UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
VITA VIKUU VYA DUNIA, MAAJABU YA NAMBA NA MAAJABU YA KURUANI
Alhamdulilah leo Tarehe 18/09/2022. Namshukuru Mwenyeezi Mungu kutupa uzima na Afya. Ni Jumapili Jioni na Hali ya hewa ni Shwari. Wakati mzuri kuelezea Maajabu ya Namba zinazohusika na Vita Vya Dunia. Sikupendelea Kuandika Habari hii kwani hakuna anayependa Vita. Na pia sipendelei Kufuatilia Lugha ya Namba katika Utafiti huu kwani Inababaisha na Jambo la Kuruani Tukufu ni Hatari sana kwani wakati mwingine Namba huweza kutupa Habari isiyo ya kweli. Kuruni Ni Muujiza Mkubwa sana na Maandishi yake ni Muujiza mkubwa ambao hauna mwisho na pia Unababaisha ukifuatilia kwa njia isiyofaa. Kuruani siyo kitabu cha kupigia Bao au Kitabu cha Sayansi na kwa hiyo Tusiifanye kama ni Elimu tu ya maisha kama Elimu nyinginezo lakini Lazima tuelewe kwamba Kuruani ni Maneno makubwa Ya Mwenyeezi Mungu ambayo lengo ni Kutuongoza. Ni Kitabu cha Mafundisho katika Maisha yetu. Ni Muongozo wa maisha yetu na majini pia. Tuisome Kuruani kwa Kuifahamu na Kuifuata. Tunaposoma Miujiza iwe tu kwa lengo la kutuzidishia Imani lakini sio lingine. Tusiitumie kwa njia nyingine isiyofaa kama vile kazi za Munajim za Bao hiyo ni Haramu na Pia Kuyatumia Maneno ya Kuruani katika Upuuzi Mwingine.
Siku ya Leo Nitawazungumzia utafiti wa Profesa Kutoka Nchi Ya Iraq .Nilikutana Naye hivi Karibuni na Tulizungumza Habari za Kushangaza sana. Mazungumzo yalikuwa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiarabu. Nimefasiri kwa Kiswahili. Kuna Nyongeza na Pungufu katika Maandishi haya lakini Muhimu uelewe Madhumuni ya Mazungumzo yetu.
PROFESA:Tarehe za Vita Vikuu vya dunia zinashangaza sana tena sana na inatisha sana. Ngojea Nikuelezee Utafiti wa Tarehe hizi kisha tufikiri maajabu mengine yanayotokana na Namba hizi. Lakini uelewe tu Muujiza wa Kuruani na usichukulie kama utafiti huu ni sawa na Kupiga Bao au Ramli kwani Ni Haramu
AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa Asante sana. Ni habari ya kutisha sana lakini ningependelea kuijua.
PROFESA: Nisikilize Vizuri.
Vita Vya Kwanza Duniani Vilifanyika Tarehe
28/7/1914
Unaweza kuhakikisha Tarehe Hii katika Chombo cha utafiti “Google” ili uamini. Na Tarehe hii ni ya kweli.
Vita Vya Pili Duniani Vilifanyika Tarehe
01/09/1939
Unaweza kuhakikisha Tarehe Hii katika Chombo cha utafiti “Google” ili uamini. Na Tarehe hii ni ya kweli.
Na Vita Vya Mwaka Huu Yaani Russia na Ukraine Vilianza Tarehe
24/02/2022
Unaweza kuhakikisha Tarehe Hii katika Chombo cha utafiti “Google” ili uamini. Na Tarehe hii ni ya kweli.
AL-AMIN ALI HAMAD:Nakusikiliza Vizuri. Endelea Profesa.
PROFESA: Sasa Tuone hapa Chini Maajabu Yafuatayo:
Ngoja Nipange Tarehe hizi kisha Tujumlishe;
28/7/1914= WWI (First World War)
01/09/1939=WW2 (Second World War)
24/02/2022=Russia +Kuivamia Ukraine
Hebu Angalia Maajabu:
Tujumlishe Namba Hizi kisha Tuone Maajabu:
28 + 7 + 19 + 14=68
01 + 09 + 19 + 39=68
24 + 02 + 20 + 22=68
AL-AMIN ALI HAMAD:Profesa Haya Maajabu Sana. umejumlisha Namba za Vita Ya Kwanza kisha Ya Pili na Vita Hivi vya karibuni na Jawabu ya Tarehe hizi zote Tatu ni sawa yaani 68. Kwa vipi mbona Inashangaza. Yaani Je Hivi vita vya Russia na Ukraine ni Vita Vya Tatu? Je tupo mwanzoni mwa Vita Vya Tatu? Mbona Unanitisha?
PROFESA: Nilikuambia Kwamba Usiamini Namba kwani huenda siyo kweli kwani zinababaisha lakini mimi mwenyewe sijui huenda ni vita vya tatu. Kwa kweli sina uhakika kwani sifanyi kazi ya Bao au Mzimwi. Tusome tu na iishie hapa. Usiogope kwani kuogopa kunatokana na Mashetani. Hizi ni Hesabu tu.
AL-AMIN ALI HAMAD: Asante Profesa kwa kunitia Moyo.Unasema Kweli kwani anayejua Ni Mwenyeezi Mungu tu na Tusiingilie kazi zake. Hatujui ya baadaye.
PROFESA: Jambo la kushangaza ni kwamba ukitoa Miaka Hii kutoka katika Jumla ya idadi ya Aya za Kuruani tunapata Maajabu Mengineyo.
AL-AMIN ALI HAMAD:Hebu nionyeshe Profesa hesabu hiyo.
PROFESA:Ngoja nipange zile tarehe hapa chini kisha nikuonyeshe maajabu mengine:
28/7/1914= WWI (First World War)
01/09/1939=WW2 (Second World War)
24/02/2022=Russia +Kuivamia Ukraine
Jumla ya Aya za Kuruani ni 6236 sasa tutoe Miaka tuliyotaja hapo juu tuone maajabu mengineyo:
6236-1914=4322
na 4322-1939=2383
na 2383-2022=361
Na namba hii 361 ni sawa na 19 x19
Je unaona Namba 19 ni namba ambayo imetajika katika kuruani kama ni Mojawapo ya Muujiza Mkubwa na Pia Ukigeuza Jina La Msikiti mkubwa wa Kiislamu Huko Palestina yaani المسجد الاقصا au Masjid Al-Aqsa
katika Thamani ya Herufi za Kiarabu zilizitumika Hapo zamani wakati namba zilikuwa bado kujulikana. Waarabu na Mataifa Mengineyo walitumia Herufi Kuwakilisha Namba. Na Kwa hiyo Ukitafuta Thamani Ya المسجد الاقصا utapata 361 pia.
AL-AMIN ALI HAMAD: Kuna uhusiano gani kati ya Msikiti huu na jawabu la Miaka 361 tuliyopata hapa juu ya Vita Kuu za Dunia?
PROFESA: Labda ina maana kwamba huenda Palestina watapata Uhuru karibuni au labda Msikiti usiwe tena chini ya Hukumu ya WaIsraeli. Kwa kweli sipendelei kuingilia mambo ya Baadaye lakini namba hizi zinaonyesha maajabu sana. Je huoni Namba zinavyotatanisha? Je huoni Maajabu siyo madogo?
AL-AMIN ALI HAMAD:Naona bora tumuachie Mwenyeezi Mungu na tusiingilie kazi zake. Kwa kweli inashangaza sana.
PROFESA:Maajabu hayajakwisha kwani bado sijamaliza:
Hebu tufanye hesabu nyingine tuone maajabu yasiyo na mwisho:
28/7/1914= WWI (First World War)
01/09/1939=WW2 (Second World War)
24/02/2022=Russia +Kuivamia Ukraine
Sasa tujumlishe Namba hizi moja moja tuone jawabu na tulinganishe.
Vita Vya Kwanza:
2 + 8 + 7 + 1 + 9 + 1 + 4=32
Vita Vya Pili:
1 + 9 + 1 + 9 + 3 + 9=32
Vita Vya Russia Na Ukraine
2 + 4 + 2 + 2 + 0 + 22=32
Jawabu ni 32 na linafanana. Je unaona ya maajabu namba hizi tatu zinawiana. Kwa nini Zinafanana kiajabu hivi? kuna siri gani? Hakuna ajuae isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake. Tusichokonoe chokonoe siri za Muumbaji. Tusicheze cheze kwa ujinga kwani ni hatari kubwa. Tunapofika Mwisho wa Elimu au Ujuzi basi Tuseme. Allahu Akbar. Na Tuombe Mwenyeezi Mungu Tuepushie Balaa la Vita Lakini Usiendelee kuchokonoa chokonoa kwani hatukupewa Elimu ya Ghaibu. Tumche Mwenyeezi Mungu na Tumuogope sana. Vita siyo mchezo na harari sana. Vita Huleta Njaa na Maafa Makubwa sana tena sana. Allahu Akbar.
AL-AMIN ALI HAMAD:Profesa Mbona tarehe ya Vita Vya Russia Na Ukraine hukujumlisha namba 22 moja moja kama vile
2 + 4 + 2 + 2 + 0 + 2 + 2=14
lakini wewe umeziacha namba hii 22 kama mwanzo wa hesabu yetu yaani hivi:
2 + 4 + 2 + 2 + 0 + 22=32
PROFESA: Ili tupate namba 32 imekuwa sina budi bali kuiacha namba 22 hivyo hivyo kwani ningeliijumlisha moja moja kama vile 2 + 2 basi hesabu ya 32 tusingeipata. Kwa kweli inashangaza. Nimeiacha hivyo hivyo.
lakini tujaribu hesabu nyingine kama unataka namba za mwisho ziwe mbili mbili na tukifanya hivyo tutapata Muujiza Mwingine wa Kushangaza sana.
Hebu tuone hapa chini:
Vita Vya Kwanza: 28 + 7 + 1 + 9 + 1 + 4=50
Vita Vya Pili: 01 + 9 + 1 + 9 + 3 + 9=32
Vita Vya Russia Na Ukraine
24 + 2 + 2 + 0 + 2 + 2=32
AL-AMIN ALI HAMAD:Sasa mbona Namba ya Vita Vya Kwanza tukijumlisha tunapata jawabu ni 50 na siyo 32 kama tulivyoona mwanzo sasa wapi huo Muujiza?
PROFESA: Naam, Haya ndiyo maajabu kwani ukijumlisha Majawabu Haya Matatu tuliyofanya hapa juu tunapata 32 + 32 + 50=114
Tunapata Namba ya kushangaza sana nayo labda inaashiria Jumla ya Sura za Kuruani ambazo ni 114
AL-AMIN ALI HAMAD: Eeeeeeeeee Profesa Yayayayaya Mbona Haya Maajabu makubwa. Mbona Hizi Namba Zinashangaza.. Kwanza Namba tulizopata zilikuwa Zinafanana. Kisha Uhuru wa Msikiti wa Palestina huko Israeli sasa mbona Namba 114 ni Jumla Ya Sura za Kuruani? Kwa kweli inashangaza sana tena sana.
PROFESA: Mimi siwezi kukujibu kwani Mara nyingi namba huwa zinadanganya. Uwe macho usifuatilie sana.
AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa unaaema kweli lakini ninashangaa sana, sana sana. Kwani Mwenyeezi Mungu ameumba Dunia Kwa Kutumia Namba. Na Kwa kweli Ulimwengu ni Kuruani Tunayoiona kwa macho na Kuruani ni Ulimwengu tunausoma. Kwa nini isiwe kweli? mambo haya yana maajabu sana.
PROFESA: Wakati wa usiku umeingia na ningeona bora tufanye kukutana tena kesho Mwenyeezi Mungu akipenda kwa Mazungumzo zaidi.
AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa Asante sana kwa kunipa habari mpya leo hii. Mwenyeezi Mungu akubariki. Leo usiku nitakapokuwa kitandani nitawaza sana Namba hizi na hasa Vita Vya Dunia Kwani Inatisha sana.
PROFESA:Usiogope Namba zinababaisha. Usifuatilie mambo bila ya Uhakika. Mwachie Mwenyeezi Mungu tu. Wewe Omba Dua tu Mwenyeezi Mungu atuepushie na Hatari za Vita Vua Dunia.
AL-AMIN ALI HAMAD: Asante Sana Profesa. Inshaallah Tutatonana Kesho mwenyeezi Mungu akipenda.
PROFESA: Amin
INAENDELEA…………………………………….