SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Wanavyuoni/Wataalamu

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

Sheikh Shariffudin Khalifa

Video-1 na Video-2  hapa chini ni za Sheikh Sharifudin Khalifa huko Tanzania.Akihutubia watu bado mdogo sana. Ni mifaano yake mwenyeezi mungu katika ulimwengu huu. Akiamua jambo basi anafanya anvyotaka kama alivyowema katika kuruani takatifu;

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡىِۦۤ أَن يَضۡرِبَ مَثَلاً۬ مَّا بَعُوضَةً۬ فَمَا فَوۡقَهَا‌ۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡ‌ۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلاً۬‌ۘ يُضِلُّ بِهِۦ ڪَثِيرً۬ا وَيَهۡدِى بِهِۦ كَثِيرً۬ا‌ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦۤ إِلَّا ٱلۡفَـٰسِقِينَ

Menyeezi Mungu anasema hapa kwamba Hakika Mwenyeezi Mungu haoni haya kutoa mfano wowote wa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale wanaoamini, wao hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa mola wao; lakini wale waliokufuru husema “Ni nini analotaka Mwenyeezi Mungu kwa mfano huu”(Mwenyeezi Mungu) huwaachia wengi kupotea kwa mfano huo na huwaongoza wengi kwa mfano huo pia; lakini hamwachii yoyote kupotea kwa mfano huo (na mwingineo)isipokua wale wavunjao amri (zake).

Video-1

Video-2

Mashekhe Katika Nchi Ya Afghanistan

Kama tunavyoona katika Video-3  hapa pembeni Hawa Mashekhe huko Afghanistan wanaomba dua kisha Maji yanatiririka kutoka katika milima kwa kutumia kuruani tukufu. Je Mnaona Ajabu ya maneno ya mwenyeezi mungu? hawa wachamungu huko Afghanistan wanasoma kuruani na huku wakitarajia maji kutoka katika Majabali ya milima. Na hii ni kawaida mara nyingi mwenyeezi mungu ukimnyenyekea vizuri na huku unafuata sheria za dini ya kiislamu basi atakupa chochote unachokihitaji. Kwani Dua sio za kuchezea. Ukifikilia kumcha mungu kama ipasavyo basi usiwe na wasiwasi mwenyeezi mungu atakuruzuku unachokitamani maadamu kitu hicho hakina madhara. Kwani Mola anasema katika kuruani kwamba “Unaweza kupenda kitu na huku kina madhara na wewe na pia huenda ukachukia kitu na hali kuwa kina kheri na wewe”

Video-3

Sheikh Mala Ali Mwananchi Wa Nchi Ya Iraq Kurdistan

Kama unavyoona katika Video-4 and Video-5  hapa chini za  Sheikh Mala anawatibu wote wawili  kipofu na pia kibubu ambaye pia alikuwa hawezi kutembea lakini wote wawili aliwatibu na kufanikiwa.

Sheikh Mala amezuka miaka hii ya karibuni bado hatumjui maisha yake lakini ana Video  za matibabu mbalimbali. Aliwahi kutiwa jela kwa kutuhumiwa lakini alitolewa na kuendelea na juhudi zake.

Anatibu watu wa dini zote na hata wasiokuwa na dini pia.

Kuna Video nyinginezo anatibu maradhi yanayohusiana na Majini. Huu uwanja wa ulimwengu wa Majini sipendelei kuingilia wala kushauri kwani ni ulimwengu mwingine pia unatisha sana.

Mshangao wangu ni maradhi tunayoyajua. Lakini ukweli ni kwamba kuruani ni Muujiza mkubwa ambao ukiamini yanaweza kufanyika haya na wala sio jambo la kushangaza. Mwenyeezi Mungu ametuletea Kitabu hiki ili kitufae kwa njia nzuri. Kwa kuruani chochote kinawezekana kwani ni maneno yake mwenyeezi Mungu.

Huyu Sheikh hivi sasa yupo hapa Ulaya kwa shughuli zake, anatembelea nchi mbalimbali na pia kuwatibu watu wenye dini mbalimbali na sio waislamu tu pekee.

Baada tu ya kutibu ugonjwa wowote ule anatoa nasiha tufuate kuruani na kumcha mungu na anasema ukweli kwamba dawa kubwa ni kumcha Mungu tu na hakuna dawa nyingine yeyote. Inaonyesha kwamba Sheikh Mala amepewa zawadi na mwenyeezi Mungu ya uwezo huu wa ajabu sana.

Video-4

Kufuatana Na Hadithi Ya Mtume Iliyopokelewa Na Bukhari Haipendezi Kumtegemea Mwingine Atufanyie Rukya Kwani Ukiwa Na Imani basi Uombe Mungu Mwenyewe Kwa Matibabu Ya Rukya. Ukijifanyia Mwenyewe Ni Vizuri akuepushie Mtihani lakini Usitegemee mwingine akuombee. Ndugu waislamu Tusome Dini Vizuri.

KURUANI TUKUFU

KURUANI YA WATAALAMU MBALIMBALI ULIMWENGUNI.

Hapa chini kuanzia Video namba 6, 7 na 8 ni za Kuruani tukufu za baadhi ya  wasomi mbalimbali mashuhuri ulimwenguni

Video-5

Kuruani inasomwa kwa ufundi mkubwa na Sheikh Wa kwanza kusoma katika Radio ya huko Misri mwaka 1934. Rikodi ya maisha yake inatueleza kwamba alizaliwa mwaka 1882 na akafariki mwaka 1950. Alihitimisha kuifadhi kuruani yote alipokuwa umri wa miaka kumi na kisha akaendelea kusoma sheria za kuruani.

Video-6

Sheikh Mohamed Al-Kurdi mzaliwa wa Afghanistan na maarufu sana kwa kisomi cha Kuruani, kama hapa katika video hii kuruani anaisoma kwa utulivu na kila aya anaisoma kwa ufundi mkubwa, sikiliza na ikiwezekana fuatilia sura hiyo kwa Tafsiri Ya Quruani Kwa Kiswahili ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy.

Video-7

Qurani na Sheikh Hady Toure mzaliwa wa Senegal Inasomwa huko Dakar mji mkuu wa Senegal. Tafsiri ya maneno ya Kifaransa yaliandikwa hapa juu ni “Sheikh Hady Toure Anatingisha Mji Wa Dakar Kwa Kisomi Chake” Mwenyeezi Mungu ambariki kwani kisomo chake kinaliza watu kama utakavyoona katika Video hii.

Ukubwa Wa Mwenyeezi Mungu Na Utukufu Wa Mtume wake Mohamed.

Video Namba 9 inahusiana na Maoni Ya Mwanachuoni Khalid Yasin Kuhusu  Utukufu Wa Mtume Mohamed Na Katika Na Video ya 10 Mwanachuoni Ahmad Ally anatuelezea utukufu na ukubwa wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu.

Video-8

Khalid Yasin Anaelezea Ukubwa Wa Mtume Mohamed Miongoni Mwa Wakubwa Wengineo Ulimwenguni

Video-9

Sheikh Ahmed Ali Anatuelezea Maoni Yake Kuhusu Ukubwa wa Mwenyeezi Mungu. (Arshi Ya Mwenyeezi Mungu) Throne of Allah

Video-10

Sheikh Ahmad Kutoka Uganda. Alitoa Hotuba Hii Huko Pakistan karibu miaka 11 iliyopita. Video Muda Mfupi lakini Maneno anayozungumza siyo madogo. Video Inasisimua. kama sikosei Alitoa Hotuba hii mwaka 2010. Mwenyeezi Mungu ambariki na ampe kila la kheri katika Maisha Ya Dunia Na Akhera.

MAONI YA WANASAYANSI MAARUFU ULIMWENGUNI JUU YA KURUANI TUKUFU

MAONI YA WANASAYANSI MAARUFU ULIMWENGUNI JUU YA KURUANI TUKUFU

Katika Video Ya 11 hapa chini wanavyuoni wa kisayansi wakubwa ulimwenguni wanashuhudia utukufu wa kuruani na wanakiri kwamba kuruani sio kauli za binadamu bali kutoka kwa mwenyeezi mungu mtukufu. Kwa kifupi kila mwanachuoni hapa ame somea kazi yake vizuri na kila mmoja anapata katika kuruani yanayohusiana na uwanja wake kinachozidisha imani. Kuruani siyo kitabu cha sayansi bali kuna alama mbalimbali za kimuujiza ambazo ni hoja kwa watu wote wenye kutaka kuifahamu na jibu kwa kila anyepinzana nayo ili iwe hoja siku ya kiama. Hakuna atakayedai kwamba hakupata ujumbe.

MAONI YA WANAVYUONI WASIOKUWA WAISLAMU KUTOKA NYANJA ZA ELIMU MBALIMBALI ULIMWENGUNI KUHUSU MTUME MOHAMED (Sala Na Amani Yake Mola Zimfikie)

Video mbili zinazofuatia (Video-12 na Video-13) zimekusanya maoni ya baadhi ya wana vyuoni maarufu wasiokuwa waislamu na fikra zao juu ya mtume Mohamed. Kila mmoja katika hawa wamemsifu Mtume Mohamed kwa kila sifa za hali ya juu. Hawa ni baadhi tu na sio wanavyuoni wote. Kila mmoja wa hawa ametoa sababu zilizomfanya kumchagua Mtume Mohamed kuwa ni kiongozi anayestahiki utukufu

Video-11

Video-12

Video-13

WANAVYUONI WALIOCHANGIA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA SAYANSI ZA LEO

KATIBA YA KWANZA DUNIANI

Katiba ya Kwanza Duniani ni ile iliyoandikwa na Mtume Mohamed inayojulikana kama The Constitution of Medina (دستور المدينة, Dustūr al-Madīnah), also known as the Charter of Medina (Arabic: صحيفة المدينة‎, Ṣaḥīfat al-Madīnah; or: ميثاق المدينة, Mīthāq al-Madīnah “Covenant of Medina”). Aliiandaa Katiba hii baada tu ya Kuhama Madinna ilipokuwa ikijulikana kwa jina la Yathrib.Katiba hii iliwahusu makabila mbalimbali yaliyokuwa wakati huo.Makabila yaliyokuwa hapo Madinna na Waislamu waliokuja kutoka Mecca. Watu wengi bado hawaelewi kwamba Katiba Hii ndiyo ya mwanzo duniani kwani hakuna Katiba iliyokamilika kama hii kabla ya karne ya 7.

MODERN OPTICS

Elimu Ya Sayansi Tunayoisoma Leo inayojulikana kama Modern Optics ilianzishwa na Mwanachuoni wa Kiislamu anayejulikana kwa jina kama Ibn Al-Haytham anyejulikana katika nchi za ulaya kwa jina la Alhacen au Alhazen. AlIzaliwa mwaka 965 huko Basra-Iraq na kufariki hko Cairo-Egypt mwaka 1040. Elimu hii ya Optics inatumiwa leo hii katika nyanja mbalimbali za sayansi. Camera, Television, X-Rays, Matibabu ya Macho na Katika Nyanja mbalimbali nyinginezo Hatuwezi kutaja hapa yote kwani Elimu hii ipo kila pahali ya maisha yetu. Kwa kifupi Al-Haytham ndiyo baba wa Elimu hizi za sasa. Mwenyeezi Mungu ambariki Shekhe huyu.

COMPUTER NA IP PHONES -DIGITAL WORLD

Mohamed Ibn Musa Al-kwarismi ambaye alijulikana katika nchi za Ulaya kwa jina la Algorithmi kwani ndiye aliyekuja na Elimu ya Algorithm. Alizaliwa mwaka 780 na kufariki mwaka 850. Aliandika vitabu katika nyanja za Mathematics, Astronomy na Geography. Alitunukiwa kupewa cheo cha Astronomer na pia Mkuu wa Library ya house of Wisdom Hulo Bagdad-Iraq. Algorithm ndiyo msingi wa Computer, Simu za mkono na mengi mengineyo. Asingetuletea Elimu hii ya Algorithm tusingekuweko Digital IP Phones na Computer Leo hii. Kwa kifupi huyu ndiye sababu za kuweko Mawasiliano ya kisasa ulimwenguni. Nitaishia Hapa kwani habari zake ni ndefu na amefanya mengi yenye faida.

RAMANI ZA ULIMWENGU

Waislamu walifanya kazi kubwa katika Kuchora Ramani za Ulimwengu. Hapo awali Kusini ilichorwa Juu na Kaskazini Chini (Upside Down). Hapo baadaye Wazungu wakabadili mchoro wa Kusini na Kaskazini. Kusini ikawekwa chini na Kaskazini Juu katika Ramani. Hapa tutawataja baadhi tu ya Wanachuoni Maarufu kwani walikuwa wengi. Al-balkhi katika karne ya 9/Al-istakhri, Ibn Hawkal na Ibn Masudi Katika Karne ya 10/Mahmud Elkasgari karne ya 11/ A-lidrisi kaika karne ya 12 na wengi wengineo. Fadhila nyingi zinarudi kwa hawa wanavyuoni wa kiislamu katika kuchangia michoro ya Ramani kubwa kubwa za Dunia.

AVIATION-AEROPLANE-SAFARI ZA ANGA

Abu al-Qasim Abbas ibn Firnas ibn Wirdas al-Takurini (c. 809/810 – 887 A.D.), aliyejulikana kama Abbas ibn Firnas (Arabic: عباس بن فرناس‎), aliyejulikana ulaya kwa jina la Armen Firman alikuwa asili yake kutoka Spain (Ibn Firnas was born in Spain in 810AD. However, he lived in Cordoba) alikuwa inventor, astronomer, physician, chemist, engineer, Andalusi musician, na Mshairi wa lugha ya Arabic. Alifanya juhudi zake katika kutafuta njia za kupaa angani Wataalamu wanatuambia yafuatayo: (He was reported to have experimented with a form of flight.According to John Harding, Ibn Firnas’ glider was the first attempt at heavier-than-air flight in aviation history. Ibn Firnas made various contributions in the field of astronomy and engineering. He constructed a device which indicated the motion of the planets and stars in the Universe. In addition, Ibn Firnas came up with a procedure to manufacture colourless glass and made magnifying lenses for reading, which were known as reading stones).

MZUNGUKO WA DAMU MWILINI

Ibn al-Nafis Alizaliwa mwaka 1213 na kufariki huko Cairo mwaka 1288 Wataalamu wanatuambia kwamba Ibn Al-Nafis ndiye wa kwanza duniani kuelezea mzunguko wa damu mwilini kabla ya William Harvey. (He is known for being the first to describe the pulmonary circulation of the blood. The work of Ibn al-Nafis regarding the right sided (pulmonary) circulation pre-dates the later work (1628) of William Harvey’s De motu cordis).