SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Miujiza Ya Kuruani-2

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

Maisha Ya Marehemu Dakitari Mkuu Wa Jinai Aliyekuwa Maarufu Huko Ufaransa Na Utafiti Wake Katika Kuruani Tukufu. Maiti Ya Firauni (Mummy) Ambayo ililetwa Ufaransa Kutoka Egypt Kwa Utafiti Wa Kisayansi, Jambo Lililomshangaza Bwana Maurice Ni Jawabu la Suala Gumu Alilopata Katika Kuruani Tukufu.

Video-2

Maurice Bucaille -Sehemu Ya Kwanza

Video-3

Maurice Bucaille- Sehemu Ya Pili

KISA CHA NABII MUSA NA FIRAUNI KATIKA MISRI NA UTAFITI WA BWANA MAURICE BUCAILLE

Katika Kuruani Mwenyeezi Mungu anatuelezea habari za Firauni na wakati alipompa Nabii Musa Ujumbe ili kwenda kuwaokoa Watumwa wa Kiisraeli waliokuwa chini ya mamlaka ya Firauni.

Historia inatuambia kuwa ilikuwa karibu miaka 1300 kabla ya kuzaliwa nabii Isa na kwa hiyo karibu miaka 1900 kabla ya uislamu.

Kuruani pia inatuelezea yatakatotokea baadaye wakati Maiti ya huyo Firauni (Ramsees II) mlezi wa nabii Musa itakapofufuliwa na kuwa fundisho kwa ulimwengu mzima.

Kuruani Inatuambia kuwa maiti hiyo itakapofufuliwa itakuwa fundisho kwa ulimwengu mzima ili binaadamu wasirudie makosa aliyoyafanya Firauni ya kudai Uungu.

Bwana Maurice Bucaille alikuwa anajulikana huko Ufaransa kama ni dakitari mkuu wa utafiti katika Jinai “criminology” naye alikuwa maarufu sana katika uwanja wa elimu hiyo. Alitakiwa na seriakli ya ufaransa kufanya utafiti katika maiti ya firauni iliyofufuliwa huko Misri,Cairo katika majengo ya Pyramids. Maiti hiyo ililetwa Ufaransa katika kipindi cha Rais Bwana Sadaat wa Misri alichotawala kuanzia mwaka 1970-1981 baada ya kuitikia ombi la Rais wa Ufaransa wakati huo ambaye alikuwa Georges Pompidou (na baadaye akifuatiliwa na Valery Giscard d’Estaing katika mwaka 1981). Dakitari Maurice Bucaille akafanya utafiti na akatatizwa na jibu la suala lifuatalo;

“kwa vipi maiti hiyo imeweza kuwa katika hali nzuri bila kuharibika baada ya miaka mingi kwa wakati ambapo maiti nyinginezo zilizofufuliwa huko Misri hazikutunzika kama hiyo” (Historia zinatueleza itikadi za mafirauni kwamba walikuwa wanautengeneza mwili kabla ya kuzika kwa kupaka madawa ya wakati huo kisha wakazika kwa njia maalum ili kuutunza mwili usioze. Ekimu hiyo inaitwa “mummification” karika dini yao waliamini kuutunza mwili ili usioze na upate kuishi katika ulimwengu utakaokuja).

Waligundua chumvi katika mwili ya maiti hiyo na ni dalili kwamba maiti hii ilizamishwa baharini kisha ikatolewa. Bwana Maurice alikuwa anaelewa kisa katika Biblia kinachohusiana na Nabii Musa na Firauni ambaye historia inatuambia ndiye aliyejulikana kwa jina la “King Ramesses II” lakini Biblia hailezi kwa kinaganaga kisa hicho.

Waislamu wakamnon’gonezea bwana Maurice Bucaille kwamba Kuruani pia ina kisa kama hicho lakini kwa ukamilifu.

Kuruani inasema kwamba maiti ya firauni itatunzwa na mwenyeezi mungu mwenyewe ili iwe fundisho karika ulimwengu mzima. basi bwana Maurice akaisoma Kuruani na akashangaa sana kupata jibu la suala hilo gumu.

Aya ifuatayo hapa chini ilimpatia jibu bwana huyu na pia ndiyo sababu ya yeye kuiamini kuruani kwamba ni maneno ya mwenyeezi mungu.

وَجَـٰوَزۡنَا بِبَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ وَجُنُودُهُ ۥ بَغۡيً۬ا وَعَدۡوًا‌ۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَدۡرَڪَهُ ٱلۡغَرَقُ قَالَ ءَامَنتُ أَنَّهُ ۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱلَّذِىٓ ءَامَنَتۡ بِهِۦ بَنُوٓاْ إِسۡرَٲٓءِيلَ وَأَنَا۟ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ (٩٠) ءَآلۡـَٔـٰنَ وَقَدۡ عَصَيۡتَ قَبۡلُ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ (٩١) فَٱلۡيَوۡمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنۡ خَلۡفَكَ ءَايَةً۬‌ۚ وَإِنَّ كَثِيرً۬ا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنۡ ءَايَـٰتِنَا لَغَـٰفِلُونَ (٩٢)

Tafsiri ya aya hii ni Na tukawapitisha wana wa israeli katika bahari;na firauni na majeshi yake wakawafuata kwa dhulma na ujeuri. Hata kulipomfikia firauni kuzama alisema: “Naamini ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila yule wanayemuamini wana wa Israeli, na mimi ni miongoni mwa wanaotii (kama wanavyotii wao)”(90) (Malaika wakamwambia) “Sasa (ndiyo unaamini hayo)! Hali uliasi (mda mrefu) kabla ya hapa na ukawa miongoni mwa waharibifu”(91) Basi leo tutakuokoa kwa (kuuweka) mwili wako, ili uwe dalili kwa ajili ya wa nyuma yako (wajue yakuwa hukuwa mungu).” Na watu wengi wameghafilika ishara zetu.

Basi mtaalamu huyu akaamua kuwenda Arabuni kusoma Arabic Language ili aifahamu kuruani na baadaye akendelea kufanya utafiti na akaandika vitabu mbalimbali. Katika baadhi ya vitabu vyake maarufu ni “The Bible, The Qur’an and Science” Biblia , Kuruani na Sayansi” “What is the origin of man” Je ni nini asili ya binaadamu. “Moses and Pharaoh in the Bible Quran and HIstory” Musa na Firauni katika Biblia, Quruani na Historia Na kuna vinginevyo ambavyo havikutajwa hapa. Na vitabu vyake vyote aliviandika kwa lugha yake ya asili ya kifaransa na vilifasiriwa baadaye kwa lugha kubwa za ulimwenguni kama vile kiingereza.

Baada ya utafiti huo maiti hiyo ilikwenda katika majengo ya makumbusho mbali mbali ulimwenguni na hivi sasa ipo katika jengo la makumnusho huko Misri. kama alivyosema mwenyeezi mungu katika kuruani tukufu “ili uwe dalili kwa ajili ya wa nyuma yako”

Waganga wenye kupiga bao au ufumo mara nyingi wanatuelezea yatakayokuja lakini hawatuelezi yaliyopita. Na hizo kazi zao ni Batili kwani hairuhusiwi katika dini ya kiislamu. Je waganga wa Mfumo wa leo wanaweza kushindana na mwenyeezi mungu? Kwani wao mara kwa mara wanatabiri yatakayokuja bali hapa mwenyeexi mungu anatueleza yaliyopita na yatakayokuja. kabla na baada kwa maelfu ya miaka.Utabiri wa hali ya juu ambao hakuna binaadamu anyeweza hivyo!!!!

Bwana Maurice Bucaille alishangaa sana kusoma katika Kuruani habari zenye uhakika na akakiri kuwa Kuruani siyo maneno ya Mtume bali yanatoka kwa Mwenyeezi Mungu. Hakuna uhakika kama bwana huyu aligeuza dini lakini alikubali kwamba Kuruani ni maneno ya ukweli. Ijapokuwa kicha cha Video hii kinasema aliukubali uislamu.

UMRI WA MTUME MOHAMED UMEASHIRIWA KATIKA KURUANI TUKUFU (PIA SIKILIZA KWA KIREFU HABARI HIZI KATIKA VIDEO YA KUMI NA MBILI KATIKA MLANGO WA SAUTI ZA MWANDALIZI WA WEBSITE HII)

UMRI WA MTUME MOHAMED KATIKA KURUANI NI MUUJIZA MKUBWA

Umri Wa Mtume Mohamed katika Kuruani Takatifu Katika Mlango huu Tutazungumzia Muujiza Unaohusiana na Umri Wa Mtume Mohamed (sala na amani za mwenyeezi mungu zimfikie) Kuruani Ni Muujiza mkubwa ambao tumeachiwa ili itufae katika maisha yetu. Na Mweneyeezi Mungu ameweka maajabu yasiyo na mwisho ambayo ni dalili ya kuthibitisha kwamba kuruani siyo maneno ya binaadamu. Haiwezekani kwa binaadamu kuweza kutamka maneno yaliyopangika kwa hali ya juu kama ilivyo kuruani. Kwa kweli inashangaza sana tena sana. Binaadamu na Majini wote tumeshindwa kutunga au kutoa elimu kama hii ya kuruani. Baadhi wa waandishi wanatuambia kwamba Mtume alizaliwa mwaka 570 C.E na Kufariki mwaka 632 CE na kwa tarehe hizi tunapata miaka 62 (632-570=62) yaani umri wa mtume ni miaka 62 ya hesabu ya jua lakini ni miaka 63 ya hesabu ya miezi. Kwa kweli tofauti ni miaka ya wenye kuhesabu miezi (sidereal calendar) au kuhesabu jua (sinodical calendar). Kwa wale wenye kutumia miezi kama vile calendar ya kiislamu basi tunapata umri wa mtume kuwa ni miaka 63 na wale wanaotumia miaka ya jua miaka inakuwa 62 kwani mwaka wa kiislamu ni mdogo kwa siku 11 (One Sinodical Year has 365 days which is equavalent to 554 days of Sidereal Year). Kwa hiyo tusibabaike kwani tofauti hii ni Calendar za kiislamu na Nyinginezo.

Muujiza Katika Kuruani

Katika kuruani tutapata uhakika wa umri wa Mtume na kwa kweli huu ni muujiza mkubwa sana. Kuna Aya mbalimbali katika kuruani ambazo zinazungumzia kufariki kwa mtume Mohamed (sala na amani za mwenyeezi mungu zimfikie) na mfano pia kwetu kwamba tutafishwa lakini hazitupi umri. Na mfano wa aya hizo ni kama zifuatazo:

{ إِنَّكَ مَيِّتٌ وَ إِنَّهُمْ مَيِّتُونَ } [الزمر: 30]

{ وَ مَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ }  [آل عمران: 144]

{ اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنْفُسَ حِينَ مَوْتِهَا}  [الزمر: 42]

{ قُلْ يَتَوَفَّاكُمْ مَلَكُ الْمَوْتِ }  [السجدة: 11].

Ama Aya zinazozungumzia kufishwa kwa mtume Mohamed na pia kuashiria umri wake ni kama zifuatazo

فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَۚقٌّ۬ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ (٧٧)

Tafsiri Ya Aya Basi subiri, hakika ahadi ya Mungu ni kweli.Na kama tukikuonyesha (papa hapa ulimwenguni)baadhi ya yale Tunayowaonya au Tukikufisha (kabla yake; yote ni sawa sawa, Tutawaadhibu tu). Marejei yao ni Kwetu. Kisha Mwenyeezi Mungu ni Shahidi juu ya (yote) wanayoyatenda. Aya Namba 77 Sura Namba 40-Ghafir Aya Hii ilishuka mwanzoni mwa kulingania dini Mume alipokuwa na miaka 40

——————

وَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَـٰغُ وَعَلَيۡنَا ٱلۡحِسَابُ (

٤٠) Tafsiri Ya Aya Na kama tukikuonyesha (papa hapa ulimwenguni)baadhi ya yale Tunayowaonya au Tukikufisha (kabla yake; yote ni sawa sawa, Tutawaadhibu tu). Marejei yao ni Kwetu. Kisha Mwenyeezi Mungu ni Shahidi juu ya (yote) wanayoyatenda. Aya Namba 40 Sura Namba 13-Raad Aya Hii Ilishuka Mecca katika mwaka wa 13 na baada ya hapo akahamia Medina.

—————————–

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ ٱللَّهُ شَہِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ (٤٦)

Aya Namba 46 Sura Namba 10-Yunus Tafsiri Ya Aya Na kama tukikuonyesha (papa hapa ulimwenguni)baadhi ya yale Tunayowaonya au Tukikufisha (kabla yake; yote ni sawa sawa, Tutawaadhibu tu). Marejei yao ni Kwetu. Kisha Mwenyeezi Mungu ni Shahidi juu ya (yote) wanayoyatenda.

Aya Hii ilishuka Medinna ilikuwa mwishoni mwa mwaka wa 10 na baada ya hapo haikuchukua muda mrefu Mtume akafariki dunia.

————————-

Ukizifikiri aya hizi tatu ambazo zinafana nazo zimeshuka katika sura tatu mbalimbali basi utaona katika aya hizi muujiza wa umri wake mtume Mohamed Na pia Vitabu vinavyozungumzia maisha ya Mtume Mohamed vinasema kwamba Mtume Mohamed aliishi miaka 63. Alishushiwa Kuruani na kupewa utume alipokuwa na miaka 40 (Mecca) Aliishi na kulingania Dini ya kiislamu hapo Mecca kwa muda wa miaka 13 (Mecca) Aliishi na kulingania dini ya kiislamu huko Medinna kwa muda wa miaka 10 Kwa hiyo Jumla ya miaka ni: 40 + 13 + 10=63 Ukichunguza Namba za sura utaona kwamba Aya ya kwanza ipo katika Sura namba 40 na Aya ya pili kutoka katika sura namba 13 na Aya ya tatu kutoka katika sura namba 10 na Jumla ya namba ya sura hizi ni 40 + 13 + 10=63 Lakini ajabu sana utaona kwamba namba 40 ni mwanzo wa Mtume alipopewa ujumbe wa dini ya kiislamu.Namba 13 inayofuatia ni Miaka 13 aliyoishi Mecca na Namba 10 ya mwisho ni miaka 10 ya mwisho aliyoishi Medinna kabla ya kuondoka dunia.Na ajabu aya hizi tatu zinazungumzia habari ya kufishwa mtume Mohamed yaani atondolewa duniani.

Na jambo lingine la kushangaza ni kwamba idadi ya maneno katika sura hizi tatu ni kama ifuatavyo:

Yunus=1833

Raad=854

Ghafir=1219

Jumla= 3906 (63 X 62)

Hizi namba hazikuja kwa bahati au hovyo hovyo bila ya mpango kwani Namba 62 ni umri wa mtume kwa kutumia hesabu ya Sinodical Calendar Na Namba 63 ni umri wa mtume kwa kutumia hesabu ya Sidereal Calendar Na kwa kweli mwenyeezi Mungu anatuthibitishia hekima yake katika kuruani kwa kauli yake anayosema katika sura ya HUD Aya namba 1

الٓر‌ۚ كِتَـٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَـٰتُهُ ۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ (١)

Alif, Lam, Ra. [This is] a Book whose verses are perfected and then presented in detail from [one who is] Wise and Acquainted. Yaani Aya za kuruani zilipangwa na kuandaliwa kabla ya kushushwa. Umri wa Mtume pia umeashiriwa katika Sura Ya Annasr

سُوۡرَةُ النّصر بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ (١) وَرَأَيۡتَ ٱلنَّاسَ يَدۡخُلُونَ فِى دِينِ ٱللَّهِ أَفۡوَاجً۬ا (٢) فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُ‌ۚ إِنَّهُ ۥ ڪَانَ تَوَّابَۢا (٣)

Hii ni sura ya mwisho iliyoshushwa katika kuruani tukufu na mtume alikuwa na umri wa miaka 63. Na Ibn Abbass aliona ishara katika sura hii kwamba inaonyesha kuondoka kwa mtume duaniani na ndivyo ilivyotokea kweli. Na hii sura ilishuka kwa mtume alipokuwa na umri wa miaka 63. Jambo la kushangaza ni katika sura hii ambalo linaashiria umri wa mtume mohamed. Angalia hapa chini habari hizi za in Abbas katika sherehe ya Ibn Kathir:

From Tafsir of Ibn Kathir Al-Bukhari recorded from Ibn `Abbas that he said, “Umar used to bring me into the gatherings with the old men of (the battle of) Badr. However, it was as if one of them felt something in himself (against my attending). So he said, `Why do you (`Umar) bring this (youth) to sit with us when we have children like him (i.e., his age)’ So `Umar replied, `Verily, he is among those whom you know. Then one day he called them and invited me to sit with them, and I do not think that he invited me to be among them that day except to show them. So he said, `What do you say about Allah’s statement, ﴿إِذَا جَآءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ ﴾   (When there comes the help of Allah and the Conquest.)’ Some of them said, `We were commanded to praise Allah and seek His forgiveness when He helps us and gives us victory.’ Some of them remained silent and did not say anything. Then he (`Umar) said to me, `Is this what you say, O Ibn `Abbas’ I said, `No.’ He then said, `What do you say’ I said, `It was the end of the life of Allah’s Messenger that Allah was informing him of.

Allah said, (When there comes the help of Allah and the Conquest.) was revealed, the Messenger of Allah said, «نُعِيَتْ إِلَيَّ نَفْسِي» (My death has been announced to me.) And indeed he died during that year.” Ahmad was alone in recording this Hadith.

Al-Bukhari recorded that `A’ishah said, “The Messenger of Allah used to say often in his bowing and prostrating,

Na ndiyo maana Maswahaba waliitia jina lingine lenye maana ya (“Attawddiy’) yaani ni sura ya kumwaga mtume. Na sura hii inambashiria mtume kwamba watapata mafanikio ya kuichukua Mecca na pia inaashiria kufikia mwisho wa kazi au jukumu alilopewa mtume Mohamed. Sura Hii inakamilisha mafanikio yaliyopatikana katika mkataba wa Hudaybiya ambao ulikuwa ni matokeo na zawadi kubwa aliyopewa Mtume na Mwenyeezi Mungu. Na Mwenyeezi Mungu alishusha Sura Ya Alfath kuwaliwaza waislamu walipozuiliwa na makafiri wa Mecca kuingia Mecca kwa Hija ambayo mwanzo wake walimtii mtume alipooteshwa kuelekea Mecca kwa ajili ya ibada. Omar Ibn Khatab na Baadhi ya mawaswahaba hawakufurahi lakini Mtume alikuwa imara na wala kuhuzunika kwani yeye aliitii amri ya mola wake na alijua kutakuwa na sababu maalum. Basi Sura hiyo ya Alfath inamliwaza Mtume na maswahaba kama walivyoambiwa kwamba wamepata ushindi mkubwa wa Treaty (mkataba) huo waliufanya baina yao na makafir wa Mecca katika makubaliano ambayo yalisababisha taifa la kiislamu litambulikane na kukua. Muujiza hapa ni kwamba ukihesabu sura hii ya Alfath mpaka sura Ya Annasr basi utapata Jumla sura 63 ambazo pia zinaashiria umri wa mtume mohamed wa kuishi duniani. Na muujiza mwingine ni aya hii ambayo limetajwa jina la mtume:

مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّهِ‌ۚ pamoja na Rasullullah Aya Namba 29-Sura Namba 48 Alfath

مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّهِ‌ۚ وَٱلَّذِينَ مَعَهُ ۥۤ أَشِدَّآءُ عَلَى ٱلۡكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيۡنَہُمۡ‌ۖ تَرَٮٰهُمۡ رُكَّعً۬ا سُجَّدً۬ا يَبۡتَغُونَ فَضۡلاً۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٲنً۬ا‌ۖ سِيمَاهُمۡ فِى وُجُوهِهِم مِّنۡ أَثَرِ ٱلسُّجُودِ‌ۚ ذَٲلِكَ مَثَلُهُمۡ فِى ٱلتَّوۡرَٮٰةِ‌ۚ وَمَثَلُهُمۡ فِى ٱلۡإِنجِيلِ كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُ ۥ فَـَٔازَرَهُ ۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ يُعۡجِبُ ٱلزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِہِمُ ٱلۡكُفَّارَ‌ۗ وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ مِنۡہُم مَّغۡفِرَةً۬ وَأَجۡرًا عَظِيمَۢا (٢٩)

katika kuruani nzima hii ni aya pekee inayomtaja Mtume jina lake na Rasulu pamoja.

————

Lakini kuna aya ninginezo tatu ambazo zinataja jina la Mtume peke yake. Yaani Mohamed nazo ni: Aya Namba 2 Sura 47 Mohamed

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ۬ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّہِمۡ‌ۙ كَفَّرَ عَنۡہُمۡ سَيِّـَٔاتِہِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ (٢)

———————-

Aya 144 Sura Namba 3 Imran

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ۬ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُ‌ۚ أَفَإِيْن مَّاتَ أَوۡ قُتِلَ ٱنقَلَبۡتُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَـٰبِكُمۡ‌ۚ وَمَن يَنقَلِبۡ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ فَلَن يَضُرَّ ٱللَّهَ شَيۡـًٔ۬ا‌ۗ وَسَيَجۡزِى ٱللَّهُ ٱلشَّـٰڪِرِينَ (١٤٤)

———————–

Aya Namba 40 Sura Namba 33-m Alahzaab

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٍ۬ مِّن رِّجَالِكُمۡ وَلَـٰكِن رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمً۬ا (٤٠)

Ukitafuta herufi za aya tuliyoitaja hapo juu kutoka katika Aya Namba 29-Sura Namba 48-Alfath katika sura ya Annasr مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّهِ‌ۚ utapata herufi pia 63 ambazo zinaashiria umri wa mtume Mohamed.

م=  1 ح=3   م=  1  د  =   3  ر  = 4  س  = 3 و   =6 ل    =  7 ا    =17 ل=  7  ل =  7 ه=4 1 + 3 + 1 + 3 +4 + 3 + 6 + 7 + 17 + 7 + 7 + 4=JUMLA 63 NI UMRI WA MTUME 

ambao ni umri wa Mtume Mohamed. Utume katika hii Sura Ya Annasr: Na pia tunapata muujiza mwingine katika sura hii kwamba: Kufuatana na hadithi ya Mtume

حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عَمَّارٍ، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ ” الرُّؤْيَا الْحَسَنَةُ مِنَ الرَّجُلِ الصَّالِحِ جُزْءٌ مِنْ سِتَّةٍ وَأَرْبَعِينَ جُزْءًا مِنَ النُّبُوَّةِ

” It was narrated from Anas bin Malik that the Messenger of Allah (ﷺ) said: “A good dream from a righteous man is one of the forty-six parts of prophecy. Grade : Sahih (Darussalam) Reference : Sunan Ibn Majah Hadithi hii inasema kwamba Ndoto ya mcha mungu ni sehemu moja ya sehemu 46 ya utume. Na ajabu au muujiza katika sura hii ya Annasr ni kwamba herufi za jina النبي محمد zilizotumika katika sura hii ni 46 nazo zinathibitisha utume wake kwazi kweli alikuwa mtume.

ا =17 ل  =7  ن =4  ب  =6   ي =4      م =1    ح=3      م =1  د =3

Jumla ya herufi hizi ni= 17 + 7 + 4 + 6 + 4 + 3 + 1 + 3 + 1 = 46

Muujiza juu ya Muujiza bila mwisho, maelfu ya miujiza ambayo inathibitisha kwamba Mtume ni wa kweli na Kuruani ni maneno ni yake Mwenyeezi Mungu na wala sio uongo isipokuwa wajinga ndiyo pekee wanaokanusha haya. Na utakuta umri wa mtume Mohamed umeashiriwa katika sura anyinginezo kama vile Sura Ya Mohamed na Mudathir ambazo sura anazojulikana kwa jina lake..

CALENDAR YA ULIMWENGU (COSMOLOGICAL CALENDAR)

CALANDAR YA ULIMWENGU-COSMOLOGICAL CALENDAR

Kuruani inaashiria kwa hekima kubwa uwiano wa umri wa dunia kulinganisha na ulimwengu. Kwamba imechukua siku mbili kuumba dunia peke yake.

Na Ulimwengu pamoja na dunia umechukua siku sita. Hii ni uwiano wa 2 kwa 6 ambayo ni sawa na uwiano wa 1 kwa 3 (2/6=1/3) na ukilinganisha na hesabu za kisayansi unapata jibu kama hili kutoka katika kuruani. Sayansi inatuambia Umri wa Dunia ni Miaka Bilioni 4.5 na Umri wa Ulimwengu ni Miaka Bilioni 13.7 . Uwiano wa 4.5 kwa 13.7 (4.5/13.7=1/3) na jawabu ni 1 kwa 3.

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ۬ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ يُغۡشِى ٱلَّيۡلَ ٱلنَّہَارَ يَطۡلُبُهُ ۥ حَثِيثً۬ا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٲتِۭ بِأَمۡرِهِۦۤ‌ۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُ‌ۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٥٤)

Mwenyeezi Mungu anatuambia hapa kwamba (kipande nilichopigia mstari)ameumba mbingu na ardhi kwa muda wa siku 6. 

Na hili ni jambo la kushangaza kwani kuruani inakubaliana na hesabu hizi kwa hekima kubwa sana. Mwenyeezi Mungu anataja siku sita lakini kwa wakati wetu wa dunia yetu ni miaka Bilioni 4.5 kwani siku zetu ni tofauti na siku katika sehemu nyingine za malimwengu.

Kwa hiyo wakati unabadilika kufuatana na sehemu katika malimwengu yake mwenyeezi mungu. Kila sehemu ina wakati tofauti na nyingine.Katika ulimwengu wetu mwenyeezi mungu amejaalia masaa ishirini na nne usiku na mchana na kwa hiyo tunapata masiku 30 na miezi 12 katika mwaka Na katika malimwengu mengine mwenyeezi mungu anaashiria kwa hekima kubwa kutufahamisha kwamba ziko sehemu nyinginezo zina wakati tofauti na wetu na leo hii tunagundua haya ni muujiza mkubwa.

Wanasayansi wote akiwamo kiongozi wao Einstain wamezungumzia haya katika nadharia maarufu inayojulikana kama Relative Theory. Na tunaambiwa kwamba kila sehemu ulimwenguni ina TimeFrame yake. Jambo la kushangaza ni kwamba kuruani imezungumza nadharia kubwa kama hizi miaka mingi iliyopita na leo hii wataalamu wanagundua leo hii kwa kutumia elimu na vyombo vya kitaalamu mbalimbali.

Mwanasayansi mwenye elimu mbalimbali za Anga kutoka Amerika Anayejulikana kwa jina “Carl Sagan” alikuja na Fikra Ya Calendar ya Universe (Ulimwengu). Aliielezea katika kitabu chake kinachojulikana kama “The Dragons of Eden mwaka 1977”.

Na Fikra yake ilikuwa ni kufupisha Tarehe Ya Kuumbwa kwa Ulimwengu katika Muda wa Mwaka Mmoja. Yaani muda wa kuumbwa Ulimwengu unaojulikana ni Miaka Bilioni 13.7 au 13.8. Nayo katika ramani imefanyiwa Scale ya Miezi kumi na Mbili. (Scale to 12 months) Yaani kila mwezi unawakilisha Miaka Bilioni 1.15 Na ukiangalia Calendar hiyo Utaona ardhi iliumbwa katika tarehe 24 ya December. Na Binaadamu wote wapo katika siku ya mwisho wa mwezi wa December

Lakini Bwana Carl alikuwa hakujua kwamba Kuruani imetangulia Elimu hii na kwa hali ya juu kwa kuja na fikra hii katika aya zake zinazotumia neno “YAWM” lenye maana ya siku na pia zinawakilisha muda wa kipindi kirefu. Ulimwengu umeumba kwa vipindi 6 yaani siku sita ambayo inawakilisha miaka bilioni 13.8. na iwapo tutarekibisha ramani ya Ulimwengu basi badala ya miezi kumi na mbili tutapachika siku sita. (Scale to 6 days) na Itakuwa kila siku (YAWM) itawakilisha miaka Bilioni 2.30 Na ikiwa binaadamu ni hodari na ameweza kufupisha Calendar ya mabilioni ya miaka katika muda mfupi wa miezi kumi na mbili basi mwenyeezi Mungu ametufupishia kwa siku sita (vipindi sita) ili kuwakilisha umri wa ulimwengu!!!  sasa ni nani hodari wa kufupisha hapa.

Ni Mwenyeezi Mungu au Wanasayansi?

Juhudi zote alizofanya Mwanasayansi Huyu na Mwisho wa  uwezo wake wote aliweza kufupisha miezi 12 na Mwenyeezi Mungu ametufupishia katika kuruani kwa siku 6 tu!!!

Huoni Ukubwa huo? Huoni  Nguvu hizo?

Jibu Ni Nguvu za Mfalme wa Wafalme wote naye Ni  Mwenyeezi Mungu.  

مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ- ٤     

Mfalme  Wa siku ya Mwisho. 

ISHARA AU ALAMA ZA KUSHANGAZA ZA NUMBER ( Pi π ) au 3.14 (AREA OF THE CIRCLE CALCULATION) NA PIA 360 DEGREES KATIKA KURUANI TUKUFU.

HISTORIA FUPI YA “Pi π”

Archemedes alikuwa Mwanasayansi wa Kigiriki (Mathematician, Astronomer, Physist, Engineer and Inventor) Mashuhuri katika kipindi chake cha Classical Antiquity. Alizaliwa na Kufariki katika nchi ya  Italy. (Alizaliwa Mwaka c. 287 BCE-Akafariki Mwaka 212/211 BCE).

Mojawapo ya juhudi zake ilikuwa kutafuta ENEO la Duara (Area of The Circle). Njia alizotumia za kutafuta ENEO hilo ilikuwa Kutumia Duara mbili zenye Pembe mbalimbali.(Zinajulikana katika Hesabu Polygon) Moja aliingiza ndani ya Duara na Nyingine akalizungushia Duara. (Yaani Moja Nje and nyingine ndani ya Duara). Alianza na Duara Yenye pembe 12 kisha 24 kisha 48 na Mwisho Duara (Polygon) Yenye pembe 96. Hakuzidisha zaidi ya Pembe 96. Kwa hiyo Akachukua Urefu wa Polygon hizo Mbili (Nje na Ndani ya Duara) na akaziweka pamoja na kuchagua urefu wa katikati ya Polygon hizo mbili na katika kufanya hivyo akapata kipimo ambacho tunatumia mpaka leo katika kutafuta ENEO za duara. Urefu wa Polygon ya nje alioupata ulikuwa 3.142714 na wa Polygon ya Ndani ulikuwa 3.141032. Na Namba ya katikati aliyoichagua (baada ya kuifupisha kwa kuondoa namba baada ya Decimal)ni 3.14. Namba hii katika Hesabu inajulikana kama Pi (Yaani Perimeter au kipimo cha Urefu wa Duara au Degrees 180) Ambayo inalingana na  Diameter Tatu za Duara na mabaki ya sehemu ndogo ya Diameter yaani 0.14. Katika Elimu ya Hesabu ukitafuta ENEO la Duara yoyote ile na Ukipewa Diameter au kipimo cha Mapana Ya Duara basi utatumia Namba hii ya Pi (3.14) kisha utazidisha na Kipimo hicho. Na ukipewa Nusu ya Mapana basi utatumia Namba hii na Kuzidisha na Nusu hiyo (Mara mbili) 3.14 X 2 X Radius.

MUUJIZA WA NAMBA HIZI KATIKA KURUANI

Kuruani siyo kitabu cha sayansi lakini kuna maajabu ambayo yanatuzidishia imani. Kuruani ni muujiza mkubwa sana usio mfano. Utashangaa sana ukiambiwa kwamba Namba 96 Ya Polygon na Pia Namba 3.14 zipo katika Sura Ya Al-Alaq. Sura Hii ni Namba 96 ambayo inalingana na namba hiyo ya Polygon aliyetumia Archemedes mwanasayansi katika kutafuta ENEO la Duara. Na La kushangaza zaidi katika Sura ya Alaq kuna pia kipimo hicho cha 3.14.

Katika Aya Namba 8 Ya Sura Ya Al-Alaq.

SURA YA AL-ALAQ NAMBA 96 

سُوۡرَةُ العَلق

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ (١) خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِنۡ عَلَقٍ (٢) ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ (٣) ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ (٤) عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ (٥) كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَـٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ (٦) أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ (٧) إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ (٨) أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِى يَنۡهَىٰ (٩) عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ (١٠) أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ (١١) أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ (١٢) أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ (١٣) أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ (١٤) كَلَّا لَٮِٕن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ (١٥) نَاصِيَةٍ۬ كَـٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ۬ (١٦) فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُ ۥ (١٧) سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ (١٨) كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡ وَٱقۡتَرِب ۩ (١٩)

TAFSIRI YA AYA ZA SURA YA AL-ALAQ  AYA  1-8

Kwajina Ia Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

1. Soma kwa. jina Ia Mola wako Aliyeumba

2. Amemuumba mwanaadamu kwa panqe Ia damu.

3· Soma, na Mola wako ni Karimu sana

4· Ambaye Amemfundisha (Binadamu ilimu zote hizi) kwa wasita (msaada) wa kalamu; (zilizoandika vitabu, watu wakapata ilimu)

5.Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui.

6.Sivyo hivi (we Binad’amu)! Kwa hakika binadamu hutakabari

7.Akijiona amepata utajiri!

8.Bila shaka marejeo (ya wote) ni kwa Mola wako (tu).

SHEREHE YA MANENO YENYE UHUSIANO NA ELIMU YA HESABU

1- Neno ARRUJAA ٱلرُّجۡعَىٰ lina maana ya Kurudi (yaani kurudi kwa Mwenyeezi Mungu) Na inafahamika kwamba unaporudi nyuma basi lazima ugeuze njia na kurudi ulikotoka. na Kihesabu itakuwa umefanya mzunguko wa 180 Degrees ambayo ni sawa na Pi Radians.(Pi Radians= 180 degrees).

2-Ukihesabu Herufi Za Kila Aya (Aya Kwa Aya) Kisha Ukajumlisha namba zote Kuanzia Aya Ya Mwanzo ya sura ya Al-alaq Mpaka Neno ARUJAA Yaani Aya Namba 8 utapata kipimo tulichokitaja hapo juu (314) Kwa mfano Herufi Za kila neno katika Aya Ya Kwanza

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ ni sawa na 42=3+2+1 + 4+3+2+1 + 3+2+1 + 4+3+2+1 + 4+3+2+1 (hapa tunahesabu kulia kwenda kushoto kama tunavyosoma kuruani) Ukihesabu Herufi Ya Aya Zilizobakia 7 na ukijumlisha na Aya ya kwanza utapata namba zifuatazo: 42+36-41-37-43-45-34-36 ambayo jumla ya namba hizi ni 314 na namba hii inaashiria hiyo Pi inalingana na kipimo cha kutafutia ENEO la duara ijapokuwa hakuna Decimal baina ya 3 na 14. lakini inaashiria namba ile ile ya kipimo yaani Pi.

3-Hapo zamani Mayahudi, Waarabu na Mataifa Mengineyo walitumia Herufi badala ya Namba (Namba 0,1,2,3,4,5,6,7,8,9 zilikuwa bado hazijulikani katika wakati huo) Na kwa Hiyo tukitafuta Thamani Ya herufi Za Neno ٱلرُّجۡعَىٰٓ Kwa kutumia Namba za Gematrical Values (ambazo zinajulikana kama Elimu Ya Jumal) tutapata kama ifuatavyo: Alif + Lam + Raa +Jim +Ain + Ya= 1 + 30 + 200 + 3 + 70 + 10= 314 ambayo jumla ya namba hizi ni 314 na namba hii ni hiyo Pi ni kipimo cha kutafutia ENEO la duara ijapokuwa hakuna Decimal baina ya 3 na 14 lakini inaashiria namba hii (Elimu Ya Gematrical Values tumezungumzia katika mojawapo ya Video za Muujiza wa kihesabu sehemu ya “Sauti ZaMwandalizi” kwa hiyo hatutarudia kuelezea hapa)

4-Na Ukitafuta Thamani Ya Aya Namba 8 Yote yaani

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ 

628=314 + 20 + 2 + 200 + 10 + 30 + 1 + 50 + 1 (Kuanzia Herufi Ya Kwanza ya neno إِنَّ “INNA” mpaka neno “ARRUJAA” – ٱلرُّجۡعَىٰٓ neno la mwisho katika Aya Hii) Kwa kutumia namba za Herufi walizokuwa wanatumia Waarabu hapo zamani Na kuzijuumlisha basi utapata namba nyingine ya kushangaza nayo ni 628 na Namba hii ni mara mbili ya kipimo tulichotaja hapo juu (314 X 2=628). Tafsiri mojawapo hapa ni kwamba “Tumeletwa duniani na kisha tutarudishwa kwa Mwenyeezi Mungu) Kihesabu kama kwamba Kitendo cha kuletwa duniani kimechukua Degrees 180 na Kitendo cha kurudishwa pia Degrees 180 na ukjuumlisha vitendo hivi viwili unapata 628. (Yaani Kuja na Kurudi) Jambo la kushangaza sana ni kwamba kama tulivyoona namba 96 na namba 3.14 zinapatikana katika sura hii kiajabu sana. Hii ni dalili kwamba Herufi za Kuruani zimebeba Elimu na mengineyo tusiyoyajua Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akasema kwamba Kuruani haikuacha kutaja chochote. Utafiti huu huenda ukawa na ukweli na huenda ukawa na kosa Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi kwani Elimu zetu ni changa sana. Lakini tunapata imani zaidi tunaposoma haya kwani vijana wengi hivi leo wanadharau dini na kufikiri kwamba ipo nyuma na sayansi imeendelea. Tunajirudisha nyuma kwa kudharau dini na kuruani tukufu kwa ujinga wetu wenyewe. Angalia Utafiti huu je huoni maajabu? Elimu kubwa kubwa zimehifadhiwa (CODIFIED) katika Herufi za Kuruani Tukufu. Allahu Akbar, Allahu Akbar.

360 DEGREES KATIKA SURA YA ANNAJM NAMBA 53

Na Sura Ya Annajm ina maneno 360 na ajabu ni kwamba sura hii ina Aya inayosema فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ Neno قَابَ (Kaba) li maana ya Kipimo (yaani kiasi) na neno قَوۡسَيۡنِ (Kawsayni) ni kama vile Upinde uliopinda na ncha zake mbili kukaribiana. Nazo zimekaribiana sana katika kufanya DUARA ambalo kihesabu ni 360 Degrees. Tusisahau kwamba maana ya Aya kuhusu makaribiano siyo ya kitu au vitu au kiwiliwili bali Kimaana yaani kuwa karibu na rehema na utukufu wake mola. Lakini Kidunia inashangaza kupata neno قَوۡسَيۡنِ ambalo katika Elimu ya Hesabu kuna pia Maneno mawili katika Mlango wa Trigonometry yanayojulikana kama Cosine and Sine. Ni vipimo vinavyotumika katika Elimu ya Trigonometry kutafutia pembe (Angles) na Pande (Sides) ya Pembe Tatu (Triangles) na katika kazi hiyo tunaona uhusiano wake na Degrees na vipimo vinginevyo kama vile centimeter au meter etc. Na maneno haya mawili Yana matamshi ya Cosine na Sine yanalingana na قَوۡسَيۡنِ “Kawsayni”. katika utafiti wetu huenda tukakosa lakini inashangaza sana kwani Kuruani ni Muujiza Mkubwa. Kuruani Ni Yake na Elimu zote pia ni zake Mwenyeezi Mungu kwa hiyo siyo ajabu yeye kuzitaja katika kuruani na pia sisi kuzisoma kwani itatusaidia ili tusidanganyike na Elimu ndogo ndogo za duniani na tusisahau kwamba Mwenyeezi Mungu ndiye aliyetuumba na kila kitu. Allahu Akbar.

Mwenyeezi Mungu Anajua Zaidi. Sisi Binaadamu tunatafuta na huenda Tumesibu au Tumekosa Na Kwa Hiyo Tutatumia neno “Huenda” Na Kwa Hiyo Tunawaachia Wasomaji Wafikiri Pia Na Wafate Maoni Haya au Yao)

Archimedes ndiye aliyegundua kipimo cha kupimia Area ya Duara kinachojulikana kama Pi. Alianza na Poygon na baadaye akazidisha nyinginezo mpaka kufikia 96 ndani ya duara. Njia hii ilimsaidia kuja na Nadharia inyojulikana kama Pi. Angalia chini maelezo zaidi.

Picha hi ni mfano wa Polygon yenye pembe 96. Mwana Sayansi Archemedes alitumia Polygon katika Utafiti wake wa kutafuta ENEO la Duara. Alianza na Polygon mbili zenye pembe mbalimbali hatimaye akaishia na Yenye pembe 96.

MUUJIZA WA NAMBA 7. SHEREHE IMEANZIA MWISHONI MWA MLANGO WA “ELIMU”

SEHEMU YA MWISHO WA MUUJIZA WA NAMBA 7 INAENDELEA KUTOKA KATIKA MLANGO WA “ELIMU”

Milango ya Moto Wa Jahanam Mwenyeezi Mungu anatuambia katika kuruani tukufu ni 7 kama anavyosema Mwenyeezi Mungu katika Sura Ya Alhijr Namba 15 Aya Ya 43 na 44

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ (٤٣) لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٲبٍ۬ لِّكُلِّ بَابٍ۬ مِّنۡہُمۡ جُزۡءٌ۬ مَّقۡسُومٌ (٤٤)

Tafsiri .

(43)Na bila shaka Jahanamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote ‘ (44). Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa (ya kuwa hii ya mlango fulani na hii ya mlango fulani).

Namba 7 Inashangaza sana kwa mfano Aya Za Kuruani zinazotaja Neno Jahannam ni 70 (7 X 10=70)

Mara ya Mwanzo kutajika namba 7 katika kuruani ni katika sura ya Albakarah 2 Aya namba 29 Na mara ya mwisho kutajika Namba 7 ni katika sura ya (Al-Nabaa 78 Aya namba 12) .Baina ya sura hizi mbili kuna sura 77 .Na idadi za Aya baina ya Aya hizi mbili ni 5649 ambayo (807 X 7=5649) ni multiple ya 7 .Na Ukihesabu Aya ya mwanzo (kutajika namba 7) kuanzia sura ya Albakarah (2:1) mpaka Aya ya mwisho (kutajika namba 7)ya sura ya Alnabaa (78:40) utapata Aya 5705 ambayo pia ni Multiple ya namba 7 (815 X 7=5705)

Jina “Allah” Limetajika kwa mara ya kwanza Katika sura ya Alfatiha Aya ya Kwanza (Al-Fatihah 1:1) Na mara ya Mwisho Kutajika ni Katika Aya ya pili ya Sura ya Al-Ikhlas (Al-Ikhlas 112:2), Na Baina ya sura hizi mbili kuna sura 112  ambayo ni Multiple ya 7 (16 X 12=112). Kutoka Aya ya Kwanza (Sura 1: Aya 1) mpaka Aya ya pili ya sura hizi mbili (Sura112: Aya 2) kuna Aya 6223 na hii namba ni Multiple ya 7 (889 X 7=6223) Jumla ya Herufi katika Aya hizi Mbili (1:1) na Aya ya (112:2) ni 28 ambayo ni Multiple ya 7 (7 X 4=28) Jumla ya herufi(Alif + Lam + Ha) za Jina Lake Mwenyeezi Mungu katika Aya Hizi Mbili (1:1) na (112:2)= ni herufi 14 ambazo ni Multiple ya namba 7 (7 X 2=14).

Namba Ya Herufi  zisizokariri katika Herufi za Muqatwaa (“disjoined letters” or “disconnected letters) ni 14 nazo ni (Alif,Lam,Mim,Sin,Raa,Yaa,Kaf,Haa,Ta,Qaf,Nun,Swad, Ain,Ha) (Ni   7  X2=14) Namba za Ibara (Sets) za herufi Muqatwaa (“disjoined letters” or “disconnected letters)nazo zisizokariri ni 14 nazo ni Alif Lām Mīm الم/Alif Lām Mīm Ṣād المص/Alif Lām Rā الر/Kāf Hā YāʿAin Ṣād كهيعص/Ṭā Hā” طه/Ṭā Sīn Mīm طسم/Ṭā Sīn طس/Yā Sīn” يس/Ṣād ص/Ḥā Mīm حم/Ḥā Mīm-Ain Sīn Qāf حم عسق/Nūn ن/Alif Lām Mīm Rā المر/Qāf “Qāf” ق hizi pia ni Multiple ya namba 7 (7 X 2=14).

-Katika kuruani Herufi za Hijai (Arabic Alphatets ni 28) ni Multiple ya namba 7 yaani (7 X4=28)

-Jumla ya idadi ya maneno katika Aya ya Mwanzo na Ya mwisho ni 7 (Bismillahi ina maneno 4 na Minaljinnati Wa nnasi ina maneno 4 jumla ni 7)

-Jina la Sura Ya Ikhlas (Herufi Saba) Na Jina la Sura Alfatiha (Herufi 7)

-Mtume (Sala na Amani Zake Mola Zimfikie)ameishi miaka 63 (7 x9=63)

-Kaaba huko Mecca Tunazunguka Mara 7

-Safa Na Marwa huko Mecca ni Mara 7

-huko Mecca hutupwa Vijiwe 7

-Tunakatazwa tujiepushe na Madhambi makubwa 7

وعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال‏:‏ ‏”‏اجتنبوا السبع الموبقات‏”‏ قالوا‏:‏ يا رسول الله وما هن‏؟‏ قال‏:‏ ‏”‏الشرك بالله، والسحر وقتل النفس التي حرم الله إلا بالحق، وأكل الربا، وأكل مال اليتيم، والتولي يوم الزحف، وقذف المحصنات المؤمنات الغافلات‏”‏ ‏(‏‏(‏متفق عليه‏.‏ ‏”‏الموبقات‏”‏ المهلكات‏)‏‏)‏‏.‏

Translation

Abu Hurairah (May Allah be pleased with him) said: The Prophet (ﷺ) said, “Keep away from the seven fatalities.” It was asked: “What are they, O Messenger of Allah?” He (ﷺ) replied, “Associating anything with Allah in worship (i.e., committing an act of Shirk), sorcery, killing of one whom Allah has declared inviolable without a just cause, devouring the property of an orphan, the eating of usury (Riba), fleeing from the battlefield and accusing chaste believing women, who never even think of anything touching their chastity.” [Al-Bukhari and Muslim].

-Aina za Watu 7 ambao watakuwa chini ya Kivuli siku ya Kiyama

وعنه قال‏:‏ قال رسول الله ، صلى الله عليه وسلم‏:‏‏”‏سبعة يظلهم الله في ظله يوم لا ظل إلا ظله‏:‏ إمام عادل، وشاب نشأ في عبادة الله ، ورجل قلبه معلق في المساجد، ورجلان تحابا في الله، اجتمعا عليه، وتفرقا عليه، ورجل دعته امرأة ذات منصب وجمال، فقال‏:‏ إنى أخاف الله، ورجل تصدق بصدقة فأخفاها حتى لا تعلم شماله ما تنفق يمينه، ورجل ذكر الله خالياً ففاضت عيناه” ‏(‏‏(‏متفق عليه‏)‏‏)‏ ‏

Translation 

Abu Hurairah (May Allah be pleased with him) reported: Messenger of Allah (ﷺ) said, “Seven people Allah will give them His Shade on the Day when there would be no shade but the Shade of His Throne (i.e., on the Day of Resurrection): And they are: a just ruler; a youth who grew up with the worship of Allah; a person whose heart is attached to the mosques, two men who love and meet each other and depart from each other for the sake of Allah; a man whom an extremely beautiful woman seduces (for illicit relation), but he (rejects this offer and) says: ‘I fear Allah’; a man who gives in charity and conceals it (to such an extent) that the left hand does not know what the right has given; and a man who remembers Allah in solitude and his eyes become tearful”. [Al-Bukhari and Muslim].

-Viungo vya sala ni 7 (Mikono miwili, Miguu Miwili, Magoti Mawili na Paji la Uso)

-Ardhi ina matabaka 7  (Tumezungumzia kaika Mlango wa “Sayansi za Anga”)

Na katika Sura Ya Yusuf  Mwenyeezi Mungu anatuelezea Kuhusu Ndoto Ya Mfalme iliyohitajia Tafsiri ambayo inahusiana na N’gombe Saba na Pia Mashuke Saba. 

Sura Ya Yusuf Namba 12  Aya namba 43

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّىٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٲتٍ۬ سِمَانٍ۬ يَأۡڪُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٌ۬ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَـٰتٍ خُضۡرٍ۬ وَأُخَرَ يَابِسَـٰتٍ۬‌ۖ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِى فِى رُءۡيَـٰىَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ (٤٣) 

Tafsiri Ya Aya

Na (siku moja) mfalme (Firauni aliota) akasema (kuwaambia mawaziri wake). “Hakika mimi nimeona (ndotoni) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba ving’onda. Na nimeona mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka. Enyi wakubwa! Nipeni Tafsiri ya ndoto yangu ikiwa nyinyi mnaweza kufasiri ndoto (kuotoa).”

Ndugu Waislamu Mnaona Maajabu Haya Katika Namba Hii Ya 7 ? Je haitutoshi kumwogopa Mwenyeezi Mungu. Je hatuoni Miujiza ambayo haiishi kama alivyosema katika kuruani kwamba Miti yote ingekuwa kalamu na mabahari kuwa wino vingekwisha vyote hivyo kabla ya elimu yake kwisha. Allahu Akbar, Allahu Akbar. Tumche Mungu na Atusaidie katika kila kitu. Na autakabalie vitendo vyetu kwani Hatujui iwapo vitapokelewa. 

MUUJIZA WA KIHISTORIA KUHUSIANA NA FIRAUNI

FIRAUNI NA MAANDISHI WALIYOTUMIA

Sura Ya Al-Dukhan Aya Namba  17-29

سُوۡرَةُ الدّخان ۞

وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٌ۬ ڪَرِيمٌ (١٧) أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَىَّ عِبَادَ ٱللَّهِ‌ۖ إِنِّى لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٌ۬ (١٨) وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِ‌ۖ إِنِّىٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَـٰنٍ۬ مُّبِينٍ۬ (١٩) وَإِنِّى عُذۡتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ (٢٠) وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِى فَٱعۡتَزِلُونِ (٢١) فَدَعَا رَبَّهُ ۥۤ أَنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ قَوۡمٌ۬ مُّجۡرِمُونَ (٢٢) فَأَسۡرِ بِعِبَادِى لَيۡلاً إِنَّڪُم مُّتَّبَعُونَ (٢٣) وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًا‌ۖ إِنَّہُمۡ جُندٌ۬ مُّغۡرَقُونَ (٢٤) كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّـٰتٍ۬ وَعُيُونٍ۬ (٢٥) وَزُرُوعٍ۬ وَمَقَامٍ۬ كَرِيمٍ۬ (٢٦) وَنَعۡمَةٍ۬ كَانُواْ فِيہَا فَـٰكِهِينَ (٢٧) كَذَٲلِكَ‌ۖ وَأَوۡرَثۡنَـٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ (٢٨) فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡہِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ (٢٩)

TAFSIRI

17-Na hakika kabla yao Tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwajia Mtume ahishimiwaye

18-(Akasema); “Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu, (hawa Mayahudi nitoke nao hapa Misri mnapowataabisha). Kwa hakika mimi ni Mtume muaminifu (niliyeletwa kwenu) “

19-“Na msitakabari mbele ya Mwenyezi Mungu; mimi kwa yakini nitakuleteeni dalili zilizo wazi (za kuonyesha Utume wangu).”

20-“Nami najikinga kwa Mola wangu na (ndiye) Mola wenu (pia) ill msinipige mawe.”

21-“Nakama hamniamini, basi jitengeni nami, (msinidhuru).”

22-Ndipo akamuomba Mola wake kwamba Hawa ni watu waovu, (nihami nao).,

23-(Mwenyezi Mungu akamwambia): “Basi nenda pamoja na waja wangu (hawa Bani Israil) usiku, na mtafuatwa kwa yakini “

24-“Na iache bahari (vivyo hivyo imeachana baada ya kwisha kupita wewe na watu wako, usiifanye kukamatana tena mpaka apite Firauni na watu wake; wakipita itaambatana waghariki); hakika wao ni jeshi litakalozamishwa “

25-Mabustani mangapi na chemchem ngapi waliziacha (baada ya kugharikishwa)

26-Na mimea na mahali pazuri!

27-Na neema (kubwa kubwa) walizokuwa wakijistareheshea

28-Namna hivi (tumewafanya) Na tukawarithisha haya watu wengine.

29-Mbingu na ardhi hazikuwalilia. Wala hawakupewa muda (wa kurejea tena ulimwenguni).

HISTORIA FUPI YA MISRI

Jina FIRAUNI lilitumika hapo zamani kama “Nyumba Ya Mfamle” au “Royal Palace” lakini maana yake ikabadilika na kutumiwa kwa kila Mfalme wa huko Misri katika Kipindi cha “New Kingdom” neno hili hapo nyuma lilitumika kama Royal Palace. Wana Historia wanagawanya Egypt katika Mafungu Matatu (Old, Middle and New Kingdom). Egyptian hieroglyphs ni maandishi waliyotumia Wamisri katika maisha yao. Kwa kifupi ni maandishi ya michoro. Mawasiliano yalikuwa kwa kutumia michoro hiyo inayojulikana kama Hieroglyphs. Maandishi haya yalipotea kwa miaka mingi sana lakini katika karne ya 19 Maandishi haya yaliyofukuliwa huko Misri katika Pyramids na sehemu nyinginezo yalishughulikiwa na hatimaye kufasiriwa kwa ukamulifu baada tu ya kufukuliwa Jiwe linalojulikana kama Rosetta Stome ambalo lilikuwa limeandikwa kwa maandishi ya aina Tatu; hieroglyphic, Demotic, na Ancient Greek.

MUUJIZA MKUBWA WA KIHISTORIA KATIKA KURUANI TUKUFU

Katika miaka mbalimbali za harakati za kufasiri maandishi haya walikuta maandishi yaliyoandikwa yenye kuashiria Namna Wamisri walivyokuwa wakiomboleza maiti za Firauni, maombolezo yenye kuwapa Ukuu na utukufu Mkubwa Mafirauni na yenye kusema “Mawingu Yanalia” “Nyota Zinatingisika” “Waangalizi wa Miungu wanatetemeka na watumishi wao hukimbia wakati wanamwona Mfalme akiinuka kama roho” Katika maandishi haya yaligunduliwa katika Karne za hivi karibuni kwa msaada wa Wataalamu wakubwa duniani. Lakini habari hizi zilikuwa zimefukiwa kabla ya wakati wa Ukristo yaani katika miaka mingi sana iliyopita. Kuruani imeshuka katika Karne ya 7 na Ajabu kubwa sana ni Kwamba kuna Aya katika Kuruani yenye Kufichua siri hii ambayo hakuna aliyejua wakati huo kabla ya Uchambuzi wa maandishi haya katika karne ya 19. Utabiri kwa kawaida ni kwa mambo Yatakayokuja lakini hakuna Mtu wala Mtaalamu yeyote aliyeweza kufichua historia ya miaka Maelfu yaliyopita. Lakini Kuruani imefichua habari hizi katika Aya namba 29 sura ya Al-Dukhan hapa juu yaani Mtume anajuulishwa habari hizi za miaka chungu nzima iliyopita. Angalia Muujiza huu wa ajabu katika Sura Ya Adukhan Aya Namba 29 inayomjibu Firauni kwamba “Mbingu na Ardhi Hazikuwalilia” yaani haikulia kama walivyodhani na kuamini hao Mafirauni wakati huo. Waliamini kwamba Mbingu na Ardhi italia wanapokufa kina Firauni. Kama hii Kuruani siyo ya ukweli basi Mtume alijua vipi habari hizi ambazo zimejulikana hivi karibuni katika Karne ya 19? Yaani zimejulikana baada ya miaka 1200 tangu kushuka kuruani tukufu.