UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
MILANGO YA ELIMU YA FIQH (JURISPRUDENCE)
DIBAJI
FIQH ni Elimu kubwa na kwa hiyo Mwenyeezi Mungu akipenda nitaelezea kila siku kidogo kidogo.Tusisahau Metali isemayo “Ndo Ndo Ndo Hujaza Ndoo”
Inshallah Kwa Uwezo wake Mwenyeezi Mungu nitajitahidi kurahisisha Elimu hii ili ipate kueleweka kwa urahisi kwani baada ya utafiti wa muda mrefu sijapata kitabu au vitabu vilivyokusanya Elimu hii kwa ukamilifu na kwa maelezo mepesi.
Kuna Vitabu mbalimbali vinavyozungumzia sheria zinazohusiana na Sala, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi Mtukufu, Kwenda Hija, Kufunga Ndoa, Kufanya Mazishi, Biashara, Kufanya Udhu na Mengineyo Mbalimbali. Na kuna vitabu vinginevyo vinavyozungumzia Namna ya Sheria hizi zilivyopatikana au Asili ya Sheria hizi zilivyopatikana. Kuna vitabu vingine vimetumia misamiati migumu ambayo hayafahamiki hata kwa kutumia kamusi na hali hii inasabisha watu waiogope Elimu hii. Ukichunguza utaona Vitabu Vingi viliandikwa kwa ajili ya Wanafunzi mashuleni. Kwa hiyo nimeona bora niielezee kwa njia nyingine nikiwa na tamaa kwamba huenda itaeleweka na watu wote na siyo mashuleni peke yake. (Academic Purposes). Sisemi kwamba Katika website hii nitaelezea Elimu yote ya FIQH lakini nitajitahidi kuelezea Kwa ufupi na kwa kutumia lugha na maelezo kwa njia rahisi (Simple).
UTANGULIZI
Elimu Hii siyo ndogo. Wataalamu/Wanavyuoni walifanya kazi kubwa ambayo matunda yake tunayaona katika maandishi yaliyopo leo. Wakati wa Mtume (Sala na Amani zake Mola zimfikie) kulikuwa hakuna tatizo kwani kunapokuwa na swali lolote basi Mtume (Sala na Amani zake Mola zimfikie)alikuwa akijibu maswala ya watu yanapozuka. Baada ya Kufariki kwa Mtume na baada ya muda mrefu kupita wanavyuoni ilibidi watumie mbinu mbali mbali ili kutatua maswali hayo. Elimu mbali mbali ilibidi zitumike katika kusaidia kujibu masuala hayo. Kwa mfano Usul Al-Fiqh (Science of Jurispudence). Na Elimu nyinginezo kama vile Hadithi na Tafsiri pia zilichangia katika kutatua mizozo yanayotokana na masuala ya dini.Nitagusia Misamiati ya Elimu Ya FIQH, Malengo Ya Elimu Hii, na Madhehebu yalivyoibuka Kisha tutaendelea na Masuala Mengineyo ya FIQH na USUL-ALFIQH.
FIQH
MAANA YA NENO FIQH
Kwa kifupi Neno FIGH maana yake “FAHAMISHO” yaani kufahamisha, au kufundisha.
Hebu tuangalie Tafsiri ya Aya ifuatayo ili tupate kuelewa maana ya neno FIQH.
Aya Sura Ya Hud Namba 11 Aya Namba 91 Mwenyeezi Mungu anasema
قَالُواْ يَـٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرً۬ا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَٮٰكَ فِينَا ضَعِيفً۬اۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَـٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٍ۬ (٩١)
Neno نَفۡقَهُ katika Ibara مَا نَفۡقَهُ كَثِيرً۬ا مِّمَّا تَقُولُ lina maana ya kufahamu. Tafsiri Ya Aya Ni
91- Wakasema: “Ewe Shuebu! Hatufah’amu mengi katika hayo unayoyasema. Na sisi tunakuona mdhalilifu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tungekupiga mawe, wala wewe si mTu mtukufu kwetu! (ila tunachunga hishima ya jamaa zako tu).”
Na kuna Hadithi Ya Mtume (Sala na Amani zake Mola Zimfikie)
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عُفَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ قَالَ حُمَيْدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ سَمِعْتُ مُعَاوِيَةَ، خَطِيبًا يَقُولُ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ “ مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ، وَإِنَّمَا أَنَا قَاسِمٌ وَاللَّهُ يُعْطِي، وَلَنْ تَزَالَ هَذِهِ الأُمَّةُ قَائِمَةً عَلَى أَمْرِ اللَّهِ لاَ يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللَّهِ ”.
Tafsiri ya kipande nilichopigia mstari ambacho kina neno FIGH ni kama ifuatavyo:
“Yule ambaye Mwenyeezi Mungu atamtakia Kheri basi atamfahamisha (atamfundisha) dini”.
Tafsiri Ya Hadithi Yote kwa Kiingereza ni kama ifuatayo hapa chini
I heard Allah’s Messenger (ﷺ) saying, “If Allah wants to do good to a person, He makes him comprehend the religion. I am just a distributor, but the grant is from Allah. (And remember) that this nation (true Muslims) will keep on following Allah’s teachings strictly and they will not be harmed by any one going on a different path till Allah’s order (Day of Judgment) is established.”
Hadithi Hii imekusanywa katika kitabu cha Imam Al-Bukhari na Kama tunavyoelewa Hadithi za Bukhari ni Sahihi.
Kufuatana na Ushahidi hapa juu tunasoma kwamba neno FIQH kwa lugha ya kiswahili maana yake ni Kufahamisha, kufundisha au kuelewesha.
Maana Ya FIQH kwa Kiingereza (Definition of FIQH):
Fiqh is Islamic jurisprudence. Fiqh is often described as the human understanding and practices of the sharia, that is human understanding of the divine Islamic law as revealed in the Quran and the Sunnah (the teachings and practices of the Islamic prophet Muhammad and his companions).
LENGO LA ELIMU YA FIQH
Kwa hiyo Lengo la Elimu ya FIQH ni kufahamisha Sheria za milango mbali mbali ya dini. Kwa mfano FIQH imekuja kutufahamisha na kutufundisha namna ya kuswali Swala Za Faradhi na Sunnah, Kufunga, Kutoa Zaka, Kufunga mwezi mtukufi wa Ramadhan, kwenda hija, Kufanya Udhu Na mambo mengineyo katika Dini.
USU AL-FIQH
Asili ya Hizi Sheria za FIQH ni Kuruani na Hadithi Za Mtume (Sala na Amani zake mola zimfikie). Yaani Sheria mbalimbali za Dini asili yake ni Kuruani na Sunnah. Na Elimu inayotakikana katika kuzalisha Sheria Hizi kutoka katika Kuruani na Sunnah ni USUL AL-FIQH.
Usul al-fiqh, the sources of Islamic law and the discipline dedicated to elucidating them and their relationship to the substantive rulings of the law.
Katika Website hii haiwezekani kuelezea Elimu zote za FIQH na USUL AL-FIQH. bali nitajitahidi kuelezea kwa njia rahisi na ufupi kwa kutumia mifano.
MADHEHEBU (SCHOOL OF LEGAL THOUGHTS)
Elimu hii ya FIQH imesababisha kuzaliwa kwa Madhehebu Mbalimbali kama vile Hanafi, Awza’i, Maliki, Zaydi, Laythi, Thawri, Shaf’i, Hambali, Dhahiree, na Jareeri. Katika Madhehebu haya kuna mengineyo ambao yalikufa na katika yaliyobaki Manne tu ndiyo yaliyoenea kwa wingi Duniani ambayo ni Hambali, Shafi’i, Maliki na Hanafi.
Yaani kule kutofautiana katika kufasiri Baadhi ya Aya za Kuruani na Sunnah (Vitendo na Kauli za Mtume Mohamed Sala na Amani yake mola zimfikie) na Yale Masuala ambayo hayakujibiwa na Kuruani au Hadithi za Mtume (Sala na Amani Yake Mola Zimfikie) yalitatuliwa kwa kutumia vyombo mbali mbali, hali hii ilisababisha kuzaliwa kwa makundi mbali mbali ya Wanavyuoni ambao kila kikundi kilikuwa na kiongozi wake. Kila Kikundi au Shule (Madhhab) kilitofautiana na kingine katika Kutumia Vyombo hivi Vya Utafiti wa Sheria. Au kwa Lugha Nyingine walitofautiana METHODOLOGY au njia ya kutatua maswali yaliyokuwa hayana jibu kutoka katika Kuruani na Hadithi
Vikundi hivi vinajulikana kwa Jina MADHHABS au kwa lugha ya kiingereza “School of Legal Thoughts.
Kwa Mfano Madhehebu Manne Maarufu Ni Kama Zifuatazo:
Hanafi Madhhab
Shafii Madhhab
Hambali Madhhab
Maliki Madhhab
Na kuna Vikundi vinginevyo ambavyo vilizuka lakini katika website hii tumechagua vile mashuhuri au maarufu peke yake.
Kila Kikundi au Shule kilikusanya Wanavyuoni ambao walikuwa wataalamu katika nyanja mbalimbali za FIQH Kwa lugha ya leo tunaweza kuwaita Professors. (Wataalamu)
MADHEHEBU DUNIANI
Shule au Madhehebu Manne; Hanafi, Maliki, Shafi’i na Hambali yamesambaa na kuenea duniani kama ifuatavyo:
Hanafi Imeenea karika nchi zifuatazo: Turkey, the Balkans, the Levant, Central Asia, Indian subcontinent, China, Alexandria Egypt, Na Russia’s Muslim community.
Maliki Imeenea North Africa, West Africa Na Eastern Arabia
Shafi’i katika nchi zifuatazo: Kurdistan, Indonesia, Malaysia, Brunei, Cairo Egypt, East Africa, Southern Yemen, na Southern parts of India
Hanbali katika Saudi Arabia
WANAFUNZI NA WAFUASI WA MADHEHEBU MANNE
Kila Shule au Madhehebu ilikusanya Maelfu ya Wanafunzi waliokuwa Wataalamu wa Nyanja mbali mbali za dini ya kiislamu. (Walikuwa Wataalamu au Experts of Hadith za Mtume (Muhadithuun) , Experts of Tafseer (Mufasiruun) Experts of Fiqh (Fuqahaa), Experts in Arabic) Orodha ya Wanavyuoni hapa chini ni Baadhi chache ya hao.
IMAM SHAF’II (Abū ʿAbdillāh Muhammad ibn Idrīs al-Shāfiʿī (Arabic: أَبُو عَبْدِ ٱللهِ مُحَمَّدُ بْنُ إِدْرِيسَ ٱلشَّافِعِيُّ, 767–820 CE)
Katika baadhi ya wanavyuoni waliomfuata Imamu Shafi’i ni Bayhaqi,Al-Suyuti, Al-Dhahabi, Al-Ghazali, Ibn Hajar Asqalani, Ibn Kathir, Yahya ibn Sharaf Al-Nawawi, Al-Mawardi na Al Muzani.
IMAM MALIKI (Malik ibn Anas (Arabic: مَالِك بن أَنَس, 711–795 CE / 93–179 AH)
Katika baadhi ya Wanavyuoni waliomfuata Imamu Maliki ni Ibn Rushd (Averroes) (1126–1198 philosopher and scholar) Al-Qurtubi (1214–1273) Ibn Battuta (February 24, 1304 – 1377), explorer Ibn Khaldūn (1332/AH 732–1406/AH 808), scholar, historian and author of the Muqaddimah Usman dan Fodio (1754–1817), founder of the Sokoto Caliphate and Omar Mukhtar (1862–1931), Libyan resistance leader
IMAM ABU HANIFA Abū Ḥanīfa al-Nuʿmān b. Thābit b. Zūṭā b. Marzubān (Arabic: أبو حنيفة نعمان بن ثابت بن زوطا بن مرزبان; c. 699 – 767 CE),
Wanafunzi maarufu wa Abu Hanifa ni Imam Abu Yusuf aliyekuwa Mkuu wa Mahakimu wa kwanza katika Uislamu, Mwanafunzi mwingine maarufu ni Imām Muhammad al-Shaybani aliyekuwa mwalimu wa FIQH katika shule ya Imam Al-Shafi’i. Yusuf ibn Abd al-Rahman al-Mizzi amewataja wanafunzi wengine 97 ambao walikuwa maarufu katika Elimu ya FIQH na ambao hadithi zao zipo katika vitabu vya Sahih al-Bukhari, Sahih Muslim na vutabu vinginevyo vya hadithi.Imām Badr al-Din al-Ayni amewataja wanafunzi 200 ambao wamsoma hadithi na FIQH kutoka kwa Abu Hanifa.
1/Abdullah ibn Mubarak 2/ Abu Nuāim Fadl Ibn Dukain 3/ Malik bin Mighwal 4/ Dawood Taa’ee 5/ Mandil bin Ali 6/ Qaasim bin Ma’n 7/ Hayyaaj bin Bistaam 8/ Hushaym bin Basheer Sulami 9/ Fudhayl bin Iyaadh 10/ Ali bin Tibyaan 11/ Wakee bin Jarrah 12/ Amr bin Maymoon 13/ Abu Ismah 14/ Zuhayr bin Mu’aawiyah 15/ Aafiyah bin Yazeed
IMAM HAMBALI (Aḥmad ibn Ḥanbal (أَحْمَد ابْن حَنۢبَل), or Ibn Ḥanbal (ابْن حَنۢبَل)(780–855 CE/164–241 AH),
Alikuwa na wanafunzi wengi na hapa nitataja baadhi ya wanafunzi wake.
1. Abu Al-Hasan Ali Ibn Muhammad Al-Mawardi 2. Abu Bakr Al-Athram 3. Salih Bin Ahmad (Imam’s son) 4. Abdullah Bin Ahmad (Imam’s son) 5. Abu Dawood Sulayman (famously known as Abu Dawood) 6. Hambal bin Ishaaq. 7. Imam Bukhari 8. Imam Muslim.
BAADHI YA MISAMIATI YA ELIMU YA USUL AL-FIQH NA MAANA YAKE
Kuna Misamiaiti mingine ambayo sikuweza kuielezea yote bali baadhi yake ambayo yanatosha kwa Darasa la Mlango huu wa FIQH
Kwanza Ningependelea kuzungumzia maana ya Neno IJTIHAD.
IJTIHAD
Katika FIQH neno hili lina maana ya Ni kutatua Masuala Ya Dini kwa kutumia Fikra. Hii Ni Kazi ya Hakimu wa Kiislamu katika Elimu ya FIQH. (Jurisprudence) Watafiti wanasema kwamba Milango ya IJTIHAD ilisimakishwa kuanzia karne ya Tatu yaani tangu kuja kwa Uislamu Kufuatana na Calendar ya Kiislamu na ni sawa na Karne ya 9 Ya Calendar za Kileo yaani Solar Calendar. Milango hii ilisimamishwa baada ya wanavyuoni hawa kuona kwamba Hakuna Masuala Yaliyobaki ambayo yanahitaji IJTIHAD au Kutumia Fikra (Reasoning). Kufungwa kwa milango ya IJTIHAD (“Closing the door of Ijtihad”) na wanavyuoni walikuja na Fikra nyingine ya Kutumia TAQLIYD
Ijtihād, (Arabic: “effort”) in Islamic law, the independent or original interpretation of problems not precisely covered by the Qurʾān, Hadith (traditions concerning the Prophet Muhammad’s life and utterances), and ijmāʿ (scholarly consensus)
TAQLIYD
Katika FIQH neno Taqliyd ni Kukopi Majawabu ya masuala ya dini magumu kutoka katika Kipindi cha Mtume na kuisimamisha IJTIHAD ambayo inahitaji FIKRA. Wanavyuoni waliogopea kutumia FIKRA kwani inaweza kusababisha kuzusha Mapya yaani BID’AA. Yaani Mambo mapya ambayo hayapo katika Dini Ya kiislamu. Aliyepewa madaraka kushughulika na IJTIHAD anajulikana kama MUJTAHID na Yule aliyepewa madaraka katika Elimu ya TAQLIYD ni MUQALID
Taqliyd in Islamic law, the unquestioning acceptance of the legal decisions of another without knowing the basis of those decisions. … Henceforward, all were to accept the decisions of the early authorities—i.e., to exercise taqlīd toward them. This doctrine is usually expressed as “the closing of the gates of ijtihād.”)
Wanavyuoni wa kila Shule (School of Thought) walifuata utaratibu ufuatao katika Utafiti wa Masuala ya Kiislamu kutumia Nyanja au asili zifuatazo:
1/KURUANI TUKUFU
Kitabu Kilichokusanya Maneno Matukufu ya Mwenyeezi Mungu aliyetukuka. Ni Hotuba yake kwetu sisi binaadamu na majini.
2/SUNNAH ZA MTUME (Sala na Amani yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Ni Vitendo na Kauli za Mtume Mohamed. (Sala na Amani yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)
3/IJMAA (Katika FIQH Neno IJMAA ni Makubaliano (Concensus) ya Wanavyuoni kuhusiana na Suala katika kutafuta Jawabu).
(Ijmāʿ, (Arabic: “consensus”) in Islamic law, the universal and infallible agreement of either the Muslim community as a whole or Muslim scholars in particular. … In Muslim history, ijmāʿ has always referred to consensuses reached in the past, near or remote, and never to contemporaneous agreement)
Kuruani na Sunnah ni Asili ambazo wamekubaliana mashule yote ya sheria. Kwanza wanatafuta majawabu ya masuala yao kutoka katika Kuruani Tukufu na Sunnah Za Mtume na wasipopata jawabu wataendelea kutafuta kwa kutumia IJMAA yaani Rai ya Wanavyuoni wote na isipopatikana jibu wataendelea na Nyenzo mbalimbali za IJTIHAD yaani Reasoning. Wanavyuoni wengi wanakubaliana kwamba Kizazi (Generation)cha kwanza Tangu kuja kwa Uislamu na wengine wanasema Vizazi vitatu vya kwanza ndivyo pekee vilivyokubaliwa katika kutumia IJTIHAD Kwa kupitia Milango hapa chini kama vile
1/QIYAS
Katika FIQH Neno QIYAS ni njia mojawapo ya kutafuta Jawabu kwa kulinganisha Sunnah Za Mtume na Aya Za Kuruani na kisha kutafuta Jawabu kwa njia ya Kulinganisha
(Qiyas, Arabic qiyās, in Islamic law, analogical reasoning as applied to the deduction of juridical principles from the Qurʾān and the Sunnah (the normative practice of the community).
2/ISTIHSAN
Katika FIQH Neno ISTIHSAN ni njia nyingine ambayo wanavyuoni wanitumia kwa kulinganisha sheria zenye uhusiano na swali kisha wanachagua sheria iliyo sahihi na bora yenye kuwiana na Jawabu la suala
The literal meaning of istihsan is to consider a thing good. Since a jurist departs from the law established for a certain case, he obviously prefers a law which he considers good to the law already es tablished for that case. In this sense, istihsan is a preferential reasoning
4/URF
Katika FIQH Neno URF ni mojawapo ya Nyenzo ambazo wanavyuoni wanatumia kwa kuchunguza Desturi za Jamii ambazo lazima zikubaliane na Sheria za Dini)etc.
Abstract: ‘urf is something that has been fixed (consistent) in the soul, recognized and accepted by the intellect, and it is an argument and easy to understand. … ‘Urf in Islamic legal theory (ushul fiqh) gives meaning to the many roles and dynamics of Islamic law
5/MASLAHA
Neno MASLAHA katika FIQH lina maana ya Kupitisha Sheria kwa kuangalia Maslahi ya Wananchi. Sheria yetote lazima iwafae wananchi yaani isilete dhara nchini. Kuna Nyenzo nyinginezo ambazo sikuzitaja hapa bali chache ambazo zinatosha kutupa mwanga wa historia fupi ya Elimu ya FOQH. Maslaham or maslahah
(Arabic: مصلحة, lit. ‘public interest’) is a concept in shari’ah (Islamic divine law) regarded as a basis of law. … The concept is acknowledged and employed to varying degrees depending on the jurists and schools of Islamic jurisprudence (maddhab).
6/SUNNAH MUTAWATIR
Hadithi Mutawatir ni Hadithi iliyotamkwa na Wanavyuoni wengi wenye kuaminika na kwa hesabu tunaweza kusema Milolongo ya wasimuliaji kumi
A Mutawatir hadith is one which is reported by such a large number of people that they cannot be expected to agree upon a lie, all of them together.
7/SUNNAH AHAD
Hadithi Ahad Ni Hadithi iliyotamkwa na Watu wachache. Na kwa hesabu tunaweza kusema Mlolongo wa wasimuliaji Mmoja.
Linguistically, hadith ahad refers to a hadith narrated by only one narrator. In hadith terminology, it refers to a hadith not fulfilling all of the conditions necessary to be deemed mutawatir.
8/ISTISHAB
Sheria Inakubaliwa liendelee mpaka kuwe na Ushahidi wa sheria mpya wenye kukataza jambo hilo lisiendelee
Islamic legal term for the presumption of continuity, where a situation existing previously is presumed to be continuing at present until the contrary is proven. … Accordingly, a person is presumed to be free from liability until the contrary is proven.
9/MAQASID
Malengo Ya Sheria. Sheria Zote lazima ziwe na Malengo Maalum na siyo hovyo hovyo. Maqasid
(Arabic: مقاصد, lit. goals, purposes) or maqāṣid al-sharīʿa (goals or objectives of sharia) is an Islamic legal doctrine.
10/Sadd al Dharai (Blocking the means)
Kuzuia Sheria ambayo inayoweza kuleta Dhara au Matokeo mabaya
Dharai is the plural of Dhariah which signify means. Sadd means to block. In Usul, it means blocking the means to evil. Sadd al Dharai is often used when a lawful means is expected to produce an unlawful result.
11/Fath adh-dhara’i (Deblocking the means)
Kuhalifu Sheria ili kuondoa baya lingine kubwa zaidi Kama vile Kutoa Malipo ya fidia kwa majambazi ili kumkomboa aliyekamatwa. Hapa siyo vizuri kuwapa pesa majambazi lakini unafanya hivyo ili kusaidia aliyekamatwa aachiwe
Fath adh-dhara’i or facilitating the means is allowing something that is prohibited which may contain evil but is more likely to bring benefit(maslahah or manfaat). If it is a benefit, it is desirable to allow it because benefit is sought, and that is called ‘facilitating means’.
TOFAUTI BAINA YA SHULE NNE KATIKA MATUMIZI YA NYENZO ZA KUTAFUTA NA KUTATUA ASILI ZA SHERIA (SOURCES AND METHODOLOGY)
Wanavyuoni wa Madhehebu Manne (Hanafi, Maliki, Shaf’ii na Hambali) wanakubaliana kwamba Kuruani ndiyo ya kwanza katika uchunguzi wa Suala lolote lile la dini au dunia. Lakini kama hawakupata Jibu basi wote watachunguza Vitendo na Kauli Za Mtume Mohamed iwapo kauli au kitendo chake kinajibu suali au masuali. Na iwapo hawakupata jawabu basi itabidi watumie mbinu mbali mbali. Hizi Mbinu zinatofautiana baina ya Madhehebu yote manne. Kutofautiana kwao ni Neema kwetu sisi. Kwa Mfano Sheria Ya Imamu Shafii kuhusiana na Kumguza Mwanamke kwamba inatengua Udhu na kwa hiyo inabidi ufanye tena Udhu kwa ajili ya kugusana na Mwanamke. Lakini kuna wakati mwingine Mazingara hayaruhusu kujikinga na kitengua udhu kama hicho, kwa mfano ukienda Hija basi huenda utagusana na Mwanamke katika Tawafu bila kutegemea na kwa hiyo katika hali kama hii unaweza kuridhika na sheria ya Madhehebu ya Hanafi inayosema kwamba Udhu hutenguki kwa kugusana na Mwanamke katika wakati huo. Na ndiyo maana Hakuna Aya wala Hadithi iliyo wazi wazi katika suala hili na Huenda Mwenyeezi Mungu anatuhurumia sana na ndiyo katuachia uhuru katika Masuala kama haya. Kama Madhehebu yako yanaharimisha kitu Na Mazingara hayakubaliani na Sheria za Madhehebu yako basi fuata Madhehebu yeyote katika haya madhehebu manne ambayo yanatatua suala lako na hutakwenda mrama kwani kila kikundi katika hivi vinne kina wataalamu wakubwa.
Kila Shule katika Shule Nne za Sunnah zilijishughulisha na Kutatua masuala ya FIQH kwa kuchunguza Kuruani, kisha Sunnah (Hadithi za Mtume) na Nyenzo nyinginezo mbalimbali ikiwa Masuala hayakujibiwa na Kuruani au Hadithi za Mtume. Kwanza walianza utafiti katika Kuruani na kisha Sunnah. Na baada ya Hapo hatua kwa Hatua walifuata Nyenzo Mbali Mbali ambazo kila Shule ilitofautiana kidogo na Nyingine katika Uchaguzi wa Nyenzo hizo walizotumia.
SHULE YA IMAM HANAFI
Asili za Sheria Zinazotokana na Maandishi
HATUA 1/Kuruani Tukufu
HATUA 2/Hadithi za Mtume (Sunnah Mutawatir za Mtume)
Baadhi Ya Asili za Sheria Zinazotokana na Fikra (Reasoning)
HATUA 3/
1/IJMAA ZA SWAHABA2/RAI ZA KILA SWAHABA 3/QIYAS 4/ISTIHSAN 5/URF etc
SHULE YA IMAM MALIKI
Asili za Sheria Zinazotokana na Maandishi
HATUA 1/Kuruani Tukufu
HATUA 2/Hadithi za Mtume (Sunnah Mutawatir za Mtume)
Baadhi Ya Asili za Sheria Zinazotokana na Fikra (Reasoning)
HATUA YA 3/
1/A’MAL AHL AL-MADINAH 2/IJMA’A ZA SWAHABA 3/RAI ZA KILA SWAHABA 4/QIYAS 5/DESTURI AU UTAMADUNI UNAOKUBALIANA NA DINI 6/ISTISLAH 7/U’RF
SHULE YA IMAM SHAF’II
Asili Zinazotokana na Maandishi
HATUA 1/Kuruani Tukufu
HATUA 2/Hadithi za Mtume (Sunnah Mutawatir za Mtume) Baadhi Ya Asili za Sheria Zinazotokana na Fikra (Reasoning)
HATUA YA 3/
1/IJMAA 2/RAI ZA KILA SWAHABA 3/QIYAS 4/ISTISHAB
IMAM HAMBALI
Asili Zinazotokana na Maandishi
HATUA 1/Kuruani Tukufu
HATUA 2/Hadithi za Mtume (Sunnah Mutawatir na Marfuu za Mtume)
Baadhi Ya Asili za Sheria Zinazotokana na Fikra (Reasoning)
HATUA 3/
1/RAI ZA KILA SWAHABA 2/IJMAA YA SWAHABA 3/QIYAS 4/MASLAHA
MISAMIATI MINGINEYO YA ELIMU YA FIQH
FATWA
FATWA ni Sheria itakayopitishwa na Mkubwa wa Wataalamu Mbali mbali wenye kuhusika na Sheria za FIQH kama vile MUJTAHID na wengineo. Sheria Hiyo itapimwa isipingane na Desturi ya Sehemu au Nchi. Mkubwa Huyu anajulikana kwa Jina Kama MUFTI
A fatwa is basically a legal pronouncement. It is the opinion of someone called a mufti; that is an Islamic legal scholar who is capable of pronouncing his judgments, his opinions on any kind of legal issue with regard to Islam.
MUAMALAAT
Muamalat ni Maingiliano Ya Kimaisha kama vile katika Biashara na mengineyo ya Kidunia
Muamalat (also muʿāmalāt, Arabic: معاملات, literally “transactions” or “dealings”) is a part of Islamic jurisprudence, or fiqh. Sources agree that muamalat includes Islamic “rulings governing commercial transactions”and Majallah al-Ahkam al-Adliyyah).
IBADAAT
Ibadaat Ni Ibada tunazofanya katika dini ya Kiislamu.
Ibadah (Arabic: عبادة, ‘ibādah, also spelled ibada) is an Arabic word meaning service or servitude.[1] In Islam, ibadah is usually translated as “worship”, and ibadat—the plural form of ibadah—refers to Islamic jurisprudence (fiqh) of Muslim religious rituals.
BID’AAH
Bid’ah ni lolote jipya lililongezwa katika dini ya Kiislamu na jipya hilo halina ushahidi wowote wa Kuruani na Sunnah za Mtume.
Bidʿah, in Islam, any innovation that has no roots in the Quran and Traditional practice (Sunnah) of the Muslim community.
MAQASID
Neno Maqasid ni Malengo. Maqasid Al-Sheriah Ni Malengo ya Sheria katika kulijenga Taifa katika njia nzuri yenye kuleta faida na kueneza haki kwa watu wote.
Maqasid (Arabic: مقاصد, lit. goals, purposes) or maqāṣid al-sharīʿa (goals or objectives of sharia) is an Islamic legal doctrine. Together with another related classical doctrine, maṣlaḥa (welfare or public interest), it has come to play an increasingly prominent role in modern times.
Lengo la Sheria nii kuondoa uharibifu katika Taifa. Malengo ya Sheria za FIQH hayalengi Ibada au kujenga imani peke yake bali yanalenga kuhifadhi haki za binaadamu na kuwasaidia katika kuwaepushia shari au balaa. Malengo ya kuinua Jamii na Kuiongoza katika mazuri. Imamu Ghazali ametaja katika kitabu chake kinachitwa “al-mustasfa” Madhumuni ya Malengo au Maqasid ni Manne. La Kwanza ni kuhifadhi Imani za Watu, Pili Kuhifadhi maisha ya binaadamu, Tatu Kuhifadhi Ukoo, Nne Kuhifadhi Mali za Watu. (safeguard humanity’s faith, life, intellect, lineage and wealth).
Maqasid Pia Yamegawanywa katika Mafungu matatu;
1/Dharuriyyat (Mahitajio Ya Lazima-essentials kama vile faith, life, intellect, lineage and wealth,)
2/Hajiyyat (Mahitajio Muhimu-complementary needs- “Needs” are purposes that are less essential for human life. Examples of needs are marriage, trade, and means of transportations. Islam encourages and regulates these needs).
3/Tahsiniyyat (Mahitajio Yaliyo Mazuri-or luxuries or embellishment-The Shariah thus encourages cleanliness of the body and attire for worship and recommends, for example, the wearing of perfume when attending the Friday congregational prayer, the wearing of nice clothing, and having beautiful homes).
Sheria zinazotokana na FATWA lazima zipimwe na Malengo haya tuliyoyataja. Ni Lazima Sheria ilenge Maqasid tuliyoyataja. Kwani Sheria Itakayopingana na Maqasid basi italeta matatizo. Kwa Mfano Kufanyika Kwa Mawlid hakuna Aya au Hadithi iliyotaja wazi wazi na kwa hiyo ni BId’ah lakini ni Bidaah Mustahabu yaani Ni Bidaah inayopendeza na siyo Mbaya na Kwa hivyo inakubaliana na Maqasid. Ukiiondoa basi itakuwa ni kinyume na Maqasid kwani watu watagombana na kuweza kudhuriana. Kwani kuna wale ambao wanapenda ifanyike na kuna wale ambao hawapendi ifanyike kwa kutoa Rai zao kwamba ni Bidaah. Ni Kheri kuliepusha Shari Kubwa baya kwa kufanyika kwa Bid’ah Mustahabu ambayo vipengele vyake siyo Haram. Kwani katika Mawlid Kila kipengele siyo kibaya. Kunasomwa Kuruani Tukufu, Kuswaliwa kwa Mtume na pika Watu wanasikiliza Hayo mazuri. Kisha Watu wanakutana kwa jambo lisilo baya. Hivi Vipengele ni Bora kuliko kwa Watu Kupigana kwa kuondoa Mawlid.
TOFAUTI YA MADHEHEBU MANNE KATIKA SHERIA ZA IBADA NA MUAMALAAT
Wanavyuoni wa Madhehebu Manne wanatofautiana katika kutatua Masuala Magumu ambayo majibu yake hayapatikani katika kuruani na Sunnah za Mtume.
Madhehebu Ya Maliki, Sha’fii na Haanafi wanasema kwamba kila kitu ni halali isipikuwa kilichoharimishwa na Kuruani na Sunnah za Mtume
Madhehebu Ya Hambali wanasema kwamba Kila kitu ni Haramu isipokuwa kilichohalalishwa na Kuruani na Sunnah za Mtume.
Na ndiyo maana Hambali hawakubali jipya katika IBADA na lolote jipya wanaliita BID’AA.
Na madhehebu matatu mengineyo; Hanafi, Sha’fii na Maliki wanakubali mapya katika IBADA iwapo kuna Hadithi zenye kuashiria Suala wanalotafuta.
Shule au Madhehebu ya Hambali wanakataa Jipya katika IBADA lakini hawana tatizo katika MUAMALAAT. Wanasema kwamba Mtu yeyote asichezee IBADA kwa nyongeza yoyote isipokuwa wanakubali kama ni Mengineyo ya Kidunia yenye Ushahidi kama vile Muashirio wa Hadithi za Mtume.
TOFAUTI ZA MAMBO YA DINI NA KUSABABISHA BIDAA AU JIPYA
Tofauti za masuala ya dini tuliyonazo leo katika dunia asili yake yanatokana na tofauti ya Haya Mashule tangu hapo zamani. Na ndiyo maana MAWLID inapigwa vita na nchi zenye kumfuata imam Hambali kama vile Saudi Arabia kwa sababu Nchi hiyo inamfuata Imamu Hambal ambaye alianzisha shule ya Hambal na shule hiyo inakataa jipya lolote ambalo halikuhalalishwa na kuruani au Sunnah za mtume. Na Egypt wana halalisha MAWLID kwa sababu nchi hiyo inafuata mafundisho ya Imamu Shaf’ii ambaye aliyeanzisha shule ya SHAF’ii na shule hii inakubali jambo lolote jipya maadam halikukatazwa na Kuruani au Sunnah. Sasa Unaona tofauti hizi. Ukifikiri utaona Hakuna tatizo lolote kwani tofauti hizi ni ndogo na kila Imamu wa Madhehebu alikuwa na sababu maalum na ushahidi wa kutetea sababu zake. Ikhtilafu katika Taifa ni Neema kubwa. Maadamu unafuata Imamu mmojawapo katika hawa Wanne wa Sunnah basi hutapotea.Kila Shule katika hizi Nne zina Maelfu ya Wanafunzi waliokuwa wataalmu wa kila Elimu za Kidini.
BIDA’AH NA MIGAWANYIKO YAKE
Baada ya FATWA kufanyika Masuala Yaliyofutuliwa yatapimwa kufuatana na Migawanyiko mbali mbali ya BId’ah ambayo tumeielezea hapa chini. Inachunguzwa iwapo suala hilo lililotatuliwa ni zuri au baya kufuatana na Maqasid (Tutaelezea Maqasid hapa Chini) ya Taifa.
Baadhi ya Waislamu walitaka mabadiliko katika baadhi ya vitendo katika Ibada na kwa hiyo ili kuinusuru fikra hIyo ya BId’ah ili iendelee kutumika wakaja na fikra ya kugawanya BIda’ah katika mafungu mbali mbali kufuatana na Masuala Mbali Mbali katika Bid’ah Nzuri na Mbaya kama ifuatavyo:
1/HASSAN au MAHMUDAH (Yaani Bida’ah Nzuri au ile yenye kustahiki sifa nzuri) Good Bid’ah
2/SAYYIAH au MADHMUMAH (Yaani Bida’ah Mbaya au ile yenye kustahiki sifa mbaya) Bad Bid’ah
Na baadaye Wanavyuoni wakaendelea kuyagawanya tena katika mafungu mengine matano kama yafuatayo:
1/FARDH /WAJIB- (Mfano kufunga mwezi wa Ramadhan)Obligatory or Compulsory
2/MUSTAHAB/ MAMDUB-Sio Lazima bali inapendeza kuitenda- Recommended
3/MUBAH/ JAIZ- Chaguo lako kutenda au kuacha yaani sio lazima. Choice.
4/MAKRUH- Kitendo sio Haramu wala Halali, ukikifanya hupati dhambi-Discouraged / Tolerated
5/HARAM-ni Kitendo Haramu kukifanya./Forbidden
NIPO KATIKA MAANDALIZI. INSHAALLAH MUNGU AKIPENDA NITAENDELEA NA SHEREHE HIVI KARIBUNI