SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Usul Al-Hadith

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

ELIMU YA HADITHI

AHADI YA MWENYEEZI MUNGU

Sura Ya Al-Hijr Namba 15 Aya Namba 9

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُ ۥ لَحَـٰفِظُونَ (٩)

TAFSIRI

Kwa hakika Bila ya shaka tumeishusha Kuruani na hakika tutaihifadhi

MUHTASARI WA ELIMU YA HADITHI ZA MTUME (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Ahadi aliyotoa Mwenyeezi Mungu katika Aya hii إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُ ۥ لَحَـٰفِظُونَ ni ya kweli kwani Kuruani ilishuka tangu karne 14 zilizopita na mpaka leo haikuguswa kwa kuongezwa au kupunguza. Yaani Kuruani kuanzia kushushwa mpaka leo ipo vile vile. Lakini watu wengi wanasahau kwamba Ahadi aloyotoa Mwenyeezi Mungu katika Aya hii inahusisha pia Hadithi za Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu zimfikie) Hadithi za Mtume zinabainisha Aya za Kuruani. Na huwezi kufahamu Kuruani vizuri isipokuwa kwa kutumia Hadithi za Mtume kwani zimekuja kwa lengo hilo.

Hapo awali Mwenyeezi Mungu aliihifadhi Kuruani hii isiharibiwe na kuvurugwa baada ya Maswahaba waliohifadhi kuruani Kufariki dunia katika Vita vya kidini kwa kuwaongoza Makhalifa (Viongozi wa Kiislamu)-baada ya makubaliano na Maswahaba-kuikusanya Kuruani katika Kitabu kimoja kwani maandishi haya yalisambaa katika vifaa mbalimbali kama vile Kuhifadhiwa (Memory) na Baadhi ya Maswahaba, Katika Mifupa, Ngozi na vifaa vinginevyo. Aliihifadhi kutokuguswa na Maadui wa Kiislamu wa wakati huo kama vile Mitume ya Uongo, na kuwajaalia Mamilioni ya Watu kuihifadhi kwa urahisi.Aliihifadhi kwa kuwasaidia maelfu ya watu kuihifadhi(Memorize) na kufundisha wengine, na kuwazalisha watu wenye uwezo mkubwa wa kuihifadhi na kufundisha katika kila Karne.

Na hivyo hivyo Mwenyeezi Mungu alihifadhi Sunnah (Hadithi za Mtume) kwa kuwajaalia Maswahaba na waliofuata (Mwenyeezi Mungu awaridhie)kuhifadhi hadithi za Mtume. Aliwawezesha Kuandika Aliyonena Mtume (S.A.W.), Vitendo Vyake na pia Kuwawezesha kuifuata Sunnah hiyo.

Na Baada ya Muda kupita Mwenyeezi Mungu alijaalia Taifa la Kiislamu Kuzalisha watu wenye Elimu Kubwa na Fahamu za hali ya juu sana (Incredible Memory-Skills) na Utaalamu wa hali ya Juu katika Uchambuzi (Analytical Expertise) baina za Hadithi sahihi na sizizo sahihi. Akawapa Uhodari wa kusafiri ili kutafuta hadithi zilizo sahihi na bila ya kuchoka wakasafiri katika miji mbali mbali huku wakifanya kazi ngumu ya uchambuzi kwa kutumia ufundi wa hali ya juu. Mwenyeezi Mungu akawajaalia Kugundua Njia mbalimbali ambazo ulisababisha kuzaliwa kwa Elimu ya Hadithi (Science of Hadith). Hawa Walifanya juhudi hizi za kuchambua Hadithi zisizo Sahihi ambazo zilizotokana na wale ambao walikuwa na Fahamu Dhaifu (Weak Memories). Na Zile ambazo zinatokana na Waongo na wenye Nia mbaya kama vile Hadithi zilizotungwa ili kuwavutia watu wafanye kitendo kwa masilahi ya kidunia na hali Mtume hakusema wala kutenda. Mwenyeezi Mungu akawaongoza kuchambua Hadithi zilizokusanywa na Maswahaba ambao walifundisha katika Vikao (Vyuo au Madrasa mbalimbali) Vya Elimu kueneza Ukweli aliozungumza na alivyotenda Mtume Mohamed(Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie). Wanvayuoni hawa walifanya kazi kubwa na wakafanikiwa kuchambua maneno ya Mtume ya ukweli kufuatana na Sira ya Maisha (Biography) Ya Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie).Waliofuata (Waislamu Waliodhamiria Kufanya Mwamko wa Kiislamu-Renewers of Islam) walizalisha pia kazi hiyo ya Kuzihifadhi Hadithi za ukweli kwani zile ambazo hazina uhakika ziliendelea kuongezwa na wasio na Elimu yeyote. Lakini Elimu ya Hadithi imewezesha kuzichambua Hadithi za Mtume na kizigawa Baina Ya zile za ukweli na zile ambazo hazina Uhakika wowote.

Hadithi ambazo zimetiliwa Shaka zimekusanywa kwa Uwezo wake Mwenyeezi Mungu na Mungu akipenda tutazitaja na kuzizungumzia katika Mlango huu.

Elimu hii ni kubwa sana na Ni “Source” au “Chanzo” cha pili baada ya Kuruani. Yaani Ni Bahari ya pili. Tutagusia Utangulizi ambao Kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu utatupa msingi ili kutuelekeza na kusoma zaidi Elimu hii kwingineko.

MUHTASARI WA HISTORIA YA Mustalah al-Hadith” (Classification of Hadith)

Nidhamu ya Kuchambua hadithi za ukweli imesababisha kuzaliwa kwa Elimu inayojulikana kama “Mustalah al-Hadith” (Classification of Hadith). Ilibidi kuwa na Nidhamu kwani bila ya hivyo kila anayetaka angelisema anachotaka na wengine wangefuata na kusambaza Hadithi zisizo na Uhakika Na kwa Hiyo Mungu akipenda tutachambua Hadithi Za Mtume (Sala Na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) huku tukifuata Ramani ya Picha ambayo nimembatanisha katika website hii. Tutachukua Hadithi na Kuielezea na Kisha tutapima Kuashiria Vipengele hivyo katika Ramani Hii. Tukimaliza Vipengele Hivi tutaendelea Kuzama zaidi na kusoma Milango mbali mbali ya Elimu ya Hadithi. Lazima tuelewe kwamba Hapo awali kila Mwanachuoni alikuwa na Misamiati ya Elimu ya “Mustalah al-Hadith” yaliyotofautiana na Mwingine.Lakini Nidhamu na Lengo ni moja yaani Uchambuzi wa Hadithi zilizo za Ukweli kutoka katika zile zisizo za ukweli.

Na Wale waliopokea na kuzitaja Hadithi za Mtume “Elimu ya Rijal al-Hadith” (the study of the reporters of Hadith) Ilikuwa Muhimu sana kwani Ina Uhusiano na ISNAD. Kwani lazima Umwelewe aliyepokea na kutangaza Hadithi je alikuwa mkweli au mwongo na sifa nyinginezo ambazo tutazielezea baadaye.

Inabidi tuelewe kwamba Hadithi Imegawanyika katika sehemu tatu-MATN (TEXT), (ISNAD) na (TARAF). MATN ni yale yaliyozungumzwa au kitendo kilichofanywa na Mtume na ISNAD ni majina ya wale waliopokea Hadithi, na TARAF ni ibara mwanzoni mwa Hadithi yenye kutujuulisha iwapo  “alisema” au “Alihadithia” au alitenda au sifa yeyote nyingineyo baada tu ya  ISNAD (Chain of Reporters)

Kwa hiyo Elimu mbili zilihitajika katika Kutafuta Hadithi (Authentic) Ya ukweli na ile ambayo isiyo na Ukweli yaani Elimu inayohusiana na TEXT na pia Inayohusiana na MATN.

Migawanyiko yote Niliyoitaja hapa Juu na katika picha hapa chini tutaielezea kwa mifano kwa hiyo usiwe na wasiwasi wowote kama hujaelewa vizuri maana yake kwa hiyo fanya subira na tutaichambua kwa mifano na hakuna haraka yoeyote kwani hapo juu ilikuwa ni Utangulizi. Kabla ya kuzama na kuanza madhumuni ya Mlango huu ningependelea kutaja kwamba Wanavyuoni wa Elimu ya Hadithi za Mtume wanajulikana kwa jina “Muhadithuun” au Kwa Kiswahili “Wanavyuoni wa Hadithi za Mtume” (Sholars of Hadith “Traditionists”). Namuomba Mwenyeezi Mungu atujaalie Elimu hii itufae hapa duniani.

Hadithi zimekusanywa na Wanavyuoni Mbalimbali na ningependelea kutaja baadhi ya Vitabu vya wanavyuoni mashuhuri.

VITABU SITA MASHUHURI-Kutub al-Sittah, the Six Canonical Books of Hadith

SAHIH AL-BUKHARI-صحيح البخاري-by Imam Muhammad al-Bukhari (d. 256 AH/870 AD

SAHIH MUSLIM-صحيح مسلم-by Imam Muslim ibn al-Hajjaj al-Naysaburi (rahimahullah)

SUNAN AN NASA’I-سنن النسائي-by Imam Ahmad an-Nasa’i (rahimahullah)

SUNAN ABI DAWUD-سنن أبي داود-by Imam Abu Dawud Sulayman ibn al-Ash’ath as-Sijistani (rahimahullah)

JAMI AL-TIRMIDHI-جامع الترمذي-by Abu `Isa Muhammad at-Tirmidhi (rahimahullah)

SUNAN IBN MAJAH-سنن ابن ماجه-by Imam Muhammad bin Yazid Ibn Majah al-Qazvini (rahimahullah)

Vitabu Vinginevyo ambavyo vimekusanya Hadithi Za Mtume

Muwatta Malik-موطأ مالك

Musnad Ahmad-مسند أحمد- by Imam Ahmad ibn Hanbal (d. 241 AH/855 AD – rahimahullah)

An-Nawawi’s 40 Hadith-الأربعون النووية

Collections of Forty-الأربعينات

Riyadh As-Salihin-رياض الصالحين-by Imam Yahya ibn Sharaf an-Nawawi

MIshkat Al-Masabih-مشكاة المصابيح-by Imam Khatib at-Tabrizi. 

Al-Adab Al-MUfrad-الأدب المفرد

Ash-Shama’il Al-Muhammmadiyah-الشمائل المحمدية

Bulugh Al-Maram-بلوغ المرام

Hisn A-Muslim-حصن المسلم

Katika Safari Yetu ya Kusoma Elimu ya Hadithi tutakuwa tukifuata Ramani iliyofupishwa hapa Chini ya Maneno (Terminology) na Migawanyiko (Sections)  mbalimbali ya Elimu hii. Na tutatoa Mifano Mbali Mbali ya Hadithi za Mtume.(Amani Na Sala Zimfikie).  Mungu  akipenda Tutadokeza Pia Vidondoo vinginevyo na Mengineyo nje ya Ramani Hii. Tutafasiri Na Kutumia Lugha ya Kiswahili kila Neno Mungu Akipenda. Alhamdulilah.  

Ramani Hii Imefupishwa na Ni Nzuri kwa Kuanza Kusomea Elimu hii na Kwa hiyo Tutafuata Mgawanyiko Huu ambayo imefupishwa. Na Mungu akipenda Tutaendelea Na Mengineyo ambayo hayapo katika Picha Hii

HADITHI YA KWANZA

حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ ، قَالَ : حَدَّثَنَا سُفْيَانُ ، قَالَ : حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْأَنْصَارِيُّ ، قَالَ : أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ ، أَنَّهُ سَمِعَ عَلْقَمَةَ بْنَ وَقَّاصٍ اللَّيْثِيَّ ، يَقُولُ : سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَلَى الْمِنْبَرِ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: ” إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى دُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ إِلَى امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ “

TAFSIRI

Omar Ibn Khatab alisema kwamba alimsikia Mtume (Sala Na Amani Ya Mola Zimfikie) akisema kwamba Malipo ya Vitendo  yanategemea Nia na Kila Mtu atalipwa malipo kufuatana na Nia Yake. Kwa Hiyo yeyote  atakayesafiri kwa lengo la kutafuta manufaa ya kudunia au kwa ajili ya kuoa, basi safari yake itakuwa ni kwa ajili hiyo. (Yaani utapata malipo kufuatana na nia yako. Kama ulisafiri kwa ajili ya Mungu basi utalipwa kufuatana na nia yako. Na kama ulisafiri kwa ajili ya kutafuta riziki na mengineyo basi utalipwa kwa nia hiyo)

ENGLISH TRANSLATION

(I heard Allah’s Messenger (ﷺ) saying, “The reward of deeds depends upon the intentions and every person will get the reward according to what he has intended. So whoever emigrated for worldly benefits or for a woman to marry, his emigration was for what he emigrated for.”)

MGAWANYIKO WA HADITHI KATIKA SEHEMU TATU (SANAD/TARAF/MATN

Nimegawa Hadithi Ya Mtume (Amani Na Sala Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Katika Sehemu Tatu.

Sehemu Ya Kwanza Ni ISNAD  (Wapokezi wa Hadithi)

حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ ، قَالَ : حَدَّثَنَا سُفْيَانُ ، قَالَ : حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْأَنْصَارِيُّ ، قَالَ : أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ ، أَنَّهُ سَمِعَ عَلْقَمَةَ بْنَ وَقَّاصٍ اللَّيْثِيَّ ، يَقُولُ : سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَلَى الْمِنْبَرِ، قَالَ

Sehemu ya Pili Ni TARAF (Mtume Alisema)

يَقُولُ

Sehemu Ya tatu Ni MATN  (Kauli Ya Mtume) 

” إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى دُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ إِلَى امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا، فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ “

HADITHI hii ni  Marfu’  yaani inakwenda moja kwa moja kwa Mtume. Hadithi hii inasema  “Mtume Kasema” kwa hiyo imerufaishwa kwake yaani yeye ndiye aliyesema. Hadithi ya aina hii inajulikana kama Marfu’ na kama kungekuwa hakuna  ibara “Mtume Kasema”  au Ibara yeyote nyingine kama vile cha kuoneysha kitendo cha Mtume basi  isingekuwa Marfu’ bali kuna Majina Mengine kama ilivyoelezwa katika Ramani Hapa Juu.  Kurufaishwa Yaani  Elevated au Directly kutoka Kwa Mtume. Hadithi Hii ni ya Kwanza katika Kitabu Cha Al-Bukhariy na Ni Hadithi  SAHIHI.

Kwa Hiyo  tumeigawa Hadithi hii katika Mafungu Matatu.  SANAD/TARAF/MATN  na Ni Hadithi  Sahihi na Pia Marfu’  Sababu ya kuwa Hadithi sahihi ni kwamba Imekusanywa katika Kitabu cha Bukhari na Huyu Mkusanyaji wa Hadithi alitumia Elimu Ya Kuchambua Hadithi zilizo Sahihi na ambazo sio Sahihi na Vitabi vyake vimekusanya Hadithi Sahihi.  Akafanya kazi hiyo kubwa sana. Na Mwenyeezi Munfgu alimpa Akili na Famamu Nzuri. Alisoma Sifa na maisha ya Wale waliopokea Hadithi  na baada ya Juhudi kubwa akaandaa vitabu vyake ambavyo ni Vya Kwanza katika Vitabu  Authentic Vya Hadithi za Mtume. Na isitoshe Hadithi hii ameiweka Ya Kwanza katika Vitabu Vyake. Ni Ya Kwanza Katika Kitabu/Mlango   cha WAHYI  au Revelation.

Kwa Kifupi 

Kufuatana na The Reference to a Particular Authority (Hadithi inatokana na….) Hadithi hii ni Marfu’ Na Kufuatana na Reliability and Memory of the Reporters (Ukweli na Sifa Nzuri za Wapokezi wa hadithi) hadithi hii ni Sahih. (Angalia Picha Ya Ramani Ya Mgawanyiko wa Mustahaat (Terminology)  Za Elimu Hii Hapa Juu)

Kwa Hiyo hii ndiyo Hadithi Ya kwanza Na nimeichambua Kufuatana Na Elimu Ya Hadithi.

Leo Naishia Hapa, Nitaendelea Mungu Akipenda Na Nitakutana Nanyi katika Hadithi Ya Pili.