu au nimefanya makosa. Ni Utafiti ambao Lengo ni kupata Thawabu. Alhamdulilah.
Bado Sijamaliza Kuelezea Elimu ya Philosophy katika Kuruani kwani kuna Mifano mbalimbali. Kwa leo naishia hapa. Nia Yangu ni kuendelea baadaye Mwenyeezi Mungu Akitupa Uhai. Kwa hiyo tutakutana Tena Hivi karibuni Inshaallah……………..