UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
HISTORIA FUPI YA TAFSIRI YA KURUANI
DIBAJI
Haiwezekani kuelezea historia ya Tafsiri ya kuruani katika sehemu ndogo ya website kama hii. lakini kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu nitajitahidi kuelezea Muhtasari wa Asili Ya Tafsiri kwa ufupi sana. Na Kwa hiyo siwezi kumaliza kwa siku moja bali masiku mengi na itakuwa kidogo kidogo Mungu akipenda.
UTANGULIZI
Mungu akipenda nitazungumzia katika Mlango huu Historia Fupi ya Kuruani Kuanzia Kushuka kwake, Kuhifadhiwa kwa Kuruani kwanza katika Nyoyo za Mtume Mohamed (Sala Na Amani Yake Mola Imfikie) na Kisha Maswahaba Zake.
Kukusanywa kwa Kuruani katika Kitabu Kimoja Baada Ya Kiongozi (Amir) Abu Bakar kukubali nasiha liyopewa na Omar Ibn Al-khatab aliyekuwa Kiongozi (Amir) wa Pili baada ya Abu Bakar.
Kuchaguliwa kwa Lahaja (Dialect) Moja ya kuruani (Dialect) na kuondolewa nyinginevyo (yaani LAHAJA za makabila mengineyo ya wakati huo na LAHAJA ni Lugha zenye Asili moja lakini kuna tofauti ndogo ndogo za kilugha mfano wa Kiswahili cha Pemba, Zanzibar, Mombasa, Kingazija na nyinginezo) chini ya Uongozi wa Othman Ibn Affan.
Nitagusia kuhusu Mazingara au ASBAAB AL-NNUZZUL ya Kushushwa kwa Aya Za Kuruani.
Nitagusia Tafsiri za Makundi Ya Wapotevu ili tujiepushe nayo.
Nyenzo mbali mbali zilizotumiwa katika Tafsiri.
Maana Ya Misamiati Mbali Mbali ya Elimu Ya Tafsiri.
Masharti au Sifa ambazo Wafasiri wa Kuruani wanawajibika kuwa Nayo.
Aina Ya Tafsiri za Kuruani na Majina Ya Waandishi.
Kwa kifupi haya ndiyo mambo ningependelea kuyazungumzia kwa Ufupi katika Mlango huu na Nia Yangu ni kufupisha na Kwa Njia iliyo Rahisi Ili tupate Mwanga ambao utatulinda na Njama mbalimbali zenye kunasibisha uongo katika Dini ya Kiislamu.
Kwa mfano Makafiri na Maadui wa Kiislamu wanadai kwamba Versions za Kuruani ni zaidi ya Moja ambazo madhumuni yake yanapingana na hizi zinaonyesha kwamba ni Maandishi Ya Kibinaadamu na siyo Mwenyeezi Mungu na Versions zote hizi zilichomwa Moto katika Enzi ya Othman Ibn Affan na kubakizwa moja tu ambayo tuliyonayo leo hii na ambayo wanafananisha na vitabu vya dini nyinginezo ambavyo vimeguswa kwa kubadilishwa, kuzidishwa na kupunguzwa.
Huu Ni Uongo mkubwa sana kwani ukweli ni kwamba Kuruani ilishushwa kwa muda wa miaka 23 ya Uhai wa maisha ya Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Imfikie) lakini katika Dialect au LAHAJA saba za Makabila yaliyoishi wakati huo.
Kwa hiyo kuruani ni Moja tu kuanzia kushushwa mpaka leo.
Na LAHAJA nyinginezo ziliondolewa kwa sababu mbalimbali na siyo Versions kwani Version ni Moja tu kuanzia mwanzo wa WAHYI lakini Maadui wa Kiislamu wanatafuta kila njia ili kutia Doa katika dini ya kiislamu. Watu wengi wasiojua wanachanganya kati ya Versions and Dialect.
Inshaallah Nitazungumzia yote haya katika Mlango huu ili Historia hii ieleweke.
Huu ni Utangulizi kwa hiyo nitaongeza na kubadili lakini kwa sasa upate mwanga yatakayokuja baadaye kwa ufupi.
IPO KATIKA MAANDALIZI. INSHAALLAH MUNGU AKIPENDA NITAENDELEA HIVI KARIBUNI